Biashara ya Mishikaki
LIFESTYLE

Biashara ya Mishikaki

Biashara ya Mishikaki

Hii ni moja kati ya biashara inayofanya vizuri kila siku, na inayoweza Kuanzisha kwa mtaji mdogo wa Fedha.

Mahali pa kufanyia biashara ni eneo lolote lenye watu wengi na hauhitaji fremu, mahali hapo panaweza kuwa jirani na soko, maeneo ya kituo cha mabasi, shuleni, vyuoni, ufukweni au eneo lenye wapitaji wengi.

Ujuzi

Ujuzi unaotakiwa ni kuchoma mishikaki mitamu kwa kuchanganya viungo vyote vinavyohitajika pamoja na jinsi ya kukata vyama vipande na bei yako(500 inafaa sana kwa kuanzia)

Kama huna ujuzi usiogope tembea youtube kuna mafunzo mengi ya kutengeneza mishikaki mitamu na viungo vyote

Mahitaji
VITU VINAVYOTAKIWABEI
Tatufa jiko (Nenda sehemu wanapochomelea unaweza kuongea nao vizuri jiko linapatikana ukiwa na 23000Tsh).23,000
Pata nyama isiyo na mifupa (Steki Kwa kuanza na kilo 2 Bei ya kilo ni 8000Tsh maeneo mengi)16,000
Mkaa Kopo Tatu @ 15001,500
Viungo vyote vinavyohitajika (Makadirio) 5,000
Vijiti vya mishikaki 2,500
JUMLA48,000

Kwenye 2kg unaweza pata faida ya 10,000 TSH baada ya kutoa matumizi yako vyote.
Na biashara umeanza kwa mtaji wa 23,000+8,000X2+1,500+5,000+2,500 = 48,000 tu.

Note: Ukataji wa vipande unahakisi faida, mfano tuseme ili upate faida ya 10,000Tsh lazima upige hesabu.

📟Hesabu ya kulenga faida kwenye mishikaki ipo kwenye vipande, sasa ili kujua vipande unavyotakiwa kukata:
vipande=(mtaji+faida unayolenga)/(bei ya kipande)
mfano kwa kilo 2(mtaji=48,000, faida nayolenga ni 10,000 kipande nauza 200)
vipande=(48,000+10,000)/200
vipande=290
📍Kwa hivyo ili kupata faida ya 10,000 kwenye 2kg ya steki natakiwa nikate vipange 290.

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment