Maswali 10 ya Kumuuliza Mwanamke Mkitoka Date
LIFESTYLE

Maswali 10 ya Kumuuliza Mwanamke Mkitoka Date

Maswali 10 ya Kumuuliza Mwanamke Mkitoka Date
1. Ni kitu gani ushawahi kufanya, lakini hautafanya tena?

Swali kama hili litamfanya kufikiria sana. Swali hili laweza kufanya ujue mambo yake ya chini ya maji zaidi. Mwanzo labda unaweza kugundua ya kuwa kuna mambo ambayo mnagawa pamoja.

2. Tabia gani ya ufidhuli ambayo uko nayo?

Kila mtu ana tabia yake ya ufidhuli ambayo amezaliwa nayo. Hivyo swali kama hili litamfanya mwanamke kama huyu kujieleza zaidi hivyo kujiskia huru kuongea nawe zaidi na zaidi.

3. Rafiki yako wa dhati ni nani?

Rafiki wa dhati ni muhimu zaidi kama unataka mahusiano yako na mwanamke yafaane. Hivyo lazima ujipendekeze na kujihusisha na rafiki ya mwanamke unayemzimia ili kufunga mahusiano yenu yawe mazito. Unaweza kupanua mawazo yako kwa kumuuliza maswali kama alikuwa rafiki yake tangu lini? Ulimjuaje? nk [Soma: Sababu 11 za wewe kufanya mapenzi na rafiki yako]

4. Ni jambo/kitu gani ulichofanya kitambo ambacho ungetamani usingekifanya?

Kufanya makosa ni vigumu kuelewa na kukubali. Hivyo kumuuliza swali kama hili na akiweza kulijibu basi kunaashiria ya kuwa una nafasi kuu ya nyinyi wawili kuwa kitu kimoja.

5. Kitu gani unachoogopa zaidi?

Uoga ni kawaida. Ukijua uoga wa mtu kunakufanya uwe makini naye. Hivyo mwanamke akikuambia uoga wake anakupa ruhusa wa kutumia nafasi hii kumkinga na kumlinda mbeleni.

SIMILAR: Good Morning Messages to My Wife

6. Sehemu gani hapa ulimwenguni ungetamani kuishi?

Swali hili linatoa nafasi kwa mtu kuwa mbunifu na kutoa hisia zake za ndani ya mwili. Pia swali hili linakupa nafasi kwako kujua matamanio yake hivyo unaweza kuchagua sehemu ambayo unaweza kumtoa out ama deti. Pia kuuliza hivi kunakupa kumjua zaidi mwanamke.

7. Ungependa kuchagua pesa au mapenzi?

Swali kama hili lafaa liwe mapenzi. Pili hivyo bila shaka mwanamke huyo tutamweka katika kategoria ya kuwa gold digger. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa kutumia macho]

8. Kumbukumbu ipi ya utotoni mwako unaipenda?

Kumbukumbu za utotoni humfanya mtu kuingiwa na furaha na tabasamu. Hivyo kumuuliza mwanamke swali hili kunatoa fursa ya kujua mambo ambayo yamekuwa yakimfurahisha kitambo.

9. Ni jambo gani la aibu zaidi ushawahi kufanya?

Mambo ya aibu humkumbusha mtu na kumfanya kucheka. Hivyo tumia fursa hii ya kumfanya mwanamke acheke.

10. Deti ya ndotoni mwako unapenda ingekuwa vipi?

Swali hili lina manufaa kwako. Hivyo akikujibu unaweza kutumia nafasi hii kupanga jinsi ambavyo utamtoa deti kama saprize. Utamwacha kwa giza.

Check more LIFESTYLE articles;

Leave a Comment