Mr. Blue Msanii Bora wa mda wote - Mchango wake kwenye Bongofleva
LIFESTYLE

Mr. Blue Msanii Bora wa mda wote – Mchango wake kwenye Bongofleva

MP3 DOWNLOAD Mr Blue – Mungu Unanipenda
Mr. Blue Msanii Bora wa mda wote – Mchango wake kwenye Bongofleva

Ukimtaja Mr Blue kwenye kizazi hiki cha sasa wengi wao wanaweza kumfananisha au wakahisi msanii ambaye alifanya muziki ilimradi tu kwa sababu anajua kuimba.

Kwa watu wanaojua muziki na wameufuatilia muziki tangu zamani ukitaja jina la Mr blue lazima nywele zisisimke kutokana na yale aliyoyafanya kwenye muziki huu wa Bongo Fleva.

SIMILAR: Highest Paid Actor in Africa

Mr. blue ni miongoni mwa wasanii bora wa muda wote kutoka hapa Tanzania kutokana na aina ya muziki alioufanya na namna alivyokubalika kwenye jamii.

Mr Blue aliwahi kulikamata soko la muziki wa Bongo Fleva na kufanya kila mtu aweze kumzingatia na kuupenda muziki wake pia aliitwa kipenzi cha warembo.

Huyu ndio aliyeaminisha wasanii na jamii kwenye upande wa kuvaa kuwa anajua kuvaa na ndio aliyekuwa na Swaggz kwa uvaaji wake, Uongeaji wake na hata Uimbaji wake.

Ni miongoni mwa wasanii waliowahi kukubalika zaidi ndani na nje ya Tanzania lakini kubwa zaidi ni miongoni mwa wasanii walianza muziki wakiwa na umri mdogo zaidi.

Mr. blue ana zaidi ya miaka 20 kwenye game lakini mpaka leo ana dunda na anaheshimika kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Mr. Blue Msanii Bora wa mda wote - Mchango wake kwenye Bongofleva
Mr. Blue Msanii Bora wa mda wote – Mchango wake kwenye Bongofleva

Kwenye kipindi chake kila msanii alitamani kufanya nae kazi, anasifika kwa majina mengi sana ila majina yake maarufu ni Mr Blue, Byser, Bablon na zamani alikuwa anajiita SIMBA na mengine kwa sasa akijiita NYANI ZEE.

Jina lake halisi ni Herry Sameer Mzaliwa wa Dar Es Salaam. Mr blue ni miongoni mwa wasanii waliochonga njia kwenye soko la muziki wa Bongo Fleva.

SIMILAR: Diamond Platnumz Atangaza Kuachana na Zuchu I’m Single Boy

Kubwa na mbaya zaidi hajawahi kushinda Tuzo yoyote..!

Kipi umekimisi kutoka na Blue Byser Mr blue

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment