Jinsi ya kuongeza na kunenepesha mwili kwa kutumia vyakula.
LIFESTYLE

Jinsi ya kuongeza na kunenepesha mwili kwa kutumia vyakula.

LEO nitaongelea jinsi ya kuongeza na kunenepesha mwili kwa kutumia vyakula, kwa wale wanaotaka kunenepa.Kuongeza mwili kuna changa­moto nyingi ambazo huchangia watu wengi kukata tamaa kama vile kujua ni vyakula gani wale. Vyakula vinavyonenepesha ni hivi:
Jinsi ya kuongeza na kunenepesha mwili kwa kutumia vyakula.

LEO nitaongelea jinsi ya kuongeza na kunenepesha mwili kwa kutumia vyakula, kwa wale wanaotaka kunenepa.Kuongeza mwili kuna changa­moto nyingi ambazo huchangia watu wengi kukata tamaa kama vile kujua ni vyakula gani wale. Vyakula vinavyonenepesha ni hivi:

NYAMA NYEKUNDU

Nyama nyekundu kama vile nyama ya ng’ombe ni muhimu sana hasa kwenye kujenga mwili. Nyama nyekundu huwa na leucine (amino acid) yenye kusaidia misuli ya mwili kwenye kutanuka kwa kutu­mia protini. Hivyo, ni vyema kutumia nyama nyekundu zaidi ya mara mbili kwa wiki ili kujihakikishia ukuaji na utanuzi wa misuli ya mwili.

KARANGA NA SIAGI

Karanga ni aina ya chakula ambacho kina mafuta na calorie (ni aina ya kipimo cha nguvu kilicho ndani ya chakula kinacho­pimwa kwa uwezo wa kupandisha gramu moja ya maji kwa nyuzi 1).

Karanga na siagi kwa pamoja huwa na ladha nzuri mdomoni na pili huchangia uongezekaji wa mwili kwa kiasi kikubwa.

PARACHICHI

Parachichi ni tunda zuri na hupendwa na wengi na pia huwa na ladha ya kuridhisha mdomoni na hutumika na watu wengi duniani. Mbali na hapo, para­chichi ni tunda lenye uwezo wa kuongeza calories 322 kwa kila parachichi moja mtu atakalokula. Pia parachichi huongeza mafuta kwenye mwili ambayo ni muhimu kwenye kujenga misuli ya mwili.

ISIKUPITE HII: Njia mbili rahisi za kukuza uume wako kiasili.

Mafuta ya asilia

Watu wengi hula na kupikia ma­futa mbalimbali majumbani bila kujua athari na faida ya mafuta hayo, hivyo leo nitawajuza kwa kugu­sia sua­la hili. Mafuta hasa ya asili kama vile mafuta ya Olive na Karanga yanajenga na kuimarisha zaidi mwili kwani hutokana na mimea asilia ambayo ni rahisi kutumika na mwili tumboni kulinganisha na mafuta mengine. Hivyo, mtu anayetaka kuongeza mwili atumie mafuta asili.

MAZIWA

Maziwa ni aina moja ya lishe iliyojaa virutubisho vingi ambavyo huhitajika mwilini kama vile carbs, protini na ma­futa. Maziwa ni muhimu sana kwa watu wenye kutaka kuongeza mwili na inashauriwa sana kwa wabeba vitu viz­ito. Kunywa angalau lita moja mpaka mbili kwa siku ili kujihak­ikishia uongezekaji wa mwili.

MATUNDA YALIYOKAUSHWA

Matunda yaliyokaushwa ni muhimu sana kwa maana huwa na vitamini na madini zaidi ukilinganisha na matunda ambayo hayajakaushwa na hivyo kuongeza utengenezaji wa misuli kwa kuongeza calories nyingi mwilini. Hivyo basi in­ashauriwa kula japo mara mbili ili kuhakikisha ukuaji wa mwili.

VIAZI

Viazi ni aina ya vyakula am­bavyo huhitajika sana mwilini kwa mtu anayetamani kuongeza mwili, mbali na sifa zake za kuwa na uwezo wa kusaidia mi­suli ya mwili kwenye kuhifadhi glycogen, viazi huwa na madini mengi. Hivyo basi ningependa kushauri watu wanaotaka ku­jenga miili kutumia viazi.

Kwa vyakula hivyo basi ni rahisi sana mtu kuongeza mwili wake na akiwa anafanya ma­zoezi huwa rahisi zaidi kwake kuwa na monekano mzuri.

NB: Usitumie vyakula hivi kwa wingi kama hutaki kunenepa.

Zoezi la kuongeza ukubwa wa uume bila kutumia dawa.

Leave a Comment