Unahitaji Masaa 22 Kutengeneza BFF Mpya
LIFESTYLE

Unahitaji Masaa 22 Kutengeneza BFF Mpya

Unahitaji Masaa 22 Kutengeneza BFF Mpya
Unahitaji Masaa 22 Kutengeneza BFF Mpya

Kabla ya yote nikuulize kwanza, kwa uzoefu wako unadhani unahitaji muda gani ‘kuunda’ urafiki ulioshiba na Mtu mwingine? ……..wakati ukinitafutia jibu kuna huu utafiti mpya uliochapishwa katika Jarida la mahusiano ya kijamii na kibinafsi nchini Marekani ambao umeonesha kuwa itamchukua Mtu jumla ya saa 200 ( dakika elfu 12) za kukaa pamoja na Mtu ( kwa nyakati tofauti) ili kujenga uhusiano na urafiki wa karibu.

SIMILAR: Diamond Platnumz Atangaza Kuachana na Zuchu I’m Single Boy

Jeffrey Hall wa Chuo kikuu cha Kansas, Marekani ndiye amefanya utafiti huu na kugundua kuwa inachukua takriban saa 200 kutengeneza ‘urafiki bora’ na kujenga mazoea na Mtu mwingine lakini pia akagundua kuwa inachukua jumla ya saa 50 ( dakika elfu 3 ) kwa Mtu kutengeneza urafiki wa kawaida na Mtu anayefahamiana nae, vilevile inachukua jumla ya saa 90 ( dakika 5400) kubadilisha hiyo kuwa ‘marafiki’ wazuri zaidi.

Jeffrey alisisitiza pia kwamba Watu wanapotumia muda mwingine kutaniana, kufanya mazungumzo ya maana na kuonana inachangia pakubwa kwenye ukuaji wa haraka wa urafiki.

Kibongobongo inachukua muda gani kuunda urafiki au ushkaji ulioshiba?

SOURCE: @millardayo

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment