Hofu Sehemu ya Kwanza
NEW AUDIO

Ep 01: Hofu

SIMULIZI Hofu
Hofu Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA : ARISTABLUS ELVIS MUSIBA (A.E MUSIBA)

Simulizi : Hofu

Sehemu Ya Kwanza (1)

PORT ELIZABETH

Ilikuwa tarehe 24 Machi, baada ya mauaji ya kikatili ya waafrika 19, katika kitongoji cha Langa, karibu na Vitenhage; mji ulio karibu na ule mji wa viwanda wa Port Elizabeth, katika Jimbo la Cape Mashariki. Mauaji hayo yalikuwa yamefanyika tarehe 21 Machi, siku ya kukumbuka mauaji ya kikatili kwenye mji wa Sherpville mnamo mwaka 1960. Wakati wazalendo 69 walipouawa kikatili. Mnamo tarehe hiyo ya 24 Machi, huko mjini Port Elizabeth kulifanyika mkutano katika ofisi ya Mkuu wa Polisi mnamo saa sita usiku.

Ndani ya chumba cha mkutano huo walijumuika watu ambao wamekuwa chanzo cha vilio na malalamiko mengi kutoka kwa wazalendo wa Afrika Kusini dhidi ya makaburu. Katika mkutano huo alikuwemo waziri wa sheria na usalama wa makaburu, Kamishna wa Polisi, Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la makaburu na Kamanda wa kikosi cha Jeshi kiitwacho ‘KULFUT’yaani ‘Gongo la Chuma’ wote hao walikuwa ni makaburu. Lakini vile vile mkutano huo ulihudhuliwa na watu weusi ambao walikuwa wameitwa haraka haraka.

Hawa walikuwa wamefanyiwa mipango maalumu ya usafiri ili mladi wafike kwenye mkutano huo muhimu. Walikuwa wamesafiri kwa kutumia ndege ya Jeshi la Anga la makaburu. Weusi hawa walikuwa ni Mkuu wa Magaidi wa UNITA, wenye kupinga Serikali ya Angola, Mkuu wa Magaidi wa MNR wenye kupinga Serikali ya Msumbiji na Mkuu wa Magaidi wa LLA wenye kupinga Serikali ya Lesotho, kwa kifupi tu ni kwamba, Magaidi wote hawa ni vibaraka wa Serikali ya Makaburu na ilikuwa ni serikali ya makaburu iliyowagharamia kufanya ujahili dhidi ya nchi zilizo mstari wa mbele katika Ukombozi wa Afrika Kusini, ili kuzizorotesha kisiasa na kiuchumi kwa nia ya kuziangusha hatimaye. Waziri wa sheria, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, alianza kwa kusema;

“Kwanza lazima nitoe shukrani zangu kwa nyinyi wote kuweza kufika hapa kwa muda uliopangwa, shukrani zangu za dhati ziwaendee nyinyi wageni wetu ambao mmetoka nje ya nchi hii. Pili tumeitana hapa usiku wa manane kuzungumzia suala muhimu sana. Ningependa tufanye na kumaliza mazungumzo yetu usiku huu ili muweze kuondoka kabla hapajapambazuka, kwani shughuli hii ni ya siri sana. Mimi nikiwa mwana siasa nitazungumza tu kwa ujumla kuhusu nia ya mkutano. Halafu nitawaachia wataalamu wa utekelezaji walio hapa kuchambua vipengele vinavyohusika kwa undani zaidi”.

“Nafikiri nyote mnaelewa kwamba kumekuwa na wimbi la maasi la waafrika katika nchi nzima ya Afrika Kusini. Wimbo hili, kwa kiasi fulani limetutia wasiwasi. Migomo imeongezeka katika sehemu za kazi kiasi cha kutishia uchumi wa nchi yetu. Maandamano yameongezeka kiasi cha kutishia utulivu na amani ya wananchi. Vitendo vya hujuma vinavyofanywa na magaidi wanaojiita wapigania uhuru’wa Afrika Kusini vimeongezeka kiasi cha kutishia mashirika ya nje yenye raslimali zao humu nchini.

“Sasa Serikali imeamua kukomesha vitendo vyote hivi. Serikali ilikuwa na nia ya kulegeza vipengele fulani fulani katika sheria zetu kwa manuafaa ya weusi. Lakini imegundulika kuwa kufanya hivyo kutawafanya watu hawa kuwa kichwa ngumu zaidi. Na kama alivyosema Rais wetu, hakuna mtu yeyote Ulimwenguni atakaetuzuia kulinda usalama wa nchi yetu na watu wake wapendao amani!’. Na hapa nasisitiza tena hatutaki mchezo.

“Ghasia hizi ambazo zimekuwa zinaendelea zimefanya mashirika na makampuni kutoka nje kuwa na mtazamo mpya. Yanaanza kuwa wasiwasi juu ya uwezo wetu na pia kuelekea kuwa na imani katika vyama vinavyodai vinapigania uhuru. Hali hiyo siyo nzuri na ni tishio kubwa kwetu”.

“Uchumi wetu umeanza kuanguka. gharama za maisha zimepanda kwa kadri asilimia kumi na saba!, ukame umeathiri uzalishaji wa chakula. Bei ya dhahabu imeanguka saba mwaka huu na kufanya bei za vitu muhimu, kama vile Petroli, kuongezeka kufuatana na kushuka kwa thamani ya fedha yetu, ukilinganisha na thamani ya dola ya kimarekani. Jumuia ya Kimataifa inapiga kelele na kuyataka makampuni yasiweke raslimali na vitegauchumi vyao nchini mwetu”.

“Mambo yote haya yanatokana na mwamko wa Ulimwengu dhidi ya siasa yetu ya ubaguzi. suala la kuzungumzia ni nini kufanyike ili kulekebisha hali hii ndio sababu leo mko hapa kutafuta ufumbuzi. kuanzia sasa tunataka kufanya macho ya Jumuia ya Kimataifa kuelekea sehemu nyingine ili sisi tupate nafasi ya kurekebisha mambo humu nchini. Macho yao yanataka yaelekee kwenye nchi zilizo mstari wa mbele na vile vile Namibia. Tutafanya vitendo katika nchi hizo vitaifanya Jumuia ya Kimataifa kushughulikia sana; ikitafuta njia za kuwasaidia wananchi wa hizo. Wakati Jumuia ya Kimataifa inashughulika kiasi hicho, sisi tutaanza kuwapa fundisho hawa watu weusi wanaoleta ghasia hapa nchini. Jumuia ya Kimataifa ikija kugeuza macho yake kuyaelekeza kwetu. tutakuwa tumeisha wakomesha hawa watu weusi ambao ni wakorofi watakuwa wamenyooka kama mpini”.

“Hivyo tumeamua kuanzisha ‘UTAWALA WA HOFU’ dhidi ya weusi walio humu nchini na pia walio katika nchi zilizo mstari wa mbele kwa ujeuri. Ni imani yangu kuwa mmenielewa na ninawashukru tena kwa kunisikiliza. Wakuu wote wa usalama wako hapa. watawaeleza jinsi utekelezaji wa jukumu hili utakavyokuwa. Ahsanteni sana”.

Alipomaliza kusema hayo, Waziri wa sheria na usalama alifunika jalada lake, kisha akasimama na wengine wakasimama pia. Huku akiwapungia mkono wa kwaheri, Waziri alisindikizwa na Kamishina wa Polisi mpaka kwenye mlango. Alifunguliwa mlango huo na kutokomea gizani.

Baada ya Kamishina wa Polisi kurudi kwenye nafasi yake, Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la Makaburu alichukua uwanja kueleza namna ya utekelezaji wa mpango huo.

“Nafikiri nyinyi wote mmemsikiliza waziri kwa makini. Mambo ni kama hayo na hatuna budi kutekeleza, nyinyi wenzetu wa UNITA, MNR na LLA tunahitaji msaadawenu kikamilifu. Tumesaidiana mambo mengi sana. Bila sisi kusingekuwepo na UNITA, MNR au LLA”, alisema huku akiwakazia macho viongozi wa vyama hivyo vya magaidi.

Wote walimwemwesa huku wakionyesha kwa vichwa vyao ishala ya kukubaliana nae.

“Kuanzia sasa misaada kwenu inaongezwa mara dufu”. Wote walishangilia kwa kupiga makofi.

“Lakini”, aliendelea Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Makaburu, “Misaada hii haikuongezwa bure. Kutakuwa na kazi kubwa ya kufanya. Alinyamaza huku akiwaangalia viongozi wa magaidi kujua kama walikuwa wanampata. “Mmesikia kuwa tunaanzisha utawala wa hofu’ dhidi ya watu weusi waliomo humu nchini na pia nchi zilizoko mstari wa mbele pamoja na Namibia. Utekelezaji wa mpango huo utakuwa kama ifuatavyo.

“Kwanza sisi tutajitangazia uhuru nchini Namibia. Baada ya kufanya hivyo tutapambana na SWAPO. Kama ikibidi tutauwa watu Namibia kwani nchi ile ni lazima kuitawala. Tumeanzisha Jeshi linaloitwa KULFUT, yaani Gongo la Chuma’. Hili ndilo Jeshi litakalosababisha Hofu huko Namibia na nchi fulani fulani zinazojidai kuwa mstari wa mbele. Jeshi hili limeundwa na Makomandoo watupu na lenye uwezo mkubwa.

Limefundishwa kwa kipindi cha miaka kumi sehemu mbali mbali Ulimwenguni na sasa liko tayari kabisa kutia hofu popote litakapotumwa. Upande wetu umejiweka tayari. Baadhi ya vikosi vya Jeshi hili vitaletwa kwenu”.

Wajumbe walipiga makofi.

“UNITA”, aliendelea “Kazi yenu itakuwa kutia hofu huko Angola. Hakuna mazunguzo na Serikali ya Angola tena. Mtapewa kila msaada wa hali na mali. Lazima kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi hiyo unaanguka kabisa. Kamanda wa KULFUT yupo hapa atapewa kikosi cha Jeshi hilo kusaidia katika dhima hiyo, wapiganaji wenu wasiwe na huruma, bali kuchinja na kuua kiumbe chochote kilicho mbele yenu. Hakikisha mnawaangamiza wale wote wanaojiita wapigania uhuru wa Namibia. Sisi tuko nyuma yenu kwa lolote lile litakalotokea. Nguvu zetu mnazijuwa. Kwa hoyo hakuna atakayechezea”.

“Nyinyi MNR”, alimgeukia kiongozi wa MNR, “Kazi yenu mnaijuwa. Kama watakavyofanya hawa watu wa UNITA. Fanyeni vurugu ndani ya Msumbiji. Watu wapate hofu kuliko wale walioishi wakati wa NAAzI iliyosababishwa na Wajerumani”.

Mara alimuona Kamanda wa MNR amenyoosha kidole akitaka kuzungumza.

“Eh, unasemaje?, aliuliza kwa shauku kubwa.

“Sisi tuko tayari kabisa”, alisema Kamanda wa MNR, “Lakini lazima niseme kwamba mkataba wenu wa Nkomati unatutatanisha. Ni mkataba wa amani kati ya Msumbiji na Afrika Kusini. Sasa kwetu sisi kuendeleza mapambano inakuwa vigumu ingawa mnatusaidia. Mkataba huo unatuathiri sana”.

Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Makaburu alijibu. “Achana na siasa. Mkataba wa Nkomati ni siasa tu. Sahau kabisa. Tangu uwekwe saini hakuna mtu ambaye ameutekeleza. Ndio sababu misaada kwenu imeendelea. Kazi yenu ni kama nilivyosema: fanya hali ya Msumbiji iwe ya hofu tupu. Lengo la mkataba wa Nkomati ilikuwa kuwachota akili viongozi wa serikali ya Msumbiji. Tumegundua kwamba wanawaogopa sana nyinyi watu wa MNR. Nyinyi ndio mlikuwa chanzo cha mkataba huo. Walitaka amani. Sasa kinachohitajika ni kuwatia hofu zaidi kwa vita na si ajabu mkachukuwa madaraka. La sivyo, angalau waje kusujudu kwetu na kutulamba miguu. Kwa hivyo sahau kitu kama mkataba wa nkomati”.

“Nakuapia”, alisema Kamanda wa MNR, “Watakiona cha mtemakuni”.

Ndipo Mkurugenzi wa shirika la Ujasusi la Makaburu alipoendelea, “Kazi ya LLA haina tofauti na wengine askari kutoka jeshi la KULFUT watawasaidia kuleta vurugu na hofu kubwa huko Lesotho na Botswana. Sisi tuachieni Zimbabwe, Zambia na Tanzania. Vikosi vyetu maalumu vya uhujumu katika Jeshi la KULFUT vitazionyesha cha mtemakuni nchi hizo. Ili kuonyesha nguvu zetu, sisi tutaanzia Tanzania. Tunataka tutie vurugu na kuleta rindi la hofu katika nchi hiyo dunia itashangaa. Tanzania haijawahi kupewa fundisho kwa sababu hiyo nchi ina kiburi na ndio shina la hawa wanaojiita wapigania uhuru”.

“Bila Tanzania, hawa watu wasingetupa taabu kiasi hiki. Nchi hiyo inawapa hifadhi watu hao na kuwapatia mafunzo ya kijeshi. Baadae inawapenyeza kwetu na kutupa shida, shambulizi tutakalofanya huko Tanzania. litawatia hofu hao wanaojiita wapigania uhuru na kuwafanya wasambae bila mpango, itawachukua karne nzima kuweza kujikusanya tena. Litakuwa pigo takatifu ambalo litaiacha dunia nzima inagwaya. Mipango ya awali juu ya kipigo hicho iko tayari na hatuna wasiwasi”.

Mkuu wa UNITA aliamusha mkono ikiwa ni ishara yake ya kuomba kusema.

“Eh, unasemaje?”. Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Makaburu alimuuliza Mkuu wa UNITA.

“Mimi nasikia moyo wangu unakwenda mbio kwa shauku”, alisema Mkuu wa UNITA. “Kama kweli mtaipa kipigo Tanzania mpaka ikakoma kutamba, basi sisi kazi yetu itakuwa rahisi kama kunywa maji. Nchi hiyo ina kiburi na ndio inayowapa kichwa ngumu wale wanaodai kupigania uhuru, na nchi nyingine za mstari wa mbele. Iwapo Tanzania itashika adabu, basi vyama vyetu vitapata ushindi wa kutawala. Lakini napenda kukutahadhalisha kuwa nchi hiyo ni imara sana. Mimi nimewahi kuishi huko na ninajua kazi yenu haitakuwa rahisi”.

Mara alikatizwa na Mkurugenzi.

“Usiwe na wasiwasi”, Mkurugenzi alianza kujitapa. “Hakuna nchi itakayonusurika. Na Tanzania itakuwa ya kwanza. Nyinyi mtasikia. Kusema kweli baada ya kipigo hicho, hao wapigania uhuru; na pia nchi nyingine zilizo mstari wa mbele watabaki wanagwaya”.

“Ili yakutoke mashaka”, alidakiza Kamanda wa KULFUT, “Matayarisho ya kipigo hicho yalianza siku nyingi. Jeshi la KULFUT likishikiana na Shirika la Ujasusi hakuna wasiwasi kuhusu kipigo hicho, nakuhakikishia kuwa Tanzania na wenzake watakipata cha mtemakuni. Tumetumia miaka kumi kujitayarisha na muda huo siyo mchezo”.

“Saa zimekwenda sana. Tumetumia muda mwingi sana kuzungumzia suala hili wakati ambapo nyie mnapaswa kuondoka kwa siri sana kabla ya mapambazuko”. Hapa Mkurugenzi alinyamaza kidogo kisha akaendelea kusema. “Kamanda wa KULFUT’ atawapatia msaada mnaohitaji katika kutekeleza mpango huo. Hatuwezi kukubali kushindwa kwani hiyo ina maana kuwa huo utakuwa ndio mwisho wetu – kitu ambacho hakiwezekani. Lazima nipate ripoti ya maendeleo ya mpango huu kila siku ili niweze kuipa taarifa serikali. Kamishina wa Polisi anasema hana wasiwasi juu ya weusi wa hapa kwani atawatia vurumai mpaka wajute kuzaliwa”.

:Nafikiri mmesikia kuwa mwezi Februali tuliwakamata vingozi wa vyama vya upinzani. Hao tumewaweka kiporo na baada ya kuipa kipigo Tanzania. Nyinyi mtasikia vurumai tutakavyoifanya, au uongo Kamishina?”.

Akionyesha majivuno, Kamishina wa Polisi alijibu, “Watajuta kuzaliwa kwani walikuwa wanaleta mchezo. walikuwa wamediliki kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe hapa nchini. Kitu kama hicho hakiwezi kutokea wakati bado niko hai”.

Mkurugenzi alifunga mkutano huo kwa dharura kwa kusema, “Ahsanteni sana. Ni mategemeo yangu kuwa mmeelewa hali halisi na hivyo mtatekeleza itasavyo. Naamini tutakapokutana tena kwenye mkutano kama huu hali haitakuwa hivi, bali kusherekea ushindi dhidi ya adui. Sura ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara itabadilika kwa kupata tawala mpya”.

Mkutano ulifungwa saa kumi na moja alfajiri.

HARARE

Ilikuwa tarehe 1 Aprili, Juma moja baada ya Mkutano uliofanywa na Maafisa wa Makaburu na vikaragosi vyao Mjini Port Elizabeth. Siku hiyo kulifanyika mkutano mwingine. Mkutano huo ulikuwa kati ya watu tofauti na wale Makaburu, mikutano yao ilikuwa na uhusiano. Mkutano huu ulifanyika mjini Harare, Zimbabwe, katika ofisi za wapigania uhuru wa Afrika Kusini. Tofauti na ule mkutano wa Makaburu uliofanyika usiku, mkutano wa wapigania uhuru ulifanyika mnamo saa nne hivi asubuhi. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Chama cha kupigania uhuru. Waliohudhuria mkutano huu ni yeye Mkuu wa Upelelezi, Mkurugenzi wa Upelelezi na Serikali ya Zimbabwe pamoja na kijana mmoja aitwae Bon Sipele.

Huenda itakuwa kwa faida yako kama nitakueleza kidogo juu ya kijana huyu mradi usiniite mmbeya. Lakini kwa kuwa mimi huwa sisengenyi, fahamu kwamba mambo nitakayokueleza ni kweli tupu. Kijana Bon Sipele alikuwa na umri yapata miaka ishirini na nane. Kijana huyu alikuwa mzalendo wa Afrika Kusini ambaye alizaliwa katika kijiji cha Soweto. Kijana huyu alianza kujulikana kama mwana mapinduzi akiwa bado mbichi. Alipokuwa na umri yapata miaka kumi na tisa, yeye na wenzake baada ya kumaliza darasa la kumi na nne walivamia mitaa wakiwa na mawe na chupa kuupinga utawala wa kibaguzi wa Makaburu. Serikali ilijibu kuwa kuwauwa baadhi ya vijana hao na kuwatia ndani wengine. Bon pamoja na wenzake walipata bahati ya kutoroka. Huku wakisaidiwa na wapigania uhuru, waliweza kuingia Zambia na hatimaye Tanzania. Bon alijaa uchungu kutokana na vitendo vya kikatili vya Makaburu. Hivyo aliapa kuwa angejitoa mhanga kupigania uhuru wa nchi yake.

Bon alipewa nafasi ya kwenda nje ambapo alipata mafunzo ya kijeshi kijana huyu alipitia mafunzo magumu huko Urusi, China, Cuba na Korea Kasikazini. Aliporudi kutoka kwenye mafunzo alikuwa na ujuzi wa hali ya juu. Aliombwa kukaa katika ofisi za wapigania uhuru zilizo Tanzania ili awe mkuu wa idara ya uendeshaji vita. Lakini, Bon alikataa kazi hiyo kwani alitaka kuishi katika hali halisi ya vita. Hivyo alikwenda moja kwa moja mpaka Msumbiji kupambana na Wareno na Makaburu huko msituni. Baadaye aliweza kuhujumu viwanda kadhaa, mitambo ya umeme pamoja na Reli ndani ya Afrika Kusini. Bon aliwatia homa Makaburu.

Vyama vya wapigania uhuru viliona Bon alikuwa anafaa kuwa mpelelezi ili awakabiri majasusi wa Makaburu kutokana na ujasili wake na mafunzo aliyokuwa nayo. Baada ya muda siyo mrefu Bon alitokea kuwa mpelelezi aliyesifika na kuogopwa katika sehemu hii ya Kusini mwa Afrika. Makaburu walimhala kutokana na hasara kubwa aliyowatia. Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa inamtafuta bila kufanikiwa. Kijana huyu ndiye Bon Sipele.

Tunarudi kwenye mkutano uliokuwa ukifanywa na watu hao watatu.

Mkurugenzi wa upelelezi wa Zimbabwe ndiye alikuwa mtu wa kwanza kutoa hoja yake. Alisema, “Tumekusanyika hapa ili niweze kuwaeleza ama sote kuzungumza suala muhimu. Habari kuhusu suala hilo nimezipata kutokana na kazi yangu, suala hili linawahusu nyinyi pia. Ndio sababu nimeona ni vizuri niwahusishe”.

Alimeza mate kulainisha koo akaendelea, “Mnakumbuka kuwa hapa majuzi watu wetu walifanya operesheni kwenye sehemu ya Beitbridge katika mpaka wetu na Makaburu. Mtakumbuka pia kuwa watu wetu waliweza kuvunja kundi la Majasusi waliokuwa wanafanya ujahili dhidi ya nchi yetu kutokana na amri za Makaburu”.

“Tunakumbuka”, walijibu kwa pamoja.

“Katika operesheni hiyo”, Mkurugenzi aliendelea, “Tuliweza kuwakamata Majasusi ishirini. Baada ya kuyakamata, vijana wetu kama mjuavyo walishughulika kikamilifu. Baada ya kuhojiwa mmoja wao alitoa taarifa ambayo imetufanya tuwe macho. Kwa sababu hiyo nimelazimika kuwapa habari hizi. Kutokana na ripoti niliyopata ofisini kwangu ni kwamba, Makaburu wamebuni mpango wa kukomesha mashambulizi dhidi yao. Utekelezaji wa mpango huo ni kwamba Makaburu watatoa kipigo kitakatifu ambacho kitamaliza kabisa nguvu za wapigania uhuru kiasi kwamba wale watakaobahatika kubaki hawatathubutu kufanya mashambulizi dhidi yao. Vile vile kuna mpango wa kushambulia nchi yetu baada ya kipigo dhidi ya wapigania uhuru. Sasa kama inavyofahamika, viongozi wa wapigania uhuru wamesambaa katika nchi mbali mbali. Wako kwenye nchi zilizo katika mstari wa mbele. Vilevile wako katika nchi kadhaa za Afrika na hata nchi rafiki za Ulaya. Hivi tumefikiri sana juu ya hali hii lakini hatujapata ufumbuzi. Ndio sababu imeonekana ni vizuri tutafute ufumbuzi wote kwa pamoja”.

Mkurugenzi wa upelelezi wa Zimbabwe alipomaliza kusema chumba kikajaa ukimya.

Baada kimya kirefu kilichoambatana na kutafakari maelezo hayo, Bon alisema, “mtakumbuka tarehe 21 machi, siku ambayo yalitokea mauaji ya kikatili katika kitongoji cha Langa. Siku mbili baadaye niliweza kujipenyeza na kuingia Afrika kusini. Wakati huo wazalendo walikua wamepamba moto wakiwaua polisi wa kiafrika waliomo katika jeshi la polisi makaburu. Mimi na watu wetu walio ndani ya Afrika kusini tuliweza kumpata mmoja wa polisi weusi aliyekuwa anakimbia. Kabla wazalendo hawajamfikia sisi tulimkimbiza na kumshika. Lakini tulimfanya asituogope kwani tulimridhisha na akaamini tulikua upande wake. Tulimchukua na kumficha.

“Tulipomwuliza maswali alitwambia kuwa watu weusi walikuwa hawajui kwamba Makaburu walikuwa hawawezekani. Kwamba weupe walishaamua kuua weusi bila kujali mpaka ghasia ikome kabisa. Vile vile nchi zote zinazosaidia wapigania uhuru zitakiona cha mtema kuni kwani sasa hivi makaburu walo jeshi liitwalo Gongo la chuma’ambalo halijawahi kutokea duniani. Sasa hivi jeshi hilo lipo tayari kufagia aina yeyote ya upinzani baada ya kutayarishwa kwa muda wa miaka kumi. Nakumbuka niliporudi nilileta ripoti hii. Sasa ukilinganisha ripoti yangu na maelezo aliyotoa mkurugenzi sasa hivi ni dhahiri kwamba yanaoana. Hii inaonyesha ni kwamba ni kweli Makaburu wanao mpango huo.”

“Hata mimi naafiki kuwa yaliyosemwa ni kweli,” alisema mkuu wa upelelezi wa wapigania uhuru. “Lakini kitu ambacho ni lazima kukiweka maanani ni hicho kipigo wanachotishia watakifanya. Je kipigo hicho kitafanywa wapi; lini na kwa namna ipi?”

Hapo mkurugenzi wa upelelezi wa Zimbabwe aliinua kichwa akasema, Hata mimi jambo hilo ndilo linalonipa wasiwasi maana kutokana na maneno ya jasusi tuliyemteka, nchi zetu zitaanza kushambuliwa mara tu baada ya kipigo hicho. Huenda wanataka kutupumbaza ili watushambulie wakati sisi tunasubiri watoe kipigo kwa wapigania uhuru kwanza . Hata hivyo ni lazima tupate ufumbuzi wa suala hili.”

“Mnajua kwamba sasa hivi makaburu wana wasiwasi mkubwa na wanatuogopa. Hivyo sasa hivi hawana njia yeyote ile bali kutafuta njia za kututeketeza. Uchumi wao umeanguka. Hivi juzi juzi tu wafanyabiashara wa Uingereza waliitisha mkutano huko mjini Leeds na kuwataka wafanya biashara wa Afrika Kusini wajaribu kutetea haki za wafanyakazi weusi. Waliwataka pia waibane Serikali yao ili iwaruhusu weusi kufanya biashara kwenye sehemu wanazoishi weupe. Vile vile waliwataka wapinge vikali siasa ya kibaguzi ili Waingereza waendelee kupeleka rasilimali zao huko Afrika kusini. Hivyo makaburu wamehaha kwani msimamo huo umewauma sana. Ni kama mjuavyo, mtu anayehaha anaweza kufanya jambo lolote. Hatuna budi kuwa macho kabisa kwani hali hii imewafanya makaburu kujizatiti. Sasa hivi wamebanwa sana ndani na nje”.

“Nilikuwa nikifikiri sana sasa hivi”, Bon alianza kusema na hapo hapo wale Wakuu wawili wakageuka kumsikiliza yeye. Walikuwa wanajuwa kuwa Bon alikuwa kijana mwenye akili sana na ubongo wake ulifanya kazi kama komputa. Kila lilipotokea tatizo, Bon aliweza kutoa ufumbuzi sahihi. Ndio sababu alihusishwa katika mikutano ya ngazi za juu kama huu.

“Mnajuwa kuwa mwezi ujao kutafanyika mkutano wa pekee wa wapigania uhuru wote wa Afrika Kusini huko Tanzania, baada ya ule uliofanyika mwaka 1969. Kuna uwezekano kwamba Makaburu wameshapata habari na wanajitayarisha kutushambulia huko. Maana kama wakiweza kutekeleza tishio lao hilo la kipigo, wakateketeza wajumbe wote kwenye mkutano huo. Basi hivyo wanavyojigamba itakuwa ni sahihi kabisa. Viongozi wetu wote kutoka sehemu mbalimbali duniani watakuwapo pamoja na watu wale wanaotuunga mkono”.

Wakuu wale walimwangalia Bon na kumsikiliza kwa makini.

“Bila hata kuzungumza zaidi, nafikiri Bon amesema ukweli kabisa”, Mkurugenzi alisema huku akikiri rohoni kuwa kweli Bon alikuwa kijana mwenye akili za kuzaliwa. “Hata mimi nafikiri hilo ndilo jawabu lake, asante sana Bon. Lakini kuna jambo moja, Tanzania iko mbali sana. Sijui watatumia mbinu gani?”, aliuliza Mkuu wa Idara ya Upelelezi huku akiwaangalia wale wajumbe wawili.

Akidakia haraka kujibu swali hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Zimbabwe alisema, “Usiwachezee hawa Makaburu. Wanao uwezo wa kufanya jambo lolote. Wako mbali na Tanzania ndio, lakini wakijigamba ujuwe wanao mpango madhubuti. Hivyo ni juu yetu kujiweka tayari kutekeleza jukumu letu”.

“Jibu tumeshalipata”, alipaza sauti Mkuu wa Idara ya Upelelezi. “Hakuna haja ya kuhangaisha vichwa vyetu zaidi. Lililobaki ni kwamba mimi nitaitisha mkutano wa wenzangu niwaeleze tuliyogundua. Halafu tuzungumzie nini la kufanya kabla ya mkutano huo kuanza. Makaburu wasije wakatuchezea kama watoto wadogo”.

“Hata mimi nafikiri hilo ndilo wazo la busara wazee wenzangu. Tusipochukua hatua za tahadhari tutaadhirika.” Bon alijibu huku akili yake ikiwa mbali kwani alishachekecha akilini mwake na kuona jinsi jukumu hili lilivyokuwa gumu na la hatari sana.

“Yote niachie mimi alirukia mkuu wa idara ya upelelezi. Leo hii nitaitisha mkutano ili mpango yote ya tahadhari ikamilike. Ahsanteni sana. Mimi nitawajulisha kila hatua ambayo tutafikia. Nitawapa habari zote kuhusu matokeo ya mkutano. Bon usiondoke hapa mjini. Kila wakati nataka kujua mahali utakapokuwa. Ninaweza kukuhitaji ghafla. Kuhusu wewe ndugu mkurugenzi, mimi nitakujulisha tarehe ya mkutano hapo baadaye kwani ni lazima uwepo.”

Mkutano ulifungwa na watu watatu hao wakaagana

NAIROBI

Mike Maina aliingia ofisini kwa mkubwa wake wa kazi akiwa ameshika jalada mkononi. Maina alikuwa ofisa upelelezi katika idara ya upelelezi nchini kenya. Kijana huyu alikuwa anategemewa sana na serikali ya Kenya kwa kazi yake kubwa ya kulinda usalama dhidi ya hujuma za kisiasa, kijeshi na kiuchumi. Alikwisha tokomeza mipango mingi dhidi ya serikali.

“Ehe, hebu nieleze Maina .” Mkurugenzi wa upelelezi alisema, “Ingawa nimeitwa huko Ikulu, afadhali tuzungumze kwanza ndiyo nielekee huko baadaye.”

Katika kumkumbusha mkubwa wake wa kazi, Mike alitasua midomo yake na kusema, “Unakumbuka mwaka 1981 wakati mamluki, wakiongozwa na Michael Hoare, walipojaribu kuiangusha serikali ya visiwa vya Shelisheli; halafu wakashindwa?”

“Ndivyo, kwani vipi? Wanataka kuishambulia Shelisheli tena?”

“Hapana. Unakumbuka serikali ya Shelisheli iliilaumu serikali ya Kenya kwa kuhusika; na serikali yetu ikakanusha vikali madai hayo? Unakumbuka serikali hata hivyo, ilituamuru tuchunguze suala hilo. Unakumbuka kuwa mimi ulinipa kazi hiyo?”.

“Nakumbuka sana, mike.”

Ripoti yangu ilionyesha kwamba, ingawa serikali haikuhusika, kuna watu binafsi au hata wakazi tu waliohusika. Kutokana na ushahidi tulioupata watu wengine wenye heshima wamepoteza kazi zao. Wakazi wengine hata wamefukuzwa nchini.”

“Nakumbuka.”

“Wakati wa upelelezi wetu kuna mtu ambaye tulimshuku sana. Lakini kutokana na kukosa ushahidi thabiti, hakuchukuliwa hatua. Hata hivyo jalada lake lilibaki wazi. Niliweka kijana kuchunguza mienendo yake. Vile vile nilikuwa nimemwagiza achimbe historia ya maisha yake toka kuzaliwa kwake mpaka hivi leo. Mtu huyu anaitwa Peter Gerrit. Yeye ni mfanya biashara. Anayo kampuni ya kuhudumia watalii ijulikanayo kama Kinyonga Tours and Safaris.”

“Lo, jina lenyewe linasisimua,” alisema kwa mzaha mkurugenzi.

“Sasa jana huyu kijana wetu aliniletea ripoti ambayo ilinifanya niwe na wasiwasi mkubwa kiasi kwamba lazima nikueleze. Kwa muda wote huu kijana wetu alikuwa anampeleleza mtu huyu.”

“Mtu huyu anajulikana katika idara ya uhamiaji kama Mjerumani. Vile vile Idara ya uhamiaji inayo taarifa kwamba biashara hii ya kuhudumia watalii aliianza huko huko Ujerumani. Baadae aliamua kuja kuianzisha hapa nchini Kenya. Hayo tu ndiyo wanayoyafahamu maafisa wa Uhamiaji. Lakini sisi kitu kinachotugutua ni kwamba siku ambayo askari wa kukodiwa walipovamia Visiwa vya Shelisheli, huyu Peter alikuwapo. Na wakati askari hao walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Victoria. Maana ripoti inasema Peter alikuwa uwanjani hapo. Ni baada tu ya kugutushwa na mapigano yaliyotokea pale wakati Peter alipojisalimisha kwa majeshi ya usalama ya shelisheli.

“Wakati wa kuhojiwa Peter alieleza kwamba alikuwa hapo uwanjani kusindikiza rafiki zake waliokuwa kwenye ndege ya shirika la ndege la India ambayo ilitekwa nyara. Askari wa Shelisheli walipoangalia pasipoti yake na kuona kuwa yeye ni mkazi wa Kenya na mfayabiashara ya utalii walimwachia mara moja. Wakati wa uchunguzi wetu tulipata fununu kuwa huyu Peter alikuwa kwenye uwanja wa ndege kwa nia ya kuwapokea askari wa kukodiwa. Lakini kwa kuwa tulikosa ushahidi wa kutosha, hatukuweza kumchukulia hatua, bali tulibaki tunamtuhumu tu. Wewe unajua tena jinsi mahakama zetu pamoja na serikali vinavyotaka haki itekelezwe. Heri kumwachia huru mhalifu kuliko kumwadhibu yule asiye na hatia.

“Sasa katika uchunguzi uliofanywa na kijana huyu kwa muda wa miaka yote hii. umegundua mambo yenye kututia wasiwasi. Kwanza kijana wetu amegundua kwamba Peter hakuzaliwa Ujerumani, bali yeye ni mzaliwa wa Afrika kusini. Ila mjomba wake alikuwa anaishi Ujerumani. Ndiye huyo huyo aliyemchukua Peter na kumpeleka huko. Aliishi na kukulia huko ambako alipata masomo. Alipofikia umri wa miaka ishirini alirudi Afrika kusini katika mji wa kwao wa Pietermaritzburg. Inasemekana aliisha fanya kazi kwa Michael Hoare kama askari wa kukodiwa. Baada ya hapo alipotea na kisha akaibuka huko Ujerumani. Wakati huo mjomba wake alikuwa ameanzisha kampuni ya kuhudumia watalii ambayo alijiunga nayo. Baada ya muda kitambo, ndipo akaja Kenya. Sasa unaweza kuona kuwa kuwako kwake Shelisheli hakukuwa kwa bahati tu ila kwa sababu maalumu.

“Zaidi ya hayo, kijana wetu amegundua kitu ambacho kimetia wasiwasi na pia kunifanya mimi nifanye hima . Nikwamba kwa muda wa majuma mawili sasa kumekuwa kunakuja wazungu wanaume wawili wawili kila baada ya siku tatu. Wazungu hao wanakwenda nyumbani kwa Peter huko Red hill kwenye njia ya kwenda Limuru. Kijana wetu anahisi kwamba baada ya hao wazungu kuingia nyumbani hawatoki nje tena. Wako kama watu sita sasa. Unajua kuwa analo shamba kubwa na pia nyumba kubwa. Katika shaba hilo kuna nyumba za wafanyakazi. Sasa tunajiuliza hivi: kama kweli hawa ni wageni wa kawaida, kwa nini hawaonekani angalau kutembea tembea au hata kwenda mjini? kwa nini wasithubutu hata kuzurura hapo kwenye shamba?”

“Huenda wanatembea usiku,” alipendekeza mkurugenzi.

“Kama kweli ni usiku, kwa nini usiku? aliuliza Mike.

“Nafikiri unayo sababu nzuri ya kuwa na wasiwasi. Kufuatana na maelezo yako inabidi mtu huyu apelelezwe kikamilifu zaidi kwani huenda akawa na jambo. Bali kama mtu huyu anayo mahusiano na serikali ya makaburu, yafaa apelelezwe kwa uangalifu na tahadhari zaidi. Akigundua kuwa anachunguzwa si ajabu akateleza tena kama alivyofanya hapo kwanza. Hivyo, kwa baraka zangu, nakuruhusu uendelee na kazi ya kumpeleleza ili tujuwe hasa anapanga kufanya kitu gani. Umesema kuwa kipindi fulani alikuwa haonekani na haikujulikana alikuwa wapi. Basi ni dhahili kuwa anaweza kuwa jasusi wa makaburu ambaye alikuwa mafunzoni. Hapa inawezekana kaja kikazi, kwa hiyo chunga sana mtu huyu kwani anaweza kuwa hatari|”.

“Asante. Nitafanya hivyo na kisha nitakujulisha maendeleo ya kila siku”.

Mike Maina alichukuwa jalada na kutoka nje ya ofisi ya mkubwa wake.

Mike alipofika ofisini kwake alimwambia Katibu Muhitasi wake amuite kijana Mwaura. Kwa muda wa miaka yote hii Mwaura ndiye alikuwa akimpeleleza Peter.

“Mwaura”, Mike alisema mara Mwaura alipoingia ofisini kwake. “Nimezungumza na Mzee na tumekubaliana kwamba tuendelee na upelelezi wetu. Sasa nitakuongezea vijana wengine na ninataka ripoti juu ya maendeleo yote ya mtu huyu, kila kitu atakachofanya, na mahali atakapokwenda”.

“Nashukru sana, Bosi”. Mwaura alijibu. “Nafikiri ukinipa vijana wawili, kama vile Onyango na Kipukoachi, kazi itafanyika vizuri”.

“Maombi yako yatatimizwa mara moja, unafanya kazi nzuri Mwaura. Kuna haja ya idara kufikiria kuongeza maslahi yako”.

“Asante sana, Bosi, kazi kwanza”.

“Ningependa kazi hii ianze mara moja leo hii na mhakikishe kwamba Peter hapati mwanya wa kufanya jambo lolote dhidi yetu”, alisema Mike.

“Kitu ambacho nimekosea bosi ni kwamba tangu asubuhi sikuweka mtu wa kuendelea na uchunguzi juu ya maendeleo ya mtu huyu. Katika muda huu wa masaa tisa huende amefanya majambo”, Mwaura alijilaumu.

“Tusililie maji yaliyomwagika. Kuanzia sasa hivi fanya kazi kama kawaida”.

Wakati Mike anazungumza na Mkurugenzi wa Upelelezi, ofisini mwa Peter Gerrit, katika mtaa wa Koinange, ambako ndiko yaliko Makao ya Kinyonga Tours and Safaris, simu ya siri ilikuwa ikilia. Simu hii ilikuwa inajulikana na watu wachache sana. Kila simu ilipokuwa inalia moyo wa Peter ulishtuka kidogo.

“Hallo, Peter hapa,”Peter alisema mara baada ya kuunyakua mkono wa simu na kuupachika katika sikio lake la kulia.

“Masoga hapa,” upande mwingine wa simu ulimwitikia.

Masoga alikuwa ni afisa mwingine katika kurugenzi ya upelelezi. Lakini alikuwa kwenye orodha ya kulipwa na Peter Gerrit. Masoga alikuwa ni msaliti wa serikali ya wananchi wa Kenya kwa sababu ya tamaa ya pesa. Hivyo alikuwa anampa habari muhimu sana Peter ambazo alikuwa anzitumia dhidi ya wanamapinduzi wa Afrika.

Wajati Mwaura alipokuwa anamweleza Mike asubuhi ile jinsi alivyokuwa na wasiwasi juu ya wageni waliokuwa wakiingia nyumbani kwa Peter, Masoga alikuwa amepitia ofisini kwa Mike akiomba ruhusa kwenda nje. Na kwa vile hawakuwa na wasiwasi nae, Mwaura aliendelea kueleza wasiwasi wake kuhusu Peter Gerrit na wageni wake. Ndipo Mike aligeuka na kutaka kujuwa Masoga alikuwa na shida gani. Lakini Masoga alikuwa amesikia sehemu ya mwisho ya taarifa ya Mwaura juu ya wazungu walikuwa wakienda kwa Peter.

“Ehee, kuna nini?. Peter aliuliza kwa sauti kali.

Masoga alikuwa anapiga simu kwenye kibanda cha posta kando ya posta kuu, alisema, “Kuna habari ofisini kwetu kuwa unao wageni nyumbani kwako ambao wanaingia tu lakini hawatoki, idara yetu inao wasiwasi, vipi?”.

Bila kujua umuhimu wa habari alizokuwa akizitoa kwa Peter, Masoga alitabasamu.

“Wana wazimu! naona sasa idara yenu haina kazi ya kufanya. Mimi sina wageni wa namna hiyo. Kama wana wasiwasi, kwanini wasije kuona?”. Hivi ni nani anasema maneno hayo?”, Peter aliuliza kana kwamba hajali kitu ingawa kwa kweli moyo wake ulikuwa ukidunda vibaya kwa hofu aliyokuwa nayo.

“Kijana mmoja anayeitwa Mwaura”.

“Acha nae”. Peter alimjibu. “Huenda anapalilia cheo”.

“Huenda. Lakini mimi niliona ni vizuri kukwambia.

“Hivyo ni sawa. Lakini hakuna chochote wala usiwe na wasiwasi. Hata hivyo, asante. Njoo umuone Kanabhai. Utakuta anayo bahasha yako.

“Asante”, alijibu Masoga huku anasikia raha alipojuwa kuna bahasha yake.

Baada ya Peter kuweka simu chini, alianza kufikiri. Alikuwa ameshangazwa na habari hizi kwani hakutarajia kabisa kuwa idara ya upelelezi ya Kenya ilikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa kiwango cha juu kiasi hicho. Ni kweli kwamba Peter alikuwa na makomandoo maarufu kumi na wawili nyumbani kwake kutoka kwenye jeshi hatari la makaburu liitwalo KULFUT. Watu hawa walikuwa wameingia nchini Kenya kwa siri na ni yeye aliyetayarisha mpango huo. walikuwa wameingia nchini Kenya kupitia Mombasa. Walisafiri kwa mashua mpaka kwenye Bandari ya Mombasa baada ya kushushwa katika Bahari ya Hindi kutoka kwenye Meli moja ya makaburu walikuwa wamefika kwenye ufuko wa Nyali walipojifanya wao ni watalii waliokuwa wakicheza tu na mashua. Peter alikuwa ametayarisha kila kitu.

Akitumia wadhifa wake kama mfanyabiashara wa kuhudumia watalii, aliweza kuwasafirisha. Awamu kwa awamu, hadi Nairobi. Aliamua kutowasafirisha kwa mkupuo ili asije kugutukiwa. Hivyo watu hawa walikuwa nchini Kenya kinyume cha sheria. Idadi yao ya watu kumi na wawili kuwa yenye nguvu sawa na kikosi kizima cha jeshi. Vile vile walikuwa wamepewa mafunzo ya kila aina kuhusu kuua. Wawili kati ya hao walikuwa NINJA. Ninja ni mtu aliyehitimu mafunzo ya pekee ya karate na kung fu huko Ujapani na Korea. Kuelezea ninja kwa kirefu inaweza kuchukua siku nzima. Hivyo ridhika na ukweli huu kwamba ninja anakuwa amejifunza zaidi ya njia elfu moja za kuua. Mtu mmoja anaweza akakiangusha kikosi kizima. Ni watu wachache katika ulimwengu huu ambao wamehitimu mafunzo hayo. Askari jeshi mia moja na silaha zao hawawezi kufua dafu kwa ninja mmoja.

Makomando hawa wa makaburu walikuwa bado kufika mwisho wa safari yao. Walikuwa wanaelekea Tanzania. Hivyo kama wangegutukiwa bado wakingali Kenya, Peter angepata matatizo makubwa kutoka kwa wafadhili wake. Hivyo ilibidi abadili mpango haraka ili aweze kuingia Tanzania ambako ndiko walikuwa wakafanye kazi. Peter aliendelea kujifikiria yeye mwenyewe. Yeye pia alikuwa ni komando katika jeshi la KULFUT kwenye kikosi cha ujasusi. Alikuwa amehitimu kila aina ya mafunzo ya upiganaji na ujasusi. Alikuwa ameletwa Kenya kusubiri wakati wake wa kufanya kazi. Alikuwa tayari kufanya kazi wakati wowote alipohitajiwa na wakubwa wake. Na wakati huo sasa ulikuwa umewadia. Wakubwa zake Peter walikuwa wameamua kufanya kazi sehemu hii ya Afrika mashariki.

Kila wakati alipofikiria mpango huu na utekelezaji wake, Peter alisisimkwa na damu. Alikuwa amefikiri sana juu ya siasa za nchi huru za afrika na kuona vyema kuzitokomeza ili Afrika kusini iweze kulitawala bara zima la Afrika. Aliamini kabisa kwamba mtu mweusi hakuwa na haki ya kujitawala. Mtu mweusi alipaswa kuwa mtumwa wa wazungu. Kwake Peter mtu mweusi alikuwa kama paka au kwani hata mbwa anayo thamani. Mara nyingine alishangaa aliposikia mtu mweusi anazungumza neno la busara. Kwake yeye kama makaburu na pia kufuatana na walivyofunzwa na kulelewa, aliona mtu mweusi kama kitu kisichokuwa na thamani yoyote. Kwa sababu hiyo Peter alisisimkwa damu alipofikiri kuwa yeye mwenyewe angeshiriki kuwaangamiza watu weusi katika nchi zao ambazo walidai ni huru.

Ili mipango yake isije ikaharibika, Peter aliinua simu akazungusha namba kazaa, kisha kusubiri kuitikiwa.

“Hallo, hapo ni Arusha ?” Peter aliuliza baada ya kuitikiwa.

“Ndiyo. Habari gani, P. G.?”

“Nzuri, F. K.”

“Mipango imebadilika. Tungoje mpakani saa mbili usiku. Naamini mipango yote iko shwari mpakani.”

“Nimeisha suka kila mpango kama tulivyozungumza. Hakuna tabu kamwe.”

“Ahsante F. K.”

“Ahsante P G.”

F. K

“Nyoka Tours and Safaris,” Tondo aliitika kwenye simu.

“Njoo nyumbani haraka.” Tondo alisikia sauti ya tajiri wake ikimwamrisha.

“Sawa mzee,” aliitika kwa unyenyekevu.

Tondo aliweka simu chini na kuinuka. Bila hata kuaga alielekea kwenye gari lake ili aende kwa tajiri yake. Alipoangalia saa yake aliona inaonyesha saa nane na nusu mchana.

Chris Tondo alikuwa meneja mkuu wa kampuni ya Nyoka tours and Safaris ya mjini Arusha ambayo ilikuwa ni mali ya Mhindi mmoja. Mhindi huyo alikuwa anajulikana kwa jina la Firozali Kassam na watu wengi walimwita F. K. Yeye alikuwa tajiri sana. Alikuwa akiishi sehemu ya Them Hill ambako alijenga nyumba kubwa sana ambayo mashabiki waliita “White House” au Ikulu ya Arusha.

F. K alipendwa sana na wakazi wa Arusha kutokana na tabia yake ya kuwasaidia watu wenye uwezo mdogo wa kipesa. Alikuwa mtu mkarimu sana. Inasemekana nusu ya teksi zote za Arusha zilinunuliwa na wenyewe kwa mkopo usio na riba kutoka kwa F. K. Inasemekana kuwa alifuta madeni mengi ya watu walioonekana hawana uwezo wa kulipa. Ingawa hakuwa muumini wa dini ya kikristo, F. K alisaidia kujenga makanisa mengi ya madhehebu mbalimbali mjini Arusha.

Kwa muda mrefu F.K alikuwa mstari wa mbele katika kusaidia Chama na serikali katika mkoa huo, kufanya shughuli zake nyingi. Inasemekana. Kwa mfano alichanga pesa nyingi kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya chama cha mkoa. Hivyo alipewa heshima kubwa sana na wakuu wa chama na serikali hapo mkoani Arusha. Kusema kweli kama angetokea mtu akasema kwamba F.K alikuwa ni mtu mbaya, basi angeuawa kwa kupigwa mawe hadhalani.

F.K alijulikana kama mtu wa watu, raia mwema na mpenzi wa watu wa rika zote. Alikuwa mtu maarufu na murua. Watu wote walimwelewa hivyo. Sifa zake zilizidi kuvuma kwani F. K alikuwa mfadhili, asiyebagua mtu awe mweupe au mweusi, masikini, fukala au tajiri. Watu wote mbele ya F.K walijiona sawa. Huo ulikuwa upande mmoja tu wa F.K.

Lakini F.K alikuwa na upande mwingine ambao ni watu wachache sana walioujuwa. Hata mtu kama Chris Tondo nae alimjuwa F.K juu juu tu.

F.K alikuwa mzaliwa wa Dar es Salaam, Tanzania, baba yake alikuwa mfanyabiashara maarufu sana Jijini Dar es Salaam, alikuwa na maduka makubwa matatu ya vipuri vya magari na alikuwa wakala wa makampuni mengi ya nchi za nje hapa Tanzania. Hivyo huyo mzee Kassam alikuwa tajiri sana. F.K alizaliwa mnamo mwaka 1945. Baada ya kusoma shule ya msingi hapo nchini, baba yake alimpeleka Uingereza ambako alipata elimu ya sekondari na chuo kikuu. Hii ilitokana na kwamba baba yake alikuwa na uwezo wa kumlipia F.K ada ya shule.

Mnamo mwaka 1967 serikali ya Tanzania ilitaifisha makampuni makubwa ya watu binafsi na kuyaweka katika mikono ya wananchi. Hatua hiyo ilifuatia kutangazwa kwa siasa za ujamaa na kujitegemea katika Azimio la Arusha. Mnamo mwaka 1972 serikali ilichukuwa hatua nyingine zaidi. Majumba makubwa ya watu binafsi yaliyaifishwa vilevile.

Wakati huo F.K alikuwa anasoma chuo kikuu huko Uingereza. Baba yake alimpigia simu na kumweleza mkasa uliokuwa umewapata nyumbani. Alimfahamisha kuwa nyumba zao therathini ambazo walikuwa wamejenga na nyingine kununua vile vile zilikuwa zimetaifishwa. Aliposikia vile F.K alipatwa na wazimu. Aliilaani serikali kiasi ambacho hajapata kusikia.

Siku hiyo jioni alienda kwenye baa na kuchapa mtindi barabara. Mara alisikika akiapa, “Naapa kwa jina la Mungu, kuna siku nitalipiza kisasi dhidi ya serikali ya Tanzania”, Kwa bahati mbaya au nzuri katika baa ile kulikuwemo jasusi mmoja kutoka Afrika Kusini lililokuwa kwenye shughuri zake lenyewe. Liliposikia hivyo lilikumbuka kuwa shirika la ujasusi la Afrika Kusini lilikuwa linamtafuta mtu raia wa Tanzania ambaye angelifanyia kazi ya kijasusi huko.

Hivyo ndivyo alivyopatikana F.K na kuwekwa katika orodha ya kulipwa na shirika la ujasusi la Afrika Kusini. Pamoja na kulipwa ili afanye kazi ya ujasusi, F.K aliahidiwa kuwa angepewa msaada kulipiza kisasi dhidi ya serikali ya Tanzania. Inasemekana kuwa baadae alipotea kwa muda wa miaka mitatu na haikujulikana mahali alipokuwa. Lakini habari zilisema kuwa alikuwa huko Afrika Kusini akipewa mafunzo ya kijasusi kwenye makambi mbali mbali.

Aliporudi Tanzania alikuta wazazi wake wako kwenye pilikapilika za kuhama na kwenda Canada F.K alikataa kuondoka na wazazi wake na kusema kwamba yeye alikuwa mzaliwa wa Tanzania hivyo hakuwa na sababu ya kuihama nchi yake na kwenda nchi nyingine. Hivyo familia yake ilimugawia sehemu ya mali iliyobaki naye akaamua kuhamia mjini Arusha. Huko ndiko alikoanzisha kampuni yake ya kuhudumia watalii iliyojulikana kwa jina la nyoka tours and safaris.

Alichagua jina hilo kwa sababu alizozijua mwenyewe. Mabwana zake walimpa fedha nyingi ambazo alizitumia kufanya mambo niliyoyaeleza na pia kujenga white house. Kutokana na utajiri wake F.K aliweza kuisarti nchi bila mtu yeyote kumshuku. Fedha zake ziliwafumba watu macho. Nyumba hiyo iliyoitwa White House ilikuwa imejengwa kwa aina yake. Ilikuwa imejengwa kwa shabaha ya kufanya ujasusi. Nyumba hiyo ilikuwa na vyumba vingine chini ya ardhi. Kulikuwa na barabara kadhaa chini kwa chini ambazo zilitokea nje ya sengenge ilizunguka ekali kumi na mbili za kiwanja cha nyumba hiyo.

F.K alikuwa hajaowa wala kuwa na watoto. Hivyo aliishi katika nyumba hii peke yake. Watumishi wake waliishi kwenye nyumba kando kando ya jumba lake. Kwa muda wote huo F.K alifanikiwa kujenga kwa nje, akaonekana kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo. Alionekana mzuri kwa nje lakini alikuwa hatari kwa ndani.

Dhamila yake kubwa ilikuwa ni kulipiza kisasi. Kwa kufanya hivyo F.K angekuwa amefanya kazi katika upande wa adui namba moja wa Afrika huru na Ulimwengu mzima kwa ujumla. Hii ndiyo ilikuwa upande wa pili wa F.K ambayo ilikuwa sura yake halisi.

Chris Tondo ambaye sasa alikuwa anaelekea Themi Hill ndiye aliyejuwa F.K hakuwa mtu mzuri kama watu wengine wa mjini Arusha walivyoamini. Yeye Tondo walikuwa wakionana na kufahamiana kiajabu. Tondo alikuwa na umri karibu sawa na F.K. Walionana mara tu baada ya Tondo kustaafishwa kutoka Jeshi la Polisi kwa manufaa ya umma. Alikuwa tayari amefikia cheo cha Kamishna Msaidizi, akiwa kati ya waafrika wa kwanza kufikia ngazi hiyo. Tondo alichukulia kustaafishwa kwake kama kitendo cha fitina na hivyo alikuwa na chiki dhidi ya serikali. Aliamini kuwa alionewa wivu kwani alikuwa na nafasi nzuri ya kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba huyu Chris Tondo alikuwa akitumia cheo chake kusaidia wahujumu uchumi. Aliwasaidia kutorosha vipusa vyote vya thamani kwa njia ya magendo. Alipostaafishwa jina lake lilitolewa kwenye magazeti ya kila siku. Kwa njia hiyo F.K ambaye alishaambiwa habari za Tondo na wale wahujumu aliowasaidia, alijuwa kuwa amepata mtu aliyekuwa akimuhitaji. F.K alijuwa Tondo hakuwa mwaminifu kwa serikali. Vile vile alishakuwa mtu mkubwa na hivyo mwenye uzito katika jeshi la polisi. Huyu ndiye mtu aliyefaa katika mpango wake waliokuwa nao F.K pamoja na wafadhili wake.

Siku moja F.K alimfuata Tondo Jijini Dar es Salaam. Alimdanganya kwamba kuna mtu amemwelekeza kwake. Alimwambia kuwa kama ingewezekana alipenda wafanye kazi pamoja kwa kuwa hakuwa na kazi. Bila kusita Tondo alikubali akaona ni bahati iliyoje. Siku hiyo Chris Tondo alimweleza jinsi alivyoichukia serikali ya Tanzania akidaiwa kuwa ilimstaafisha bila sababu ya msingi.

“Wewe tulia tu, kuna siku mtu atalipa”, F.K alimhakikishia.

Baada ya kusikia maelezo ya Tondo, F.K alijuwa amempata mtu aliyekuwa akimtafuta. Tondo aliteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Nyoka Tours and Safaris. Kusema kweli kampuni hiyo ilikuwa ni kisingizio. Mambo ambayo F.K na Tondo walifanya kwa siri katika kuhujumu uchumi aliyejuwa ni Mungu peke yake.

Tondo alisimama na kuegesha gari nyumbani kwa F.K. F.K alifungua mlango na kumkaribisha ndani Tondo.

“Karibu ndani.

“Asante”, alijibu Tondo.

“Nimekuita ghafla kwa sababu nimepata habari sasa hivi kutoka kwa yule rafiki yangu wa Nairobi kwamba wale wageni waliokuwa wafike kesho wataingia leo jioni. Kitu ninachotaka ufanye ni kwenda kubadiri mipango huko mpakani. Kama nilivyokuwa nimekueleza awali, watu hawa wataingia bila kupitia sehemu za kawaida. Wageni hao wanayo mizigo ambayo sitaki ikaguliwe wala wao wasionekane na mtu yeyote”, alieleza F.K na kisha akaelekea kwenye chumba fulani. Aliporudi alikuwa amebeba pasporti kumi na mbili na bahasha moja.

“Pasporti hizi ni za hawa wageni. Nenda nazo huko mpakani kwa mtu wetu akugongee mihuri ya idara ya uhamiaji. Unajuwa ni siku nyingi hatujaangalia maslahi yake. Hivyo mpelekee hii bahasha yake”.

F.K alimkabidhi Tondo hivyo vitu.

“Aidha nenda kwa Hasanali mwambia kuwa wale wageni watakwenda nyumbani kwake kwa kupitia njia ya porini mnamo saa mbili usiku. Mimi nitafika hapo kuwachukuwa mnamo saa mbili na nusu usiku, na yeey tuonane hapo. Kazi ifanyike kama kawaida Tondo”.

“Sawa nitatekeleza yote kama ulivyosema”.

Tondo alibeba mzigo wake akaelekea nje huku akisindikizwa na mwenyeji wake.

Wakati akielekea nyumbani kwake alifikiri kwamba wakati mwingine mambo waliyofanya yalikuwa ya ajabu kama sasa alishangaa alipoona F.K anazo pasporti za watu ambao walikuwa bado kuingia nchini hata hivyo Tondo alijuwa haikuwa juu yake kuuliza maswali. kazi yake kubwa ilikuwa utekelezaji.

Tayari alikuwa amejenga nyumba tatu. Nyumba moja ilikuwa Dar es Salaam na aliipangisha kwa Ubalozi kwa elfu hamsini kwa mwezi. Nusu ya kodi hiyo Tondo alilipwa kwa fedha za kigeni. Nyumba nyingine alikuwa amejenga nyumbani kwao Njombe ambayo kwa viwango vya huko nyumba hiyo ilikuwa ya hali ya juu. Nyumba ya tatu ni hiyo aliyojenga Arusha. Tondo alikuwa hajawahi kuoa lakini alikuwa na watoto watatu aliowapata nje ya ndoa. Watoto wake wawili wakubwa walikuwa wanasoma shule ya msingi huko London, wakati yule mdogo alikuwa anakaa na mama yake huko Njombe.

“Tangu nistaafishwe na kuungana na F.K mafanikio yangu yamekuwa ya makubwa kuliko ya mtanzania wa hali ya juu. Kweli kazi hii inanifaa shauri yao watanikoma”, Tondo alijisemea kimoyomoyo.

Mara alikutana na gari lilimumulika kwa taa zake. Kabla ya kupishana alitambua ni Nyaso, hivyo akapunga mkono, Nyaso naye akampungia mkono pia.

Nyaso alikuwa ni msichana mrembo sana. Hapakuwepo msichana mwingine mjini Arusha ambaye wangeweza kushindana naye kwa urembo. Nyaso alikuwa hawala yake F.K. Watu waliojuwa penzi lao walisema kuwa Nyaso alikuwa saizi ya F.K kutokana na utajiri wake. Bali tu walishindwa kufahamu kwanini hawakuoana. Hata hivyo rafiki zake na F.K ndoa ingekuwa kinyume cha mila za wahindi. Kwa kuamua kuishi na Nyaso kama hawala kulionyesha watu unafiki wa F.K na Wahindi wengine. Waliopenda kufanya mapenzi na waafirika lakini ilikuwa mwiko kuwaoa. Wahindi walitembea na wasichana wa kiafrika na baadaye kuwatupa jalalani.

Kila wakati Tondo alipofikiria uhusiano wa watu hawa wawili aliona kuwa Nyaso hakumhitaji sana F.K. Alijuwa msichana yule alitaka pesa zake tu. Hii ilionyeswa na majibu ya mkato aliyompa F.K mara kwa mara. Lakini hata hivyo F.K alikuwa amemjengea Nyaso nyumba nzuri sana. Nyaso alikuwa haruhusiwi kwenda kwa F.K. Hivyo F.K alikuwa akienda kulala kwa Nyaso. Hata Tondo hakujuwa kwanini F.K hakupenda Nyaso aende kwake bali alilidhika alipoambiwa na F.K kwamba hiyo ingekuwa kukiuka mila za Kihindi.

“Acha mtoto wa Kitanzania amule kidogo Mhindi huyu”, Tondo alijisemea.

Aliegesha gari yake nyumbani kwake halafu akajitayarisha kwa safari ya kuelekea mpakani.

Wakati Mike anazungumza na Mkurugenzi wa Upelelezi, ofisini mwa Peter Gerrit, katika mtaa wa Koinange, ambako ndiko yaliko makao ya Kinyonga Tours and Safaris, simu ya siri ilikuwa ikilia. Simu hii ilikuwa inajulikana na watu wachache sana. Kila simu ilipokuwa inalia moyo wa Peter ulishtuka kidogo.

DAR ES SALAAM

Jijini Dar es Salaam, Tanzania, siku hiyo watu walikuwa wanasherehekea Sikukuu ya Iddy El Fitri kwa hoi hoi na vifijo. Mchana huo watu walikuwa wamejaa katika hoteli ya Kunduchi. Baadhi yao walikuwa wanaogelea, wakati wengine wakitafuna na kula vitu laini. Watu wengine walikuwa wanacheza disco la mchana. Vile vile kuna wale ambao walibaki nyumbani kwa kujuwa wangekosa nafasi kwani hoteli ya Kunduchi ilikuwa imejaa kibati.

Nje ya hoteli hiyo, karibu na ufukwe, kulikuwepo na meza moja kubwa. Kwenye meza hiyo walikaa vijana wanane. Wanaume wanne na wasichana wanne hii ina maana kuwa kila mtu alikuwa na kitu chake. Wote hawa walikuwa wamefika kusherehekea Iddy pia. Walikuwa wamekaa wakibishana huku wanauchapa mtindi. Wakati huo walikuwa wanabishana juu ya siasa ya ujamaa nchini Tanzania.

“Mimi nawaambieni, hii siasa ndio inayoturudisha nyuma. Mbona kabla ya siasa hii mambo hayakuwa hivi?”, Eddy aliuliza.

“Lakini nchi nyingine zina shida vile vile”, alijibu Khadija, “Siyo. Sisi peke yetu”.

“Shida za nchi nyingine siyo kama zetu. Ukienda nchi za jirani, utaona wana kila kitu. Kwanini?, kwa sababu hawana siasa hii, bwana. Tusidanganyane”, Eddy alisisitiza.

“Hata mimi nakubaliana na wewe Eddy”, Rashid aliunga mkono.

“Mimi nilikulia kijijini. kulikuwepo mabasi manne kila siku, lakini juzi nimekwenda huko sikukuta basi hata moja. nilitembea kwa miguu umbali wa kilometa arobaini. Hivi sasa sina hata hamu ya kwenda likizo nyumbani”.

“Sikilizeni jamani”, Esther alianza kutoa nasaha zake, “Dunia nzima ina matatizo. Mimi naamini siasa yetu ni nzuri, ila kuna mahali ambako makosa yamefanyika. Mnajuwa kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Inawezekana siasa hii imeleta madhala ya kiuchumi, lakini tumefaidika kwa upande mwingine watanzania tumekuwa watu wanaopendana na kuheshimiana. Tunao umoja, na mtu mkubwa hamnyanyasi mdogo. Hatuna ukabila. Katika nchi nyingine mnazozungumzia, kama wewe ni mtu mdogo kama sisi wengine hapa unaonekana huna thamani hata kidogo. Achani jamani, siasa hii imetuletea hadhi na haki kwa kila kitu”.

“Kwenda zako! wewe utakula au kuvaa heshima?, hii siasa inatuumiza, bwana, acheni”, alijibu Rukia kwa hasira.

Mmoja wa vijana hao aliyekuwa anasikiliza maendeleo ya mabishano alimwemwesa, kisha akasema, “Rukia, usikasilike. Hapa tunazungumza tu na kila mtu anatoa mawazo yake. Hivyo poa mtoto, ngoja mimi niwaelezeni jinsi nyinyi mnavyobishana bila msingi. Mnajuwa, kama mtu anataka kubishana juu ya jambo fulani, lazima alielewe kwa undani jambo lenywe. Kila mtu hapa anasema ujamaa ndio umeleta hali ngumu. Lakini hali hiyo imesababishwa vipi na siasa hii?”.

“Haya basi, tueleze kama unafahamu”, Sammy alichokoza. “Wewe si unajiita mchumi?”, Kwanza nyinyi mliosomea uchumi ndio mnatoa ushauri mbaya kwa wanasiasa hapa nchini”.

Hapa vijana wote waliangua kicheko.

ITAENDELEA

Hofu Sehemu ya Pili

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment