Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024
E NEWS

Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024

Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024
Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024

Mshiriki wa Mashindano makubwa ya urembo ya Miss World kutoka Jamhuri ya Czech, Krystyna Pyszkován ameshinda taji la Miss World 2024.

SIMILAR: Alikiba azindua redio yake, Crown Fm 92.1

Mashindano hayo yamefanyika Mumbai Nchini India leo March 09,2024 ambapo amevalishwa taji hilo na Miss World aliyekuwa anashikilia taji hilo, Karolina Bielewaska.

Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano hilo, Miss Tanzania Halima Kopwe @halimakopwe amefanikiwa kuingia kwenye orodha ya Warembo 40 bora waliowania taji la Miss World 2024 kwenye mchujo ambao umewaacha nje Warembo wengine 72 kutoka kwenye idadi ya jumla ya Washiriki 112.

Kwenye Top 40 hiyo Bara la Afrika limeingiza Warembo 13, Ulaya 10, Asia na Oceania 9 pamoja na Amerika 08 ambapo mara ya mwisho Mrembo anayeiwakilisha Tanzania kuingia katika Top 40 hiyo ilikuwa ni mwaka 2005 ambapo Nancy Sumari aliingia na baadaye kutangazwa kuwa Miss Africa.

Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024
Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024

Fainali za Miss World ambazo ni fainali za 71 toka kuanzishwa kwa Mashindano hayo duniani, zimefanyika leo kwenye Jiji la Mumbai, India.

Source: Millard Ayo

Check more LIFE HACK articles;

Leave a Comment