Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela
SIMULIZI

Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela

Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela
Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela

Washirika wa Chapo walimuona Emma kama ni msaliti baada ya kutapika ukweli wote huko mahakamani kuhusiana na biashara haramu za mumewe El Chapo. Kwa kuiona hatari hii walikubaliana isomwe hukumu ‘ya mchongo’ isiyozidi miaka 10 kwani akiwa gerezani anakua salama.

Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela
Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela

Emma ni nani “Emma Modesta Coronel Aispuro ni malkia wa zamani wa urembo wa Kimarekani. Anajulikana kwa kuwa mke wa Joaquín “El Chapo” Guzmán, anayechukuliwa kuwa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya Mexico hadi akafungwa maisha.”

Emma (33) ambaye walikutana kwa mara ya kwanza na Chapo akiwa na miaka 17, alikamatwa mwaka 2021 na kuanza kutumikia kifungo hicho. Inaelezwa kuwa baba yake mzazi Ines Coronel ni kiongozi mkubwa wa kundi la kihalifu la Sinaloa Cartel linalomilikiwa na Chapo.

Mwaka 1993 El Chapo alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa uhalifu huo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani, lakini baada ya siku chache alitoroka.

July 17, 2019 Chapo alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja na miaka 30 juu kwa biashara zake za dawa za kulevya alizokuwa akizifanya tangu miaka ya tisini, lakini hakukaa sana gerezani akatoroka.

Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela
Sababu ya mke wa El Chapo Kufungwa Jela

Mwaka 2001 Chapo alitoroka katika gereza hatari la Puente Grande Prison huko Mexico alikokuwa amefungwa maisha kwa makosa kama hayo. Watu 78 inaelezwa walihusika na kutoroka kwake wakiwemo hata viongozi wa serikali.

Mwaka 2014 Chapo alitoroka tena gerezani alikokua anatumikia kifungo cha maisha kwa makosa kama hayo ikiwa ni siku kadhaa tuu baada ya kukmatwa kabla ya kukamatwa tena mwaka 2019 ambapo yuko jela mpaka sasa.

Chapo aliyeoa mara nne na kuwa na watoto 11 aliwahi kutajwa kuwa kuwa ndiye muhalifu hatari zaidi duniani anayesakwa na serikali za Mexico na US.

Sikiliza Simulizi za Sauti PUMBAZO;

Leave a Comment