Treyzah Kuitambulisha Bongo Rnb
Mwimbaji wa Bongo Fleva (@im_treyzah) yupo kwenye harakati ya kutambulisha aina mpya ya muziki wa Bongo RnB.
Kwa mujibu wa @vanny_icon, ambaye ni Meneja wa Treyzah, lengo la kutambulisha aina hiyo ya muziki, ni kutaka kuutangaza utamaduni wa Tanzania kwenye majukwaa ya kimataifa.
SIMILAR: Jay Melody na Dayoo Vinara Boomplay Africa
“Tuna lengo la kuleta kipengele cha Bongo RnB, ambayo itakuwa genre kubwa ya kuutofautisha muziki wa RnB ya Tanzania, ambapo katika hilo tumefanikisha kolabo mbili za kimataifa zitakazokuwa katika EP itakayoweza kutoka Juni 2024. Alisema Vanny Icon alipokuwa akipiga stori na mwandishi @enkyfrank kwenye #SnSAnalyzed.
Kwenye kauli nyingine, Van Icon aliongeza kuwa, Focus yao ni kulifikia Soko la kimataifa kwa kufanya kazi zenye utofauti kuanzia beats, videos na collaboration ili kuupa heshima muziki wa Bongo RnB.
Treyzah amekuwa na muendelezo mzuri katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Akiwa na umri wa miaka 24, anao ujasiri wa kufanya muziki wenye ushawishi. Kama atapewa sikio, na kuungwa mkono kwenye harakati zake, atakuwa kwenye nafasi nzuri ya Kuitambulisha Bongo RnB kwa ukubwa na kuiwmbukiza kwa wasanii wengine wataovutiwa na ugunduzi huo.
SIMILAR: Haji Manara avujisha Video ya Dulla Makabali
Meneja wa Treyzah pia anawakaribisha, wafanyabiashara, wadau wa muziki waonaovutiwa kufanya uwekezaji kwenye muziki wa Treyzah.
Kwa- Sasa Treyzah anatamaba na wimbo ‘Nimempata’ wa 2023 ambao Ulitayarishwa na @thisiscukie.
Check more LIFESTYLE articles;