Mo Dewji na Try again wavutana usajili wa Chama
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC, Salim ‘Try Again’ Abdallah alitaka kumbakisha mchezaji nyota, Clatous Chama, lakini Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, hayuko tayari Chama kuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao.
SIMILAR: Tyla adai Tems amefungua milango ya wengi
Mo Dewji amemwambia Try Again kuwa kama anataka kumbakisha Mwamba wa Lusaka, atapaswa kutoa mwenyewe ada ya usajili, jambo ambalo Try Again hayuko tayari kufanya.
Kwa mujibu wa mchambuzi @hansrafael14, amedai Mo Dewji anataka kuleta sura mpya na damu changa kwenye timu, lakini Try Again anasisitiza kuwa Chama bado ana miaka miwili ya kutumikia Simba kwa ufanisi.
SIMILAR: Baba Levo adai kupigwa na mke wake
Kwa upande mwingine, Chama inaelezwa tayari amekubaliana na Yanga SC kuhusu masharti ya mkataba mpya, ikiwemo ada ya usajili, bonasi, mshahara, makazi na usafiri. Kilichosalia ni kusaini rasmi mkataba huo baada ya mkataba wake na Simba kumalizika.
Check more LIFESTYLE articles;