LYRICS

Goodluck Gozbert – Nyakati Lyrics

MP3 DOWNLOAD Goodluck Gozbert - Nyakati
Goodluck Gozbert – Nyakati Lyrics

Tanzanian Gospel artist and “Shukrani“ hitmaker, Goodluck Gozbert is back with another stunning banger titled Nyakati. Below are the Nyakati Lyrics written and performed by Goodluck Gozbert.

Nyakati Lyrics by Goodluck Gozbert

Hao… hao…
Hao… hao…
Hao… hao…
Hao…

Unaona kama kila unachogusa kimeharibika
Ujasiri wa kusema tena umetoweka
Maana kila unalosema wewe kama unakosea
Umechanganyikiwa ni Mungu ajua unayopitia

Na ukisema ueleze wengi kwao ni furaha
Wewe mwombe Mungu ubaki kimya
Na mengi umevumilia, moyo umenyong’onyea
Hapo ulipo sasa ng’ang’ania tena

Na Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako
Imani nusu ongeza utashinda.

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe

Moyo wako una majeraha haufaiii
Tena unasubiri kauli ya mwisho ya Mungu
Wapo wanaojua we huna mtoto
Kwa kejeli wanaulizaga ana umri gani

Tena wanaojua umefukuzwa kazi
Kwa kejeli wanaulizaga bosi wako yupo
Ila nakwambia hayatodumu ni nyakati tu
Hautobaki hapo hayo ni mapito

Jipe moyo tazama juu, mwombe Mungu Ujasiri,
Ni mapito tu jipe moyo mkuu
Japo huna nguvu yakumwomba mwishie Mungu
Ni mapito tu jipe moyo mkuu

Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako,
Imani nusu ongeza utashinda
Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako,
Imani nusu ongeza utashinda

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yupo nawe
Wewewe

Hata wakizusha maneno ya uongo wakakwambia umemwasi Mungu,
Ni sawa hawajui unakopita
Wakaja na unabii wakasema umefika mwisho wako wee,
Ni sawa hawajui unakopita.
Ooh wakainuka ndugu wa karibu wakakusema hovyo hovyo hovyo hovyo,
Ni sawa hawajui unakopita.
Ikawa kila kitu ni kimya marafiki ni kimya
Ni sawa hawajui unakopita
Kama ndoa ni yako lakini ndani ni uadui
Ni sawa hawajui unakopita
Ilaaa,

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe

Si kwa nyakati za furaha
Nawe utacheka tena
Usijali Mungu yuko nawe

Goodluck Gozbert – Nyakati Mp3 Download

Other related tracks from Goodluck Gozbert;

Leave a Comment