SIMULIZI YA MTUHUHIMIWA FULL EPISODE
SIMULIZI

Mtuhumiwa

SIMULIZI Mtuhumiwa Episode 01
SIMULIZI YA MTUHUHIMIWA FULL EPISODE

IMEANDIKWA NA : HUSSEIN TUWA

*********************************************************************************

Simulizi : Mtuhumiwa
Sehemu Ya Kwanza (1)

Jambazi hatari linalojishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya huko Marekani ya Kusini limefanikiwa kwa mara nyingine tena kuwatoroka askari wa Kikosi Cha Kupambana na madawa ya kulevya cha Marekani (D.E.A) baada ya askari hao kuizingira kambi yake.
Habari za kuaminika zinaeleza kwamba jambazi hilo, Claudio Zapata, liliwatoroka askari hao baada ya mapambano makali ya kutupiana risasi kati ya kundi lake na wana usalama wa D.E.A. Katika mapambano hayo, askari kadhaa walijeruhiwa na wawili waliuawa. Wafuasi wengi wa jambazi hilo waliuawa na wachache waliokuwa wamejeruhiwa walitiwa mbaroni.
Kutokana na hali hiyo, msako mkali wa kimataifa umeanza dhidi ya jambazi hilo hatari ukiongozwa na askari wa D.E.A

Mtuhumiwa Episode 01

Mtuhumiwa Episode 02

Mtuhumiwa Episode 03

Mtuhumiwa Episode 04

Mtuhumiwa Episode 05

Leave a Comment