Mambo 11 ya Kuepuka kwa Kijana Kama Wewe 2024
LIFESTYLE

Mambo 11 ya Kuepuka kwa Kijana Kama Wewe 2024

Mambo 11 ya Kuepuka kwa Kijana Kama Wewe 2024
Mambo 11 ya Kuepuka kwa Kijana Kama Wewe 2024

Ni muhimu kuelewa kwamba katika maisha ya vijana, kuepuka mambo mabaya na kuzingatia maendeleo ni muhimu. Baadhi ya kanuni za jumla ambazo zinaweza kuwa na manufaa kwa vijana ni pamoja na:

SIMILAR: Good Morning Messages to My Wife

Kuoa au Kuolewa Bila Kujipanga

Usiingie kwenye ndoa bila kuwa tayari( kwa kukurupuka) hata ukimpata mwenza endelea kuishi nae kwenye uchumba tu kwanza hadi ujipange.

kukaribisha Ujinga( Kutotafuta Ujuzi Na Maarifa)

Vijana wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa na ujuzi kwa sababu ya kujifanya wajuaji, epuka ujuaji na kubali kuwa elimu haina mwisho endelea kujifunza.( Ujinga ni mbaya)

kupuuza Kutafuta Pesa na Kutunza Pesa

Ukiwa kijana kipaumbele chako kikubwa iwe kutafuta pesa kwa kufanya kazi haijalishi kwa kuajiliwa au kujiajiri na acha kutumia pesa hovyo.

kughairisha Mambo (Inconsistency)

Epuka Kugharisha mambo Yako muhimu unayojipangia kufanya kwa mwaka mzima,Usiishie njiani( consistency is a key to success)

Acha Uzembe na Uvivu

Kijana una nguvu tumia ujana wako kuchapa kazi, fanya kazi zako kwa bidii kubwa.Jitume zaidi.

Usifanye Vitu Kwa Kawaida

“Don’t be an everage person” Usiwe wa kawaida kwenye kazi, ujuzi,kipaji au biashara yako.KATAA KUWA WA KAWAIDA kama wengine.Acha kufanya kwa mazoea.Fanya kwa UBORA MKUBWA.

Dhibiti Mwili Wako Juu Ya Wanawake Na Pombe

Kijana bado unajitafuta hivyo achana na wanawake + pombe.Ulevi na wanawake vitakuharibia malengo Yako usipokuwa makini.

Acha Utegemezi Wa Hovyo

“Hakuna mtu atakuja kukuokoa na umaskini usipoamua mwenyewe kujiokoa”Amua kujipambania mwenyewe kutafuta mafanikio na utajiri.

Acha Tamaa Ya Mafanikio Ya Haraka (Get Rich Quick)

Mafanikio ni mchakato kuwa mvumilivu,hata rafki zako wote wafanikiwe usipaniki/ kujilinganisha subiri na wewe siku Yako itafika( endelea kupiga kazi tu na kujiongezea ujuzi)

Acha Kulala Kupita Kiasi

Usipokuwa makini na usingizi utajikuta unashindwa kutimiza malengo Yako.Usilale muda wa kazi.AMKA mapema zaidi kwenda kazini.Kama bado unajitafuta saa 11 alfajiri unatakiwa uamke na kujiandaa na kazi.

Kutolinda Afya Yako

Linda Afya Yako kwa gharama kubwa kwani ndio mtaji wa maisha..Zingatia kanuni na Ushauri wa kiafya mfano tumia Kinga kila unapokutana na mtu ambae hamjapimaUkimwi upo.Acha kunywa pombe Kali utadhuru Afya Yako.”Usipolinda Afya Yako mwenyewe hakuna mtu atakulindia Afya Yako”

Umejifunza nini hapa?

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment