SIMULIZI The Lost Boys – Ep 5
NEW AUDIO

Ep 5: The Lost Boys

SIMULIZI The Lost Boys – Ep 5
SIMULIZI The Lost Boys – Ep 5

IMEANDIKWA NA : FRANK MASAI

*********************************************************************************

Simulizi : The Lost Boys

Sehemu Ya Tano (5)

Tofauti na Sunday,Mose.Moi na Ban,wao kila mmoja kwa wakati wake walitoka kwenye chumba chao na kuanza kuyafanya amabayo walikuwa wamepania kuyafanya.

******

Muda nao haugandi,mida ya jioni kundi la wagumu lilikuwa chumbani likijadiri mafanikio yao ambayo waliyapata kwa siku nzima tangu walipoachana mida fulani ya mchana.

“Dawa nimeipata na nadhani ni dawa bora kabisa kupata kutokea katika tafuta yangu dawa.”Alianza Sunday kufunguka kuhusu alichokuwa amepangiwa na Ban.

“Sina tatizo na wewe dokta. Nakuaminia sana Sajent Sunday.Sinaga tatizo na wewe.”Ban alimpongeza Sunday na wakati huo macho yake yalikuwa yanaangalia nyuso za Moi na Mose.

“Katika fatilia yetu,tumegundua yule Sharo anapenda sana kwenda na mtoto kule kwenye mlima. Sasa kwa kuwa anajua kuwa kuna jambo linaweza kumkuta,anaweza kubadili maamuzi. Badala ya kwenda mlimani,anaweza kwenda mahali popote, ili mradi paw tofauti na kule mlimani.”Mose aliongea kile anachokijua.

“Yap.Kweli kabisa,mmefanya jambo kubwa kujua hilo.Lakini sasa cha msingi yawapasa hiyo kesho kuwa karibu kabisa na geto lao,ili akitoka tu!Mnaanza kumfuatilia mwanzo mwisho anapoelekea.”Ban alizidi kuonesha uongozi bora kwa wale vijana aliokuwa nao mle ndani.

“Mimi nilikuwa nategemea majibu yenu ili niwapange watu wangu kwa ajili ya sapraizi kwa yule tozi kinyesi.”Ban akaweka bayana kile alichokuwa kakichukulia jukumu.

“Kwa hiyo watu wamepatikana?.”Moi aliuliza.

“Watu wapo wa kutosha tu!.”Ban akampa moyo Moi kwa jibu hilo fupi.

“Basi hamna shida ya kumfatilia sijui mpaka mlimani au wapi.

Akitoka pale ghetto,mimi nitakuwa naye nyuma bila yeye kujua. Na wakati huo nitakuwa nawapa taarifa kwa simu ni njia gani anapita. Nyie mtetega kwenye njia hizo. Akifika mnamkamata na kuanza kumremba remba ili apige gitaa,mnampa hadi kiti cha kukaa. Wewe mzee wa dawa,lazima uwe karibu naye. Akikupa kinywaji chake,unaweka kidawa hicho. Au kama hana,tunampongeza wenyewe kwa kumpa hata maji. Akinywa tu! Kaisha.”Moi alitoa pendekezo ambalo lilifikiriwa kwa muda kabla ya kupitishwa na bunge lile la watu wane.

“Yaweza kuwa njia rahisi zaidi kwani tunaweza kumkamatia penye watu wengi zaidi na tukafanya tukio kubwa kuliko hili ambalo tunataka kulifanya. Hivyo wazo la jamaa ni zuri sana tena sana. Limepita hilo Kapteni Moi.”Ban alikubaliana na wazo la Moi Shabala.

“Kwa hiyo ndio mpango upo hivyo,sitegemei kwa mpango huu kuingiliwa na nzi yeyote. Na mzee wa vi-medical,hakikisha kidawa unakiweka bila mtu yeyote kushtukia mchezo huo.”Ban alimaliza maongezi yale na kuanzisha habari nyingine ambazo alikuwa amezikusanya wakati anatafuta watu wa kushuhudia Junior akiabika.

*****

Hatimaye ikafika siku ambayo Junior alipanga kukutana na Eve.

Kama kawaida yake nay a wote mule chumbani.Junior alianza kujisafisha na kujiweka nadhifu kwa ajili ya mtoko ule wa maana na mtoto Eve.

Alinyoosha nguo zake na kuzichunguza sana ili asijefanyiwa kitu kama alichofanyiwa Fred na Hans. Wakati hayo yote yanaendelea.ni Suarez pekee ndiye alikuwa akiongea naye. Hassan na Alfred walikuwa kimya wakizuga wanajisomea na wakati walikuwa wanamwangalia kwa jicho la chini-chini.

“Ee bwana msalimie sana mrembo huyo.”Suarez alimuaga Junior aliyekuwa kapendeza vilivyo kwa kuvaa jinzi moja iliyomkaa vizuri,wanaziita modo.

Kwa juu alivaa fulana nzito yenye rangi ya kahawia na ina-alama ya fuvu na maandishi fulani ya vitisho. Ni kweli alipendeza,hasa pale alipoweka gitaa lake kwa nyuma kama vile msanii wan je aliyekuja kutalii Tanzania.

“Zimefika mkuu,na hao The Lost Boys hata kuniaga hawataki? Ni wishini lucky jamani.”Junior alitoa tabasamu la kejeli wakati ulimi na kinywa chake ukitamka maneno hayo.

“Maneno hayo. Ndio hayohayo yaliyomponza mwenzako.”Maneno toka kwa Hans yakamfikia vilivyo Junior na kumfanya aondoke zake.

*****

Hali ya hewa ya siku hiyo haikuwa mbaya sana. Na kama alivyofanya kwa Fred,Eve alimuomba Junior watembee kwa miguu.

Barabara nzima macho yalikuwa yanawaangalia vijana wale waliopendeza wakati wanatembea. Kila mmoja hakusita kuwasifia kuwa wamependeza.

Eve akiwa na ndani ya suruali fulani ya jinzi iliyokuwa mmekaa vizuri kabisa,na wakati huo kwa juu alivalia kitopu kilichoacha wazi kitovu chake mwanana,nani ambaye angesipomwonea wivu Junior?Ni kweli walipendeza sana kwa mwonekano wao muda ule wa saa tisa alasiri.

Safari yao licha ya pongezi nyingi,wao wenyewe walikuwa wanaifurahia kwa vicheko vya kuliwazana pamoja na kufurahishana.

Kila muda walicheka na kugonga viganja vyao bila wasiwasi wowote mioyoni mwao.

Safari ilienda lakini mwisho wake ulikuwa ni sehemu moja ya jiji la Dar es Salaam ambapo sehemu hiyo kulikuwa kuna watu wengi sana.

Ni kawaida ya eneo hilo kuwa na watu wengi hasa mida ile ya saa tisa,lakini kilichowashangaza wakina Eve,ni kuzungukwa ghafla na watu hao na wote walitaka Junior apige gitaa ndio aondoke pale.

Watu walikuwa ni wengi na wengine walikuwa ni wanachuo wanaomjua Junior vizuri sana. Sasa walikuwa wamewazingira.

“Junior tupigie gitaa kwanza ndio uondoke na mrembo wetu,vinginevyo,hatoki mtu hapa.”Jamaa mmoja aliyekuwa na mizuka ya muziki,aliongea hayo.

Junior alitabasamu na kumwangalia Eve aone ataitikia nini kwa maombi yale ya wananchi. Hatimaye Eve naye alitabasamu,kisha akaonesha ishara ya kumwambia awape burudani wale wananchi.

“Kitendo bila kuchelewa,kiti kililetwa pale walipokuwepo. Na Junior akapewa uwanja kwa ajili ya kufanya yake.

Alipokaa kabla hajalitoa gitaa lake,mara akaletewa maji ya kunywa. Naye bila kusita aliyapokea bila hata kumuangalia ni nani aliyempa yale maji. Kisa yaliyakuwa hayajafunguliwa, basi naye akaona yanafaa.

Akafungua maji yale na kuyafakamia kwa kiasi kikubwa tu!. Alipoweka chini chupa ya maji yale ya baridi,tayari alikuwa kapata mzuka wa ajabu.

Akaanza kulifungua begi la gitaa lake ili kulitoa dude lile kwa ajili ya kuburudisha wapiti njia.

Baada ya kulitoa,alianza kukaza nyuzi za gitaa lile ambapo alichukua kama dakika moja na nusu au mbili kabisa ili kufanya yote yale.

Pale aliponyanyuka kwa lengo la kuanza kulichakaza gitaa,mara tumbo lake alijisikia kama limekatwa na kisu. Hakika alishtuka lakini alishindwa kuonesha mshtuko wake kwa kuwa alikuwa mbele ya umati mkubwa wa watu.

Alidhani labda ni utani,lakini hali ilianza kumuwia vibaya pale aliponyanyua gitaa lake kwaajili ya kuanza kulikung’uta.

Ile kulinyanyua tu! Gitaa,mara akatoa gesi au hewa chafu kwa njia ile ya chooni. Ndio hivyo,Junior alipumua na kila mmoja aliyekuwa pale alisikia sauti ya pumzi ile.

“Vipi kaka? Gitaa zito?.”Yule jamaa mpapulishaji alimuuliza Junior baada ya lile tukio la ajabu kutoka kwa Junior.

Naliita la ajabu kwa kuwa lilitoka katika wakati usiotegemeeka kabisa. Kweli Junior alikuwa anaaibika,na ni kweli Fred na kundi lile la wagumu walikuwa wamepania kumuaibisha kijana yule.

Hali ilizidi kuwa mbaya na kupoteza muelekeo wa Junior wote wa kupiga gitaa. Jasho lilimtoka hasa pale tumbo lilipozidi kumvuruga na kumuaribia kabisa mapozi ya kukaa.

Kila alipomwangalia Eve,macho yake yalikutana na sura ya mshangao kutoka kwa kimwana yule mrembo. Ni mikono ya Eve ndio ilikuwa inamuuliza Junior ni nin kinachoendelea.

Kila Junior alipojaribu kuvumilia hali aliyokuwa nayo tumboni mwake,alijikuta akitumbukiza watu kwenye kicheko kikubwa kupita maelezo. Junior alikuwa akipumua kila baada ya sekunde kadhaa.

Mambo yakazidi kuaribika pale alipotaka kuondoka,alijikuta tumbo likimzidi nguvu na bila kupenda alirudi kwenye kiti alichokuwa kakaa mwanzo.

Tumbo la hewa likawa tumbo la haja kubwa.Akawa ni mtu wa kuumia sana na wakati huo ule umati ulikuwa upo hoi kwa vicheko,walikuwa hawajali hali ya Junior iliyokuwa inamtesa,bali wao waliona kama ile ni fahari ya macho.

Ni Eve pekee ndiye aliyekuwa na uso wa usiriazi,kati ya wale wananchi zaidi ya mia waliokuwa hawana mbavu kwa vicheko vilivyokuwa vimewashika.

Eve alienda kwa Junior na kumuuliza kwa sauti ya chini ni nini kinachoendelea.

“Tumbo Eve.”Junior alijibu kwa uchungu huku akijipinda panda pale alipokuwa kakaa.Na kile kitendo cha kuongea,ni kama nalikuwa anaruhusu haja itoke.

“Umekula nii ulipotoka?.”Eve alipouliza swali hilo,Junior mawazo yake yakaenda hadi mida fulani ya mchana,alikunywa chai huku akiwa na wakina Hans. Hapo hapo akatengeneza maelezo kuwa wakina Hans walimwekea kitu kwenye ile chai.

“Hansiiiiiiii,aaagh. Umenifanyia nini wewe? Nimekufanya nini?.”Junior alitoa maneno hayo huku machozi yakiwa karibu.

“Hans kafanyaje tena?.”Eve ilimbidi aulize baada ya kusikia lawama zile

“Hans ndiye mwenye tabia hizi. Alimuunguzia hata Fred suruali yake ulipotoka naye siku ile.Aagh.’Junior alitamka maneno hayo na kugugumia maumivu ambayo yalikuwa hayaelezeki kabisa katika wakati ule.

Eve alisimama wima na kuchanganua maneno yale huku akiwa wazi kaamini kuwa Hans ni muhusika way ale yote hasa kwa tabia yake.

Akili ya Eve ilicheza haraka na kwenda kuchukua taksi ambayo ingemsidi kiasi fulani kuficha ile aibu.Huku nyuma alimuacha Junior akizidi kuwa hoi na sasa aliona kuwa liwalo na liwe,ni heri ajisaidie kuliko kuendelea kuumia pale kwenye kiti.

Wakati Junior amejitolea kujiachia palepale,ndipo Fred alitokea haraka na mtu ambaye baadaye alijulikana kama ni dereva wa tax. Na kitendo bila kuchelewa,walimnyanyua Junior pale kitini alipokuwa kajiinamia kwa maumivu,hapo safari ya kumpeleka kwenye taksi ilianza huku Eve akiwa nyuma na gitaa la Junior.

Ilikuwa ni pona ya swala kwenye mdomo wa mamba kwa upande wa Junior. Dereva taksi aliendesha gari kwa kasi kiasi chake hadi akafika ,ahala fulani ambapo pana choo.

Hapo Junior alifunguliwa mlango wa gari ile ndogo na moja kwa moja alichomoka kama mshale na kukimbilia uwani. Kilichoendelea huko,ni yeye na lile jengo mahususi kwa ajili ya haja kama zake.

Alikuja kutoka baada ya dakika ishirini za kufanya mambo yake. Alirudi akiwa na ahueni kubwa ambayo ingemfanya aendelee kupiga gitaa,lakini kwa aibu iliyomkuta mbele ya Eve,aliona ni bora atulie kimya hadi pale Eve alipoanzisha maongezi.

“Sasa kwa nini Hans anafanya haya yote?.”Ni swali lililoanzisha maongezi kati ya wale watu wanne waliokuwamo ndani ya taksi lakini maongezi hayo mtu wa nne ambaye ni dereva,hakupaswa kuyaingilia.

“Haijulikani aisee. Hata mimi alinitegea moto kwenye suruali yangu.”Fred alikuawa anajisafisha kama si yeye aliyeyafanya yale yote.

“Itabidi keshokutwa nimtafute ili nikae naye aniambie ni sababu gani iliyompelekea afanye huu ujinga. Ujue ni utoto sana huu. Kwanza ni tabia ya kishenzi kabisa.”Eve alionesha wazi kukasirishwa na yale matendo. Wakati huo gari ilikuwa inaelekea yalipo makazi ya Eve kabla ya kwenda kwa akina Junior.

“Na nikifika namuua.”Junior aliongea kwa hasira huku uso wake ukiwa umekunjamana kama kala kipisi cha ganda la chungwa au kala mchunga.

“Amna Junii,tutayamaliza haya mimi nay eye,msije mkapoteza urafiki wenu kwa jambo la kijinga namna hii.”Eve alitoa pendekezo ambalo Junior hakuwa wazi kulisikiliza wala kulishika.

“Nakwambia Eve yule namuua. Namuua kabisa. Nampoteza kwenye dunia hii.”Maneno makali yalimyoka Junior. Wakati huo Fred alikuwa kimya akisubiri wakati wake. Wakati ambao angemshauri Junior kilichobora zaidi.

“We muache bwana. Nitaongea naye na yataisha.Mbona mambo madogo tu!Yawezekana mmefanya kitu na ndio maana nay eye anawalipizia. Hans si mkorofi kihivyo.Ngoja niongee naye tujue ukweli upo wapi.”Eve alizidi kushauri na wakati huo gari walilokuwa wamekodisha,lilikuwa karibu kufika sehemu husika.

“Mimi nitamalizana naye tu! Leo leo”.Junior akamaliza na kuangalia pembeni ambapo kulikuwa na kioo. Muda huo ilikuwa imetimia saa kumi na nusu za jioni.

“Okey. Ni shaui yako.Ila mii naomba uache hizo fikra zako. Fred mshauri mwenzako. Mbona wewe umetulia japo alikufanyia yale?Huyu Junii yeye anajidai anahasira,shauri yenu bwana. Mimi simo. Ila ukinisikiliza,keshokutwa tutayamaliza na urafiki utaendelea kama kawaida.”Eve alimaliza na kufungua mlango wa taksi ile na kuanza kuelekea yalipo maskani yake huku akiwaacha Fred na Junior wakimaliza ngwe ya safari yao.

“Wewe Junii tulia kwanza.Unakuwa na hasira,mimi mwenyewe nimempania kinoma kumlipia kwa alichonifanyia. Cha msingi tulia kama si wewe.”Fred alimshauri Junior.

“Nitulie kwa huu ujinga aliyonifanyia?Hamna hilo,leo naua mtu.”Junior alisimamia nia yake.

“We humjui Hans,nia yake ni sisi kuaibika mbele ya demu,sasa badala ya kumuua kwa nini nay eye keshokutwa anapoenda kukutana na demu asiaibike?.”Frd alitoa wazo ambalo lilimfanya Junior kukaa kitako na kuona kama ni wazo lililojitosheleza.

“Eti eeh. Na yeye tumfanyizie nini?.”Junior akili ilirudi.

“Mimi aisee siwezi Si wajua dini yangu haniruhusu kulipa kisasi japo nilimpania?Siwezi kufanya hivyo,ila ukitaka msaada,mimi nitakupatia.”Fred alionesha wazi anakaa mbali juu ya mpango ule.

“Nitafanya mwenyewe.Lazima atalipa bwege yule. Uongo kaka? Yeye kaniaibisha vyote vile,kwa nini na mimi nimwonee huruma?Lazima alipe.”Junior alipitisha mawazo yake huku akihitaji msaada wa mawazo hayo hata kwa dereva wa taksi.

“Kwa lichofanya,hata kama ni mimi,ningelipa tu!Dini ingekaa kando.”Dereva naye alionesha umafia wake.

“Sasa ngoja aon zamu yake.”Junior aliweka kituo cha maongezi yale ambayo kwa Fred yalikuwa yanafaida kubwa.

******

SAA MOJA NA NUSU LILILOPITA.

Wakati Junior anatoka mule ndani anamoishi na wakina Hans,alianza kufuatiliwa kwa ukaribu kabisa Moses Frank,kijana machachari wa Ban Diho.

Mose alikuwa anamfatilia Junior kwa makini sana. Na kila hatua ya msingi ambayo Junior alikuwa anaipiga,Mose alikuwa anawapa taarifa rafiki zake.

Pale Junior alipofika kwa Eve.Mose alitoa taarifa,na hata alipoona wanatembea kwa miguu,alitoa taarifa hizo na kutaja mahali ambapo Junior na mshirika wake wanapita.

Taarifa hizo zikaenda na kwenda hadi pale Junior na Eve walipofika eneo moja lenye watu wengi sana. Na watu hao ndio wakataka Junior awakung’utie gitaa.

Ndani ya watu hao,kulikuwa na wengine wametumwa kwa ajili ya kumpapulisha Junior afanye hivyo.

Junior alipoona ni bora awape burudani,ndipo kijana mmoja alipewa chupa ya maji na Sunday Magembe.

Chupa ile ya maji,Sunday alikuwa kaipiga sindano kwa kuminyia dawa moja ya asili,au ya miti. Dawa ile ilikuwa inauwezo wa kumfanya mtu aharishe ndani ya dakika zisizopungua ishirini baada ya kuigida.

Haijulikani anatoa wapi dawa hizo,lakini Sunday alikuwa ni fundi wa mambo yale na ndio maana Ban alimuamini na kumkabidhi jukumu lile.

Junior naye hakuchunguza sana juu ya ile chupa aliyopewa na mtu asiyemjua.Yeye aligida maji yale na baada ya dakika mbili,mambo yakageuka na kubadili hewa ya pale.

Wakina Ban walipoona wamekamilisha kazi yao,walimpigia simu Fred aje aone mtu waliyemtuma wamuaibishe. Na Fred alipofika,alilidhika na kazi iliyofanyika ila huruma ilimuingia baada ya kumuona Junior akitambaa kwa sababu ya tumbo kumshika.

Hapo mwanzo alitaka kuona Junior anajisaidia mbele ya watu,lakini alijifikiria ni kwa nini afanye yale kwa mtu ambaye kazi yake ilikuwa ni kumcheka na kumtania?Kamwe hakushiriki kwenye kumuaibisha . Mawazo hayo ndio yalimfanya Fred kumuwahi Junior na kumuingiza kwenye taksi.

Sasa walishafika yalipo makazi yao na walimkuta Hans akiwa hana habari zozote zaidi ya jamaa yule kuchat na watu wake kwa kupitia simu.

“Vipi tena? Mbona leo mapema? Au na wewe umeungua makalio”.Hans alitania baada ya Junior kuingia.

“Wewe subiri tu!.”Junior alijibu kifupi na kukaa kitandani kwake huku zoezi la kuvua viatu vyake likifuata.

Hans hakufatilia maneno yale na wala hakuyatilia maanani zaidi ya kuendelea kufanya yake hadi pale alioona kalidhika

Kesho yake Junior akiwa na wakina Hans huko wanaposoma,alianza kutaniwa na watu ambao walishuhudia tukio zima lilivyokwenda.

“Jamaa gitaa zito hadi unajiachia mwenyewe.Ha haa.”Maneno kama hayo,Junior alikutaa nayo sana. Lakini maswali yakabaki kwenye kichwa cha Suarez pamoja na Hans.Kwa nini Junior ataniwe vile?

“Vipi kijana,mbona watu wanakuzonga hivyo?.”Suarez alitupa swali na Hans aliweka sikio vizuri kusikia kitakachomtoka Junior.

“We acha tu ndugu yangu.”Junior alijibu swali lile kiuchovu na kwa upole uliochanganyika na hali ya kujihurumia.Yote hiyo ni kwa sababu ya mzomeo uliokuwa unaendelea kumkuta pale alipokuwa anatembea na wale rafiki zake.

“Nini tena? Mbona umeishia kusikitika?.”Sua alizidi kuchimba.

“Daah!Jana yalinikuta yaliyomkuta Fred bwana.”Baada ya majibu hayo,Hans alishindwa kuvumilia kibana kicheko balikukiachia kitoke kwa uwezo wake wote.

“Kwa hiyo na wewe uliungua?.”Swali hilo toka kwa Suarez ndilo lililozidisha kicheko kwa Hans na kufanya akili ya Junior ijengeke kuwa ni Hans ndiye aliyefanya yote yale.

“Dah!Heri ingekuwa kuungua aisee.Mwenzako kidogo nijisaidie mbele ya watu. Mashuzi yalikuwa yanatoka kama stendi ya mabasi.”Jibu lile baada ya kupoteza kicheko kwa Hans na lilete huruma, likaongeza vicheko hata kwa Fred aliyekuwa kimya muda mrefu akisikiliza maongezi yale.

“Kwa hiyo ikawaje?.”Swali linguine toka kwa Suarez.

“Ndiyo hivyo.Mbele ya mtoto Eve na watu kama mia hivi.Kamanda napiga honi kama shabiby au Scandinavia linataka kusepa.”Junior aliongea kama utani ,lakini alikuwa kapania kulipa kisasi kwa Hans na hasira zilimzidi kila alipokuwa anasikia sauti ya Hans ikicheka.

“Kwa hiyo ulijisaidia mwanangu mwenyewe.”Hans huku akiwa na hali ya kucheka,alimuuliza Junior aliyekuwa anamachungu juu yake.

“Tena bora unyamaze boya wewe.”Junior alijibu kwa hasira.

“Sasa ninyamaze nini? Hapo ukute linanihisi mimi ndiye nimefanya.Acha ujinga wewe,tafuta mwizi kwa mwizi kwa vithibitisho na si kunusa kama mwizi.”Hans alitoa hali ya utani na kuweka usiriaz katika suala lile.

“Hujahisiwa,ni kweli umefanya na ni tabia yako.Hata Fred ulimfanyia hivyo majuzi.”Junior alithibitisha hisia zake juu ya Hans.

“Oya eeh,masela. Tuacheni hizo bwana.Sisi marafiki,hali hii itafanya tugombane bure.”Sua alionesha wasiwasi wake hivyo akaamua kutuliza zogo lile.

“Huyo boya,kazi kusingizia watu tu! Huyu nilimunguza kwa sababu ya kauli zak chafu.Sasa wewe umenifanya nini?. Msilete uboya wenu,mkitaka bifu semeni na sio kujidai mnatoa kesi zisizo zangu hapa. Na hamnipati ng’oo.Leo silali na nyie,maana mnaweza kunibandika hata gundi ili kesho nisionane na mtoto.”Maneno yalimwagika Hans na hapohapo akafata njia yake ambayo ilimpeleka hadi anaposihi.

Huko chumbani,Hans alichukua begi dogo na kuweka nguo zake baadhi.Kisha kama kawaida akatega mambo kwenye kabati lake na kuacha ujumbe wa kutolifungua kabati lile kwani chochote chaweza kutokea.

Hans akahama kile chumba kwa muda kwa kuhofia anachoweza kuja kufanyiwa na wakina Junior usiku au siku hiyo.

****

Baada ya kuondoka na wakina Junior kuthibitisha hilo. Junior akashindwa kutafuta njia mbadala ya kulipa kisasi chake kwa Hans.

Njia zikamwishia kabisa,na ndipo alipoenda kwa Fred na kujaribu kupata ushauri.

“Sasa hapa nafanyaje Mzee wa Upako?.”Junior alitupa swali kwa Fred baada ya kueleza nia yake iliyomshinda.

“Ndio kama nilivyokwambia. Twende kujaribu kuwaona wakina Ban.Wale wanaweza kusaidia kwa sana.” Fred alitoa pendekezo ambalo Junior aliona bora afanye hivyo.

****

Baada ya dakika kadhaa,Junior na Fred walikuwa kwenye chumba cha Wagumu wakieleza shida iliyowapeleka.

“Dah!Wazee kitambo sana sijawaona.Ishu zinaendaje.”Kamanda mkuu wa kikosi cha Wagumu,bwana Ban Diho alikuwa anaongea na wale vijana wawili.

“Tupo aisee. Ila tumekuja tuna shida moja tu!.”Junior alienda moja kwa moja katika kazi iliyompeleka pale.

“Tunakuzikiliza mwanangu”.Ban akatoa ukumbi kwa Junior.Naye Junior bila kukwepesha akaeleza kile kilichompeleka pale.

“Kwa hiyo hamjui Hans kaenda wapi,si ndio eeh.”Ban aliuliza baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa Junior.

“Ndio hivyo,halafu kaaribu mambo ndio kakimbia.Na demu ankutana naye tumoro,hivyo mimi nataka na yeye kesho yamkute.”Junior akakomelea nia yake.

“Okey. Kwa kuwa umechelewa kuja halafu kazi yenyewe inamuda mchache,basi tuachie elfu sabini ili tupige kazi.”Ban alitoa pendekezo ambalo Junior alilipinga vikali huku akionesha wazi kuwa hicho kiasi ni kikubwa sana kwa kazi ile.

“Oya ongea na mwenzako bwana. Kama mnaweza,kapigeni hiyo ishu wenyewe.Sisi hatuna cha kuwasaidia.”Ban alimuelekezea maneno hayo Fred.

“Kwani we Junii unataka kulipa kiasi gani?.”Fred alimuuliza Junior mbele ya wakina Ban.

“Mi labda niwpe thelethini tu! Tena naitoa kwa sababu basi tu!.”Junior alimjibu Fred.

“Kama ni thelathini,basi sisi tutakutafutia tu huyu jamaa yupo wapi,na tutakupa cha kufanya.”Ban alitoa msimamo wa kundi lao.

“Aaag! Sasa ndio mtakuwa mmefanya nini? Mi sitaki hiyo,nataka kazi yote mpige halafu mnipe na taarifa jinsi ilivyokuwa.”Junior alipingana na ile kauli ya Ban.

“Hapo Junii hutuelewi.Hiyo elfu sabini kwako utaona ndogo kwa kitu tutakachofanya. Huyo Hans wako atalia kama mtoto mdogo. Halafu hatutokuhadithia,ni wewe wenyewe utashuhudia jinsi jamaa anavyotaabika.”Sunday aliingilia yale maongezi ili kumvuta mteja wao.

“Okey.Poa basi.Mimi na elfu hamsini,nifanyieni kwa hiyo wazee.”Junior aliingia mwenyewe mtegoni bila kujua hata Fred yupo katika biashara hiyo.

“Aaag,kaka fanya sabini bwana.Wewe mwenyewe si unacheki tupo wangapi?.”Ban alimvuta Junior ali afanye vile anavyotaka.

“Oya tunapoteza muda. Mi nakuongezea elfu ishirini,halafu tukifika home,utanirudishia.”Fred alimaliza utata ambao ulikuwa unaendelea kwa muda ule.

“Poa.Nitakupa baada ya wiki moja kwa kuwa kwa sasa nipo majalala kiaina.”Junior alikubaliana na wazo la Fred na kisha wakafanya kama inavyotakiwa kufanywa.

“Hayo ndio mambo sasa. Kesho tutakupigia simu ni wapi uje ili umuone ndugu yako anavyoumia.Ikibidi njoo na kamera kabisa.”Ban alimaliza maongezi yale ya kijinga,na kumuacha Junior hana swali tena.

Fred na Junior wakajikusanya nguvu zao na kuanza kutoka mule chumbani kwaajili ya kuelekea kwao.

Baada ya mwendo kidogo kule nje ya chumba,Fred alizuga kama kasahau kitu kule chumbani kwa akina Ban walipotoka,hivyo alimuomba Junior amsubiri mara moja kwa ajili ya kuchukua kitu hicho.

Haikuwa kweli kuwa kasahau kitu,yeye alirudi kule kwa ajili ya kuchukua hela yake. Na kweli wakina Ban wakampatia bila hiyana.Fred akarudi alipomuacha Junior.

****

Huku kwa akina Ban,timu ikapangwa kama kawaida.Waliona jinsi kumpata Hans kwa muda ule,itakuwa ni shida.Hivyo walichukua jukumu la kwenda kummendea Eve. Eidha Eve angemfata Hans au Hans angemfata Eve,hiyo ingekuwa rahisi kwao kuwafatilia wale jamaa.Kazi ya upepelezi huo,ikaenda kama kawaida kwa Moi Shabala na Moses Frank.

Sunday Magembe,alipewa jukumu lake tena la kutafuta dawa na Ban yeye alikuwa ni mzee wa kutafuta maeneo tu!.

Kazi hiyo ilianza mara mja hasa kwa Ban na Sunday. Moi na Mose,wao kazi yao ilikuwa ianze kesho.

*****

Hakuna aliyejua Hans yupo wapi hadi kesho yake ilipofika ambapo Hans alionekana maeneo anayoishi Eve akiwa kakodi taksi kwa ajili ya kumchukua mrembo yule.

Moi na Mose walipoona kuwa kuna haja ya kuchukua usafiri,waliagiza haraka bodaboda ije ili iwe rahisi kwao kuwafatilia waendako.

“Baada ya dakika kama kumi na tano,Eve alitoka ndani anapoishi na kuifata taksi iliyokuwa inamsubiri. Akapanda ndani yake na safari ilianza huku Mose na Moi wakiwa makini kuifatilia ile taksi na kuwapa taarifa kila mara wenzao.

Walijua kuwa Hans anapenda sana kumpeleka Eve sehemu zenye maji,hivyo kuna barabara ambayo walipita,walijua wazi kuwa hawa wanaelekea sehemu fulani. Hisia hizo,zikasafirishwa na kuwafikia Sunday na Ban.

Nao wakina Sunday,wakajipanga kwa ajili ya mashambulizi hayo kwa kukusanya vitu muhimu na kwenda sehemu hiyo.

Hisia zao zilikuwa ni kweli.Baada ya dakika kadhaa za bodaboda na taksi kuwa barabarani,hatimaye waliingia mahala ambapo palikuwa ni kusudio lao.

Watu walikuwa wengi sana katika sehemu ile ambao ulikuwa ni ufukwe wa Mikadi.Ufukwe ambao hauna kawaida ya kujaza sana watu kama ule wa Coco.

Hans alkuwa ni mwenye tabasamu kila mara pale alipokuwa akimuangalia Eve jinsi alivyokuwa kapendeza.

WALIJUA kuwa Hans anapenda sana kumpeleka Eve sehemu zenye maji,hivyo kuna barabara ambayo walipita,walijua wazi kuwa hawa wanaelekea sehemu fulani. Hisia hizo,zikasafirishwa na kuwafikia Sunday na Ban.

Nao wakina Sunday,wakajipanga kwa ajili ya mashambulizi hayo kwa kukusanya vitu muhimu na kwenda sehemu hiyo.

Hisia zao zilikuwa ni kweli.Baada ya dakika kadhaa za bodaboda na taksi kuwa barabarani,hatimaye waliingia mahala ambapo palikuwa ni kusudio lao.

Watu walikuwa wengi sana katika sehemu ile ambao ulikuwa ni ufukwe wa Mikadi.Ufukwe ambao hauna kawaida ya kujaza sana watu kama ule wa Coco.

Hans alkuwa ni mwenye tabasamu kila mara pale alipokuwa akimuangalia Eve jinsi alivyokuwa kapendeza.

“Leo umependeza sana.”Hans alimwaga sifa kwa kimwana yule ambaye alichanua tabasamu pana usoni pake.Hiyo ni baada ya kupata sehemu moja yenye kivuli na kukaa.

“Nawe umependeza sana. Hans ila na maongezi na wewe,tofauti na yale ya siku zote.”Eve alitoa sifa na kufunguka kilichomkutanisha na Hans kwa wakati ule.

“Niambie tu!.”Hans alijibu bila kusitasita.

“Embu nisubiri kwanza nikachukue pale koni.”Eve alinyanyuka na akiwa na mavazi yake ya ufukweni na kwenda sehemu moja ambayo kunauzwa koni.

Huku nyuma Hans akabaki peke yake akipunga upepo na ndio muda huo huo Sunday aliutumia kufanya yake.

Sunday alienda pale alipo Hans na kisha kwa utaalamu mkubwa alijidai kajikwaa na kumdondokea Hans kwenye mapaja.

Kitendo kile kilimshitua Hans lakini hali ilimrudi na kuwa nzuri pale alipogundua ni Sunday. Alimsalimia kwa furaha na Sunday naye akaitikia salamu ile huku akimuomba msamaha kwa kilichotokea.

Baada ya salamu hiyo na msamaha,Sunday alititia eneo lile kwa furaha kubwa kwa kuamini mchezo alioucheza umetimia bila shaka.

Ukweli ni kwamba,wakati Sunday anamdondokea Hans,alikuwa kashika sindano ndogo zile za kubania karatasi. Sindano ile ndio alikuwa kaipaka dawa aliyokusudi.

Kitendo cha kumdondokea,kilimpa upenyo Sunday kumchoma kidogo Hans bila ya yeye kuhisi maumivu makali kama yale ya kumdondokea.

Baada ya kufanikiwa kumchoma na kisindano kile,aimuomba msamaha na kuondoka mahala pale akimuacha Hans hana hili wala lile.

Dakika tatu mbele,Eve alirudi na makopo mawili ya koni.Moja akampatia Hans na linguine akabaki nalo yeye,kisha taratibu wakaanza kujiburudisha.

“Mimi nachotaka kujua ni kama unahusika na mambo yaliyowatokea Fred na Junior.Maana wote wanalalamika kuwa ni wewe ndiye umefanya,sasa niambie ukweli wote ikibidi niwaite wote ili mpatane maana mtu kama Junior aliapa atakuua.”Eve alianzisha maongezi hayo baada ya kubugia vijiko kadhaa vya koni aliyonunua.

“Kwa hiyo na wewe unaamini.”Hans aliuliza.

“Naweza kuamini.Lakini najua huwezi kufanya vile kama hujachokozwa.”Eve aliweka wazi hisia zake.

“Okey.Kiukweli kabisa,Fred ni mimi ndiye nimefanya lakini Junior sifahamu aliyefanya.”Hans alijibu na kusikiliza Eve atatoa maamuzi gani.

“Sasa kwa nini ulimfanyia vile Fred?.”Eve alitupa kete nyingine ya swali.

“Wanazingua wale. Ujue siku ile kule Coco eti walinirekodi kwenye kamera wakati najirusha kwenye maji,bsi ikawa utani ni utani.Huyu Fred akawa hadi ananitukana,ndio nikaona bora nilipe.”Hans akatoa sababu ambayo ilimfanya Eve acheke kidogo na kuendelea.

“Ujue ni watoto sana. Sasa hiyo inawasaidia nini?.”Swali lilitupwa lakini lilikuwa halina kitu zaidi ya Hans kunyamaza huku kainamisha kichwa chake.

“We Hans,si nakuuliza?.”Eve alimshtua Hans lakini Hans kichwa kilikuwa vilevile.

“Wewe.”Eve aliita huku anamsukuma.

“Mmmh.”Masikini Hans aliitika huku udenda unamtoka kama vile teja.

“Khaaa! Hivi nyie watu mna matatizo gani? Ona huyu naye leo.”Eve alilalamika peke yake bila mtu yeyote kumfatilia.

“Kichefuchefu.”Hans alisema maneno hayo kwa sauti ya chini kabisa.Sauti ambayo ilimfanya Eve kuuliza tena alichokisema huku anapeleka uso wake karibu namdomo wa Hans ili asikie vizuri.

Kabla hata Hans hajarudia lele neno la kichefuchefu. Eve alitapikiwa usoni na matapishi yaliyotoka mdomoni kwa Hans.

Matapishi yale yalitoka kwa wingi kwani yalijumuisha vyakula vyote alivyokula Hans tangu asubuhi ya siku ile. Yote hayo yaliishia mwilini kwa Eve ambaye alikuwa kaganda kama barafu pale kitendo kile kilipokuwa kinatokea.

Watu ambao walikuwa maeneo yale,walishindwa kuvumilia kucheka na kushangilia kwa kile walichokuwa wanakiona,amahakika Hans alipatikana na aliaibika.

Baada ya kutapika,Hans aliyekuwa kama teja,alidondokea Eve miguuni na kumfanya Eve asiweze kusimama haraka kwa muda ule.

Macho ya Hans yakiwa yaona kwa mbali,ndipo alipomuona na Junior akiwa mmoja wa watu ambao wanamcheka,tena yeye alikuwa anapiga na picha,sijui za ukumbusho au nini.

Baada ya Hans kumuona Junior,aliongea kwa sauti ya chini huku anamuoneshea kidole Junior. Hapo hapo,usingizi mzito ukambeba.

Kazi ikabaki kwa Eve kujipapatua ili ajitoe mwilini mwa Hans ambaye alikuwa kalala usingizi wa hatari.

****

Ni baada ya dakika zisizopungua mbili,ndipo aibu ile ilipomtoka Eve. Matapishi ambayo ametapikiwa na Hans alienda kwenye maji ya ufukwe ule na kujisafisha na Eve alirudi katika hali kiasi fulani. Sasa ikabaki kazi ya kumnyanyua Hans aliyekuwa kajilaza pale kichangani hajitambuni.

Ilikuwa si shuhuri ya kitoto kumnyanyua mtu kama Hans,kwani kila aliyeombwa msaada wa kufanya hivyo,alihofiwa kutapikiwa. Akili kumkichwa zikatakiwa kuchuwa nafasi katika kichwa Eve.

Alichoona cha maana mwanamke yule wa shoka ni kukimbilia nje na kumtafuta dereva taksi mmojawapo na kuja naye hadi pale alipomuacha Hans amelala.

“Haikuwa rahisi wa kitoto kumbeba jamaa yule aliyekuwa kalala fo fo fo,hajitambui wala hajielewi yupo wapi kwa muda ule.

Baada ya kufanikiwa kumpandisha katika taksi,safari iliyofuata ilikuwa ni ya kwenda hospitali.Na moja kwa moja walimpeleka katika hospitali fulani iliyopo pale Msasani na mara moja Hans akaanza kupewa huduma ya kwanza ambayo ilichukua dakika kama kumi na tano.

Dakika kadhaa nyingine,Hans alizinduka mna kuanza kushangaa ilikuwaje mpaka akawa pale. Baada ya kuvuta kumbukumbu,ndipo alipokumbuka yale yote yaliyotokea kwenye ufukwe Mikadi,na hasira zilimpanda zaidi alipokumbuka sura ya Junior ikimchukua picha.

Kitanda cha hospitali alikiona si mahala pake tena. Na kwa kuwa alikuwa hajatundikiwa dripu,aliona ni bora anyanyuke haraka ili aende walipo wakina Junior na kutaka maelezo ya kina ya kwa nini kafanya yale yote.

Alinyanyuka na kuvaa viatu vyake.Kisha alitoka nje na kukutana na Eve akiwa kwenye benchi la kusubiria huduma za pale hospitali.

Alimpita bila hata kuongea naye,kitendo kilichomfanya Eve ashangae na kumuita kwa nguvu. Lakini Hans ni kama hakusikia sauti ile na wala hakuwa na mpango nayo zaidi ya kwenda anapojua yeye.

Eve akaona hayo mengine tena. Alichofanya ni kumkimbilia kisha akamshika began a kumuuliza kulikoni.

“Wewe na wale wajinga kule,mmepanga kuniaibisha. Mmmeniwekea madawa yenu kwenye koni ili nitapike na kulala,si ndio ee.”Hans alimjibu Eve kwa hasira.

“Hee jamani,yamekuwa hayo tena.Mimi naweza kufanya hivyo jamani?.”Eve alikumbwa na taharuki ya ajabu baada ya kusikia laumu zile zilizouvunja moyo wake.

“Ushindwe kufanya hivyo kwani wewe nani?Wewe Malaika?Wewe si binadamu kama mimi tu! Mwenye kinyongo na watu na wenye chuki zilizojikita moyoni mwake. Utashindwa nini kuniwekea madawa? Kuna kitu kinamshinda mwanamke? Kuna kitu kitakushinda wewe kama hunipendi mimi?.”Hans alilopoka maneno mengi na bila hata kusubiri Eve ajitetee,aliuputa mokono wa mrembo yule na kuanza kuondoka.

“Na mwenzako Junior uliyepanga naye mchezo wote,nilimuona akinichukua picha.Sasa atakuhadithia kitakachomkuta.Wajinga nyie.”Msumali wa maneno ulikomelewa na kinywa cha Hans,kisha jamaa yule mguu na njia ukashika nafasi huku akimuacha Eve kakamata kiuno kama anaangalia ngoma ya Kisambaa au Wadigo.Hakika alipatikana,uso ulimshuka kama ngozi ya chini ya shingo ya ng’ombe.

*******

Walijua kuwa Hans anapenda sana kumpeleka Eve sehemu zenye maji,hivyo kuna barabara ambayo walipita,walijua wazi kuwa hawa wanaelekea sehemu fulani. Hisia hizo,zikasafirishwa na kuwafikia Sunday na Ban.

Nao wakina Sunday,wakajipanga kwa ajili ya mashambulizi hayo kwa kukusanya vitu muhimu na kwenda sehemu hiyo.

Hisia zao zilikuwa ni kweli.Baada ya dakika kadhaa za bodaboda na taksi kuwa barabarani,hatimaye waliingia mahala ambapo palikuwa ni kusudio lao.

Watu walikuwa wengi sana katika sehemu ile ambao ulikuwa ni ufukwe wa Mikadi.Ufukwe ambao hauna kawaida ya kujaza sana watu kama ule wa Coco.

Hans alkuwa ni mwenye tabasamu kila mara pale alipokuwa akimuangalia Eve jinsi alivyokuwa kapendeza.

“Leo umependeza sana.”Hans alimwaga sifa kwa kimwana yule ambaye alichanua tabasamu pana usoni pake.Hiyo ni baada ya kupata sehemu moja yenye kivuli na kukaa.

“Nawe umependeza sana. Hans ila na maongezi na wewe,tofauti na yale ya siku zote.”Eve alitoa sifa na kufunguka kilichomkutanisha na Hans kwa wakati ule.

“Niambie tu!.”Hans alijibu bila kusitasita.

“Embu nisubiri kwanza nikachukue pale koni.”Eve alinyanyuka na akiwa na mavazi yake ya ufukweni na kwenda sehemu moja ambayo kunauzwa koni.

Huku nyuma Hans akabaki peke yake akipunga upepo na ndio muda huo huo Sunday aliutumia kufanya yake.

Sunday alienda pale alipo Hans na kisha kwa utaalamu mkubwa alijidai kajikwaa na kumdondokea Hans kwenye mapaja.

Kitendo kile kilimshitua Hans lakini hali ilimrudi na kuwa nzuri pale alipogundua ni Sunday. Alimsalimia kwa furaha na Sunday naye akaitikia salamu ile huku akimuomba msamaha kwa kilichotokea.

Baada ya salamu hiyo na msamaha,Sunday alititia eneo lile kwa furaha kubwa kwa kuamini mchezo alioucheza umetimia bila shaka.

Ukweli ni kwamba,wakati Sunday anamdondokea Hans,alikuwa kashika sindano ndogo zile za kubania karatasi. Sindano ile ndio alikuwa kaipaka dawa aliyokusudi.

Kitendo cha kumdondokea,kilimpa upenyo Sunday kumchoma kidogo Hans bila ya yeye kuhisi maumivu makali kama yale ya kumdondokea.

Baada ya kufanikiwa kumchoma na kisindano kile,aimuomba msamaha na kuondoka mahala pale akimuacha Hans hana hili wala lile.

Dakika tatu mbele,Eve alirudi na makopo mawili ya koni.Moja akampatia Hans na linguine akabaki nalo yeye,kisha taratibu wakaanza kujiburudisha.

“Mimi nachotaka kujua ni kama unahusika na mambo yaliyowatokea Fred na Junior.Maana wote wanalalamika kuwa ni wewe ndiye umefanya,sasa niambie ukweli wote ikibidi niwaite wote ili mpatane maana mtu kama Junior aliapa atakuua.”Eve alianzisha maongezi hayo baada ya kubugia vijiko kadhaa vya koni aliyonunua.

“Kwa hiyo na wewe unaamini.”Hans aliuliza.

“Naweza kuamini.Lakini najua huwezi kufanya vile kama hujachokozwa.”Eve aliweka wazi hisia zake.

“Okey.Kiukweli kabisa,Fred ni mimi ndiye nimefanya lakini Junior sifahamu aliyefanya.”Hans alijibu na kusikiliza Eve atatoa maamuzi gani.

“Sasa kwa nini ulimfanyia vile Fred?.”Eve alitupa kete nyingine ya swali.

“Wanazingua wale. Ujue siku ile kule Coco eti walinirekodi kwenye kamera wakati najirusha kwenye maji,bsi ikawa utani ni utani.Huyu Fred akawa hadi ananitukana,ndio nikaona bora nilipe.”Hans akatoa sababu ambayo ilimfanya Eve acheke kidogo na kuendelea.

“Ujue ni watoto sana. Sasa hiyo inawasaidia nini?.”Swali lilitupwa lakini lilikuwa halina kitu zaidi ya Hans kunyamaza huku kainamisha kichwa chake.

“We Hans,si nakuuliza?.”Eve alimshtua Hans lakini Hans kichwa kilikuwa vilevile.

“Wewe.”Eve aliita huku anamsukuma.

“Mmmh.”Masikini Hans aliitika huku udenda unamtoka kama vile teja.

“Khaaa! Hivi nyie watu mna matatizo gani? Ona huyu naye leo.”Eve alilalamika peke yake bila mtu yeyote kumfatilia.

“Kichefuchefu.”Hans alisema maneno hayo kwa sauti ya chini kabisa.Sauti ambayo ilimfanya Eve kuuliza tena alichokisema huku anapeleka uso wake karibu namdomo wa Hans ili asikie vizuri.

Kabla hata Hans hajarudia lele neno la kichefuchefu. Eve alitapikiwa usoni na matapishi yaliyotoka mdomoni kwa Hans.

Matapishi yale yalitoka kwa wingi kwani yalijumuisha vyakula vyote alivyokula Hans tangu asubuhi ya siku ile. Yote hayo yaliishia mwilini kwa Eve ambaye alikuwa kaganda kama barafu pale kitendo kile kilipokuwa kinatokea.

Watu ambao walikuwa maeneo yale,walishindwa kuvumilia kucheka na kushangilia kwa kile walichokuwa wanakiona,amahakika Hans alipatikana na aliaibika.

Baada ya kutapika,Hans aliyekuwa kama teja,alidondokea Eve miguuni na kumfanya Eve asiweze kusimama haraka kwa muda ule.

Macho ya Hans yakiwa yaona kwa mbali,ndipo alipomuona na Junior akiwa mmoja wa watu ambao wanamcheka,tena yeye alikuwa anapiga na picha,sijui za ukumbusho au nini.

Baada ya Hans kumuona Junior,aliongea kwa sauti ya chini huku anamuoneshea kidole Junior. Hapo hapo,usingizi mzito ukambeba.

Kazi ikabaki kwa Eve kujipapatua ili ajitoe mwilini mwa Hans ambaye alikuwa kalala usingizi wa hatari.

****

Ni baada ya dakika zisizopungua mbili,ndipo aibu ile ilipomtoka Eve. Matapishi ambayo ametapikiwa na Hans alienda kwenye maji ya ufukwe ule na kujisafisha na Eve alirudi katika hali kiasi fulani. Sasa ikabaki kazi ya kumnyanyua Hans aliyekuwa kajilaza pale kichangani hajitambuni.

Ilikuwa si shuhuri ya kitoto kumnyanyua mtu kama Hans,kwani kila aliyeombwa msaada wa kufanya hivyo,alihofiwa kutapikiwa. Akili kumkichwa zikatakiwa kuchuwa nafasi katika kichwa Eve.

Alichoona cha maana mwanamke yule wa shoka ni kukimbilia nje na kumtafuta dereva taksi mmojawapo na kuja naye hadi pale alipomuacha Hans amelala.

“Haikuwa rahisi wa kitoto kumbeba jamaa yule aliyekuwa kalala fo fo fo,hajitambui wala hajielewi yupo wapi kwa muda ule.

Baada ya kufanikiwa kumpandisha katika taksi,safari iliyofuata ilikuwa ni ya kwenda hospitali.Na moja kwa moja walimpeleka katika hospitali fulani iliyopo pale Msasani na mara moja Hans akaanza kupewa huduma ya kwanza ambayo ilichukua dakika kama kumi na tano.

Dakika kadhaa nyingine,Hans alizinduka mna kuanza kushangaa ilikuwaje mpaka akawa pale. Baada ya kuvuta kumbukumbu,ndipo alipokumbuka yale yote yaliyotokea kwenye ufukwe Mikadi,na hasira zilimpanda zaidi alipokumbuka sura ya Junior ikimchukua picha.

Kitanda cha hospitali alikiona si mahala pake tena. Na kwa kuwa alikuwa hajatundikiwa dripu,aliona ni bora anyanyuke haraka ili aende walipo wakina Junior na kutaka maelezo ya kina ya kwa nini kafanya yale yote.

Alinyanyuka na kuvaa viatu vyake.Kisha alitoka nje na kukutana na Eve akiwa kwenye benchi la kusubiria huduma za pale hospitali.

Alimpita bila hata kuongea naye,kitendo kilichomfanya Eve ashangae na kumuita kwa nguvu. Lakini Hans ni kama hakusikia sauti ile na wala hakuwa na mpango nayo zaidi ya kwenda anapojua yeye.

Eve akaona hayo mengine tena. Alichofanya ni kumkimbilia kisha akamshika began a kumuuliza kulikoni.

“Wewe na wale wajinga kule,mmepanga kuniaibisha. Mmmeniwekea madawa yenu kwenye koni ili nitapike na kulala,si ndio ee.”Hans alimjibu Eve kwa hasira.

“Hee jamani,yamekuwa hayo tena.Mimi naweza kufanya hivyo jamani?.”Eve alikumbwa na taharuki ya ajabu baada ya kusikia laumu zile zilizouvunja moyo wake.

“Ushindwe kufanya hivyo kwani wewe nani?Wewe Malaika?Wewe si binadamu kama mimi tu! Mwenye kinyongo na watu na wenye chuki zilizojikita moyoni mwake. Utashindwa nini kuniwekea madawa? Kuna kitu kinamshinda mwanamke? Kuna kitu kitakushinda wewe kama hunipendi mimi?.”Hans alilopoka maneno mengi na bila hata kusubiri Eve ajitetee,aliuputa mokono wa mrembo yule na kuanza kuondoka.

“Na mwenzako Junior uliyepanga naye mchezo wote,nilimuona akinichukua picha.Sasa atakuhadithia kitakachomkuta.Wajinga nyie.”Msumali wa maneno ulikomelewa na kinywa cha Hans,kisha jamaa yule mguu na njia ukashika nafasi huku akimuacha Eve kakamata kiuno kama anaangalia ngoma ya Kisambaa au Wadigo.Hakika alipatikana,uso ulimshuka kama ngozi ya chini ya shingo ya ng’ombe.

HANS alikamata usafiri wa bajaji na moja kwa moja akaomba umpeleke yalipomakazi yake ya zamani.Kule ambapo alihama kwa kuhofia wakina Junior wangemtenda.

Baada ya nusu saa,alikuwa tayari chumbani na kwa bahati nzuri aliwakuta rafiki zake wote wametulia wanafanya yao.

“Ehee,we boya.Kwa hiyo mkamuua kupanga na yule mchawi wa kike ili mniwekee dawa kwenye koni,nikila nitapike,si ndio ee.”Hans alilianzisha baada ya kufika mule chumbani.

“Acha kumtukana mke wangu,nitakuharibia balaa.Wewe ulichonifanyia kizuri ee.”Junior alijibu mapigo bila kuogopa hasira alizokuwa nazo Hans.

“Anamuita Malaika wangu Mchawi?.”Fred naye akanunua ugomvi.

“Mbwa nyie mmepanga na yule fala kuniaibisha mimi?Leo mtanitambua.”Hans hakuwa na subira juu ya maamuzi yake zaidi ua kwenda pale kitanda cha chini na kuanza kumshushia ngumi za haraka Junior ambaye hakutegeea kama Hans angeweza kumvamia kwa muda ule mfupi.

Fred alipoona mwenza ke Junior anapokea kichapo cha kushtukiza halafu mpango walipanga wote na isitoshe yeye ndiye anahusika sana,aliruka toka kwenye kitanda chake cha juu na kisha akamkumba Hans na kumrushia kwa pembeni na bila kusita alijiweka sawa kwa kunja ngumi tayari kwa mpambano baina yake na Hans. Mtakatifu Fred alikuwa kabadilika na kuwa mtaka tifu na yeyote.

Junior alinyanyuka haraka kitandani huku akiwa na maumivu ya ngumi nyingi za mbavu na tumbo alizopigwa na Hans,na moja kwa moja akataka kumkumba Hans pale alipo,lakini alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwenye mikono ya Suarez,ikimuamulia asifanye lile alilokusudia.

“Mnataka kufanya nini sasa?Mnataka kufanya nini? Mnataka kupigana au kuongea yaishe kistaarabu?Nijibuni sasa hivi ili niwaachie ukumbi.”Suarez aliongea kwa sauti ya juu iliyochanganyikana na hasira ndani yake.

“Nakwambia leo naua mtu humu.Tuachie ukumbi.”Hans alijibu swali la Suarez naye akiwa na hasira.

“Tuachie ukumbi tumuoneshe huyu choko kuwa na sisi tuliumia kama yeye.”Fred alijibu kwa ujasiri bila kujali yatakayomkumba mbele.

“Okey.”Suarez alijibu nakutoka pale katikati aliposimama na kwenda mlango wa kutokea. Hapo aliuchomoa ufunguo wa mlango ule na kutoka nao nje,ambapo aliufunga mlango ule kwa nje na kuondoka zake akiwaacha wakina Hans wanatunishiana misuli mule ndani.

Sasa Hans alikuwa uso kwa uso na Fred pamoja Junior. Licha ya kutapika chakula karibu chote,lakini alikuwa anajiamini kuwa anaweza kupambana na sura zile ambazo zilikuwa zimejishindilia chakula muda si mrefu.

Hatimaye mpambano ukaanza kwa Hans kutaka kumfuata Junior maana ndiye alikuwa anahasira naye zaidi na wakati huo alisahau kuwa Fred naye anahasira na yeye kwa kumuunguza siku chache zilizopita.

Kitendo cha kumfata Junior pale alipo,kilikutana na upinzani mkubwa wa Fred kwani alirusha ngumi moja ambayo ilienda vizuri na kumkuta Hans kwenye paji la uso,au komwe au forehead kwa kiingereza,na ngumi hiyo ilimfanya Hans kutoamini kama kapigwa yeye na tena kapigwa na Fred mtu ambaye ujanja kamfundisha yeye.

“Boya umenipiga ngumi?.”Hans aliuliza huku haamini kilichotokea.

“Ulidhani nimesahau ulivyounguza suruali yangu?.”Fred alimuuliza huku anamfuata kimabavu Hans.

Hans akaona sasa kapatikana. Alichofanya ni kujitutumua ili apambane kiume sasa kwani alidhani Fred hawezi kupigana kutokana na ulokole wake,lakini ndiyo hivyo,Fred aliweka nia ya kumuumiza Hans.

Mara Hans alimrukia Fred kwa fujo kwa kumkumba na bega lake, ambapo alipiga maeneo ya tumboni kama wafanyavyo wanamieleka.Pigo lile lilimfanya Fred alie kama mbwa aliyepigwa na jiwe tumboni au kichwani.

Ni pigo moja linaloweza kukufanya utapike au utoe hewa chafu.Hans alimpa hilo Fred na kudondoka naye karibu kabisa na kwa Junior.

Junior alipoona mwenzake anasurubika,naye akaanza kumsaidia Fred kwa kumkanyaga Hans. Kwa kuwa Hans alikuwa juu na Fred chini,basi ilikuwa rahisi kwa Junior kumsurubisha Hans kwa kumkanyaga.

Hali ilikuja kumbadilikia Junior baada ya Hans kuudaka mguu wake na kuanza kunyanyuka huku bado kaushikilia. Wakati huo Fred alikuwa hoi pale chini kwa kipigo alichokipokea kwa Hans.

Sasa mguu wa Junior ulikuwa umekamatwa na Hans.Junior akawa hana mawazo ya haraka juu ya nini cha kufanya .Na wakati huo Hans alikuwa amenyanyuka wima, na kuanza kumsukumia ukutani ambapo Junior alikuwa anarudi nyuma huku anarukaruka kama kangaroo.

Walipofika ukutani,Hans alizidi kuutanua mguu wa Junior hadi akaonekana kama anapiga msamba. Junior uso ulikuwa katika kuchanganyikiwa na jinsi Hans alivyokuwa anamchanisha msamba,ndivyo Junior naye alikuwa anazidi kuumia.

“Nyie si makamanda,si mnaweza kupigana.Haya sasa,nipigeni.”Hans aliongea huku kamchanisha msamba Junior pale ukutani. Wakati huo Fred alikuwa akigaa gaa kwa maumivu pale chini.

Mara Hans aliuachia mguu wa Junior na kuanza kumwandamisha kwa makonde ya nguvu.Makonde ambayo Junior aliona ni bora achutame na kuziba kichwa chake kama vile ameona au anavamiwa na nyuki. Hans akawa ametawala kile chumba.

Zogo lile lilikuja kuisha baada ya mlango kufunguliwa na kuingia mkufunzi anayesimamia nidhamu kwa wanachuo, pamoja na waziri mkuu wa chuo kile ambaye ni Eve na huku nyuma alifatiwa na Suarez.

“Wewe embu muache ,mwenzako.”Mkufunzi alimfokea Hans huku anamfuata na kumuondoa pale alipokuwa anamwandamisha Junior kwa makonde.

“Nitawaua mimi. Mimi siyo wakunichezea kama huyu mnayemtuma aweke madawa kwenye chakula changu,nitawaua nawaambieni.”Hans Liongea huku akipumua kwa kasi kutokana na ngumi nyingi alizozirusha kumchosha.

“Nyie nyanyukeni hapo,nifateni ofisini.”Yule kiongozi alitoa amri na yeye akaanza kutoka mule chumbani.

Junior na Fred walinyanyukla taratibu na kuanza kumfata mkufunzi yule wakati huo Hans alishatoka. Eve na Saarez walikuwa wa mwisho.

*****

Huko ofisini,kesi ilisomwa na kila mtu aliongea sababu zake za kufanya yale yote lakini kamwe hawakuthubutu kuwataja wagumu au kumtaja Eve kuwa ndiye mwanamke wanayemgombania.

“Kwa hiyo wewe Junior nani aliyekuumiza tumbo?.”Yule muu wa nidhamu kwa wanafunzi alimuuliza Junior.

“Ni huyu hapa Hans.”Junior alijibu kwa uhakika.

“Sijafanya hivyo kwa huyu boya.Ila kwa huyu kweli mimi nimefanya.”Hans alijitetea huku anakubali kosa linguine.

“Kwa nini ulifanya hivyo?.”Mkufunzi alimuuliza Hans.

“Anamatusi na kejeli,nilikereka na tabia hiyo aliyonifanyia.”Hans alijibu.

“Na ni nani aliyekupa madawa hadi ukamtapikia Waziri?.”Mkufunzi alitupa swali kwa Hans.

“Ni huyu boya.Nilimuona kabisa ananipiga na icha wakati nasinzia.”Hans alijibu kwa kumtaja Junior.

“Ni kweli?.”Swali kwa mkufunzi kwenda kwa Junior.

“Ndiyo,mimi nilihusika kufanya hivyo lakini sikuweka kwenye koni bali najua mwenyewe nilichofanya atapike.”Junior alikubali kosa.

“Kwa nini ulifanya hivyo?.”Swali linguine kwenda kwa Junior.

“Ni kwa sababu yeye aliniwekea madawa ya kuharisha kwenye chakula changu.”Junior alijibu.

“Sasa mbona anakataa kuwa hajakuwekea? Au umemuhisi tu! Maana yeye hadi kakuona kwenye tukio.Wewe kwenye tukio lako alikuwepo nani ukimtoa Waziri?.”Mkufunzi alizidi kupekua ili apate jibu kamili.

Wakati huo Eve na Suarez nao walikuwepo wakifatilia ile kesi kwa makini.

“Sikuona mtu,ila baada ya kuumia sana,Eve alikuja na Fred na kuninyanyua pale nilipokuwepo.”Junior alijibu kwa usahihi swali lile.

“Waziri,ulimuita huyu Fred?.”Swali sasa likamgeukia Eve.

“Hapana.Mimi nilishangaa anajiunga na mimi kumuokoa Junior.”Eve nae alijibu kiusahihi swali lililomkabiri.

“Wewe Fred,ulijuaje kama Junior yupo pale?.”Fred naye aliulizwa lakini alikaa kimya.

“Okey.Labda swali gumu.Ngoja nijaribu hili. Unahusika na kumwekea Junior dawa ya kuhara?”.Fred aliulizwa swali na bila kusita alilijibu na kutoa sababu.

“Ndiyo nilihusika na nilifanya vile kwa kuwa alishiriki kwenye kushangilia pale nilipoaaibika. Na pia nilifanya vile ili nipate kampani ya kumkomoa huyu mjinga.”Fred alijibu swali la mkufunzi na kuwafanya Junior,Eve na Suarez kushikwa na butwaa.

“Nilijua tu!Mnazungukana wenyewe. Na uzuri mmeongea ukweli wenu,mmeokoka.”Mkufunzi aliyasema hayo huku akifunga kitabu kimoja kilichokuwa na makaratasi ambazo mara nyingi alikuwa anatolea barua za kusamisha wanachuo humo.

“Ina maana we boya ndiye uliyeniwekea dawa kwenye msosi?.”Junior allimgeukia Fred na kumuuliza swali hilo.

“Sio msosi,yale maji uliyopewa pale kabla hujaanza kupiga gitaa.Walewale niliokupeleka kwao,ndio waliiga mzigo mzima.”Fred aliongea na kumfanya Junior ashikwe na kigugumizi na wakati huo Eve na Suarez walikuwa hawaamini kama Fred naye kawa Mafia vile.

“Humu sitaki ugomvi kabisa. Nataka amani. Mmenusurika kusimamishwa chuo,msifanye nifanye hivyo,sawa?.”Mkufunzi alitoa rai yake na wote wakakubali lile suala kwa wakati ule,lakini walipanga kulianzisha baada ya kutoka mule.

“Na vilevile,huko mwendako,nikisikia mmepigana tu! Nakuja kuwasimamisha wote. Na hakuna kuhama chumba,wote mtakaa mulemule ili tuone mtafanya nini. Atakayemfanya kibaya mwenzake,wote mtaubeba msalaba,sawa?.”Mkufunzi aliongeza sheria iliyowanyong’onyeza wenye visasi.

Baada ya kesi ile,waliruhusiwa kutoka mule ofisini na kurudi chumbani kwao ambapo walikaa wamechuniana kama bi mkubwa na bi mdogo wamegombana

BAADA YA SIKU TATU.

Wakiwa hawana muda wa kuongea na kila mtu akiwa kivyake,mara kila mmoja kwa muda wake alipokea ujumbe kwa njia ya simu uklimtaka kufika eneo moja ambapo kulikuwa na ghorofa linajengwa. Ghorofa hilo siku hiyo lilisimamishwa kujengwa,hivyo meseji ile iliwaomba wale jamaa watatu waende pale.

Ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Eve na uliwataka kila mmoja afike pale muda wa saa nane mchana.

Japo ni ujumbe unaofanana lakini hakuna aliyejua kuwa Eve kawaita wote waende mahala pale. Kila mmoja alidhani ataenda pale peke yake. Kwa upande wa Hans yeye aliona ndio muda muafaka wa kwenda na kumwomba msamaha Eve kwa maneno aliyomtamkia siku mbili nyuma.

Huku Junor na Fred,wao waliwaza kwenda kutoa yao yaliyo moyoni.

Hatimaye saa saba na nusu ilipotimia,kile chumba cha hawa wanachuo kilikuwa hakina mtu bali wote walienda walipoitwa,kasoro Suarez ambaye yeye hakupata ujumbe wa Eve,ila naye hauwepo chumbani.

Muda huo wa saa saba ndipo kwenye lile ghorofa palitokea tafrani nyingine.Sura tatu zisizopendana zilikuwa zinaangaliana.

“Mmefata nini hapa.”Swali lilimtoka Hans.

“Niwashangae nyie,kazi kumfatilia mtu mgongoni kama mikia.Mnataka nini hapa.”Fred naye akaleta ubabe wake.

“Halafu mimi na hasira na wewe boya. Yaani wewe wa kuniwekea madawa mimi.Halafu bado na huku umenifuata.”Junior hakuwa nyuma kuonesha hasira zake juu ya Fred.

“Hapa wote tunahasira.Ila mkitaka hasira zangu ziondoke,sepeni hapa fasta.”Hans alitoa pendekezo ambalo lilipingwa vikali na matokeo yake likaanzisha vurugu nyingine.

Wale jamaa walianza kupigana tena na safari hii ulikuwa ni ugomvi wa ajabu kupita maelez. Wote watatu walikuwa wanapigana kwa kujitegemea.Kulikuwa hakuna kuchangiana.

Kipigo kiliendelea kwa dakika kama tano. Waligalagazana kwenye vumbi la ghorofa hadi wakawa kama wameoga simenti. Hakika walikuwa wamepania kuumizana.

Ugonvi ule ulisimama baada ya Eve kuingia akiwa na Suarez pamoja na jamaa mmoja mrefu na mweusi kiasi lakini akiwa ni mtanashati wa kutupwa.

Jamaa yule alivalia suti nyeusi aina ya tuxedo iliyokaa vyema mwilini mwake.Mguuni alivaa viatu vya gharama aina ya Gucci,na usoni alifunika macho yake kwa miwani ya D&G,hakika alipendeza hasa na marashi aliyojipulizia,basi ndio kabisa aliwaacha hata wale aliokutana nao njiani hoi.

“Nyie nini tena. Yaani kama matoto,sasa mnapigania nini?.”Eve aliwauliza baada ya vijana wale kutulia.

“Haya maboya kila mahala yananifata.”Junior alijibu huku uso wake uliwa katika mpauko uleule.

“Hawajakufuata.Mimi niliwaita mwenyewe ili wote mje hapa.Niliona nikiita na kuwataarifu kuwa wote mtakuwepo,mngetaa kuja.”Jibu hilo liliwafanya wale jamaa watulie huku wakiwa wanamwangalia yule mgeni aliyekuja naye Eve.

“Okey.Tuyaache hayo.Mimi niliwaita hapa ili umalize ugomvi wenu hasa ukizingatia mimi ndiye sababu kubwa.

Nia kubwa ya mimi kuwataka muwe mnakutana na mimi,ni kukusanya data ambazo zitanisaidia katika uendeshaji wa kipindi changu.

Kumbukeni mimi ni muandishi wa habari,na nilipata ofa ya kwenda kutangaza radio mojawapo kubwa hapa Tanzania.Nilitakiwa kuendesha kipindi cha mapenzi,hivyo wale wanaotaka kuniajiri walinitaka nisomee uandishi wa habari na wakati huo nakusanya data ambazo zitanifanya nikubalike kirahisi kwenye lile shirika habari.

Ndipo wazo lilikuja la kuwatumia nyie. Yale maongezi yenu,nilikuwa nayarekodi japo si yote hasa pale nilipokuwa naingia ndani ya maji.Ila nje ya hapo,nimerekodi yote na uongozi wangu umepitia na kukubali kazi yangu.Hivyo mwenzenu nimeajiriwa sababu yenu.”Eve aliyasema hayo huku akiwa ametabasamu.

“Pia sitaki kuwaacha hivi hivi,nitawalipa kiasi cha fedha kwa usumbufu niliowapa.”Eve aliweka nyongeza ya maneno yake na kisha alimuita yule mtanashati na kumwambia afanye kile alichokusudia.

Yule jamaa akatoa simu yake ndogo lakini yenye muonekano wa kuwa na gharama kubwa mno.

Akaomba namba za simu za wale jamaa na kisha kila mmoja akamtumia milioni moja moja kwakupitia mitandao wanayoitumia. Wakina Hans walifurahia sana ile kitu.

“La mwisho jamani.Najua mnanipenda sana ila nataka mumjue shemeji yenu. Ni huyu hapa,anaitwa Frank Masai. Yeye ni mwandishi mkubwa hapa Afrika lakini kwa sasa anafanya kazi BBC,shirika la habari la Uingereza.”Eve alimtambulisha yule jamaa mtanashati kwa wakina Hans jambo lililowafanya lile tabasamu kuwatoka.

“Ina maana swaga zote zile tulizokuwa tunakuletea,kumbe mwenzetu unatusanifu?Hadi tunagombana,kumbe tayari unamtu. Dah! Kweli umetuweza.”Junior aliongea kiupole.

“Mimi niliwaambia lakini.”Suarez aliongea kwa mara ya kwanza tangu afike pale.

“Kwa hiyo na wewe unajua hili?.”Hans alimuuliza Sua.

“Mi ndio nimejua leo. Lakini niliwahi kuwaambia mumuulize kwanza. Nyie mkajidai wazee wa swaga,haya mmekosa. Na nyie mmekuwa THE LOST BOYS. Kama tulivyowaita WAGUMU”.Suarez alizidi kuchonga domo.

“Okey.Nadhani mkataba wetu umeishia hapa.Ni kama mlivyonitumaga kwa Ban,nikatimiza. Na leo nimetimiza kingine. Kwaherini,na endeleeni kupigana,mimi nimemaliza.”Eve aliongea hayo na kumshika mpenzi mkono na kutoka kwenye ghorofa lile kwa madaha.

Huku nyuma wakabaki wale vijana wane wamesimama wasijue wanafanya nini.

“Dah!Kweli the lost boys ndio sisi.”Fred aliongea huku anakaa chini.

“The lost boy mwenyewe bwana,mimi sijashindwa.”Hans alijitetea kwa sauti ya juu.

“Kwani mwanangu uliwahi kumla mate kweli?.”Fred alimuuliza Junior.

“Aaah,zilikuwa zuga tu! Nimle mate demu gani hili,baya tu. Kwani na wewe uliwahi kumchora?.”Junipr alijibu na kumuliza swali Fred.

“Aaag.Kuchora kitu gani,labda hapa mzee wa masayansi.Oya nasikia ulimgonga huyu manzi.”Fred alimuuliza Hans.

“Aah. Demu mwenyewe hana mvuto,nitamgongaje mimi.Hana sifa za kugongwa na mimi.”Hans alijibu na yeye huku anakaa chini kama Fred.

“Kwa hiyo sisi ni The Lost Boys”.Fred alisema maneno hayo.

“Hilo jina silitaki.jiiteni wenyewe”.Hans akatoa onyo.

“Nyie ni The Lost Boys,hamna kubisha.”Suarez aliingilia yale maongezi na kufanya wale THE LOST BOYS kumwangalia kwa kumtamani,na mwisho wa siku walimkamata na kuanza kumwagia vumbi la mule kwenye ghorofa.

Suarez akapauka balaa.Hakukubali kufanyia vile. Akainuka haraka na kuanza kuwafukuza wale jamaa watatu.

Wale jamaa walipoona hivyo,wakaanza kukimbia kwenda nje huku Suarez akiwafuata kwa nyuma kwa kasi ya ajabu.

Mbele kidogo,walimuona Eve na mpenzi wake Frank wakiwa wanakaribia kufika kwenye gari lao aina ya Benz. Waliwapita kwa kasi yam shale hadi wale wapenzi wawili wakabaki wamesimama huku wanawaangalia wale The lost boys.

Haijapita hata sekunde, akapita Suarez kapauka balaa. Kilichofuata hapo ni tabasamu tu kwa wale wapenzi wawili.

Kwa mbele,Hans alimchenga Suarez na kuzunguka ambapo alitokea nyuma ya gari la akina Eve. Hakuna aliyemuona Hans kati ya Eve na Frank,hivyo upenyo huo Hans aliutumia kwa kunyata na kuziunga kamba mbili za viatu ambavyo alivaa mpenzi wa Eve.

Baada ya kufanikiwa,alirudi nyuma kwa kunyata na kwenda kule ambapo wenzake wapo. Aliwakuta wanagalagazana wenye dimbwi ambalo llina maji ya mvua,na yeye bila kufikiria,akachukua ndoo na kuanza kuyachota maji yale na kuwamwagia. Mara kibao kikamgeukia,Fred na washirika wake,wakampora ndoo na kutaka kumuogesha maji yale.

Hans kuona hivyo,akaanza kukimbia lakini anaelekea kule walipo Eve na Frank. Kufika pale,Hans akakaa mbele hatua kama tano ya mpenzi wa Eve.Fred akiwa na ndoo ya maji ya kwenye dimbwi,alifika na kuyamwaga kumwelekea Hans,lakini Hans aliinama na maji yale yakamkuta Frank.

Kimya kikachukua nafasi yake huku kila mmoja akiwa anaogopa kwa kile kilichotokea.

Fred na ndoo yake huku matone ya maji yakimmwagika,Junior naye akiwa anatweta kwa kukimbia sana hali ambayo hata Suarez anayo,walibaki wa mesimama wakiangalia ni nini hatma yao baada ya mpenzi wa Eve kukaa vizuri.

Hatimaye Frank aliamua kutaka kuwakimbiza lakini zile kamba ambazo amefungwa miguuni na Hans,zikamzuia na kumdondosha lakini uzuri hakudondokea kifua wala kidevu,aliweza kujibalansi na kujikuta akiwa kama anapiga pushapu.

Wale The Lost Boys walianza kucheka kitendo kile. Na kwa aibu kubwa,mpenzi wa Eve alinyanyuka haraka na kuingia garini.

Huku nje Fred,Hans,Junior na Suarez walihisi labda jamaa atatoka na bastola,wakaamua kukimbia huku wakirukaruka kwa furaha wakitamka kwa nguvu na sauti ya juu.

“WE ARE THE LOST BOYS.” Yaani wao ni walioshindwa.

MWISHO.

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment