My Repentance (Kutubu Kwangu) Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA: AZIZ HASHIM
*********************************************************************************
Simulizi: My Repentance (Kutubu Kwangu)
Sehemu ya Tatu (3)
Njiani nilimuuliza mume wangu kule chooni walikoenda walifuata nini? Akanijibu kwamba mmsai huyo alienda kumchanjia dawa fulani, roho yangu ikaridhika kwa sababu sasa nilikuwa na uhakika kwamba tatizo la mume wangu litafikia mwisho.
Ibra alinirudisha mpaka nyumbani, tukakaa kidogo kisha yeye akaniaga na kuondoka kurudi kazini kwani aliomba ruhusa ya muda mfupi tu. Nilimsindikiza mpaka nje, tukapigana mabusu kama kawaida yetu kisha akaingia ndani ya gari lake na safari ya kurudi kazini kwake ikaanza.
Nami nilirudi ndani kuendelea na shughuli zangu za hapa na pale. Kwa kuwa nilikuwa mwenyewe nyumba nzima, niljiachia mtoto wa kike, nikawa nimejifunga khanga moja nyepesi ambayo ililionesha vizuri umbo langu.
Nilifanya kazi za hapa na pale mpaka nilipomaliza, nikaenda kujilaza kwenye sofa na kuwasha runinga kubwa ya ukutani (flat screen), nikaanza kuangalia vipindi mbalimbali huku nikisubiri muda wa mume wangu kurudi.
Ilipofika majira ya kama saa tisa jioni, nilisikia mlango ukigongwa, nikahisi mume wangu amerudi lakini kwa upande mwingine nikawa najiuliza kwa nini amewahi hivyo wakati siyo kawaida yake? Niliinuka na kutembea kimadaha mpaka mlangoni, kabla sijafungua mlango nilijitazama jinsi nilivyokuwa nimevaa, nikajua lazima mume wangu atadata kwani huwa ananisifia sana nikiwa nimevaa khanga.
Cha ajabu, nilipofungua mlango nilikutana na rafiki yake, Evans ambaye alionesha mshtuko kutokana na jinsi alivyonikuta nimevaa, na mimi nilijisikia aibu za kikekike kwani halikuwa jambo zuri kumkaribisha mgeni wa kiume nikiwa nimevaa khanga moja tu.
Nilitaka kurudi ndani ili nikachukue nguo nyingine haraka lakini nilikuwa nimechelewa kwani Evans hakusubiri kukaribishwa ndani, aliingia mwenyewe na kwenda kukaa moja kwa moja, akawa anaendelea kunitazama huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
Tulisalimiana kisha nikatembea harakaharaka kuelekea chumbani kuchukua nguo nyingine. Kabla sijazamia kwenye korido ya kuelekea chumbani, niligeuka, nikashangaa kumuona Evans ametulia kimya huku akiwa ananikodolea macho akiwa ni kama haamini alichokuwa anakiona. Nikazidi kujisikia aibu mtoto wa kike. Nilienda kuchukua vitenge viwili, kimoja nikajifunga juu ya ile khanga na kingine nikajitanda upande wa juu, nikarudi kumsikiliza mgeni.
“Njoo ukae karibu na mimi shemeji, mbona unakaa mbali?” Evans aliniambia, nikashindwa kukataa, nikamsogelea pale kwenye sofa la watu wawili alipokuwa amekaa, tukakaa pamoja. Akawa ananipigisha stori nyingi ambazo hata hazikuwa na msingi huku mara kwa mara akipenda kugongesheana mikono na mimi.
“Mbona umewahi kutoka kazini? Mume wangu yuko wapi?” nilimuuliza Evans, akavungavunga na kuniambia kwamba alikuwa na dharura ndiyo maana aliwahi kurudi. Tuliendelea kuzungumza stori za hapa na pale nikitegemea Evans ataniambia kilichomleta pale nyumbani lakini hakufanya hivyo.
Nilishindwa kumuuliza kwa sababu mara kwa mara alikuwa akipitia pale nyumbani akiwa na mume wangu kiasi cha kuonekana kama mwenyeji. Ghafla alibadilisha mazungumzo na kuanza kunisifia kuwa mimi ni mzuri sana, nikawa natabasamu kwani mwenzenu siyo siri huwa napenda sana kusifiwa.
Aliendelea kunimwagia sifa kibao, mara akaanza kumponda mpaka mume wangu, akasema hastahili kuwa na mke mzuri kama mimi! Akadai kwamba eti mimi nilikuwa nafanana naye na kama angekutana na mimi kabla ya mume wangu, angetangaza ndoa.
Niliishia kuchekacheka tu, mara akaanza kunitongoza! Jamani wanaume hawa, yaani mtu anajua kabisa kwamba mimi ni mke wa rafiki yake lakini ananitongoza akiwa hana hata hofu, macho makavu kabisa.
Ninachotaka kuwaambia hapa wanaume, epukeni sana kuwajengea wake zenu mazoea ya kupitiliza na marafiki zenu kwani siku zote kikulacho ki nguoni mwako. Wanaume wengi siku hizi wanalalamika kwamba marafiki zao wamewachukulia wake zao bila kujua kwamba wenyewe ndiyo waliotengeneza mazingira.
Jamani wanaume msiwazoeshe marafiki zenu kuwa wanaenda nyumbani kwa wake zenu hasa kama wenyewe hampo kwani ni rahisi sana kuwachukulia wake zenu. Mi naongea haya kwa sababu nimejionea mwenyewe na sitaki mwingine akumbwe na masaibu kama yaliyonikuta mimi.
Basi shemeji Evans aliendelea kutupia mistari ya kila aina lakini kwa kuwa nilikuwa nimefundwa vizuri, nilisimamia msimamo wangu kama mke wa mtu ninayejiheshimu. Alipoendelea kuniletea upumbavu wake, nilimwambia kwamba akiendelea nitamwambia mume wangu, nikamtaka aondoke haraka kama hicho ndicho kilichomleta.
Kwa bahati nzuri alinielewa, akaaga na kuondoka huku akisisitiza niendelee kumfikiria. Alipotoka, nilifunga mlango na kwenda chumbani, nikajitupa na kuendelea kujiuliza kwa nini Evans amefikia hatua hiyo. Niliona kama amenivunjia sana heshima kwani ni bora ningetongozwa na mtu mwingine lakini siyo rafiki kipenzi wa mume wangu.
Hata hivyo nilijiapiza kuwa kamwe sitamwambia mume wangu kwa kuhofia kuwachonganisha. Kweli baadaye mume wangu alirudi na kunikuta sina raha, nikamdanganya kwamba nilikuwa najisikia vibaya. Siku hiyo ilipita bila mume wangu kujua chochote, akawa anaendelea kutumia zile dawa alizopewa na yule mmasai.
Siku kadhaa baadaye, nilianza kuona mabadiliko kwa mume wangu kuonesha kwamba zile dawa zilikuwa zimemsaidia. Hata hivyo, mabadiliko hayo yalikuwa madogo na wala hayakukidhi kile nilichokuwa nakitaka, ikawa kila nikikutana na mume wangu, naishia kukasirika kwani hakuwa akinifurahisha kama nilivyokuwa nataka.
Taratibu nikaanza kumkatia tamaa kwani kama ni kumsaidia, nilijitahidi kwa kila namna lakini haikusaidia chochote. Nikaanza kupoteza hamu ya kula ‘chakula cha usiku’ na mume wangu, huku mara kwa mara nikitoa visingizio vya hapa na pale kwani niliona kama ananichosha tu pasipokuwa na sababu.
Yule rafiki yake naye aliendelea kunisumbua mara kwa mara, akafikia hatua ya kuwa ananiletea vizawadi kwa kujiiba wakati m ntyume wangu akiwa kazini lakini bado nilishikilia msimamo wangu.
Ninachotaka kuwaambia hapa wanaume, epukeni sana kuwajengea wake zenu mazoea ya kupitiliza na marafiki zenu kwani siku zote kikulacho ki nguoni mwako. Wanaume wengi siku hizi wanalalamika kwamba marafiki zao wamewachukulia wake zao bila kujua kwamba wenyewe ndiyo waliotengeneza mazingira.
Jamani wanaume msiwazoeshe marafiki zenu kuwa wanaenda nyumbani kwa wake zenu hasa kama wenyewe hampo kwani ni rahisi sana kuwachukulia wake zenu. Mi naongea haya kwa sababu nimejionea mwenyewe na sitaki mwingine akumbwe na masaibu kama yaliyonikuta mimi.
Basi shemeji Evans aliendelea kutupia mistari ya kila aina lakini kwa kuwa nilikuwa nimefundwa vizuri, nilisimamia msimamo wangu kama mke wa mtu ninayejiheshimu. Alipoendelea kuniletea upumbavu wake, nilimwambia kwamba akiendelea nitamwambia mume wangu, nikamtaka aondoke haraka kama hicho ndicho kilichomleta.
Kwa bahati nzuri alinielewa, akaaga na kuondoka huku akisisitiza niendelee kumfikiria. Alipotoka, nilifunga mlango na kwenda chumbani, nikajitupa na kuendelea kujiuliza kwa nini Evans amefikia hatua hiyo. Niliona kama amenivunjia sana heshima kwani ni bora ningetongozwa na mtu mwingine lakini siyo rafiki kipenzi wa mume wangu.
Hata hivyo nilijiapiza kuwa kamwe sitamwambia mume wangu kwa kuhofia kuwachonganisha. Kweli baadaye mume wangu alirudi na kunikuta sina raha, nikamdanganya kwamba nilikuwa najisikia vibaya. Siku hiyo ilipita bila mume wangu kujua chochote, akawa anaendelea kutumia zile dawa alizopewa na yule mmasai.
Siku kadhaa baadaye, nilianza kuona mabadiliko kwa mume wangu kuonesha kwamba zile dawa zilikuwa zimemsaidia. Hata hivyo, mabadiliko hayo yalikuwa madogo na wala hayakukidhi kile nilichokuwa nakitaka, ikawa kila nikikutana na mume wangu, naishia kukasirika kwani hakuwa akinifurahisha kama nilivyokuwa nataka.
Taratibu nikaanza kumkatia tamaa kwani kama ni kumsaidia, nilijitahidi kwa kila namna lakini haikusaidia chochote. Nikaanza kupoteza hamu ya kula ‘chakula cha usiku’ na mume wangu, huku mara kwa mara nikitoa visingizio vya hapa na pale kwani niliona kama ananichosha tu pasipokuwa na sababu.
Yule rafiki yake naye aliendelea kunisumbua mara kwa mara, akafikia hatua ya kuwa ananiletea vizawadi kwa kujiiba wakati mume wangu akiwa kazini lakini bado nilishikilia msimamo wangu.
Maisha yalizidi kusonga mbele na kadiri muda ulivyokuwa unasonga, ndivyo hamu ya kula ‘chakula cha usiku’ na mume wangu ilizidi kupungua, ikafikia kipindi nikawa wakati mwingine nakataa kabisa kwani nilikuwa najua kuwa mwisho nitapata mateso tu, Ibra hakuwa na uwezo wa kukidhi haja zangu.
Tabia hiyo ilionekana kumsumbua sana mume wangu kisaikolojia, ule uwezo wake wa kujiamini ukaanza kupungua taratibu, licha ya kujitahidi kuchangamka tunapokuwa katika mazungumzo ya kawaida, ndani ya nafsi yake alionesha kuwa na huzuni kubwa kutokana na jinsi nilivyokuwa namfanyia.
Unajua watu wengi hawajui kuhusu siri iliyojificha kwenye tendo la ndoa. Ukiona wanaume wanalalamika kwamba wake zao hawataki kuwapa haki yao ya msingi, wengi huwa ni kwa sababu wanawaacha wenzi wao njiani.
Tabia hiyo ikiendelea, wanawake wengi huwa tuna kawaida ya kupoteza kabisa hamu ya tendo. Endapo mumeo atakuwa anakulazimisha, uwezekano mkubwa ni kwamba utaanza kumchukia hata yeye. Lakini kinyume chake, kama mwanamke anapewa ‘chakula cha usiku’ vizuri hadi anatosheka, hawezi kupoteza hamu hata siku moja.
Basi taratibu mume wangu akaanza kutafuta njia ambayo itampunguzia huzuni aliyokuwa nayo ndani ya nafsi yake kutokana na kitendo changu cha kuwa nakataa kumtimizia kile alichokuwa anakitaka. Ibra wangu alianza kunywa pombe, jambo ambalo hakuwahi kuwa analifanya hata mara moja.
Siku ya kwanza kumuona amelewa nilishtuka mno na kuhisi labda alikuwa anaumwa. Alikuwa ametoka kazini lakini badala ya kurudi nyumbani kama kawaida, alichukuana na rafiki yake, Evans mpaka wanakokujua wenyewe, akanywa pombe nyingi, ukizingatia ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza, alilewa sana.
Akarudishwa nyumbani na Evans ambaye alinidanganya kwamba eti kazini kwao kulikuwa na sherehe ya wafanyakazi na ndiko walikokunywa pombe. Nilikasirishwa sana na kitendo hicho, nikamuingiza mume wangu ndani na kwenda kumuogesha kisha nikamuacha apumzike.
Kesho yake asubuhi alishindwa hata kwenda kazini, nikamsema sana kwamba sijafurahishwa kabisa na tabia yake. Akakiri makosa na kuahidi kuwa hatarudia tena lakini kumbe ilikuwa ni kazi bure. Siku mbili baadaye alilewa tena, akaletwa na rafiki yake huyohuyo ambaye niliamini ndiye aliyekuwa akimfundisha mume wangu ulevi.
Mazoea hujenga tabia, kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndiyo tatizo la mume wangu kulewa lilivyokuwa linazidi kuongezeka, ikawa kila siku lazime anywe pombe na kulewa. Kibaya zaidi, alikuwa na kichwa kibovu sana kiasi kwamba akilewa, anaweza kulala tangu jioni hadi asubuhi bila kuamka hata mara moja.
Maskini mume wangu, hata ule usumbufu aliokuwa akinipa wa kutaka tendo la ndoa japo alikuwa akishindwa kukidhi haja zangu, safari hii uliisha kabisa baada ya kuwa ameanza kunywa pombe. Ikawa kila siku pombe, pombe na yeye!
Rafiki yake Evans ndiye aliyekuwa akimleta kila siku kwani baada ya kulewa, hata kuendesha gari alikuwa hawezi, mwenzake akawa anamleta akiwa hajitambui. Nilijaribu kuzungumza na mume wangu mara nyingi kadiri niwezavyo lakini ilikuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
Nilipoona mambo yamekuwa magumu, ilibidi niwafikishie wazazi wake taarifa, wakamuita na kumuonya lakini bado hakuelewa chochote. Ilikuwa akipumzika kulewa basi ni siku moja, siku inayofuatia lazima akanywe. Kwa kweli niliumizwa sana na mabadiliko ya mume wangu lakini sikuwa na cha kufanya.
Nilipoona juhudi zangu zimegonga mwamba kwani alishindwa hata kuwasikiliza wazazi wake, ilibidi nikae kimya kusubiri kuona mwisho wa yote hayo ungekuwa nini. Kasi ya ulevi iliendelea kila kukicha huku mwenzenu nikipata shida kubwa sana kuizoea harufu ya pombe.
“Ukitaka asiwe anakukera na harufu ya pombe, na wewe uwe unakunywa japo kidogo, utalala kwa raha mustarehe,” Evans, yule rafiki wa mume wangu alianza kunirubuni na mimi. Kwa kuwa nilikuwa nikitapatapa kama mfa maji, nilijikuta nikikosa msimamo.
Siku moja alipomleta mume wangu, alikuja na bia mbili za kopo, Redds. Akaniambia nijaribu kunywa moja nione raha yake. Nilijaribu kukataa kwani nilikuwa najua bia ni chungu sana lakini aliponihakikishia kwamba hizo alizoniletea zilikuwa tamu kama juisi, nilijaribu kuonja.
Kweli hazikuwa na uchungu kama nilivyokuwa nikiamini tangu nikiwa mdogo. Nikapiga mafunda kadhaa, mtoto wa kike nikalegea kama bamia. Evans ambaye bado alikuwa hajaondoka baada ya kumrudisha mume wangu, alikuwa amekaa pembeni akijifanya anaangalia muziki kwenye runinga.
Alipoona nimeanza kulewa, alianza kunisemesha mambo mbalimbali, mtoto wa kike maneno yakawa yananitoka bila kujielewa. Akanisogelea na kukaa pembeni yangu, tukaendelea kupiga stori huku mara kwa mara nikiangua vicheko vya nguvu, jambo ambalo halikuwa kawaida yangu. Akili za pombe mbaya sana.
Mara Evans akaugusa mwili wangu, nikashtuka kama nimepigwa na shoti ya umeme kwani kiukweli, mume wangu hakuwa amenigusa kwa kipindi kirefu mno, ukizingatia na mimi ni mwanamke niliyekamilika nikajikuta kwenye wakati mgumu mno.
Evans aliligundua hilo, akaniomba radhi na kuendelea kunihimiza nimalize bia ya kwanza, nikajitutumua mtoto wa kike nikamaliza, akanifungulia na ile bia nyingine. Nilipopiga mafunda mawili matatu nilianza kuhisi akili ikipoteza mawasiliano na mwili wangu.
Evans akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu, akaanza kuniangushia mabusu motomoto, nikawa najaribu kumtoa lakini hata sijui nini kilitokea, nikajikuta na mimi nikitoa ushirikiano. Tukaangushana kwenye sofa na kuanza kufanyiana michezo ya kimahaba huku pombe zikizidi kukolea kichwani mwangu. Kwa muda wote huo, mume wangu alikuwa amelala chumbani akikoroma kama pono.
Evans aliendelea kunifanyia visa vya kimahaba bila hata woga! Jamani wanaume hawa, sina hamu. Japokuwa nilikuwa nimelewa na nilikuwa na hali mbaya kutokana na kukosa huduma ya mume wangu kwa kipindi kirefu, nilikuwa naogopa mno kwani nilihisi mume wangu anaweza kuzinduka muda wowote na kuja kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.
“Usiwe na wasiwasi, hawezi kuzinduka sasa hivi, we mwenyewe si unamjua,” alisema Evans huku akiendelea kunifanyia vituko ambavyo vilizidi kuniacha hoi mtoto wa watu, ukichanganya na pombe ambazo sasa zilikuwa zimekolea kwenye kichwa changu, nilijikuta nikikosa kabisa msimamo.
Kuja kushtukia, Evans alikuwa amenisaula kila kitu mwilini mwangu, naye akafanya hivyohivyo na muda mfupi baadaye, tukawa tunaelea kwenye ulimwengu wa huba, palepale kwenye sofa huku mume wangu akiendelea kukoroma chumbani.
Japokuwa nilichokuwa nakifanya ilikuwa ni dhambi kubwa mbele za Mungu wangu, nilijikuta nikiifurahia dhambi hiyo. Evans akaendelea kufanya yake kwa zaidi ya dakika kumi kabla ya kutangaza kuiona theluji ya Mlima Kilimanjaro.
Japokuwa naye hakuwa amenifikisha pale nilipokuwa napataka, Evans alikuwa amemzidi mume wangu kwa vitu vingi. Kwa mara ya kwanza tangu naingia kwenye ndoa, nikajikuta nikifurahi japokuwa haikuwa kwa kiwango kikubwa kama mwenyewe nilivyokuwa nataka.
Tulipomaliza tu, harakaharaka kila mmoja alikimbilia viwalo vyake na kuvitinga, nikainuka haraka huku aibu zilizochanganyikana na hofu zikinitawala na kukimbilia bafuni.
Nikampita mume wangu akiwa anaendelea kukoroma na kukimbilia bafuni ambako nilijimwagia maji na kupunguza uchovu wa pombe pamoja na kazi ya Evans kisha nikarudi chumbani na kuvaa vizuri, nikatoka sebuleni ambapo nilimkuta Evans akiwa amejilaza kwenye kochi, akiwa hana hata chembe ya wasiwasi.
Kutokana na jinsi nilivyokuwa najisikia aibu, sikutaka hata kumtazama usoni, nikaeenda kukaa kwenye kochi lingine huku bado pombe zikiendelea kuzunguka kwenye kichwa changu. Evans akahama tena pale alipokuwa amekaa na kuja kukaa pembeni yangu, akanisogezea ile chupa ya pili ya bia yangu ambayo sikuwa nimeimaliza.
Akawa ananihimiza ninywe huku akinimwagia sifa luluki, akakiri wazi kwamba hajawahi kukutana na mwanamke kama mimi maishani mwake. Sijui nini kiliendelea lakini baada ya kumaliza ile bia ya pili, nililewa sana, Evans akaitumia vizuri nafasi hiyo kwa kurudia kufanya alichokuwa anakitaka kisha akatokomea bila kuaga na kuniacha nimelala pale kwenye kochi.
Nilipokuja kushtuka, tayari ilikuwa ni saa mbili za usiku, nikasimama kwa tabu na kujikagua, nikakuta nimetumika kwa mara nyingine huku uchovu mkali uliochanganyikana na pombe ukinitesa kisawasawa. Niliinuka kwa tabu na kukimbilia bafuni ambako nililala kwenye jakuzi kwa muda mrefu mpaka pombe zilipopungua.
Nikaamka na kurudi sebuleni ambako nilipanga vitu vizuri ili kuondoa ushahidi na kurudi chumbani kwangu, ile napanda tu kitandani, nilipitiwa na usingizi mzito mpaka kesho yake asubuhi.
Nilipoamka, pombe zikiwa zimeisha kichwani, nilianza kujiuliza juu ya kilichotokea jana yake, nikajikuta nikitetemeka mno na kuilaumu sana nafsi yangu kwa dhambi kubwa niliyomfanyia mume wangu. Niliamka na kuanza kumuandalia nguo kwa ajili ya kwenda kazini huku nikiendelea kujilaumu.
Baadaye nilimuamsha mume wangu huku nikijitahidi kuificha hofu yangu, nikajitahidi kumuonesha mahaba ya dhati ambayo yalimfanya asishtukie chochote. Nikampeleka kuoga kisha nikamuandalia kifungua kinywa kizuri na baadaye alipokuwa tayari, nikamsindikiza mpaka kwenye gari na kumwagia mvua ya mabusu huku nikimsisitiza kuwa jioni asinywe tena pombe.
Akaondoka akiwa na furaha kisha nikarudi chumbani na kujitupa kitandani, kumbukumbu za kilichotokea jana yake zikawa zinajirudia kichwani mwangu kama mkanda wa video.
Nilichomwambia mume wangu asubuhi hiyo ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa kwani jioni ilipofika, aliletwa tena na Evans, akiwa amelewa kuliko hata jana yake, nikajisikia vibaya sana. Nikaenda kumlaza chumbani kisha nikatoka na kukaa na Evans pale sebuleni huku muda wote shemeji huyo asiye na haya akitabasamu na kunitazama kwa jicho la uchu.
Kama kawaida yake, alinipa tena pombe na kuniambia ninywe tena. Kwa sababu nilikuwa na hasira kali juu ya mume wangu, siku hiyo sikujivunga tena, niligida chupa ya kwanza mpaka ikaisha, Evans akanipa nyingine, nayo ikaichangamkia na ilipofika nusu, tayari akili zangu zilikuwa zimebadilika kabisa.
Sikuwa mimi tena, zile aibu zote ziliisha, kujiheshimu kwangu na heshima niliyokuwa nayo kwa mume wangu, vyote viliyeyuka kama barafu iyeyukavyo juani. Nikamgeukia Evansi ambaye alikuwa ametulia kimya kama fisi anayesubiri mzoga, huku akinitazama kwa macho ya matamanio.
“Mbona leo una kasi sana? Umeanza kuzizoea?” Evans aliniuliza, nikatingisha kichwa kumkubalia huku macho yangu nikiyarembua kama ninayesikia usingizi. Sikusubiri Evans anianze, nilimvutia kwangu kisha tukagusanisha ndimi zetu, nikahisi mwili wangu ukisisimka kama nimepigwa na radi.
Naye alinipokea vizuri, akaanza kunifanyia utundu wa hapa na pale, mashetani yangu yakapanda kiasi cha kuanza kutoa miguno ya hapa na pale bila kumhofia tena mume wangu ambaye alikuwa amelala chumbani, akikoroma kama mashine mbovu.
Evans hakutaka kulaza damu, sijui nini kilitokea lakini muda mfupi baadaye, sote tulikuwa tumevaa suti kama zile tulizotoka nazo kwenye matumbo ya mama zetu, Evans akiwa juu yangu. Tukasaidiana kukiingiza chombo baharini kisha tukawa tunapiga makasia kwa nguvu, safari ikapamba moto.
Tuliendelea kupasua mawimbi huku nikionekana kuwa na papara kuliko kawaida, baada ya dakika kadhaa, Evans alinitangazia kurusha nanga, chombo kikaanza kusogea pwani na hatimaye tukawa tumefika mwisho wa safari yetu ya kwanza.
Licha ya kuwa nilikuwa nikifanya kitendo kibaya sana, wala nafsi yangu haikunisuta hata kidogo, ni kama nilikuwa nimeonjeshwa asali na sasa nilikuwa nimeamua kuchonga mzinga kabisa.
Nilijizoazoa na kuinuka pale kwenye sofa tulipokuwa tukifanya yetu, nikaokota nguo zangu na kukimbilia bafuni huku Evans naye akichukua zake na kujisitiri. Nilimpita mume wangu akiwa amelala, akiendelea kukoroma na kupitiliza mpaka bafuni, nikajimwagia maji na kupunguza uchovu na pombe ambazo zilikuwa zimenikolea kisawasawa.
Nilirudi chumbani na kubadilisha nguo, safari hii sikutaka shida tena, nilijifunga upande mmoja tu wa khanga na kutoka huku nikitembea kwa maringo mpaka pale Evans alipokuwa amekaa, nikajibwaga kisha tukaanza kupiga stori za hapa na pale.
Jamani wanaume waongo hawa! Sijapata kuona. Maneno aliyokuwa ananiambia Evans, yalinishangaza sana, akaniambia kuwa tangu siku ya kwanza aliponiona, kabla hata sijaoana na rafiki yake, alitokea kunipenda sana na kama yeye ndiyo angekuwa wa kwanza kukutana na mimi, angenioa.
Sijui ni kwa sababu ya akili za pombe au kitu gani kwani nilifurahishwa mno na kauli yake japokuwa nilikuwa najua kabisa kwamba ananidanganya. Akaendelea kunipa mistari huku akinihakikishia kwamba hata siku ikitokea rafiki yake akagundua na kuniacha, alikuwa tayari kunioa.
Kwa mara nyingine tukajikuta tukiwa kwenye kina kirefu cha bahari ya huba, tukasafiri huku kila mmoja akionesha kuifurahia safari hiyo mpaka tulipokifikisha chombo pwani. Nikamshukuru sana kwa huduma yake, naye akanimwagia sifa mpaka nikaanza kuona aibu.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, Evans aliniaga na kuondoka, akaniambia kuwa kesho yake atakuja tena kama kawaida. Alipoondoka nilirudi sebuleni na kuanza kupangapanga vitu vizuri, nikamalizia bia yangu kisha nikajikokota mpaka chumbani.
Nilipojitupa kitandani tu, nilipitiwa na usingizi mzito na sikushtuka mpaka kesho yake asubuhi. Tofauti na siku zote, mume wangu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka kabla yangu. Hata niliposhtuka, sikutaka kusumbuliwa kwa chochote, sikutaka kumuandalia mume wangu kifungua kinywa wala kumpigia nguo pasi.
Kwa kuwa mwenyewe alishajua kwamba nimekasirika kwa sababu hakunisikiliza nilipomkataza kunywa pombe, hakuniuliza chochote, akajiandalia kila kitu mwenyewe na alipokuwa tayari, aliniaga.
Hata hivyo, sikutaka kumjibu chochote, nikauvuta mdomo kwelikweli, mume wangu akaondoka kuelekea kazini huku akiniacha naendelea kujigeuzageuza pale kitandani. Mara kwa mara nilikuwa nikimfikiria Evans na mapenzi ya wizi aliyokuwa akinipa, japokuwa hakuwa mzuri kama mume wangu, nilijikuta nikianza kumpenda.
Kwa kuwa jana yake alipoondoka aliniachia namba yake ya simu, nilichukua simu yangu na kumuandikia sms ya mapenzi nikimsifia na kumueleza jinsi nilivyokuwa nampenda. Wakati wa kutuma sms hiyo, sijui akili zangu zilikuwa zikiwaza nini kwani badala ya kumtumia Evans, nilijikuta nikiituma kimakosa kwenye namba ya simu ya mume wangu.
Mapigo ya moyo wangu yalinilipuka na kuanza kwenda kasi utafikiri nimetoka kukimbia mbio za mita mia moja. Japokuwa kulikuwa na kibaridi cha kiyoyozi, nilijikuta nikitokwa na kijasho chembamba, sikujua nitamjibu nini mume wangu.
Sekunde chache baadaye, simu yangu ilianza kuita, nilipotazama namba ya mpigaji, alikuwa ni mume wangu, nikazidi kuchanganyikiwa mtoto wa kike nikiwa sijui cha kufanya. Nilianza kuiona ndoa yangu ikivunjwa kwa mikono yangu mwenyewe.
Sikuwa na ujasiri wa kuipokea simu hiyo, iliita mpaka ilipokata, huku nikitetemeka niliichukua na kuangalia kwenye meseji nilizotuma na kurudia kuisoma ile meseji niliyomtumia mume wangu kimakosa badala ya Evans.
“Nakupenda sana mpenzi wangu, tangu umeingia kwenye maisha yangu umenibadilisha vitu vingi sana, huu ni mwanzo tu lakini naamini utafaidi sana kwangu, mwanaume wa shoka unayejua nini cha kumfanyia mwanamke ili afurahi, nakupenda sana my love,” niliisoma meseji hiyo na kushusha pumzi ndefu.
Kwa bahati nzuri sikuiandika jina la Evans na kwa jinsi ilivyokuwa, isingekuwa rahisi mume wangu kuhisi kwamba nimekosea ingawa sikuwa na mazoea ya kumtumia mume wangu meseji za kimapenzi hasa baada ya ndoa yetu kuanza kuyumba.
Nikiwa bado sijui cha kufanya, simu ya mume wangu ilianza kuita tena, nikapiga moyo konde na kuipokea huku nikizidi kutetemeka.
“Mke wangu!”
“Abee mume wangu.”
“Kumbe unanipenda kiasi hiki? Umefikiria nini mpaka kunitumia meseji nzuri kiasi hiki wakati asubuhi nimeondoka tukiwa hatuelewani?” mume wangu aliniuliza swali ambalo sikulitegemea, akawa amejiingiza mwenyewe kwenye kumi na nane zangu.
“Nakupenda sana mume wangu, sifurahishwi na maisha tunayoishi kwa sasa, natamani urudi kuwa yule ambaye mimi namjua, acha kunywa pombe mume wangu, nakupenda sana,” nilisema huku nikijikamua sauti ionekane kama nilikuwa nalia.
Maskini mume wangu! Kweli aliuamini uongo wangu na akaniahidi kuwa japokuwa alikuwa na kazi, ataacha kila kitu na kuomba udhuru kazini kwao ili arudi nyumbani tuje tuzungumze vizuri.
Alipokata simu, niliinua mikono juu kumshukuru Mungu, harakaharaka nikaifuta namba ya Evans iliyokuwa kwenye simu yangu na kuondoa ushahidi wote ambao ungeweza kumtia wasiwasi mume wangu.
Nikaenda kuoga na kurudi chumbani ambapo nilijipodoa sana, nikajipulizia manukato mazuri kisha nikajilaza kitandani nikimsubiri mume wangu. Hata hivyo, bado nilikuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wangu kwani ni jana yake tu nilikuwa nimetoka kuchepuka na Evans, nikawa nahisi kwamba mume wangu anaweza kugundua.
Baada ya takribani dakika arobaini, nilisikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yetu, nikajiweka tayari kumpokea mume wangu. Kweli alikuwa ni yeye, meseji ile naona ilimgusa sana na kuamua kuacha kazi kuja nyumbani tuyaongee bila kujua kwamba mwenzake nilikuwa nimekosea namba.
Kwa kuwa aliwahi kurudi, hakuwa amelewa kama kawaida yake, alipoingia tu, nikainuka kitandani huku nikiwa nimejifunga mtandio tu ambao ulilionesha vyema umbo langu zuri, nikatoka sebuleni kumpokea ambapo kitu cha kwanza ilikuwa ni kumkumbatia kwa mahaba na kumbusu sehemu mbalimbali za mwili wake.
Sisi wanawake tuna mbinu kali sana tukiamua kumdanganya mwanaume, sikumpa mume wangu hata dakika moja ya kupumua, nilimdaka juujuu na kumpeleka mpaka chumbani, nikambwaga kitandani huku nikionesha kuzidiwa, naye akawa ananipa ushirikiano. Muda mfupi baadaye, tayari tulikuwa kama tulivyoletwa duniani, kazi iliyokuwa imesalia ilikuwa moja tu.
Ibra wangu alijitahidi sana kwenye uwanja wa fundi selemala, akawa anaonesha mbwembwe ambazo sikuzizoea kwake kiasi cha kunishangaza sana. Eti cha ajabu, alinishughulikia kwa nguvu kumzidi hata rafiki yake, Evans.
Nikiri kwamba tangu anioe, sikuwahi kumuona akiwa imara kiasi hicho, nikajikuta nikijilaumu sana ndani ya moyo wangu kwani kumbe kama ningekuwa na subira kidogo, mume wangu angeweza kunitimizia shida zangu vizuri bila hata kumsaliti.
Nilijisikia vibaya sana, mpaka tunahitimisha ngwe ya kwanza, uso wangu ulikuwa umelowa kwa machozi kutokana na jinsi nafsi yangu ilivyokuwa inanisuta. Mume wangu hakujua kilichokuwa kinanisumbua, maskini! Akawa ananifuta machozi na kuniomba msamaha kwa yote aliyokuwa ananifanyia kwa kipindi chote hicho.
Sikuweza kumjibu chochote, tukapumzika kidogo kisha akainuka na kwenda kujimwagia maji. Aliporudi na mimi nilienda kupunguza uchovu. Niliporudi, hata dakika mbili hazikupita, nikamuona mume wangu akijichaji tena na kunihitaji, jambo ambalo pia halikuwa kawaida yake.
Tukaingia msambweni kwa mara nyingine, akaonesha mabavu yake kuliko hata mwanzo, nikazidi kushangaa mwenzenu kwani kila kitu kilikuwa kigeni kwangu. Sijui alitafuna mzizi gani siku hiyo, mpaka ananiachia, nilikuwa hoi bin taaban.
“Nilikuwa nakunywa pombe kwa sababu sikujua kama ipo siku naweza kupata ufumbuzi wa tatizo langu la kukosa nguvu, lakini namshukuru sana Mungu nimepona na kuanzia leo nakuahidi kwamba sitakunywa tena pombe,” mume wangu aliniambia kwa sauti ya upole, huku mkono wake mmoja ukibarizi kwenye mwili wangu.
Kiukweli nilijisikia raha sana siku hiyo kwani huyo ndiye mume niliyekuwa namtaka ingawa bado moyoni sikuwa na amani kabisa kutokana na tukio kubwa na baya nililomfanyia mume wangu.
Kutokana na uchovu wa kazi ya kikubwa, tulipitiwa na usingizi muda mfupi baadaye, tukalala tukiwa tumekumbatiana kimahaba mpaka baadaye tulipozinduliwa na mtu aliyekuwa akigonga mlango.
Niliamka haraka na kukimbilia bafuni, nilipotoka nilivaa nguo kwenda kufungua mlango. Kumbe aliyekuwa anagonga alikuwa ni Evans, ile namfungulia tu mlango, nikiwa bado nimepigwa na butwaa, alinivaa mwilini.
“Waooo mpenzi wangu, mwaaah!” alisema Evans akiwa amenikumbatia kwa nguvu, akanibusu kimahaba, jambo ambalo lilinishtua mno. Nikamtoa mwilini na kumsukuma kwa nguvu, akabaki amepigwa na butwaa kwani hakuwa akijua kwa nini nimemfanyia vile.
Nikamuoneshea ishara kwamba mume wangu alikuwa ndani, nikamtaka aache mambo yake ya mapenzi kwani mume wangu angegundua mara moja na kunihatarishia ndoa yangu. Namshukuru kwamba alinielewa, akaanza kuvungavunga huku akijifanya kumuulizia rafiki yake kwa sauti ya juu.
“Yupo ndani amepumzika,” na mimi nilimjibu kwa sauti kubwa ili mume wangu asikie, nikamkaribisha kiti na kurudi chumbani kumuamsha mume wangu. Nikamwambia rafiki yake amemfuata kumsalimia, akaonesha kushangaa kwani walikuwa wote kazini asubuhi na walionana.
Hata hivyo kwa kuwa walikuwa wamezoeana sana, aliinuka na kutoka, Evans akajifanya kumuulizia kwamba kwa nini hakumuaga wakati anaondoka.
“Mimi nilihisi una matatizo ndiyo maana nikaona ngoja nikupitie nyumbani,” alizidi kujivunga. Maskini mume wangu, hakujua chochote kinachoendelea, wakapiga stori za hapa na pale na baada ya muda, Evans akataka aondoke na mume wangu wakanywe tena pombe lakini alimkatalia.
Ikabidi aondoke kwa shingo upande huku naye akionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake. Alipoondoka, nilijitahidi kuificha hofu iliyokuwa ndani ya moyo wangu. Nikaendelea kukaa vizuri na mume wangu mpaka usiku ambapo tuliingia tena mzigoni, akanipa nilichostahili kisha yeye akalala.
Usiku sikupata kabisa usingizi, nilikuwa nikiendelea kujilaumu kwa kitendo nilichokifanya. Kibaya zaidi, nilikuwa nimekutana na Evans katika siku zangu za hatari, tena bila kuchukua tahadhari yoyote.
Kesho yake niliwahi kuamka kuliko kawaida, nikaanza kumuandalia mume wangu kifungua kinywa cha nguvu, nikamnyooshea nguo zake za kazini na nilipomaliza, nilienda kumuamsha kwa upole. Nikambusu kwenye paji lake la uso kisha nikamuinua na kumpeleka bafuni kuoga.
Nilijaribu kumuonesha mapenzi mazito ili angalau ile hatia iliyokuwa ndani ya moyo wangu ya kumsaliti ipungue lakini haikusaidia chochote. Niliendelea kujilaumu sana kwa kumsaliti Ibra wangu, akaoga na alipomaliza, nilianza kumuandaa.
Alipomaliza, tulikaa mezani na kuanza kupata kifungua kinywa. Alipomaliza, nilimsindikiza mpaka nje, akaingia kwenye gari na kuwasha, akaanza kuondoka taratibu kuelekea kazini huku akinipungia mkono. Akaondoka mpaka alipopotea kwenye upeo wa macho yangu.
Nikarudi ndani na kujibwaga kitandani, bado sikuwa nimepata majibu kuhusu nguvu za ghafla alizokuwa nazo mume wangu. Nilitamani kumuuliza ametumia dawa gani mpaka amekuwa imara kiasi kile lakini nilishindwa kwa sababu bado nilikuwa na langu rohoni.
Niliamka na kufanya shughuli ndogondogo za hapa na pale huku mara kwa mara nikimtumia mume wangu meseji nzuri za kimapenzi. Nilipomaliza, nilienda kuoga na kurudi chumbani, nikajilaza huku nikindelea kutafakari juu ya hatma yangu.
Muda mfupi baadaye, nilisikia mlango ukigongwa, nikainuka kichovu na kwenda kufungua, nikiwa nimejitanda khanga mbili, moja juu na nyingine chini.
Nilipofungua mlango, moyo wangu ulilipuka kwa hofu na mapigo yakaanza kunienda mbio baada ya kugundua kuwa alikuwa ni Evans. Safari hii alikuwa amewahi kuliko kawaida, sijui hata kama kazini alienda. Nikiwa bado namshangaa, alisikuma mlango na kuingia mpaka sebuleni.
“Sikiliza shemeji, tumefanya makosa makubwa sana kufanya mapenzi wakati unajua mimi ni mke wa rafiki yako kipenzi. Kiukweli naijutia sana nafsi yangu, sitaki tena kumkosea mume wangu kwa hiyo naomba leo iwe mwanzo na mwisho kuja hapa nyumbani peke yako,” nilimwambia Evans huku nikiwa ‘sirias’ kwani kiukweli nilikuwa najisikia vibaya sana kutoka ndani ya moyo wangu.
Japokuwa mimi sikuwa na masihara, Evans alicheka kwa dharau kisha akaniambia kwamba kamwe hataweza kuniacha kwa sababu ameshaonja asali na sasa alikuwa tayari kuchonga mzinga.
“Uchonge mzinga? Kwa nini usitafute na wewe mke wako umuoe badala ya kudoea mali za wenzako?”
“Nimeshakwambia siwezi kukuacha, na nakuomba uwe mpole sana vinginevyo nitakufanyia kitu ambacho hutakuja kuamini, ndoa yako mimi ndiyo nimeishika mkononi mwangu,” Evans alisema kwa kujiamini huku akitoa simu yake, akanioneshea ishara nisogee nijionee mwenyewe.
“Mungu wangu!” nilijikuta nikishtuka kuliko kawaida kutokana na kile nilichokuwa nakiona. Evans alikuwa amerekodi video wakati tukivunja amri ya sita, hata sijui aliirekodi lini na ilikuwaje lakini sote wawili tulionekana vizuri kabisa, tena tukiwa kama tulivyoletwa duniani.
“Ukiendelea kujifanya mjuaji nitamuonesha mumeo ili liwalo na liwe, ukimwaga ugali mi namwaga mboga, wewe ni wangu na nitaendelea kukutumia mpaka siku nitakayochoka mwenyewe,” alisema Evans huku akiinuka na kutaka kuondoka.
Nilijihisi kama nimepigwa na radi, nikainuka haraka na kumkimbilia Evans huku nikimpigia magoti na kumsihi asifanye alichokusudia kukifanya. Nikamsihi sana na kumwambia kuwa nitakuwa tayari kufanya chochote anachokitaka, nikamuona akiachia tabasamu hafifu kisha akarudi na kukaa kwenye sofa.
Nilikosa raha kuliko kawaida, muda wote nilijiinamia huku machozi yakinitoka kwa wingi, nikawa naijutia nafsi yangu kwani ama kwa hakika nilikuwa nimepatikana. Bila kujali hali niliyokuwa nayo, Evans aliinuka na kunisogelea pale nilipokuwa nimejiinamia, akaanza kunifanyia vituko vya kimahaba huku akiniambia kwamba kama nitafanya vile anavyotaka, hakuna mtu yeyote atakayejua kuhusu uhusiano wetu wa kimapenzi. Bila hata huruma akaanza kunisihi nikubali tena kuangukia dhambini, jambo ambalo sikulikubali kwa urahisi.
Ilibidi niwe mkali kwani kama ningemchekea, Evans alikuwa anataka kunitumia kama chombo chake cha starehe. Nikakataa katakata na kumwambia kama alichokuwa anakitaka ni mapenzi yangu, basi atafute sehemu nyingine siyo nyumbani kwangu.
Alicheka sana na kuniambia kuwa hilo siyo tatizo kwake, kuna gesti nzuri tutakuwa tunaenda kila anaponihitaji. Nilimkubalia kwa sababu sikutaka aendelee kukaa pale nyumbani kwani nilihisi mume wangu anaweza kurudi muda wowote bila taarifa na kumkuta, jambo ambalo lingeleta matatizo makubwa kwenye ndoa yangu.
Baada ya kuona nimeshikilia msimamo wangu, ilibidi Evans aage na kuondoka huku naye akishangaa kwa nini nimebadilika haraka kiasi hicho. Alipoondoka nilijifungia mlango kwa funguo na kwenda kujitupa kitandani chumbani kwangu, nikaanza kulia kwa uchungu kwani ama kwa hakika maji yalikuwa yamenifika shingoni.
Nililia kwa muda mrefu mpaka usingizi uliponipitia. Nilikuja kuzinduka baadaye baada ya kusikia kengele ya mlango wa nje ikilia, nikakurupuka harakaha na kukimbilia bafuni ambako nilinawa uso ili mume wangu asijue kwamba nilikuwa nalia, nikaenda kumfungulia ambapo alishangaa kwa nini nilikuwa nimejifungia mlango mchana.
“Najisikia vibaya, kichwa kinaniuma tangu asubuhi, nilikuwa nimelala,” nilimdanganya mume wangu, akanikumbatia na kunipa pole sana, akawa ananilaumu kwa nini sikumpa taarifa mapema kwani angeweza hata kuomba ruhusa kazini na kuja kuniangalia.
Nikamuomba radhi ambapo tulienda chumbani, akatafuta dawa za kutuliza maumivu na kunipa, akanisimamia mpaka nilipokunywa kisha nikalala, akanifunika shuka kwa upendo na kunitaka niendelee kupumzika. Alibadilisha nguo zake kisha akaenda jikoni kuanza kuandaa chakula cha jioni kwani kutokana na hali yangu, mpaka muda huo sikuwa nimefanya kazi yoyote. Maskini mume wangu, alinihudumia akijua kweli mkewe nilikuwa naumwa kumbe tatizo halikuwa hilo.
Kwa kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa ameishi maisha ya peke yake, mume wangu alikuwa anaweza kupika chakula kizuri utafikiri siyo mwanaume. Kilipokuwa tayari, aliandaa kabisa mezani kisha akaja kuniamsha kwa upendo, tukaenda kula ambapo alikuwa akinihimiza nile ili nipate nguvu.
Kweli tulikuwa huku akiendelea kuniambia maneno mazuri ya kunifariji, yaliyozidi kunifanya nijisikie kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu. Tulipomaliza, tulienda kulala mpaka kesho yake asubuhi ambapo mume wangu aliwahi kuamka na kuandaa kifungua kinywa. Akaja chumbani kuniamsha, tukaenda sebuleni ambapo tulianza kupata kifungua kinywa.
Wakati tukiendelea kupata kifungua kinywa, ghafla nilianza kuhisi kichefuchefu, nikainuka na kukimbilia kwenye karo dogo lililokuwa koridoni, nikaanza kutapika, jambo ambalo lilimshtua sana mume wangu, haraka akanikimbilia na kunishika, akanisaidia mpaka nilipomaliza kutapika ambapo alininawisha na kunipeleka chumbani.
“Inawezekana unaumwa malaria, inabidi twende hospitali kabla hali haijawa mbaya,” alisema mume wangu huku akifungua kabati na kunichagulia nguo za kuvaa. Akanipeleka bafuni ambapo aliniogesha kwa upendo kisha tukarudi chumbani ambako alianza kunisaidia kunivalisha.
Kiukweli mapenzi aliyokuwa ananionesha mume wangu, yalikuwa sawa na mwiba mkali ndani ya moyo wangu, nikawa najilaumu sana kwa sababu alionesha kunipenda na kunijali kwa kiasi kikubwa mno, hakustahili kulipwa mabaya hata kama kuna kipindi alikuwa na udhaifu wake.
Baada ya kumaliza kuniandaa, naye alijitayarisha kisha tukaondoka na safari ya kuelekea hospitali ikaanza. Tukiwa njiani, alipiga simu kazini kwao na kuomba ruhusa kwamba ananipeleka hospitalini mimi mkewe.
Japokuwa mume wangu alikuwa anahisi kuwa nina malaria, akilini mwangu nilikuwa na uhakika kuwa tayari nilikuwa nimenasa ujauzito. Kibaya zaidi, haukuwa ujauzito wa mume wangu bali wa rafiki yake, Evans kwa sababu nilikutana naye kimwili katika siku zangu za hatari, tena bila tahadhari. Hofu kubwa ikautawala moyo wangu kwani sikujua hatima ya ndoa yangu ingekuwaje.
Tulifika mpaka Hospitali ya Aga Khan ambako ndiko tunakotibiwa, tukaingia kuonana na daktari baada ya kukamilisha taratibu za mapokezi ambapo nilimueleza daktari kilichokuwa kinanisumbua, nikadanganya tena kwamba nilikuwa nikisikia kichwa kinaniuma, mwili unachemka na kichefuchefu.
Daktari akaniandikia nikapime malaria lakini kabla hatujatoka, mume wangu alimuomba daktari aniandikie vipimo vyote ili kama kuna tatizo lingine, lifahamike. Nikajikuta nikitetemeka mno kwani siri yangu ilikuwa karibu kufichuka na kama ingebainika kwamba nina ujauzito, mume wangu angegundua kuwa si wake kwani kabla ya kupatana siku chache zilizopita, tulikaa kipindi kirefu bila kupeana haki ya ndoa. Hofu kubwa ikaingia ndani ya moyo wangu.
Baada Ya kutoka kwenye chumba cha daktari, tulielekea maabara huku mapigo ya moyo wangu yakizidi kunienda mbio. Sikutaka kabisa ukweli wa kilichokuwa kinanisumbua ujulikane na ndani ya moyo wangu nilishaanza kujiandaa kwenda kuichoropoa mimba hiyo.
Tuliingia maabara ambapo wahudumu walikichukua kile cheti changu na kuanza kusoma maelezo ya daktari, wakanitolea vichupa viwili, kimoja cha haja ndogo na kingine cha haja kubwa, wakaniambia nielekee chooni kwanza kisha nikirejea, watanichukua damu kwa ajili ya vipimo vingine.
Kwa jinsi mapigo ya moyo yalivyokuwa yananienda mbio, kama mume wangu angekuwa makini angeweza kugundua kitu, nikatoka harakahaharaka mpaka kwenye vyoo vya wanawake, mume wangu ikabidi abaki kwenye benchi akinisubiri.
Nilipoingia chooni sikutoka haraka kwani sikuwa na majibu ya kumpa mume wangu endapo ataugundua ukweli kwamba nilikuwa mjamzito. Nikawa naendelea kuwaza bila kupata majibu.
“Dada toka basi na sisi tuingie,” msichana mmoja aligonga mlango wa chooni baada ya kuona nimekaa muda mrefu bila kutoka, nikazidi kuchanganyikiwa. Ilibidi nitoke na kuanza kuzungumza na yule msichana aliyekuwa akinigongea, ambaye kimwonekano alionekana kuwa mwanafunzi wa sekondari.
“Samahani naomba kuzungumza na wewe mara moja,” nilimwambia huku nikimvutia pembeni kulipokuwa na karo la kunawia mikono. Nikaingiza mkono kwenye sidiria yangu na kutoa noti tano za shilingi elfu kumikumi.
“Sikia mdogo wangu, mwenzio nina matatizo makubwa hapa nilipo, ndoa yangu inataka kuvunjika kwa sababu nahisi nimebeba ujauzito wa mtu tofauti na mume wangu na sitaki mwenyewe aujue ukweli. Nakuomba ukiingia chooni, niwekee haja ndogo na kubwa kwenye hivi vichupa vyangu, hii hela utakunywa soda,” nilimwambia yule msichana huku nikimshikisha zile fedha.
Akapigwa na butwaa kubwa na kunishangaa usoni, nikaendelea kumbembeleza ambapo alikubali lakini kabla hajaingia, nikamuuliza swali lingine ili niwe na uhakika na ninachokifanya.
“Kwani wewe unaumwa nini?”
“Naumwa sana na tumbo nahisi nina UTI .”
“Usije kuwa na wewe ni mjamzito?”
“Hapana, sina mpenzi na sijawahi kukutana na mwanaume tangu nizaliwe,” alisema yule msichana, nikamshukuru Mungu na kumsihi afanye haraka kwani nilikuwa nimeshakaa sana chooni.
Aliziweka zile fedha mfukoni kisha akaingia na muda mfupi baadaye, alinitolea na kunikabidhi, nikamshukuru sana kisha nikatoka. Kwa jinsi nilivyokuwa kwenye wakati mgumu, wala sikuona kinyaa kubeba haja za mtu mwingine mkononi mwangu.
“Vipi mbona umechelewa?”
“Nilikuwa najilazimisha mume wangu,” nilimjibu mume wangu ambaye alionesha kusubiri kwa hamu kusikia majibu ya vipimo vyangu. Tuliongozana na kuelekea maabara ambapo niliwakabidhi vipimo wale wahudumu kisha wakanielekeza sehemu ya kukaa ili wanitoe damu.
Nikafanya hivyo na kwenda kukaa sehemu niliyoelekezwa, nikatolewa damu kwenye mshipa wa mkono wa kushoto kisha tukaambiwa tukasubiri majibu. Tukatoka na mume wangu na kwenda kwenye viti maalum vya kusubiria majibu. Kwa kuwa sasa nilikuwa na uhakika kwamba ‘bomu’ langu halitalipuka, nilianza kumfanyia makusudi mume wangu.
Nikawa namuegamia begani na kujishika tumbo, nikijifanya nahisi maumivu makali sana, akawa na kazi ya ziada ya kunibembeleza na kunituliza. Muda mfupi baadaye, majibu yalitoka, tukaitwa na kupewa karatasi ya majibu, tukaelekezwa kurudi kwa daktari ambapo tulipoingia, daktari alianza kusoma karatasi ya majibu kwa umakini.
“Inaonesha mkeo hana tatizo kubwa sana isipokuwa ana maambukizi kwenye njia ya mkojo au kwa kitaalamu huitwa UTI. Kirefu chake ni Urinary Tract Infection,” alisema daktari huku akiweka vizuri miwani yake, akaendelea kutufafanulia sababu zinazosababisha ugonjwa huo.
“Inabidi mjitahidi kukifanyia usafi choo chenu ikiwa ni pamoja na kunyunyizia dawa za kuua wadudu, na wewe mama usipende kujisaidia kwenye vyoo vya jumuiya kwani huko ndiko maradhi haya yanakopatikana,” alisema daktari na kuendelea kusisitiza kuwa sikuwa na tatizo lingine lolote zaidi ya hilo.
Nikamgeukia mume wangu na kumtazama, akaonekana kuwa makini kusikiliza maelekezo ya daktari. Maskini! Hakujua kwamba nimemzidi ujanja.
Tulirudi nyumbani na mume wangu na kabla hatujafika, tulipitia kwenye duka la vifaa vya usafi ambapo mume wangu alinunua dawa za kuulia wadudu chooni pamoja na vifaa vya kufanyia usafi.
Pia alininunulia matunda, juisi na vitu vingine vizuri kwani daktari alishauri niwe nakula sana matunda na juisi kutokana na dawa za UTI nilizoandikiwa. Kiukweli Ibra alikuwa mwanaume anayejali sana, ukiachilia mbali matatizo yake machache lakini kiukweli, kila mwanamke angependa kuwa na mume kama yeye.
Mambo mazuri aliyokuwa ananifanyia yalinifanya nizidi kuijutia nafsi yangu, nikawa natamani kama siku zirudi nyuma ili niweze kurekebisha makosa ya kumsaliti na rafiki yake niliyomfanyia lakini haikuwa hivyo.
Tulirudi mpaka nyumbani ambapo siku hiyo alinisaidia kufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo kufanya usafi na kupika.
Mtoto wa kike nikawa nimetulia kwenye sofa nikiangalia runinga, huku mara kwa mara nikijifanya nimezidiwa nguvu na dawa ambazo kiukweli, japokuwa mume wangu alikuwa anajua kuwa nazinywa, nilikuwa nazitupa kwani sikuwa naumwa UTI kama alivyokuwa anaamini.
Siku hiyo ilipita, kesho yake, mume wangu alitaka asiende tena kazini lakini nilimtoa wasiwasi kwamba nitakuwa sawa asijali, baada ya kumbembeleza sana, alikubali kwenda kazini ingawa aliniambia kuwa atawahi kurudi ili aje kuendelea kuniuguza.
Alipoondoka tu, na mimi nilijiandaa harakaharaka, nikatoka na kwenda mpaka kwenye duka la dawa lililokuwa jirani na pale tulipokuwa tunaishi. Nikaenda kununua kipimo cha ujauzito na kurudi nacho nyumbani kwani nilitaka kupima na kuhakikisha mwenyewe kwani japokuwa nilikuwa najua kwamba nimeshika ujauzito, sikuwa na uhakika.
Nilirudi ndani haraka na kwenda bafuni ambapo nilikichukua kipimo hicho na kukiweka kwenye kopo ambalo lilikuwa na haja ndogo, nikasubiri kwa dakika kadhaa na baada ya muda, nikakitoa. Nilichokiona kilifanya mapigo ya moyo wangu yanilipuke mno. Ni kweli nilikuwa nimenasa ujauzito, nikahisi kuchanganyikiwa kuliko kawaida.
Harakaharaka nilichukua simu yangu na kumpigia rafiki yangu mmoja ambaye kabla sijaolewa nilikuwa nikisoma naye chuo. Niliwahi kusikia kuwa ametoa ujauzito. Alipopokea, sikutaka kupoteza muda, nilimueleza tatizo langu kwamba nataka kutoa ujauzito.
“Shoga si ndiyo kwanza umeolewa? Kwa nini unataka kutoa mimba wakati raha ya ndoa ni mtoto?” aliniuliza shoga yangu huyo lakini nikamdanganya kwamba mimi na mume wangu hatukupanga kuwahi kuzaa, nikamzugazuga mwisho akaamini uongo wangu.
Alinielekeza kwamba yeye alienda kutolewa ujauzito na daktari mmoja maarufu aliyekuwa na ofisi yake Kawe, aitwaye Twalipo. Nilimuomba anielekeze ofisi yake ilipo na ikiwezekana anipe namba zake. Kweli alifanya hivyo, akanielekeza na kunitumia namba yake.
Kwa jinsi nilivyokuwa na hofu ndani ya moyo wangu, sikutaka kupoteza muda, nilipokata tu simu, nilimpigia Dokta Twalipo na kumueleza tatizo langu, akaniambia niende ofisini kwake kesho yake asubuhi, akanitajia na gharama za kazi hiyo kisha akakata simu.
Nilishusha pumzi ndefu na kumshukuru Mungu kwnai japokuwa nilikuwa nikienda kufanya kitendo cha kishetani, lakini hatimaye ndoa yangu ingekuwa salama tena kama ningefanikiwa kuuchoropoa ujauzito huo. Nilirudi chumbani na kujilaza kitandani, muda mfupi baadaye nikasikia mlango ukigongwa.
Nikajua ni mume wangu kwani aliahidi kurudi mapema, nikajifunga khanga moja tu na kuinuka, nikaenda kufungua. Tofauti na nilivyotegemea, hakuwa mume wangu bali Evans ambaye japokuwa ulikuwa ni mchana wa jua kali, alionesha kulewa tilalila.
Moyo ukashtuka kupita kiasi kwani nilijua muda mfupi baadaye, mume wangu atarudi na akimkuta akiwa katika hali iwe, hawezi kunielewa. Ikabidi nivae ukauzu, nikabamiza mlango na kuufunga kwa ndani, nikafunga na funguo kabisa, jambo ambalo Evans hakulitegemea.
ITAENDELEA
My Repentance (Kutubu Kwangu) Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;