NMB Yaleta Account Isiyo na Malipo
E NEWS

NMB Yaleta Account Isiyo na Malipo

NMB Yaleta Account Isiyo na Malipo
NMB Yaleta Account Isiyo na Malipo

Naiona 2024 ikiwa nyepesi kwa Watanzania wengi kupitia hili toleo jipya la NMB lililotangazwa leo ambalo ni kampeni mpya ya “NMB PESA HAACHWI MTU” ya kuhamasisha na kuwawezesha Watu wengi zaidi kufungua akaunti hiyo wanufaike na faida za kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa fedha.

SIMILAR: Diamond Platnumz Atangaza Kuachana na Zuchu I’m Single Boy

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB (@nmbtanzania ) Filbert Mponzi amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kusaidia kuongeza idadi ya Watu wenye akaunti za benki nchini na wale wanaohudumiwa na Taasisi hiyo ambao sasa hivi ni zaidi ya Wateja milioni sita.

“Utafiti wa Finscope hivi karibuni unaonesha kwamba kwa sasa ni asilimia 22 tu ndio wana akaunti za benki kati ya wote wenye sifa za kuwa nazo ndio maana NMB imeingilia kati kusaidia kutatua changamoto hiyo kwa kuendesha kampeni hii inayowalenga hasa Wananchi wa kawaida hususani Mama ntilie, Wamachinga na Waendesha bodaboda na wengine”

Katika kufanikisha zoezi hilo, Mponzi amesema akaunti ya NMB PESA inafunguliwa kwa kuanzia shilingi elfu moja tu (1,000 ) na haina makato ya kila mwezi yote hii ni kufanya unafuu na kuondoa dhana ya kuwa kufungua akaunti Benki ni uamuzi wa gharama au linalohitaji Mtu awe na fedha nyingi “Ufunguaji akaunti hii utafanyika kirahisi sana mahala popote kidijitali na utafanywa na Maafisa mauzo wetu ambao ni maalumu kwa ajili ya kazi hiyo”

Faida za akaunti hiyo ni pamoja na kuunganishwa na huduma ya NMB Mkononi ambayo faida zake nyingi ni pamoja na mikopo ya MSHIKO FASTA isiyokuwa na dhamana wala isiyohitaji Mteja kwenda Benki inayoaanzia shilingi elfu moja hadi laki tano (500,000).

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment