Aslay – Likizo Lyrics
LYRICS

Aslay – Likizo Lyrics

MP3 DOWNLOAD Aslay - Likizo
Aslay – Likizo Lyrics

Top-rated Tanzanian young star and Pusha hit songmaker, Aslay is back with a brand new banger titled Likizo.

SIMILAR: Aslay – Kilangakomo

Likizo Lyrics by Aslay

Message zako nimeziona
Ati umechoka visa vyangu
Ohh mama aaah
Mbona unakufuru Mungu
Si ungesema kama umechoka penzi langu
Oh mama nijitakatae

Ale tate nane
Hutaki hata tuonane
Vibaya hivyo oh mama
Oh tate nane
Unapenda tufokeane
Vibaya hivyo ooh mwana

Nakuonaga tu snapchat
Au Insta picha ukiposti
Ni block basi mama nisikuone
Anakujaga tu ibilisi
Natamani kwenda kwenu kushtaki
Maneno yako yanafanya ninyong’onye

Sababu nakupenda sana
Ndo maana unafanya visa niumie
Mwenzako bado mi kijana
Nahitaji fursa nipe nitulie

Kamoyo kanaenda mbio
Nakaribia kukata roho
Mwanzako sina kimbilio ndo ushanipiga KO

Nipunguzie adhabu basi
Eeeh eeh
Unipe likizo tu
Mi bado nakupenda mama
Unipe likizo tu
Ona unadhulumu yangu nafsi
Unipe likizo tu
Utaniua mama aaah
Unipe likizo tu

Za chini ya kapeti nimepata habari umetolewa posa
Inamaana hunitaki umepata kibosile kinakupa mapesa (eeh)
Kwangu ulifuata kiki uliishi na mimi kusafiria nyota eeeh
Kweli kisichoridhiki hakiliki
Ona unavyonitesa

Kwenye harusi nitakuja
Nione walivyokupamba mamaaaa
Ninajua itaniuma ila nitajikaza sana
Nitaleta na zawadi nitampa mkono jamaa
Kisha sitokaa sanaa nitaanza ondoka mama

Hali tate nane
Hutaki hata tuonane
Vibaya hivyo oh mama
Oh tate nane
Unapenda tufokeane
Vibaya hivyo ooh mwana

Nipunguzie adhabu basi, ehh
Unipe likizo tu
Mi bado nakupenda mama
Unipe likizo tu
Ona unadhulumu yangu nafsi
Unipe likizo tu
Utaniua mama, mamaa
Unipe likizo tu

Mola nipe subira
Nitampata kisura
Nitaishi na yeye, anipende mwenyewe, mwenyewe
Mola nipe subira
Nitampata kisura
Nitaishi na yeye, anipende mwenyewe, mwenyewe

Aslay – Likizo Mp3 Download

More hit songs from Aslay;

Leave a Comment