Dimbwi la Damu Sehemu ya Tatu
MAISHA

Ep 03: Dimbwi la Damu

SIMULIZI Dimbwi la Damu
Dimbwi la Damu Sehemu ya Tatu

IMEANDIKWA NA: ERIC SHIGONGO

*********************************************************************************

Simulizi: Dimbwi La Damu

Sehemu ya Tatu (3)

Maisha yao yaliendelea vizuri katika jiji la Ottawa nchini Canada! Kwa pesa aliyokuwa nayo Shabir alifungua vituo vya mafuta kumi na sita katika jiji hilo, vilimchanganyia kiasi cha kutosha na kwa kutumia ujanja wa kukwepa kodi aliotoka nao Tanzania alizidi kujitajirisha kiasi kwamba katika muda wa miaka mitano alikuwa miongoni mwa mamilionea nchini Canada.

Ilikuwa ni familia yenye furaha na maisha ya Victoria yalikuwa mazuri kupita kiasi, wakati huo alikuwa kidato cha tatu katika shule ya St. George, ilikuwa ni shule maarufu ya vipofu nchini Canada.

Tayari Victoria alikuwa msichana aliyekomaa alishavunja ungo! Alipelekwa shuleni na gari na alinunuliwa nguo nzuri na mpya karibu kila baada ya miezi mitatu! Ilikuwa si rahisi hata siku moja kugundua hakuwa mtoto wa familia hiyo, kitu pekee kilichowafanya watu wahisi hakuwa mtoto wa Shabir ni rangi ya ngozi yake.

Shabir na Leah kwa maisha na matunzo waliyompa Victoria walifikiri alikuwa na raha sana katika maisha yake lakini ukweli haukuwa huo, alikuwa ni miongoni mwa watu wenye huzuni sana duniani na yote hiyo ilikuwa ni sababu ya kaka yake Nicholaus! Kila siku alimkumbuka na kulia machozi, chakula na mavazi aliyopewa hayakutosha, siku zote aliamini Nicholaus pekee ndiye alikuwa furaha yake.

Nicholaus alizidi kuning’inia huku akiyagusa maji kwa mikono yake bila kujua ni kitu gani kilikuwa kimeng’ang’ania shati na suruali yake kwa juu! Ghafla aliona kitu kama kenge mkubwa kikiyakata maji kumfuata, alipoangalia vizuri aligundua ni Mamba! Akajua alikuwa chakula chake siku hiyo, kifo alianza kukiona karibu yake kwa mara nyingine na alitetemeka mwili mzima.

Lakini alishangaa kuona anavutwa kutolewa ndani ya bwawa huku akisikia miungurumo ya wanyama wenye hasira shingoni kwake! Alijikuta akitupwa kwenye nyasi na wanyama hao walimvamia hapo hapo ardhini na kuanza kumshambulia. Walikuwa ni mbwa wakali na wakubwa kama ndama, aliwakumbuka mbwa hao waliokuwa wakimkimbiza kabla hajadumbukia ndani ya bwawa.

Pamoja na kuumwa sana na mbwa shingoni na matakoni bado Nicholaus alifurahi kwa sababu alikuwa ameokolewa, kwani alijua wazi bila mbwa hao kumnasa na kumtoa ndani ya bwawa ni lazima angeliwa na Mamba na huo ndio ungekuwa mwisho wake! Angekufa bila kumwona dada yake Victoria jambo ambalo hakutaka kabisa litokee na alimwomba Mungu aliepushe.

“Stooooooop!” (Achaaaa!) Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume ikitokea upande wa pili, mbwa wote walitii amri hiyo na kuacha kumuuma Nicholaus! Alikuwa ni mwanaume mrefu na mnene na mwenye ndevu nyingi kama ilivyo kawaida ya watu wa Iran.

Alianza kumsemesha kwa lugha ya Kiirani lakini Nicholaus hakuelewa kitu kilichosemwa, alibaki amekusanya mikono yake miwili na kupiga magoti chini akimwomba msamaha mwanaume huyo aliyeonekana kuwa mlinzi akiwa na gobole lake mkononi.

“Forgive me and please save my life!”(Nisamehe na tafadhali okoa maisha yangu)

“You….! You…! Are you engrish?”(Wewe…! Wewe…! Wewe ni Muingereza?) Aliuliza mlinzi huyo kwa kiingereza kibovu akitaka kujua kama Nicholaus alikuwa Muingereza.

“I’m a Tanzanian!”(Hapana mimi ni Mtanzania!) Alisema Nicholaus na mwanaume huyo alimmulika tochi na kumwangalia kwa makini usoni.

“Ha!My God!”(Ha! Mungu wangu!) Mlinzi alionekana kushangaa alipoiona sura ya Nicholaus na palepale alianza kumvuta kumrudisha hospitali.


Akiwa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya vipofu ya St. George, Victoria alishabadilika kiasi cha kutosha! Alikuwa msichana mrefu mwembamba na zaidi ya sifa hizo alikuwa na umbile la kike haswa! Alikuwa amebadilika kutoka umbile la minyoo hadi umbile la herufi ‘d’

Alijaliwa maumbile makubwa kwa nyuma yaliyotingishika kila alipotembea, alikuwa na mguu mkubwa uliojaza kama chupa ya bia aina ya Primus! Kifupi katika wakati huo Victoria alimvutia kila mtu aliyemwona na haikuwa rahisi kugundua alikuwa kipofu kama mtu alimkuta amekaa kwa jinsi alivyoonekana mzuri!

Wakati mwingine alipojipapasa kwa nyuma na kujilinganisha na wasichana wenzake aliowagusa waliokuwa na maumbile ya kizungu shuleni aligundua maumbile yake hayakuwa ya kawaida!

“Mama au mimi nina ugonjwa?” Victoria alimuuliza Leah baada ya kugundua umbile lake halikuwa la kawaida.

“Kwanini?”

“Hili umbile langu linanishangaza, wanafunzi shuleni wananizomea sana!”

“Mbona hata mimi nilikuwa hivyo! Huo si ugonjwa”

Kwa Victoria, Leah alikuwa ni kama mama yake, alihesabu ndiye ndugu peke yake aliyekuwa amebakiza duniani, hakumhesabu tena kama mtumishi wa ndani kama ilivyokuwa wakati wa uhai wa wazazi wake! Siku zote alimwita Leah mama na Leah alimchukulia Victoria kama mtoto ingawa walipishana miaka michache sana kati yao.

Shabir alimpenda Victoria kuliko hata Manjit mtoto wake wa kuzaa! Alimpa Vicky kila alichohitaji katika maisha yake, kila siku za Jumapili ilikuwa ni lazima amshike mkono na kumtembeza sehemu mbalimbali za jiji la Ottawa na alifanya hivyo kwa madai ya kutaka kumfanya ajisikie vizuri!

Kwa upendo huo wa Shabir ulimfanya Victoria alizidi kujisikia kupendwa, kitu pekee kilichopungua maishani mwake kilikuwa ni Nicholaus kaka yake alitamani angekuwepo Canada ili wafaidi maisha pamoja.

“Sijui hivi sasa atakuwa wapi Nicholaus, nafikiri atakuwa yupo hai mahali fulani, si ajabu siku moja nitapokea simu kutoka kwake nina uhakika siku hiyo ndiyo itakuwa siku ya furaha kuliko zote maishani mwangu!” Aliwaza kila mara Victoria.


Wakati Shabir anamwoa Leah huko Arusha miaka mingi kabla ya kuhamia Canada, Leah alikuwa kitu cha uhakika, alikuwa mrembo kupindukia! Maumbile yake ya nyuma yalikuwa ya utatanishi, mtoto alijaliwa na akajaliwa kwelikweli! Ni kitu hicho ndicho kilichomchanganya akili Shabir.

Siku zote alipenda sana wanawake wenye makalio makubwa! Hata mke wake aliyekuwa naye kabla ya kumuoa Leah alikuwa hivyo hivyo, nguo zake alilazimika kupima kwa mafundi cherehani hakupata nguo za kununua moja kwa moja dukani, zilimbana kupita kiasi na kuchanika siku chache tu baada ya kuzinunua.

Shabir alipenda maumbile ya namna hiyo! Na hivyo ndivyo alivyokuwa Leah lakini baada ya kumzaa Manjit na kumnyonyesha maumbile yake yalianza kusinyaa na mwili wake ulianza kuporomoka! Makalio yake makubwa yakapotea na kujikuta amepigwa randa!

Jambo hilo lilipunguza sana mapenzi ya Shabir kwa mkewe lakini asingeweza kumwacha kwa sababu hiyo,alizidi kuvumilia sababu walikuwa na mtoto wao mzuri Manjit!

Ingawa hakuna mtu katika familia yake aliyelijua jambo hilo lakini Shabir alikuwa miongoni mwa watu waliovutiwa sana na maumbile na mabadiliko ya Victoria kimwili, alifurahi kila alipomwona Victoria akitembea mapigo ya moyo wake yalienda sambamba na mitetemo ya maungo ya Victoria kila alipotembea.

Tangu wakati huo Shabir alibadilisha hata aina na mitindo ya nguo alizomnunulia Victoria akawa ananunua nguo za kumbana na viblauzi vilivyoacha kifua na sehemu ya matiti ya Victoria wazi! Mke wake alifikiri ni jambo la kawaida lakini lengo la Shabir lilikuwa si jema alitaka kuyaona maumbile ya Victoria.

Leah aliendelea kuichukulia hali hiyo kama mapenzi ya baba kwa mtoto, hata siku moja hakuwahi kuwaza kuwa mumewe angeweza kumtamani Victoria kimapenzi.

Upendo wa Shabir kwa Victoria ulizidi kuongezeka siku hadi siku hadi alipomaliza kidato cha nne, ingawa Victoria alikuwa kipofu ilifikia wakati akawa analazimisha kwenda naye kwenda tafrija za wafanyabiashara wenzake usiku akimwacha mke wake nyumbani!

Leah hakushangazwa na mambo hayo alizidi kuitafsiri hali hiyo kama mapenzi ya kizungu kwa watoto, jambo ambalo watu wengi nchini Canada walilifanya! Halikuwa jambo la ajabu baba kutembea amemkumbatia mtoto wake wa kike au mama kutembea akiwa amekumbatiwa na mtoto wake wa kiume.

Katika tafrija alizokwenda na Victoria, Shabir alicheza naye muziki akiwa amemkumbatia, wafanyabiashara wenzake walifurahi kuona mzazi akimchangamsha mtoto wake kipofu.

“I’m trying to make my daughter enjoy life! Being blind doesn’t mean staying at home all the times!”(Ninajaribu kumfanya mtoto wangu afaidi maisha kwani kuwa kipofu haimaanishi kukaa nyumbani muda wote!) Shabir aliwajibu watu kila walipoonekana kumwangalia.

“Is she your daughter?”(Huyo ni binti yako?) Watu wengi walimuuliza.

“Yes, My foster child!”(Ndiyo mtoto wangu wa kufikia)

Ingawa alijua wazi mawazo yake yalikuwa yakimpeleka pembeni, homa ya mapenzi ya Shabir kwa Victoria iliendelea kuongezeka siku hadi siku, kila Victoria alipopita mbele yake alihisi damu mwilini mwake ikisisimka na pamoja na upofu wake mara kwa mara alimtuma vitu.

“Bwanae! Mtoto kipofu huyu akalete maji ya nini wakati sisi wenye macho tupo?” Leah alisema siku moja Shabir alipomtuma Victoria maji.

“Basi hata wewe kalete, lakini nilitaka afanye mazoezi kidogo!” Shabir alisema akiwa na amejawa na aibu.

Tabia ya Shabir ilibadilika kupita kiasi mpaka Leah akaanza kuhisi vibaya huo! Ugomvi ulianza kujitokeza mara kwa mara ndani ya nyumba yao kisa kikiwa Victoria hasa baada ya Leah kumzuia Shabir kuwa anatoka na Victoria nyakati za usiku.

Pamoja na ugomvi wao kufanyika chumbani bado Victoria aligundua kuwa yeye ndiye alikuwa chanzo cha ugomvi huo! Hakukubali tena kutoka na Shabir usiku baada ya kugundua nia yake haikuwa nzuri. Hakutaka kumkorofisha Leah kwa sababu yeye ndiye alikuwa kila kitu kwake.

Matukio hayo yalimfanya Shabir aamue kumpa mke wake likizo kwenda Bombay, kupumzika lakini hakuruhusu Victoria aondoke! Leah alilikataa jambo hilo kwa nguvu zote lakini kwa sababu Shabir alishaamua na tiketi zilishakatwa ilibidi asafiri ingawa kwa shingo upande, alihisi kitu kingetokea baada ya yeye kuondoka.

“Unalia nini? Si utabaki na bibi Sundra!”Alisema Shabir baada ya ndege kuruka alipomwona Victoria akilia. Bibi Sundra alikuwa bibi kizee mwenye umri wa miaka isiyopungua sitini na tano na raia wa Canada.

Alikuwa mfanyakazi wa ndani ya nyumbani kwa Shabir ni huyo ndiye aliyemfanyia Victoria kila kitu!

“Ninataka kwenda na mama India!”

“Utakwenda safari ijayo kwa sasa baki nikutafutie shule usome!”

Victoria alilia kutoka uwanja wa ndege hadi nyumbani kwao ambako bibi Sundra alijaribu kwa nguvu zote kumbembeleza lakini haikuwezekana! Siku hiyo alilala bila kula.

Siku iliyofuata asubuhi Shabir alimwita bibi Sundra kwa maongezi aliyoyaita maalum, bibi alitoka jikoni na kwenda moja kwa moja hadi sebuleni ambako alimkuta Shabir akimsubiri, asubuhi hiyo Victoria alikuwa bado chumbani amelala!

“I have thought about it twice!”(Nimefikiria mara mbili)

“About what Mr. Shabir?”(Juu ya nini bwana Shabir?)

“It wasn’t right to let my wife travell alone to India!”(Haikuwa sahihi kumwacha mke wangu asafiri peke yake kwenda India) Shabir alisema huku akipigapiga juu ya meza.

“Yes, my son so?”(Ndiyo mwanangu, kwa hiyo) Aliitikia bibi Sundra.

“I have made up my mind and I and Victoria will be travelling to Bombay this afternoon, so I would like you to take a one month leave till we come back, because we are closing everything!”(Nimebadilisha maamuzi yangu na mimi na Victoria tutasafiri mchana wa leo kwenda Bombay kwa hiyo naomba uchukue likizo ya mwezi mzima mpaka tutakaporudi, sababu tutafunga kila kitu!) Alisema Shabir kwa msisitizo.

“No problem, when do you want me to start my leave?”(Hakuna tatizo ni lini unataka nianze likizo yangu?)

“Right now! This is you’re cheque!”Sasa hivi na hii hapa ni hundi yako ya malipo)

“Thanks Mr Shabir!”(Ahsante bwana Shabir) Alishukuru bibi Sundra na kuipokea hundi yake lakini moyoni alisikitika kutenganisha na Victoria kwani alimpenda mno.

Yote hayo yalifanyika Victoria akiwa chumbani akiendelea kulia!Baada ya kukabidhiwa hundi yake alikwenda chumbani na kuanza kupanga nguo katika sanduku lake kisha akaenda chumbani kwa Victoria kumwaga!

“Whaaaaaaat”(Nininiiiiii?) Aliuliza Victoria kwa mshangao mkubwa.

“I’m leaving!”(Ninakwenda)

“To?”(Kwenda wapi?)

Bibi Sundra alimweleza Victoria kila kitu walichoongea na Shabir, taarifa hizo zilikuwa mbaya sana katika moyo wa Victoria alilia kwa uchungu lakini hakuubadilisha ukweli.

“No! You cant leave me here, I suspect something bad is gonna happen to me grandma!”(Hapana huwezi kuniacha hapa bibi ninahisi kitu kibaya kitanitokea!)

“No Victoria daddy will take care of you, afterall he has told me you’re leaving for Bombay this afternoon!”(Hapana Victoria baba yupo atakutunza isitoshe ameniambia mchana huu mnaondoka kwenda Bombay!)

“I don’t think so!”(Sifikirii hivyo)Alisema Victoria huku akilia mawazo yake hayakuwa sawa, pamoja na upofu wake alihisi kitu kibaya kilikuwa kikija mbele yake!


Tamaa ya Shabir ilishakithiri, alimtamani Victoria kimapenzi kupita kiasi na alitaka kutenda naye kitendo kisichostahili lakini uwepo wa mke wake na bibi Sundra ndio kilikuwa kikwazo!

Hapakuwa na safari ya Bombay kama alivyomweleza bibi Sundra bali alitaka abaki nyumbani peke yake na Victoria ili aweze kutimiza haja zake za kimwili kwa mtoto huyo kipofu! Alijua Victoria asingekataa lakini hata kama angekataa alipanga kutumia nguvu na aliamini hakuna mtu angeielewa siri hiyo kwani nyumba yake ilikuwa kubwa sauti isingesikika nje!

Bibi Sundra aliondoka chumbani na kumwacha Victoria akilia machozi ya uchungu, alitamani kubaki lakini hakuwa na namna yoyote ya kupinga mpango wa mwajiri wake Shabir, alilazimika kuondoka!

“Take care of Victoria Mr Shabir, she is a nice girl!”(Mtunze vizuri Victoria bwana Shabir ni msichana mzuri sana)

“Yes I will!”(nitafanya hivyo) alijibu Shabir huku akifunga mlango nyuma ya bibi Sundra. Bibi akawa ameondoka nyumba nzima ikabaki na watu wawili, Victoria na Shabir.

Kwa shabir huo ndio ulikuwa wakati muafaka wa kutimiza haja zake, lakini aliamua kusubiri hadi usiku uingie ndio afanye mambo yake!mate ya uchu na tamaa yalimdondoka na alitembea hadi chumbani na kumkuta Victoria amelala kitandani akilia machozi. Kwa sababu ya upofu Victoria hakumwona lakini alipomgusa begani Victoria alishtuka.

“Stop crying victoria, I’ m here for you!”(Acha kulia Victoria niko kwa ajili yako)

“No daddy! I need Leah, grandmo sundra and Manjit as well!(Hapana baba namhitaji Leah, bibi Sundra na Manjit pia)

“They will be baaack! Dont worry!”(Watarudi tu usiwe na wasi wasi) Shabir aliongea hayo akimpapasa Victory mapaja na Victoria alihisi kuna tatizo lingetokea.

Shabir alishindwa kufanya jambo lolote baada ya kusikia wafanyakazi wa nje wa nyumba yake wakiongea kwa sauti, aliingiwa na hofu na kushindwa kutekeleza azma yake, aliamua kusubiri usiku uingie! Siku hiyo mishale ya sekunde, dakika na saa kwa Shabir ilitembea taratibu zaidi.


Katikati ya usiku Vicky alikuwa amejilaza kitandani mwake, hakuwa amepata hata lepe la usingizi noti aliyoachiwa na kaka yake ilikuwa mikononi mwake, alikuwa akimfikiria Nicholaus! Machozi yalikuwa bado yamkimbubujika kwa uchungu mwili wake ulitetemeka na alihisi jambo lolote baya lilikuwa likija mbele yake ingawa hakujua ni jambo gani.

Ghafla alishutkia kitu kikiifunua neti ya mbu iliyokizunguka kitanda chake, alishindwa kuelewa ni kitu gani kilichofanya hivyo! Alinyanyuka kwa haraka na kuketi kitako kitandani huku akitetemeka, muda mfupi baadaye alimsikia mtu akihema.

“Who are yooooou?”(Wewe naniiiiiii?) aliuliza Victoria lakini hakupata jibu lolote.

“Daddy somebody in my room!”(Baba kuna mtu chumbani kwangu!) Victoria alimwita Shabir bila kujua ni yeye aliyekuwa ndani ya chumba.

Alimsikia mtu akitambaa kitandani kuelekea mahali alipokuwa amekaa! Alizidi kuuliza lakini hakujibiwa kitu chochote!

Ghafla alishtukia kitu kizito kikimwanguka kifuani kwake na kumgandamiza kitandani, alijaribu kupiga mayowe lakini alifunikwa na mkono mdomoni na palepale nguo zake zilianza kushushwa kutoka mwilini mwake, nguo yake ya ndani ilichanwa! Mtu aliyekuwa akifanya yote hayo alikuwa kimya kabisa.

Victoria alijaribu kulia lakini sauti haikutoka na kilichofuata hapo kilikuwa ni maumivu ambayo Victoria hakuwahi kukutana nayo maishani mwake! Ilikuwa ni kama kutupwa katika tanuru la moto! Damu nyingi ilikuwa ikimtoka.

“Dadyyyyyyyyyyyyyy!”(Babaaa) alilia Vicky akimwita Shabir hakujua hata kidogo kuwa mtu aliyekuwa amemfanyia unyama ni Shabir..

“Call me Shabir and not your daddy, I love you Victoria, I didnt know you were a virgin! I’m sorry for what happened!”( Usiniite baba niite Shabir, sikujua wewe ni bikira samahani kwa yaliyotokea) Sauti nzito ya Shabir ilisema na Victoria alishindwa kuamini alifikiri labda ni ndoto..

“Why do you do this to me daddy?”(Kwanini unanifanyia hivi baba?) Aliuliza Victoria huku akilia lakini Shabir hakujibu kitu alizidi kumwingilia bila kujali kiasi cha damu kilichokuwa kikitoka.

Mchezo huo uliendelea mara mbili kwa wiki mpaka mwezi ukatimia, Victoria hakupenda lakini alifanywa mtumwa wa mapenzi na kuna wakati aliwekewa kisu shingoni kabla ya kuingiliwa! Mwezi mmoja ulipotimia hakuzipata siku zake za hedhi! Ilikuwa si kawaida yake kupitiliza, ilibidi amueleze Shabir na walipokwenda kupimwa mkojo aligundulika na mimba! Alilia kutwa nzima bila kujua angemwambia nini Leah akirudi kutoka Bombay, alihisi huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake! Alitamani kufa kuliko kukutana na Leah ana kwa ana !

Mlinzi alizidi kumvuta Nicholaus kumrudisha wodini lakini kwa Nicholaus kitendo hicho kilikuwa ni kuingia hatarini! Kukamatwa kwake kulimaanisha kifo na hakuwa tayari kufa kama tayari alishanusurika na kifo katika tetemekeo la ardhi!“Wewe si ndiye uliyekuwa upigwe risasi siku ile ya tetemeko nashanga ni kwanini hawakukugundua hebu twende!” Alisema askari akizidi kumvuta Nicholaus.

“Lakini meno yanaweza kunisaidia!” Aliwaza Nicholaus na kuangaza macho yake huku na kule, nyuma yake aliona kundi kubwa na mbwa likimfuata.

“Hapana ni lazima nijaribu kujiokoa hawezi kunikamata kibwege kiasi hiki!”Aliwaza Nicholaus na hapohapo bila hata kuchelewa aliikunja shingo yake kisawasawa mdomo wake ukatua kwenye mkono wa askari.

Aliyashindilia meno yake yote ya mbele ndani ya mwili wa askari huyo! Aliyasikia yakipenya sawasawa ndani ya nyama zake, askari alilia kwa maumivu makali lakini Nicholaus hakujali alizidi kuyazamisha! Damu nyingi ilitiririka kupitia pembeni mwa mdomo wake hilo halikumfanya aache kuyazamisha meno yake, alidhamiria kujiokoa kutoka mikononi mwa kifo.

“Aaaaagh! Nakufa!” Alilia askari huyo huku akijaribu kuutoa mkono wake mdomoni kwa Nicholaus lakini haikuwezekana! Ghafla meno yakatoka na kipande cha mnofu! Askari alianguka chini kwa maumivu makali.

Kwa Nicholaus huo ulikuwa upenyo wa kujaribu tena kuokoa maisha yake! Lakini aliwaogopa mbwa waliokuwa wakimsubiri na kumuungurumia pembeni yake! Alijua kitendo chake cha kukimbia kingemaansiha kuandamishwa na mbwa na kwa umri aliokuwa nao alijua isingekuwa rahisi kuwashinda nguvu mbwa hao wakubwa kama ndama!

Akiwa katika mawazo hayo ghafla alimwona askari akijaribu kunyanyuka ardhini ili amfuate, alionekana mwenye hasira kali! Kabla hajakaa vizuri Nicholaus alimfuata na kumpiga teke sehemu ya siri! Teke lake hilo lilifanikiwa kutua moja kwa moja kwenye korodani zake, akaangua kilio kingine na kurejea tena ardhini!

“Mama yangu mtoto wewe una balaa!” Alipiga kelele.

Nicholaus hakutaka kupoteza muda zaidi palepale alianza kutimua mbio kwenda upande wa pili, kundi kubwa la mbwa wakibweka lilimfuata.

“Sijui nifanye nini sasa?” Aliwaza huku akikimbia.

Ghafla wazo jipya lilimwijia kichwani ingawa hakuwa na uhakika kama lingeweza kumsaidia, alikitemea mkononi kipande cha mnofu kilichokuwa mdomoni mwake na kukitupa nyuma yake walikokuwa mbwa, kikatua usoni kwa mbwa aliyekuwa akiongoza mbio hizo! Mbwa wote walisita na kuanza kugombania kipande hicho cha nyama! Nicholaus akapotelea gizani.

“Vipi?

“Nilikikamata kitoto kimoja kilitoroka wodini!”

“Kitoto gani?”

‘Ni kile kilichotakiwa kupigwa risasi sababu ya kuigiza madawa ya kulevya hapa Iran kabla ya tetemeko!”

“Kilikuwa wapi?”

“Kumbe kilikuwa kimelazwa wodini!”

“Sasa kipo wapi?”

“Kimekimbia!”

Yalikuwa ni mahojiano kati ya mlinzi aliyeng’atwa na Nicholaus na walinzi mwenzake wa kampuni ya Metropol Security iliyoilinda hospitali hiyo walipofika eneo hilo mbio baada ya kusikia mwenzao akilia kwa sauti!

“Kimeelekea wapi?”

“Huko wanakobweka mbwa ndiko kimekimbilia!”

Walinzi nao walisikiliza kwa makini sauti ya mbwa ilikotokea na watatu kati yao walianza kukimbia kuelekea upande huo lengo lao likiwa kumkamata Nicholaus! Walipofika walikuta mbwa wamezuiliwa na senyenge za hospitali na hakumwona Nicholaus mahali popote.

Nicholaus alishauruka uzio wa senyenge na kutua upande wa pili ambako aliendelea kukimbia zaidi, kifua kilimbana sababu ya kukimbia sana lakini hakukata tamaa alizidi kuongeza kasi akipita katika majani marefu!

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuwa katika jiji la Tehran na hakuelewa mahali popote lakini hakuogopa alizidi kusonga mbele akiwa amekaa tamaa na alikuwa tayari kwa lolote! Mbele kidogo alijikwaa kwenye chuma na kuanguka, alipotupa macho mahali alipojikwaa aliiona reli ikipita alinyanyuka na kuanza kuifuata reli hiyo.

Alijua ni ingemfikisha stesheni ilikuwa ni reli ya kuelekea kwenye visima vya mafuta vya Aldharfi, vilivyokuwa maarufu kwa uzalishaji wa mafuta katika nchi ya Iraq, reli hiyo iliunganisha nchi ya Iran na Iraq.

Alitembea bila kujua muelekeo lakini alijua kwa uhakika ni lazima angefika katika stesheni ambako angekuta watu, mpaka wakati huo hakuwa na hofu ya kukamatwa tena hivyo alizidi kutembea kwa kasi kwenda mbele zaidi! Alitembea juu ya reli na kila gari moshi lilipokuja alijificha pembeni kwenye nyasi na kulipisha! Alitembea hivyo hivyo usiku kucha bila kufikia kituo chochote.

Mpaka jua linachomoza na Nicholaus alikuwa bado akitembea katikati ya reli, tena akiwa katika pori asilolifahamu vizuri, hakujua lilikuwa na wanyama gani wakali au la! Lilikuwa ni pori lililotisha lakini hakuogopa alizidi kusonga mbele, hakukata tamaa alitaka kujiokoa.

Kwa masaa mawili alizidi kutembea porini akifuata reli lakini mbele zaidi alichoka na kukaa juu ya reli kwa sababu ya uchovu alijikuta akipitiwa na usingizi na kulala juu ya reli.

**

Treni la abiria lililobeba vibarua wapya kutoka Tehran kwenda kwenye visima vya mafuta vya Mohamed huko Iraq lilikuwa likitimua vumbi porini lilikuwa na mwendo wa kasi kupita kiasi, wafanyakazi walikuwa wakiwahishwa kazini!Walikuwa ni vibarua wapya wa tajiri Mohamed aliyemiliki visima vingi vya mafuta nchini Iran, Iraq na Kuwait.

Mzee Mohamed mwenyewe alikuwemo ndani ya treni hilo baada ya kurejea kutoka Tehran ambako mke na mtoto wake walifariki kwa tetemeko la ardhi.

Hakuna mtu hata mmoja kati ya watu wote waliokuwemo ndani ya behewa la dereva wa treni aliyejua kuwa kilometa moja mbele yao Nicholaus alilala juu ya reli akiwa usingizini na kuota ndoto juu ya dada yake Victoria! Dereva alizidi kuongeza mwendo!

“Ongeza kasi tafadhali tumechelewa sana!” Mzee Mohamed aliamuru.

“Sawa mzee! Lakini tutawahi tu leo~”

“Lakini mimi utaniacha kambini akili yangu bado haijatulia kidogo baada ya kufiwa na mke na mtoto wangu! Ninahitaji kupumzika”

“Sawa mzee!” Alijibu dereva akiwa amemwangalia mzee Mohamed alipogeuza macho yake kuangalia mbele alisikika akipiga kelele!

“Mungu wangu tumeua!”

“Nini?”

“Kuna mtu katikati ya reli!”

“Funga breki!” Tajiri aliamrisha na dereva alijitahidi kufanya hivyo lakini kwa sababu ya kasi ambayo treni ilikuwa nayo haikuweza kusimama ilijivuta kwa nguvu kuelekea mahali Nicholaus alipolala relini! Lengo la dereva lilikuwa kumuokoa lakini ilionekana siyo rahisi!

“Mama yangu wee tunakufaaa!” Vibarua ndani ya mabehewa walisikika wakipiga kelele!

Nicholaus alizisikia kelele hizo na alipofumbua macho tayari treni lilishafika karibu yake kabisa tairi zake za chuma zilikuwa kama hatua moja kutoka alipolala! Hakuwa na njia ya kujiokoa alijua hicho kilikuwa kifo! Akaanza kusali sala ya baba yetu uliye mbinguni ili asife katika dhambi.


Ulikuwa ni uhakika kuwa Victoria alikuwa mjamzito, hilo halikuwa na mjadala hata kidogo! Alilia kila siku na kushindwa kuelewa angemweleza nini Leah akirudi kutoka Bombay alikokwenda kupumzika! Ilikuwa ni aibu kubwa mno kwake na alijua wazi huo ndio ulikuwa mwisho wa uhusiano wake na mkombozi wake Leah! Aliamini hata angemwambia alibakwa asingekubali.

Alihisi mateso yalikuwa yamerejea tena, shida zake zlikuwa zimeanza upya! Alishindwa kuelewa angekwenda wapi kama Leah angemfukuza nyumbani kwao.

Alijua angerudishwa Tanzania, lakini huko angeishi na nani? Aliamini hakuwa na ndugu wa kumtegemea! Victoria alichanganyikiwa na alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa mbele yake.

Alichokuwa na uhakika nacho kilikuwa ni mateso! Alijua wakati wake wa kuteseka tena ulikuwa umefika baada ya kupumzika kwa kipindi! Alitamani kaka yake Nicholaus angekuwepo lakini asingeweza kumpata tena!

Lawama nyingi alizitupa kwa Shabir kwani kitendo alichomfanyia kilikuwa cha kinyama na hakikustahili kufanywa na mtu mzima kama yeye, wakati Victoria akilia Shabir alifurahia kitendo hicho hakumhofia Leah hata kidogo, muda wote alimfariji Victoria na kumwambia hakuhitaji kuwa na wasiwasi wowote, maneno hayo hayakuutuliza moyo wa Victoria na machozi yake hayakukatika!

“Sina uhakika kama kweli Leah atanielewa!” Aliwaza Victoria kichwani mwake.


Baadaye fikra za kutoa mimba zilimwijia kichwani na kumwambia Shabir aliyeupinga mpango huo kwa nguvu zake zote akidai yeye alitaka watoto na Leah alizaa mtoto mmoja peke yake ambaye hakutosheleza ukilinganisha na utajiri aliokuwa nao.

“Lakini kumbuka Leah ni ndugu yangu baba!”

“Usiniite baba tena!”

“Nipo tayari kuitoa hii mimba!”

“Hilo haliwezekani wewe kaa hapa, mama Manjit akirudi atachagua kukaa au kuondoka, najua hawezi kuondoka arudi Tanzania? Amechanganyikiwa?Nyie wote mtakuwa wake zangu na mimi nitakutunza vizuri sana Victoria usiwe na shaka!”

“Sitaki! Wewe ni baba yangu tu!”

“Baba yako? Wakati tayari una mimba yangu?” Alisema Shabir kwa dharau.

Maisha yaliendelea na mimba ilizidi kukua na kukomaa, hatimaye ikafikisha miezi mitatu! Kila siku asubuhi Victoria alitapika na kuugua! Alipoteza uzito mkubwa sana wa mwili wake kwa sababu ya kutokula na mawazo mengi aliyokuwa nayo kichwani mwake, hofu ilimtawala maishani.

Waliendelea kuishi wawili tu nyumbani, bibi Sundra baada ya likizo yake kwisha alirudi lakini alifukuzwa kazi bila sababu yoyote! Victoria alitamani bibi Sundra awepo lakini haikuwa hivyo.

Bibi Sundra alikwenda mara mbili kuomba arudi kazini lakini mzee Shabir alimkatalia lakini mimba ya Victoria ilipoanza kuonekana wazi aligundua ni kwanini hakutakiwa kuishi pale, alikoma kabisa kwenda nyumbani kwa Shabir! Alimhurumia sana Victoria lakini hakuwa na la kufanya kumsaidia.

“Nitaitoa mimba hii! Kweli nitaitoa!” Hayo ndiyo yalikuwa mawazo yaliyotawala kichwa cha Victoria ingawa hakujua jambo hilo angeweza kulifanya vipi.

“Ningekuwa na macho ingekuwa rahisi zaidi lakini upofu umenitesa!” Aliendelea na mawazo hayo hadi mimba ikafikisha miezi minne bila hata kupata njia yoyote ya kukamilisha jambo hilo! Kwa taarifa aliyopewa na Shabir zilikuwa zimebaki wiki mbili tu Leah arejee kutoka Bombay na Victoria hakutaka Leah aikute mimba hiyo.

“Lakini si ninaweza kufanya mwenyewe?” Aliwaza Victoria siku moja katikati ya usiku na kuanza kukumbuka somo la Biolojia juu ya uzazi alilofundishwa na mwalimu wake shuleni! Victoria alipenda biolojia kuliko masomo mengine yoyote shuleni.

“When a woman is pregnant, a sac called Amniotic sac is formed and inside the sac the feotus lies! A fluid called Amniotic fluid is found inside that sac, that fluid enables the feotus to swim! If an accident happens and the sac is punctured all the fluid will drain out and the baby will die!(ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke awapo mjamzito kuna kifuko kiitwacho Amniotic sac ambamo mtoto huogelea kwenye maji yaitwayo Amniotic fluid kama ikitokea ajali na kifuko hicho kikatoboka maji yote hutiririka na mtoto hufa!) Victoria aliyakumbuka maneno ya mwalimu wake wa biolojia darasani na yalimpa matumaini ya kuitoa mimba peke yake ndani ya chumba!

“Kumbe nikitoboa tu kifuko hicho na maji yakmwangika mtoto atakufa na mimba itaharibika!”Aliendelea na mawazo yake Victoria.

Alijua alikuwa akipanga mauaji tena ya mtoto wake lakini hakusikia uchungu wowote ndani ya nafsi kwani ilikuwa ni bora kupoteza kitu chochote duniani lakini si uhusiano wake na Leah! Aliamini bila yeye asingeishi duniani.

“Nitatumia mrija wa kunywea soda na nitausukuma hadi ndani mpaka nikitoboe kifuko na maji yamwagike!”Alizidi kupanga Victoria, alikuwa amedhamiria kuitoa mimba yake.

Kulipokucha asubuhi alimuomba Shabir aliyelala naye kitanda kimoja ampe soda ya baridi na bila kusita Shabir alikwenda kwenye jokofu akachukua soda na kumletea Victoria kitandani.

“Ahsante sana baba, nipe na mrija tafadhali!”Shabir alichukua mrija na kumkabidhi Victoria, alishangazwa na tabia ya Victoria asubuhi hiyo, alitoa ushirikiano wa kutosha kuliko siku nyingine zote.

“Leo kazini huendi baba?” Aliuliza Victoria sababu alitaka aondoke ili akamilishe lengo lake la kuitoa mimba kwa mrija wa kunywea soda!

“Nitaondoka sasa hivi acha nijiandae!”Alisema Shabir na kuingia bafuni, alipotoka alivaa na kuaga, Victoria akabaki peke yake ndani!

“Huu ndio wakati muafaka ni lazima niitoe hii mimba, siwezi kukubali Leah anikute nayo!”Baada ya kuwaza hayo tu Victoria aliweka soda yake chini akanyanyuka na kuvua nguo zote alizovaa ikiwemo nguo ya ndani kisha akachuchumaa sakafuni.

“Ee Mungu nisamehe nimelazimika kufanya kitendo hiki bila kupenda!” Alisema Victoria kwa sauti ya chini huku akilia, hakukipendea alichokuwa akikifanya hakutaka kuua!

Aliuchukua mrija na kuanza kuusukuma kuungiza ndani ya mwili wake, yalikuwa ni maumivu makali kuliko mengine yoyote aliyowahi kuyapata maishani, ingawa aliumia sana bado alizidi kuuchoma mrija ndani zaidi mpaka maji mengi yakamwangika kama bomba na kuilowanisha sakafu, kwa sababu alikuwa kipofu hakujua maji yale yalikuwa ni damu au maji ya kawaida.

Ghafla alisikia kizunguzungu na kuangukia chini, hakuelewa kitu chochote baada ya hapo hakuwa na fahamu hata kidogo.

Vumbi zito lilikuwa likitimka ilikuwa ni hali ya hatari, Nicholaus alijua kifo kimemfikia baada ya kukichenga kwa muda mrefu, lakini ghafla akili yake ilifanya kazi kama kompyuta akageuka kwa kasi ya umeme na kulala chali katikati ya reli, aliyashuhudia matairi ya treni yakipita kila upande wa mwili wake na treni likipita juu yake injini yake ikimuunguza vibaya mwilini mwake.

Yalikuwa ni maumivu makali sana yaliyompata, kwa sababu ya vumbi na joto la injini alifumba macho na muda mfupi baadae alipoteza fahamu na hakuelewa kilichoendelea.

Mbele kidogo treni lilisimama ghafla na abiria wote waliokuwemo ndani yake walishuka na kuanza kumwangalia mtu aliyemgonga, walirudi hadi nyuma wakiangalia chini ya reli hatimaye wakamkuta Nicholaus chini ya behewa moja akiwa ameungua vibaya.

Walimbeba na kumpeleka hadi mbele kwenye behewa la tajiri Mohamed akiwa hajitambui, Mohamed alimuonea huruma sana na alishindwa kuelewa ni kwa nini kijana mdogo kama yeye alikuwa katika pori lenye wanyama wakali kiasi kile.

Alijaribu kumwita ili kujua kama alikuwa hai lakini Nicholaus hakuitika sehemu kubwa ya mbele ya mwili wake ilikuwa imeungua vibaya mno hiyo ikiwa ni pamoja na uso.

“Mwambieni dereva aiondoe treni haraka tujaribu kuokoa maisha ya huyu kijana kwani tumebakiza kilometa ngapi kuingia Baghdad?”

“Mia mbili na hamsini”

“Haya tuondokeni na mwiteni daktari aanze kumshughulikia!” aliamuru tajiri Mohamed na baadae treni ilianza kuondoka kwa kasi kuliko mwanzo lengo likiwa ni kumuwahisha Nicholaus mjini Baghdad ambako angepatiwa matibabu, tajiri Mohamed alishangaa ni kwanini moyo wake uliingiwa huruma kubwa kiasi hicho juu ya Nicholaus, alitaka kufanya chochote kilichowezekana ili kuokoa maisha yake.

Waliingia Baghdad dakika arobaini na tano baadae na kilichofanyika ni kumkimbiza haraka iwezekanavyo kwenda hospitali ya jamii ya Kiislam iliyoitwa Al-Quaba, ilikuwa ni hospitali maarufu sana katika mji wa Baghdad ndio iliyotumika kuwatibu majeruhi wa vita vya Ghuba wakati Marekani ilipoishambulia Iraq.

“Amepatwa na nini huyu?”

“Ajali ya treni!”

“Ajali ya treni?”

“Mbona yuko hivi?”

“Ulitegemea aweje binti?” Mzee Mohamed aliuliza.

“Tumezoea kuwaona majeruhi wa ajali za treni wakiwa nyang’anyang’a!”

“Ilikuwa bahati kabla hatujamgonga alilala kifudifudi katikati ya reli hivyo treni likapita juu yake!”

“Sasa kwanini ameungua kiasi hiki?”

“Nafikiri joto la injini lililomuunguza lakini treni haikumgonga!”

“Kuna watu wengine pia walioumia?”

“Majeraha madogo madogo tu hawa wametibiana wenyewe tatizo ni huyu mtoto naomba mumsaidie na kama kuna uwezekano atibiwe katika daraja la kwanza mimi nitalipa!” alisema mzee Mohamed akionyesha huzuni kubwa.

“Anaitwa nani?”

“Anaitwa Abdallah Hussein!” Mzee Mohamed alilazimika kudanganya jina la mgonjwa ili kuepusha hali ya kutonekana hakuwa na uhusiano wowote na Nicholaus.

Kauli hiyo mzee Mohamed iliongeza kasi ya matibabu, haikuchukua hata sekunde tano daktari akawa ameshafika na kumuandikia Nicholaus dripu za maji ili kuyarudisha maji yaliyopotea kutokana na moto pia alimuandikia dawa za maumivu ili kumpunguzia mateso.

Mgongo na makalio yote ya Nicholaus yalikuwa yameungua vibaya kiasi cha kushindwa kuelewa ni kwa namna gani dawa ingeweza kuwekwa katika vidonda vyake, alichofanya daktari ni kuagiza Nicholaus alazwe kifudifudi na dawa imwagwe moja kwa moja kwenye vidonda.

“Put a bed cradle to prevent body and sheets contact!” (Wekeni kifaa cha kuzuia mwili na mashuka yasinatane!)

Hivyo ndivyo wauguzi walivyofanya, matibabu yalikuwa ya hali ya juu! Kilifanyika kila kitu kuhakikisha Nicholaus anapona tena kwa gharama ya mzee Mohamed mwenyewe, alihamishwa katika wodi ya kawaida na kupelekwa katika wodi ya daraja la kwanza ambako matibabu yaliendelea.


Nicholaus alizinduka baada ya siku mbili na kujikuta yu katika maumivu makali kupita kiasi,kwanza alifikiri yuko Tanzania lakini alipoangaza macho yake huku na kule chumbani alishangazwa na watu aliowaona, badala ya kuona watu weusi aliona Waarabu wakikizunguka kitanda chake.

Alishtuka sana na kushindwa kuelewa ni wapi alikokuwa! Lakini ghafla kumbukumbu zilimjia kichwani mwake na kuliona treni likija kumgonga. Aliruka kitandani na kusimama wima, dripu zote zilichomoka na hata bendeji zilidondoka! Chuma kilichokuwa juu yake kuzuia mashuka yasigusane na mwili wake kiliruka na kuanguka pembeni.

Manesi walikimbia haraka kuelekea kitandani kwakena kumshika, walimrudisha kitandani haraka na kumuomba atulie lakini hakufanya hivyo, aliendelea kupiga kelele akiomba msaada! Daktari alipoitwa alielewa kilichotokea na kuamua kumpa Nicholaus dawa ya usingizi ili apumzike.

“Ni kumbukumbu ndizo zimemsumbua hakuna kitu kingine!”

“Kweli daktari?”

“Ndiyo! Hii hutokea mara nyingi sana hasa kwa watu waliopatwa na ajali”

Alipozinduka baadae Nicholaus alikuwa ametulia kabisa na alielewa kila kitu kilichotokea, pia kumbukumbu za Tehran zilimiminika kichwani mwake, alikumbuka alipofungwa kamba na kusubiri kupigwa risasi sababu ya kuingiza madawa ya kulevya nchini humo, lakini akaokolewa na tetemeko la ardhi!

Alimkumbuka pia Neema, msichana aliyejitolea kumuokoa lakini wote wawili wakagandamizwa na udongo, Neema akafa lakini Nicholaus akaokoka.

Mwisho kabisa alipomkumbuka dada yake Victoria roho ilimuuma zaidi na kujikuta akilia machozi yaliyomtonesha vidonda vyake! Alishindwa kuelewa kama mpaka wakati huo alikuwa bado yuko hai ingawa ndani ya nafsi yake alilazimika kuamini hivyo.

Kumbukumbu ya kipande cha noti walichogawana na dada yake ilipomwijia alijikuta akipiga kelele tena na kuomba apewe suruali yake, mwanzoni alipoongea kiswahili manesi hawakumuelewa akaamua kubadilisha lugha na kuongea Kiingereza, hapo ndipo wote walimuewa na kumsogezea suruali yake karibu ingawa hakuelewa aliihitaji ya kazi gani.

Alinyoosha mkono wake wa kuume na kuudumbukiza ndani ya mfuko wa kulia wa suruali yake akijaribu kukitafuta kipande cha noti alichokiweka! Furaha aliyoipata ilikuwa ya ajabu pale mkono wake ulipokigusa kipande hicho ndani, hakutaka kukitoa nje bali aliikunja suruali yake na kuiweka chini ya godoro la kitanda chake.

Ghafla mlango ulifunguliwa akaingia mzee wa kiarabu mfupi na mwenye ndevu nyingi, alifanana kabisa na watu wa Iran wenye majina ya Khomein! Alikuwa na kilemba kichwani, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Nicholaus kumuona mzee huyo! Alishindwa kuelewa ni nani lakini alionekana mwenye furaha nyingi na alikumbatiana na wauguzi na madaktari waliokuwepo chumbani.

Nicholaus alishindwa kuelewa ni kwanini na baada ya salamu na madaktari mzee huyo alimsogelea Nicholaus kitandani na kumshika kichwani.

“How are you my son?” (Vipi hali yako mwanangu?)

“ I thank God am a little bit fine now!” (Namshukuru Mungu hali yangu ni nzuri kidogo)

“Do you know me?” (Unanitambua mimi?)

“No, thank you” (Hapana)

“I’m Mohamed Mashreef” (Ninaitwa Mohamed Mashreef)

“ Nice to meet you but what is your concern in me?” (Ninafurahi kukutana na wewe lakini nini haja yako kwangu?)

Mzee Mohamed alimueleza Nicholaus kila kitu kilichotokea na ni kwanini aliamua kumsaidia, haikuwa rahisi kwa Nicholaus kuamini kulikuwa na binadamu mwenye roho nzuri kama mzee huyo, alimpa shukrani zisizo na idadi na alimuomba aendelee kumpa msaada.

Habari za kunusurika kifo kwa Nicholaus katika ajali mbaya ya treni ziliandikwa na kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari katika nchi za Ghuba, ni gazeti la Baghdad Times lililoingia nchini Iran na kusomwa na viongozi wa kikosi cha kudhibiti madawa ya kulevya nchini humo. Wengi walimfananisha kijana aliyepata ajali hiyo na Nicholaus lakini kwa alivyoungua usoni na jina lake kuwa tofauti walishindwa kuwa na uhakika ikabidi maaskari watano watumwe kwenda nchini humo kufanya uchunguzi.


Fahamu zilimreja baada kama ya dakika kumi na tano na kukuta Maji na damu nyingi yakiendelea kumtoka ukeni, alikuwa katika maumivu makali mno lakini hakuwa na la kufanya kwa sababu alishaamua kumuua mtoto wake ili kujiepusha na ugomvi kati yake na mlezi wake Leah kwani maisha bila yeye yasingekuwa maisha tena!

Hasira aliyokuwa nayo juu ya Shabir ilimfanya anyanyuke na kuutoa mrija uliokuwa ndani yake, alitaka kuuingiza tena lakini alishindwa sababu ya maumivu! Kwa shida kubwa alinyanyuka na kuanza kujikongoja kuelekea chumbani ambako alijifunika na blanketi lake kuanzia kichwani hadi miguuni! Aliendelea kulia chini ya blanketi hilo na hakunyanyuka tena mpaka saa tatu usiku alipozinduliwa na Shabir.

“Victoria! Nini kimetokea humu ndani mbona zulia limechafuliwa na damu?” Aliuliza Shabir lakini Victoria hakujibu kitu ikabidi aulize tena mara ya pili.

“Nilikuwa nakunywa juisi ya Zabibu bahati mbaya ikamwagika, nisamehe baba!”

“Nilishakuambia usiniite baba bali kila siku niite Darling wewe hivi sasa ni mama wa mtoto wangu au siyo?”

“Hapana, hiyo haiwezekani!”

“Utafanyaje sasa wakati tayari mimba unayo? Na siku nikisikia umeitoa nitakuua!”

“Siwezi kuitoa ila namuogopa sana Leah!”

“Kwani atafanya nini? Kama hataki si arudi Tanzania?” Alisema Shabir kwa dharau wala hakuelewa kilichotokea.


Kwa siku tatu mfululizo Victoria aliishi bila maumivu yoyote zaidi ya maumivu aliyoyapata wakati wa kujitoboa mfuko kwa mrija wa kunywea soda na hakuna kitu kilichotoka zaidi ya maji yaliyomwagika! Kwa kutokuelewa kwake aliamini maji yaliyotoka ndiyo iliyokuwa mimba iliyokuwa ndani ya mfuko wake lakini siku ya nne asubuhi Shabir akiwa kazini Victoria alipatwa na maumivu makali ya ajabu ya tumbo.

Tumbo lilimnyonga kupita kiasi na aligalagala kitandani kwa maumivu, hayakuwa maumivu ya kawaida! Yalinyonga tumbo la chini mpaka kiuno chake, alipapasa kabatini na kutoa vidonge viwili vya maginiziamu akatafuna lakini bado havikumsaidia, aliendelea kuteseka namna hiyo mpaka saa nane za mchana alipojisikia kwenda kujisaidia haja kubwa.

Hakujua kama maumivu yaliyokuwa yakimsumbua ni uchungu, alipapasa ukuta hadi kwenda mpaka chooni ambako alichuchumaa kwa lengo la kujisaidia, badala ya kutoka kinyesi alishtukia kitu kikidondoka kutoka ukeni! Baada ya kitu hicho kutoka maumivu yalitulia ghafla.

Alirudi chumbani ambako aliendelea kulala, aliamini mimba yake sasa ilikuwa imetoka! Hakunyanyuka kitandani wala kula chochote mpaka alipousikia mlango wa chumba ukifunguliwa, alikuwa ni Shabir na badala ya kwenda kitandani Victoria alisikia hatua zake akikimbia kuelekea chooni, ilionyesha alikuwa amebanwa sana na haja ndogo.

Dakika kama moja baadae alishtukia akinyanyuliwa kitandani na kuanza kupigwa kwa ngumi na mateke hadi akatupwa chini! Victori alilia kwa uchungu akiuliza ni kwanini alikuwa akipigwa.

“Yaani weee kenge umemuua mtoto wangu na wewe ni lazima ufe!”

ITAENDELEA

Dimbwi la Damu Sehemu ya Nne

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment