LYRICS

Rapcha – Lissa Lyrics

MP3 DOWNLOAD Rapcha - Lissa
Rapcha – Lissa Lyrics

Tanzanian fast-rising Hip Hop and Bongo record artist, Cosmas Paul Mfoy is professionally known as Rapcha, dropped another banger titled Lissa. Below is the Lissa Lyrics written and performed by Rapcha,

Lissa Lyrics by Rapcha

Tongwe records… please
Bin Laden

Saa sita ya mchana jua la utosi
Chuo bumu limetema nimekaa kibosi hata presha ya msosi sina
“Somebody is calling” oh kumbe Lissa
Nimem-save, “Love of my life”
Nikaweka na loudspeaker nikamsikia ka anaongea akiwa analia
Nikamuuliza, “Are you okay Monalisa”
Akaniambia, “Baby siko sawa kabisa, nadaiwa ada
Na jumatatu ndio tunaanza paper yanii
Na nisipolipa siruhusiwi kufanya mitihani
Laki tano nzima ntaitowa wapi honey?”

“Oh don’t you worry nali-fix boo”
Kwa kuwa nishadaka hela ya bumu nikalibeba hilo jukumu
Nikamwambia, “Basi nakutumia usikate simu kwanza love ili uniambie ikiingia
Mh, baby mbona hii number inajina la kiume?”
Akaniambia, “Hiyo laini kaka yangu alinisajilia”

“Laki tano kwenda kwa Lisaa bonyeza moja kuthibitisha mbili kubatilisha”
Mi nikathibitisha
Laki tano na elfu tano na makato ya kutoa
Kwenye account yake pale pale ikathibitisha
She was like, “Thanks baby nimeiona jioni jua likipoa nitakuja kwako kukuona
And for real nimekumisi kinoma”
Nikamwambia, “nitafurahi sana kama nitakuona” “Ok”

Saa kumi na moja mtoto hajatimba!
“Labda ndio anatoka home acha nivunge midamida anafika”
Saa moja kamili mtoto hajatimba!
Nikasema, “Huenda foleni kubwa ila punde tu atafika”
Saa tatu usiku mtoto ajatimba giza limetinga
Nishampigia sana simu hapokei text zinadunda
Nkawaza mpa usingizi ukanichukua
Siku ya pili, simu hapokei text hajafungua
Siku ya tatu kimya nikasanuka nimcheki best yake
Huwezi amini nilijuta kumpigia

Nikamwambia, “Hey shem you good” “I’m good”
Siku ya tatu best yako kanilia buyu
Now days Lissa mbona anama-drama huyu
Akaniambia, “Shem kama unakifua ntakwambia
Ah kweli lisa ame-change anabwana mpya msanii huyo ndio anam-drivecrazy
Juzi si ulituma hela ya ada alipokulilia, hiyo ela kampa bwana wake akatumie”

Dah maumivu huwa makali ukimpa kitu mtu umpendae akampatia ampendae zaidi
Magoti yaliniisha nguvu chozi chini, mbupu ndicho
Roho iliniuma sikufichi
Dah nikaondoka home kwa hasira nimfate Lissa
Kwani jealous inanitesa na kila nikimuwaza naona kama dereva anautani na mimi
Daradara niliona inaenda taratibu nilitamani nikaiendeshe mimi

Nikafika mpaka kwa Lissa ile naukaribia mlango
Naskia mziki ila kunasauti naona kama sizielewi
Nikaona siwezi gonga mlango, nikapita nao na teke mpaka ndani
Nilichokiona sitasahau maishani
Kidume kinamkazia kitanda ndani
Ye bize analia machozi hayatoki anaifinyia ndani
Hata wa kushtuka wamuhofie nani!?
Jamaa akapiga tako nane akamwagia ndani

Nilipata kizunguzungu nusu nianguke
Sikuweza kuamini, “Lissa mbona umenitenda hivi nimekukosea nini?
Si ungeniambia tuachane ningekuacha huru
Mwisho wa siku ningepona, sasa haya yote ya nini?”

Lissa akanibadilikia sura mpaka sauti akani-changea
Akaanza kunitimua huku na matusi ananishushia
Ye na bwana wake wakaanza nipush mpaka nje
Aknipigia kelele, “Mwizi” watu wakanijazia
Watu wakanijali wameshika mawe na marungu
Wakanipiga kama mwizi huo mtaa sina ndugu

Jamani tunaua hatu-ui (tunaua)
Shehe tuache tushammaliza (hapana sheria hairuhusu)
Tena mimi mama nimesahau nini nnapresha mtanilimia, mtanilimia presha

Hakuna wa kunitetea, wakanivika tairi ya gari
Wakawasha moto fasta nikaanza teketea
Na maumivu ya moto ndio haya
Walioniunguza moyo wameuteketeza mwili vibaya
Sekunde chache za kuivuta pumzi ya Dunia nzuri
Iliojaa binadamu wengi wabaya
Sawa Lissa nakuacha ufurahi
Mapenzi niliokuonyesha umeamua kunitoa uhai

Ahadi tulizoweka zimezimwa na tamaa zako
Mi nnakwenda karma itakulipa bye bye uh
Bin Laden

Rapcha – Lissa Mp3 Download

Check More Hits Song From Rapcha;

Leave a Comment