Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
LIFESTYLE

Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Kumpa mpenzi zawadi wakati anapoendelea na hedhi inaweza kuwa njia nzuri ya kumfanya ajisikie vizuri na kuthaminiwa. Kwanza kabisa, unaweza kumtunza kwa kumpa chakula kitamu kama chocolate au matunda ambayo yatamsaidia kujisikia vizuri. Hii ni njia rahisi na ya kirafiki ya kuonyesha kwamba unajali na kujali kuhusu hali yake.

SIMILAR: Unahitaji Masaa 22 Kutengeneza BFF Mpya

Kisha, mpe muda wako wa ziada kwa ajili yake. Kwa mfano, unaweza kufanya mazoezi ya upole pamoja au kufanya kitu ambacho anapenda kama kujipamba au kupumzika kwa pamoja. Kuwa karibu naye wakati huu wa kipekee kunaweza kumfanya ajisikie kupendwa na kuthaminiwa zaidi (Period Gift).

Chocolate
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Chokoleti husaidia kupunguza maumivu ya hedhi kwa sababu ina magnesiamu ambayo hulegeza misuli. Zinapatikana kwa wingi madukani kwa mfano Tanzania unaweza kumnunulia Ivory Chocolate inapatikana kwa gharama ya Tsh 1,000 au Diary Milk inapatikana kwa gharama ya Tsh 3,000.

Pedi za kike
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Unajua bei ya pedi? Mara nyingine inaonekana kama bidhaa muhimu lakini isiyohitajika. Kununua kwa ajili yake kutakuwa ni faraja kubwa. Lavy pads zinatajwa kuwa pedi bora zaidi na zinapatikana kwa gharama ya Tsh 4,500 ila pia kuna aina nyingine kama Freestyle, HC, Cathy na nyinginezo, zinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu zaidi.

Dawa ya Maumivu (Pain Killer)
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Tafadhali usimnunulie felvin badala yake pata paracetamol, diclofenac au ibuprofen (ikiwa hana kidonda cha tumbo) ili kupunguza maumivu. Hii ni kwa wale wanawake wanaopata maumivu makali wakati wa hedhi tu.

Matunda
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Matunda anayoyapenda ni yapi? Ongeza baadhi kama vile Apple, strawberries, pineapples, zababu au ndizi au matunda anayoyapenda. Apple ni tunda bora zaidi maana Apple (tufaa) ni ishara ya upendo.

Biscuits
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi
Zawadi ya kumpa mpenzi akiwa kwenye hedhi

Pia unaweza kumpelekea biskuti aina tofauti kama vile Eet sum mor inayogharimu kati ya Tsh 3,500 mpaka Tsh 5,000, Oreo, pringles.

Pesa

Pia unaweza kumpelekea pesa pia kwa maana itamsaidia kupunguza mawazo yasiyo ya lazima kwasababu ataweza kutatua matatizo madogo madogo yanayoweza kuwa yanamkabili wakati huo akiwa period.

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment