Biashara ya Duka la Reja Reja
LIFESTYLE

Biashara ya Duka la Reja Reja

Biashara ya Duka la Reja Reja
Biashara ya Duka la Reja Reja

Karibu tuangalie Wazo la biashara ya Duka la REJA REJA Maarufu kama Duka la Mangi/Mpemba.

Ni biashara nzuri na MUHIMU sababu Mahitaji Yake hutumika kila siku na husaidia watu wenye kipato cha chini na cha kati sababu maduka haya huwekwa Karibu Sana na makazi yao au Eneo la biashara nyingi kama sokoni n.k

SIMILAR: Biashara ya Popcorn

Katika biashara hii zipo bidhaa zinazouzika kwa haraka haraka yaani kila siku japo faida yake si kubwa na zipo zile ambazo zinauzika taratibu kwa faida zaidi.

👉Mahitaji Ya Kuanzisha Biashara hii:-
💡Mfumo wa Biashara kisheria (Binafsi,Ubia au Kampuni)
💡Jina la biashara
💡Mchanganuo wa Biashara
💡TIN (namba ya utambulisho wa mlipa kodi) + Leseni
💡Uchaguzi wa bidhaa utakazouza
💡Uchaguzi wa Eneo la biashara
💡KUFAHAMU kiasi cha faida ya kila bidhaa
💡Njia za MATANGAZO (bango, vipeperushi n.k)
💡Mtu wa mauzo
💡Mtaji wa Pesa

Ukiwa kama Mmiliki au Muuza duka la rejareja unatakiwa uzifahamu bidhaa zinazouzika kwa haraka haraka na hata ikiwezekana uhakikishe hazikosekani dukani kwako hata siku moja.

SIMILAR: Biashara ya Mishikaki

Umuhimu wa bidhaa hizi zenye faida ndogo lakini hutoka kwa haraka haraka ni ile ile faida ndogo lakini unaipata kila baada ya muda mfupi ina uwezo mkubwa wa kujilimbikiza na kuwa KUBWA kwa haraka kiasi cha kushangaza.

ORODHA ya Bidhaa zinazouzika kwa haraka ni hizi:-
👉Sukari
👉Chumvi
👉Vocha
👉Unga wa Sembe, Dona, Ngano
👉Maharagwe
👉Mafuta ya kupikia
👉Majani ya Chai
👉Kiberiti
👉Dawa ya Mswaki
👉Sabuni ya Mche,ya kuogea, ya Unga, Ya Vipande
👉Vitafunwa
👉vitu vya watoto Pipi, Biscuits, Chama, karanga, Ubuyu, Big G, Peremende
👉Soda
👉Maji ya Chupa
👉Juice za Box na Chupa na
👉Mafuta ya Taa

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment