Zuchu aweka rekodi mpya Boomplay
E NEWS

Zuchu aweka rekodi mpya Boomplay

Zuchu aweka rekodi mpya Boomplay
Zuchu aweka rekodi mpya Boomplay

Baada ya kuianza wiki hii na taarifa za ushindi wa kufikisha watazamaji milioni 100 kwenye video yake ya ‘Sukari,’ YouTube, @officialzuchu amefanikiwa tena kuweka rekodi nyingine kubwa. Mwimbaji huyo wa @wcb_wasafi kupitia jukwaa la @boomplaymusic amefikisha wasikilizaji milioni 300 akiwa msanii pekee wa kike Afrika Mashariki mwenye zaidi ya wasikilizaji milioni 200.

SIMILAR: Nyimbo kali za Bongo ambazo hazina video

Kwa rekodi hiyo, Zuchu anaungana na @diamondplatnumz@harmonize_tz na @rayvanny ambao kwa nyakati tofauti wamefanikiwa kujikusanyia wasikilizaji milioni 300.

Zuchu kwa kufikisha wasikilizaji milioni 300 ameweka rekodi kubwa zifuatazo.

1. Msanii wa kike wa kwanza Afrika Mashariki kupata wasikilizaji 300m

2. Msanii aliyefikisha idadi hiyo ya wasikilizaji ndani ya muda mfupi (miaka minne), kulinganisha na waliomtangulia ambao wametafuta namba hizo kwa zaidi ya miaka 5 mpaka 7.

Wasanii Watano wa Kike – Bongo Fleva wenye wasikilizaji wengi Boomplay Music.

1. Zuchu – 300
2. Nandy – 116
3. Phina – 46
4. Maua Sama – 26
5. Yammi – 20.4

Check more LIFE HACK articles;

Leave a Comment