Tanzia: Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi Afariki Dunia
Rais Mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi, amefariki dunia mnamo Februari 29, 2024, saa 11:30 jioni akiwa anapokea matibabu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani ya mapafu.
SIMILAR: Jinsi ya kupata TIN Number Online
Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Mzee Mwinyi, aliyeiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1985 hadi 1995. Alieleza kwamba Mzee Mwinyi alikuwa akipokea matibabu tangu Novemba 2023 huko London, Uingereza, kabla ya kurejea nchini Tanzania kuendelea na matibabu jijini Dar es Salaam.
Kufuatia msiba huu, Rais Samia ameagiza siku saba za maombolezo kuanzia kesho, kuomboleza kifo cha kiongozi huyo mpendwa.
Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza Serekali ya Awamu ya Pili aliingia madarakani rasmi tarehe 5 Novemba 1985. Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Kivule, Mkuranga, mkoa wa Pwani tarehe 5 mei, 1925.
Kazi
Alikuwa mwalimu wa shule za msingi za Mangapwani na Bumbwini, Zanzibar.Kisiasa, mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alijiunga na chama cha Afro Shiraz(ASP) mwaka 1964 na kushika nyadhifa mbali mbali za serekali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile katibu mkuu, Wizara ya Elimu Zanzibar 1963, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1970 na kati ya mwaka 1982 hadi 1983 alikuwa Waziri wa Afya, Wizara ya Mambo ya Ndani, Maliasili na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Misri. Mwaka 1984 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Elimu
Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi pia ana cheti cha umahiri wa lugha ya kiingereza, alichohitimu katika taasisi ya Regent, Uingereza mwaka 1960 na cheti cha umahiri wa lugha ya kiarabu alichohitimu, Cairo, Misri, mwaka 1972-74.
Check more LIFE HACK articles;