SIMULIZI

Ep 03: The Escrow Mission

SIMULIZI The Escrow Mission Episode 01
SIMULIZI The Escrow Mission Episode 03

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi: The Escrow Mission
Sehemu Ya Tatu (3)

§§§§
Kenya Lodge ilikuwa tulivu jioni hiyo, katika kaunta ya baa kulikuwa na watu wa kuhesabika kama kumi na tanoi hivi. Kamanda Amata akapita pale akiwa na Cheupe wameshikana kimahaba.

“Ah! Kaka unaenda kujifaidia tu uuuuuh!” alisikika mlevi mmoja akipiga kelele kumwambia Amata ambaye hakufuatilia maneno hayo. Wakazipanda ngazi mpaka ghorofa waliyotaka kufika. Kabla ya kufungua mlango, Cheupe aliuzuia kwa kuukinga na mwili wake huku akimtazama Amata.

“Nini sasa?” kamanda akauliza.

“Nipe mate kabla hatujaingia huko ndani,”

“Kwani we wasiwasi wako nini mpaka utake hapa nje?”

“Nimesema nipe, mi ndio kawaida yangu mlangoni unaninyonya ndio tunaingia huko ndani,”

Kamanda Amata akamkumbatia Cheupe na kusogeza kinywa chake kwake tayari kumpa anachokitaka, akiwa katika hali hiyo akamwona Cheupe akitoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.

“Nini bebi mbona hivyo unataka kukata roho?” Amata akamwuliza Cheupe, lakini hakujibu akabaki katika hali ileile. Kitu cha baridi kikatua kwenye kisogo cha Amata.

“Mbio za sakafuni huishia ukingoni,” sauti kutoka nyuma yake ikasikika.

“Ulifikiri ungenikimbia mpaka wapi? Fungua mlango,” akamwamuru na Kamanda akafungua mlango.

“Ingieni ndani, tukafanye mapenzi wote hukohuko,” kamanda Amata akiwa na Cheupe wakaongoza mpaka kitandani na kuketi.
Alikuwa ni Jasmine, daktari wa kike katika idara ya kijasusi ya TSA, sura yake haikuonekana kuwa na mchezo hata kidogo.

“Sasa dada yangu kwani sisi tumekosa nini?” Kamanda akauliza.

“Kelele wewe! Unajifanya hujui ulichofanya ee, leo umekamatika subiri ule pingu kisha maelezo mtayapata kituoni. We mwanamke kaa upande ule, nitajie jina lako,”

“Cheupe,” akajitambulisha.

“Anhaaa ndiyo wewe Cheupe, kahaba wa Chako ni Chako?” Jasmine akauliza huku bado mkononi akiwa na bastola.

“Ndi – ndi – ndiyyoo,” akajibu kamasi jembamba likimtiririka.

“Cheupeeee, na kweli u mweupe kwelikweli. Unamjua huyo unayetembea naye?”

“Hapana,” Cheupe akajibu.

“Lo! Huyo ni jambazi tunayemsaka tangu huko Mwanza na sasa nimemtia mkononi, na bila shaka hata wewe utakuwa jambazi,”

“Hapana, hapana, dada, huyu ni mteja wangu tu, alinichukua nimburudishe kwa usiku huu,” Cheupe akajitetea tena akiwa kapiga magoti.

“Ok, keti kitandani, sasa mimi nina shida na wewe na si huyu mwanaume,” Jasmine aliposema hayo alihisi kama Cheupe anataka kupoteza fahamu.

“Nimefanya nini dada? Mi sio mhalifu,”

“We si ndio Cheupe?”

“Ndiyo, ndiyo mimi,”

“Good! Nakutafuta wewe, unaweza kuniambia jana kuanzia saa kumi nambili jioni ulikuwa wapi?” Jasmine akauliza.

“Nilikuwa Bahi hotel,” akajibu.

“Usinidanganye, ukinidanganya nakulaza ndani leo, ukinambia ukweli nakuacha huru,” Jasmine akaunguruma.

“Kweli dada, nilikuwa Bahi,”

“Na nani? Au kufanya nini?”

“NIlikuwa na bwana wangu, kama unavyojua mimi ni kahaba, hivyo jana nilipata mtu na kulala naye Bahi mpaka saa nne usiku,” Cheupe akaeleza.

“Enhe endelea nakusikiliza, na baada ya hapo ulienda wapi?”

“Baada ya hapo nilienda geti kwangu Chako ni Chako,” Cheupe akajibu na kuanza kupumua kwa nguvu.

“Una heleni ngapi masikioni mwako?” Jasmine akauliza. Kwa swali hilo Cheupe akaanza kujipapasa na kujikuta ana heleni moja tu sikioni na sikio lingine halikuwa na heleni, akahisi ganzi mwili mzima, akajipapasa mara ya pili, hakuna heleni. Jasmine akamwonesha heleni moja aliyoishika mkononi mwake.

“Nimeipata kwenye gari ya Mheshimiwa Msesema, ulikuwa naye jana?” swali hilo likaanza kumtoa machozi Cheupe. Akaitikia kwa kichwa ‘ndiyo’.

“Safi sana msichana, ninachotaka kutoka kwako ni kunieleza mazingira ya ajali ilivyotokea, au kama kuna mtu unamhisi kufanya kitu chochote kibaya uniambie,” jasmine aliendele na mahojiano na Cheupe huku akimtoa hofu ya mara kwa mara. Ijapokuwa Cheupe alionekana kutojua lolote kwa undani lakini mazungumzo yake yalionesha kuwa kuna mtu anayemhisi kuwafuatilia usiku huo tangu wakitoka Chako ni Chako lakini hakuweza kuwa na uhakika kuwa ajali hiyo ameisababisha yeye.

“…baada ya uapata ajali, nakumbuka nilimwona mtu aliyevaa sox usoni, nilimwona, nilimwona, aliondoka na gari, sikumbuki gari gani…” Cheupe alieleza kwa kusita sita.

“Ok, sasa utanisamehe lakini kwa usalama wako itabidi ukalale polisi ila kama hutaki sawa,” jasmine akapendekeza. Muda wote wa mahojiano hayo Kamanda Amata alikuwa kimya pale kitandani akifuatilia kila swali na kila jibu. Dakika hiyo hiyo mlango ukafunguliwa na vijana wawili zaidi wakaingia ndani ya chumba kile.

“Cheupe, kwa usalama wako twende ukalale polisi, ila sikulazimishi kwani hauna kosa, kama hujui aliyemuua Msesema huyo aliyevaa sox usoni anakutafuta ili usitoe siri kwa wanausalama,” jasmine alisistiza.

“Hapana, kamwe siwezi kulala polisi, mniache niondoke zangu,” Cheupe akajibu na kunyanyuka, akabeba mkoba wake na kutoka mlangoni akapotelea nje.

§§§§

MAWAZO NA HASIRA vikamshika Obobo baada ya kupekuwa lile koba la Segeratumbo na kukosa anachokihitaji, zaidi sana alikuta shilingi laki moja tu. Akili ikamzunguka haraka haraka, akaitazama saa yake, muda unayoyoma, akasonya na kutoka pale alipoketi, akakatisha barabara na kurudi pale hoteli ya Veta, hakuingia ndani, aliliweka lile koba juu ya tanki la maji hapo nje naye akatokomea kizani. Moja kwa moja breki yake ikawa Dodoma baa karib u kabisa na kituo kikuu cha mabasi. Akaagiza kinywaji na kukodoa macho kwenye televisheni moja ambayo ilikuwa ikitangaza habari kwa kiingereza na habari iliyokuwa inaunguruma ni ile ya ajali ya Msesema.

“Shiit!” Obobo alijikuta anang’aka baada ya kusikia kuwa polisi wanamtafuta mwanamke aliyekuwamo katika gari hiyo kwa uchunguzi. ‘Wakimpata nimekwisha, lazima nimuwahi mimi,’ akawaza na mara hiyo akaondoka na kuchukua taxi mpaka Chako ni Chako, kwa kuwa alikuwa anajua kuwa huyo mwanamke anapendelea kuwa hapo kwa biashara zake isingekuwa shida kumpata.

Taratibu akakiendea kiti kimoja na kuketi akiwa anaweza kuona eneo lote lile, kabla hata hajakaa sawa akamwona akitoka na kijana mmoja wakiwa wameshikana kimahaba, jicho likamtoka na kuanza kufuatilia nyendo zao, ‘lazima nimmalize leo, na atakufa bila kelele,’ akawaza. Alipohakikisha wameondoka eneo hilo kwa gari ya kukodi nay eye akafanya hivyo kuwafuatilia ili aujue mwisho wao.

§§§§
Vijana wawili wa jeshi la polisi waliovalia kiraia walikuwa na Segeratumbo ndani ya chumba chake kwa mahojiano baada ya kuitwa kufika hapo.

“Umemuona kwa sura kabisa?” mmoja akauliza.

“Ndiyo, tena anaonekana si mtanzania kwani Kiswahili chake hakijanyooka na maneno mengi anaongea kiingereza,” akajibu.
“Nikihitaji maelekezo jinsi alivyo utaweza kumwelezea?”

“Bila shaka,”

Yule kijana mwingine aliyekuwa na mwili mdogo akachukua faili lake na kutoa penseli kisha kwa kusikiliza maelekezo ya Segeratumbo aliweza kumchora Obobo kama alivyo.

“Ni hivyo tu!” Segeratumbo akamaliza na wakati huohuo mlangoni kwake hodi ikagongwa, wale polisi wakafungua mlango na kukutana na mhudumu wa hoteli akiwa na lile koba mkononi.

“Samahani tumeokota huu mkoba wa mheshimiwa hapo juu ya tanki la maji,” akaeleza.

“Aliyeweka umemwona?” akaulizwa.

“Hapana nilikuwa naenda kufungua maji ndipo nikauona nilipouliza kaunta wakasema ni mkoba wa mheshimiwa labda kausahau hapo,” akaelelza.

“Ok, asante waweza kwenda,” wakamruhusu.
Sasa Mheshimiwa mtu uliyemwona anafanana na huyu?” Yule kijana mwingine akauliza na kuigeuza ile picha aliyoichora muda mfupi uliopita.

“Yaani yuko hivyohivyo kijana, kama umempiga picha vile,” Segeratumbo akajibu kwa shauku.

“Sawa, kazi imekwisha, sasa huu mkoba tunaondoka nao ili tuweze kupata alama za vidole kisha tutakurudishia,”

“Kuna hela humo lakini kama hajaziiiba Yule hayawani, mfanye haraka kwani kuna miswada ya kibunge”. Baada ya mazungumzo hayo wale vijana wakaondoka zao na kumwacha Segeratumbo na yule mwanamke wake. Segeratumbo akainua simu yake na kumpigia Kibanio akitaka waonane popote alipo usiku huo. Wakakubaliana kuonana Dodoma Carnivole usiku huo.

5

OBOBO aliendelea kumfuatilia Cheupe mpaka katika lodge ya Kenya na kumwona akiingia ndani na kijana Yule, akasimama kwa nukta kadhaa kisha akaielekea kaunta na kuagiza kinywaji akijipanga kuendelea kumsubiri hapo nje, ‘nitamkamata tu’ akawaza huku akipokea inywaji chake kutoka kwa mhudumu wa kaunta. Obobo aliapa kumtia mkononi Cheupe ili amfunge mdomo na kujijengea usalama wake katika kazi yake hiyo. Alisubiri pale kaunta kama saa nzima hivi lakini hakumuona Cheupe wala anayefanana naye kutoka ndani ya nyumba ile, ‘atatoka tu,’ akajipa moyo na kuendelea kupiga kinywaji taratibu.

† † †

Jasmine alimwona Kamanda alivyoingia na Cheupe, kama walivyojipanga, aliendelea kutulia palepale alipokuwa ameketi na mara hiyo akamwona mtu mmoja mweusi mwenye tambo kubwa akiingia na kushangaa shngaa nguo aliyovaa ndiyo ile ailyoambiwa na wale jamaa wa bodaboda.
“Shiit” akang’aka peke yake huku akinyanyuka kuelekea ndani maana alijua wazi kuwa akichelewa tu kukamilisha kazi yao basi lazima litatokea timbwili katika eneo hilo. Akainuka na kwenda kaunta ambako alilipia huku akimgonga Yule jamaa makusudi na kugundua kuwa ana bastola upande wake wa kulia. Akatoka na kuelekea ndani ya ile loji na kumwona Kamanda na Cheupe wakipeana mabusu pale mlangoni.

† † †

Obobo akamwona Cheupe akitoka huku akitembea harakaharaka katika maegesho ya magari, akateremka taratibu kutoka pale alipoketi na kuacha noti ya 5000 akapotelea kizani kumsaka mwanadada huyo. Alisimama kwenye nguzo ya umeme na kutazama huku na kule akamwona Cheupe akiivuka barabara kwenda upande wa pili, Obobo naye akavuka n akutembea kando kando ya ile barabara kama mita mia mbili nyuma ya Cheupe hukiu akijaribu kujificha chini ya vibaraza vya nyumba kusudi asionekane na watu kama anamfuatilia binti huyo.
Cheupe aliendelea kutembea haraka haraka huku akiangalia nyuma mara kwa mara, mara moija alipoangalia nyuma akakutana uso na Obobo, akamtambua mtu huyo kwa haraka kiuwa sio mwema kwake, akaanza nusu kukimbia na nusu kutembea. Obobo hakumwacha aliongeza tu ukubwa wa hatua na kumfuata, cheupe alizidi kuongeza kasi huku akitazama nyuma na kuona Yule mtu akizidi kumkaribi. Cheupe akapita mtaa wenye maduka mengi na kutokea ule wa wauza mitumba unaoelekea ofisi za CCM. Watu wakawa wakimshangaa msichana huyo, wengine walimjua na wengine hawakumjua ila kwa mavazi yake walimtumbulia macho.

Muda huo wauza mitumba wengi walikuwa wamekwishafunga biashara zao na wachache walibaki wakimalizia huku vijiwe vya kahawa navyo tayari vilianza kukusanya watu.

“Jamani mwizi! Mwizi huyo!” Cheupe alianza kupi9ga kelele na watu wakaanza kuangaza huku n huku.

“We mwanamke huyo mwizi yuko wapi?” vijana wakaanza kuuliza
.
“Huyo nyuma, Yule pale anataka kunipora tangu nilikotoka,” akaeleza.

Obobo alipoona Cheupe anahojiwa na wale vijana akatulia na kujificha nyuma ya gari moja iliyoegeshwa mahala hapo. Mara wale vijana wakamjia na kumzunguka huku wakimwuliza maswali ambayo mwenzao alikuwa hayaelewi. Vurugu ikaanza, Obobo hakuvumilia akachomoa bastola yake na kupiga hewani wale vijana wa katawanyika.

“Ana bundukiii, ana bundukiii, jambazi huyo,” wakapiga kelele.
Mtaa mzima ukawa mshikemshike, Obobo alipopata upenyo akawatoka wale vijana ambao bado walikuwa wakimwandama.

“Paaaaahhh!” risasi moja ilisikika na mmoja wa vijana wale akaanguka vibaya barabarani akivujwa na damu.

“Mamaaaa! kaua huyo, jambazi hilo,” wakaendelea kupiga kelele wakati huo Obobo akapenya hapa na pale na kutokea barabara kubwa karibu na Viwanja vya Nyerere, akaipachika bastola mahala pake kisha akatulia akiangaza macho huku na kule ili amwone Cheupe.

‘Amenipotea,’ akajisemea moyoni huku akijiondoa eneo lile na kuifuata barabara kubwa kuelekea Chako ni Chako. Alivuka barabara mbili tatu za mitaa na kukaribia baa hiyo iliyokuwa imesheheni watu muda huo. Akapunguza mwendo na kusimama mahala Fulani akiangalia kutoka mbali kama atamuona Cheupe lakini hakumwon. Alichokiamua ni kwenda kwenye ile baa, akajipenyeza na kumkamata mhudumu mmoja kumwuliza wapi anapoisshi cheupe.

“Ametoka bado hajarudi, kama una shida naye msubiri,” Yule mhudumu akajibu huku akiondoka na kuendelea na shighuli zake zingine kabisa. Obobo akaketi kitini na kuagiza kinywaji baridi na kulipoza koo lake.

DODOMA CARNIVOLE
SAA NNE usiku ndani ya baa kubwa ya Dodoma Carnivole, muziki mzito ulikuwa ukikita kwenye spika kubwa za kisasa na kufanya watu wa rika tofauti kupata burudani katika eneo hilo. Lakini wale wenye pesa zo kubwakubwa walipewa mahala pao pa ukimya ili kuweza kujadili mambo yao bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Ndani ya chumba kimoja kilichobandikwa neno V.I.P kwa maandishi yaliyojinyonganyonga kulikuwamo watu wawili walioketi huku na kule, juu ya meza iliyowatenganisha kulikuwa na makabrasha kadhaa na huku katika vijimeza vidogodogo kila upande kulikuwa na chupa kubwa kubwa za pombe kali ambazo wawili hao walikuwa wakijimiminia matumboni mwao kila mmoja kwa uwezo wake.

“Tumepoteza,” Segereatumbo aliongea mara tu alipoikita bilauri yake iliyokaukiwa kinywaji juu ya ile meza ndogo.
Mheshimiwa Kibanio bado alikuwa akipiga funda lake ambalo ndio kwanza alikuwa akifungua koo baada ya kugonga cheers na swahiba wake huyo.

“Lakini we inakuingia akilini Msesema jinsi alivyokufa?” Kibanio akauliza huku akiitua bilauri yake.

“Ajali haina kinga mheshimiwa, yote yanawezekana,” Segeratumbo akajibu kisha ukimya ukachukua nafasi yake.

“Sikia mimi nina wasiwasi hiki kifo si cha kawaida,” Segeratumbo akaongeza kusema, “Unajua kwa nini nimekuita hapa?”

“Sijui!”

“Usiku huu nimevamiwa, nimevamiwa na lijitu, pande la mwanaume, nikiwa na shemeji yako Mwanahawa. Lile jitu likapora mkoba wangu wa kazini na kutokomea,” akaeleza.

“What? Segeratumbo, ni kweli?” Kibanio akang’aka, kisha akatulia na kufikiria jambo, “Tuna wabaya wengi sana,” akaongea kwa upole.

“Ndiyo, wameshaona wanaumbuka,”

“Segeratumbo!” KIbanio akaongea kwa sauti ya chini.

“Sikiliza Kibanio. Polisi walikuja nikawaelekeza alivyo mtu huyo wakamchora vilevile, na sasa wanashughulikia hiyo ishu. Mkoba wangu baada ya kuona alichokitaka hakipo akautupa nje kwenye maua,” Segeratumbo akaleza.

“Mzee Sege, hapa ni kukaa mkao wa kula bila ulinzi hatuwezi kuishi, hata mimi itabidi nihamishe kabrasha zangu. Kumbeeee!” Kibanio alipigwa na butwaa kwa habari hiyo.

“Na kama kauawa basi muuaji ni profesheno,”

“Ndiyo, lakini tutapataje uhakika wa hili? Inabidi tufuatilie,” Segeratumbo akashauri.

“Sijakuelewa kiongozi,” Kibanio akaonesha shaka.

“Tujiwekee ulinzi, ikiwezekana tufanye juu chini huyu jamaa akamatwe,” Segeratumbo akasema.

“Nimekupata, lakini swala si liko polisi? Atanyooshwa tu,” Kibanio akajibu huku akimimina kinywaji kwenye ile bilauri ambayo sasa ilikwishakauka.

“Kibanio, kumbuka adui yetu atakuwa amekodi mtu makini kufanikisha lengo lake, na sisi tutafute mtu makini katika kuhakikisha ukweli huu unajulikana,” Segeratumbo akaeleza.
“Sawa naungana mkono na wewe”.

Baada ya saa tatu kupita wakiwa palepale wakamaliza mazungumzo yao na kukubaliana kwa sauti moja kuimarisha ngome yao dhidi ya wahujumu uchumi ndani ya serikali. Pamoja na hilo waliona wazi kuwa vita hiyo siyo ndogo ni kubwa hivyo wakaamua kujipanga kwa nguvu zote.

§§§§
Nje ya Kenya lodge Amata alisimama kimya akimwangalia Jasmine akiwapa maelekezo haya nay ale wale askari polisi aliokuwa nao hapo nje, alipomaliza akarudi kwa Amata.

“Vipi mbona umeduwaa?” akamwuliza.

“Nilikuwa nakuangalia Master Plan unavyopanga majeshi,” akamjibu kwa utani.

“Ok, sasa nini kinafuata? Kumbuka mimi kazi yangu nimeimaliza tayari, si ajabu kesho nakuacha sina jipya hapa,” Dkt. Jasmine alimwambia Amata.

“Mh! Ndiyo ndiyo umemaliza, mimi bado inabidi nishughulikie hili swala kwa undani zaidi ili likamilike mapema,” Amata alieleza huku akitoka eneo lile na mkono mmoja kamshika Jasmine.

“Lakini we unalionaje?”

“Haliko sawa kiukweli, kuna watu nitahitaji kuonana nao kwa siri, unajua katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa marehemu alikuwa na swahiba zake wengine wawili na hili nimelipata kwenye kumbukumbu zake, ameeleza mambo mengi sana juu ya sakata lao hili, nataka nijue kama ni chanzo kabisa au kuna linguine,” akamwambia Jasmine.

“Sasa usiku huu, tunaenda kuumalizia wapi?” Jasmine akauliza huku akiweka vizuri mkufu wake wa dhahabu uliokuwa ukining’inia shingoni mwake.

“We unataka wapi? Ila kumbuka kazi hii bado mbichi na time is tissue,” akamwambia huku akisimamisha tax na wote wawili wakaingia.

“Chako ni Chako tafadhali,” Amata akamwambia dereva.

“Shiiiiit!” Jasmine akang’aka, “Kuna nini huko Chako ni Chako?” akaongeza swali.

“Nyama, kuna nyama sana pale mpenzi,” akamwambia huku dereva akiondoa ile gari na kukata mitaa kuelekea huko atakako Amata.

“Pale ndo pazuri shemeji!” Yule dereva akadakia mazungumzo.
“Si unasikia!” Amata akaongeza, “Sisi wageni bwana hapa hatujui moja wala mbili, ila mji wenu mtulivu sana,” akaongeza maneno.

“Ajali haina kinga mheshimiwa, yote yanawezekana,” Segeratumbo akajibu kisha ukimya ukachukua nafasi yake.

“Sikia mimi nina wasiwasi hiki kifo si cha kawaida,” Segeratumbo akaongeza kusema, “Unajua kwa nini nimekuita hapa?”

“Sijui!”

“Usiku huu nimevamiwa, nimevamiwa na lijitu, pande la mwanaume, nikiwa na shemeji yako Mwanahawa. Lile jitu likapora mkoba wangu wa kazini na kutokomea,” akaeleza.

“What? Segeratumbo, ni kweli?” Kibanio akang’aka, kisha akatulia na kufikiria jambo, “Tuna wabaya wengi sana,” akaongea kwa upole.

“Ndiyo, wameshaona wanaumbuka,”

“Segeratumbo!” KIbanio akaongea kwa sauti ya chini.

“Sikiliza Kibanio. Polisi walikuja nikawaelekeza alivyo mtu huyo wakamchora vilevile, na sasa wanashughulikia hiyo ishu. Mkoba wangu baada ya kuona alichokitaka hakipo akautupa nje kwenye maua,” Segeratumbo akaleza.

“Mzee Sege, hapa ni kukaa mkao wa kula bila ulinzi hatuwezi kuishi, hata mimi itabidi nihamishe kabrasha zangu. Kumbeeee!” Kibanio alipigwa na butwaa kwa habari hiyo.

“Na kama kauawa basi muuaji ni profesheno,”

“Ndiyo, lakini tutapataje uhakika wa hili? Inabidi tufuatilie,” Segeratumbo akashauri.

“Sijakuelewa kiongozi,” Kibanio akaonesha shaka.

“Tujiwekee ulinzi, ikiwezekana tufanye juu chini huyu jamaa akamatwe,” Segeratumbo akasema.

“Nimekupata, lakini swala si liko polisi? Atanyooshwa tu,” Kibanio akajibu huku akimimina kinywaji kwenye ile bilauri ambayo sasa ilikwishakauka.

“Kibanio, kumbuka adui yetu atakuwa amekodi mtu makini kufanikisha lengo lake, na sisi tutafute mtu makini katika kuhakikisha ukweli huu unajulikana,” Segeratumbo akaeleza.
“Sawa naungana mkono na wewe”.

Baada ya saa tatu kupita wakiwa palepale wakamaliza mazungumzo yao na kukubaliana kwa sauti moja kuimarisha ngome yao dhidi ya wahujumu uchumi ndani ya serikali. Pamoja na hilo waliona wazi kuwa vita hiyo siyo ndogo ni kubwa hivyo wakaamua kujipanga kwa nguvu zote.

§§§§
Nje ya Kenya lodge Amata alisimama kimya akimwangalia Jasmine akiwapa maelekezo haya nay ale wale askari polisi aliokuwa nao hapo nje, alipomaliza akarudi kwa Amata.

“Vipi mbona umeduwaa?” akamwuliza.

“Nilikuwa nakuangalia Master Plan unavyopanga majeshi,” akamjibu kwa utani.

“Ok, sasa nini kinafuata? Kumbuka mimi kazi yangu nimeimaliza tayari, si ajabu kesho nakuacha sina jipya hapa,” Dkt. Jasmine alimwambia Amata.

“Mh! Ndiyo ndiyo umemaliza, mimi bado inabidi nishughulikie hili swala kwa undani zaidi ili likamilike mapema,” Amata alieleza huku akitoka eneo lile na mkono mmoja kamshika Jasmine.

“Lakini we unalionaje?”

“Haliko sawa kiukweli, kuna watu nitahitaji kuonana nao kwa siri, unajua katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa marehemu alikuwa na swahiba zake wengine wawili na hili nimelipata kwenye kumbukumbu zake, ameeleza mambo mengi sana juu ya sakata lao hili, nataka nijue kama ni chanzo kabisa au kuna linguine,” akamwambia Jasmine.

“Sasa usiku huu, tunaenda kuumalizia wapi?” Jasmine akauliza huku akiweka vizuri mkufu wake wa dhahabu uliokuwa ukining’inia shingoni mwake.

“We unataka wapi? Ila kumbuka kazi hii bado mbichi na time is tissue,” akamwambia huku akisimamisha tax na wote wawili wakaingia.

“Chako ni Chako tafadhali,” Amata akamwambia dereva.

“Shiiiiit!” Jasmine akang’aka, “Kuna nini huko Chako ni Chako?” akaongeza swali.

“Nyama, kuna nyama sana pale mpenzi,” akamwambia huku dereva akiondoa ile gari na kukata mitaa kuelekea huko atakako Amata.

“Pale ndo pazuri shemeji!” Yule dereva akadakia mazungumzo.
“Si unasikia!” Amata akaongeza, “Sisi wageni bwana hapa hatujui moja wala mbili, ila mji wenu mtulivu sana,” akaongeza maneno.

“Lete sindano na diclofenac,” akamwamuru muuguzi aliyekuwa jirani, sekunde kadhaa tu tayari ilikuwa imefika na jasmine aliitumia kumpunguzia maumivu.
Baada ya dakika thelathini za kashi-kashi Cheupe alikuwa tayari katulia kimya na Philadelphia Collar yake shingoni. Jasmine akachukua kadi kubwa iliyoletwa hapo na kuandika kila alilofanya na hali aliyomuacha nayo mgonjwa, pia akaandika matibabu yote anayotakiwa kupata.

“Unaitwa nani?” akamwuliza muuguzi Yule aliyekuwa akimsumbua.
“Kashinde!”

“Ok, sikia Kashinde, sitaki mtu yeyote aingie humu ndani isipokuwa wewe tu, hata akija bosi wako, hata Waziri wa Afya, mwambie ni ‘order’,” Jasmine akamweleza huku akimkazia macho kiasi kwamba Kashinde alikuwa akishindwa kustahimili.

“Samahani, nikiulizwa ninyi ni nani nisemeje? Maana mmekuja tu na kujichukulia majukumu wenyewe,” Kashinde akauliza kwa woga.

“Oh! Nilisahau, jibu hili utampa boss wako tu, mwambie ni amri kutoka kwa daktari maalumu wa Ikulu,” akamwambia huku akimkabidhi ile kadi, akachukua pochi yake na kutoa shilingi elfu thelathini.

“Shika hii, kwa lolote likihitajika na hapa kama hamna, utatumia pesa hiyo, kama kuna shida nipigie,” akamkabidhi na kadi yake ya kibiashara iliyomtambulisha kwa jina la bandia isipokuwa taaluma sahihi.

“Ok, asante,” Kashinde akajibu.

Amata na Jasmine wakaondoka katika lile eneo na kutokomea.
“Wapi sasa?” akauliza Amata.

“Hotelini kwako, sijapumzika, na nimekuja hivi unionavyo,” Jasmine akajibu.

“Ok”.

§§§§
Baada ya kumaliza kazi ile Obobo hakwenda mbali, alirudi kwa wateja na kuendelea kunywa bia yake akisubiri matokeo ajue nini kinajiri. Aliziona heka heka zote mpaka mwisho. Alipomwona Cheupe akitolewa ndani kabebwa na Amata, macho yakamtoka pima. ‘Hajafa au?’ akajiuliza na kushuka pale alipokuwa kisha akaifuatilia ile tax ya akina Amata mpaka kule hospitali. Kabla hajafanya dhara lolote aliichukua simu yake na kuwataarifu wateja wake juu ya hali hiyo.

“Kama unaona ana madhara nyonga tu,” akajibiwa hivyo. Akaiweka simu yake mfukoni na kuelekea mlango wa kuingia ndani ya jengo lile lakini walinzi walimzuia kuwa muda wa kuona wagonjwa ulishapita; hakupenda kuleta vurugu, alitoka na kutazama majengo yale yalivyojipanga. Kwa haraka akazunguka nyuma na kujiweka dirishani akisikiliza mazungumzo yote ya mle ndani mpaka walipoagana na Kashinde na kuondoka. Obobo alisimama kwa muda kisha akaondoka eneo lile baada ya kusikia michakacho ya miguu ya watu. Akafika mbele kabisa ya lile jengo na kuwaona Amata na Jasmine wakiondoka.

“Shiit! Yupi anatakiwa afe kwanza?” akajiuliza kwa sauti kisha akainua simu yake kwa mara nyingine na kuomba kuonana na wateja wake haraka iwezekanavyo.

KIKUYU RESORT

OBOBO alikutana uso kwa nuso na wateja wake lakini mmoja wao hakuwamo. Mheshimiwa Matata alikuwa na Kagosho katika kikao hicho cha dharula.

“Ndiyo Bacteria tupe taarifa,” Matata alianza.

“Maana kutuita huku lazima kuna jambo na sio jepesi,” Kagosho akaongeza.

“Ndiyo kwa sababu tulishapanga tusionane mpaka kazi itakapokamilika, ila imebidi kwa kuwa kuna jambo zito na sio kidogo. Nilikuwa nimepanga kumaliza kazi yenu ndani ya siku tatu hadi tano lakini sasa naona kazi inakuwa ngumu kuliko mpango wa mkataba wetu,” Obobo akaeleza kwa kiingereza safi kabisa cha Uingereza.

“Nini kipya?”

“Kwanza kabisa nimegundua kuwa Yule mwanamke aliyekuwa na Msesema atakuwa mwiba mkali katika mpango huu, nikapanga nimwondoe kimyakimya, lakini bahati mbaya katika shambulio lile la ghafla nimegundua kuna watu wawili mmoja mwanaume na mmoja mwanamke wanafuatilia kwa karibu yendo hizi. Sasa inawezekana serikali yenu imetuma wachunguzi juu ya hili,” akaeleza.

Kagosho na Matata wakatazamana.

“Mh! hatuna taarifa kwa maana zaidi ya polisi wa hapa ambao najua kwa upeo wao hawawezi kujua kinachoendelea sidhani kama kuna wengine,” Matata akajibu.

“Any way, ngoja tulifuatilie usiku huu tutakujulisha. Lakini hawa vijana wa hapa aaaaa wasikusumbue wao watachunguza ajali basi,”

“Ni angalisho maana kama kuna watu wanachunguza hili ujue kazi inaongezeka so na malipo yatabadilika,” Obobo akawaambia.

“Hakuna shaka, sisi tunachotaka hapa ni kupoteza hili swala,” Kagosho akaongeza wakati huo Mheshimiwa Matata alikuwa katulia kimya kama akiwaza jambo, mara akainua uso na kumtazama Obobo.

“Uko sawa,” akamwambia na kumtazama Kagosho, “Kijana yuko sawa, jana nimemwona mtu ambaye nimemtilia wasiwasi. Yeye yuko idara ya Usalama wa Taifa lakini atakuja kuchunguza haya kweli?” akawaeleza na kuuliza.

Ukimya ukachukua nafasi kati yao.

“Wako wawili, hii kazi itakuwa ngumu sana kwa sababu ya hawa sasa sijui nianze na nani?” Obobo alieleza kwa kuwa alijikuta njia panda.

“Kill them all, kwa njia unazoona zinafaa,” Matata akamwambia Obobo. Mara mlango ukafunguliwa bila hodi na kila mtu akashtuka na kujiweka sawa.

“Vipi mbona mnaogopa?” Mheshimiwa Nnandi aliingia na kuwaambia.

“Nnandi nipe taarifa maana upo kitengo muhimu,” Matata akamwambia pindi tu alipojiweka vizuri kwenye kochi hilo la vono.

“Aaa taratibu za kuaga mwili zimebadilika, sasa itakuwa kesho kutwa badala ya kesho,” akawaeleza.

“Kwa nini?”

“Spika amedai tu kuwa kuna mambo ya kifamilia yanapewa nafasi kwanza,” Nnandi akaeleza. Mheshimiwa Matata akamgeukia Obobo.

“Fanya unaloweza kisha kazi ikiisha tukutane Nairobi kama tulivyokubaliana,” alipomaliza kumwambia hayo, Obobo akaondoka ndani ya chumba kile na kuwaacha watafunaji hao wakiendelea na hili na lile.

“Waheshimiwa hapa lazima tuwe makini, tutaumbuka,” Matata akasema.

“Aumbuke nani wewe! Tumejikamilisha, si mnajua hata waziri mwenye zamana ya usalama yuko upande wetu, ni swala la kumwambia tu kama kuna watu wake awaondoshe mara moja,” Nnandi alikuja na wazo jipya kabisa ambalo kwalo kila mtu alihafiki bila ubishi. Wakajipanga kumwona waziri huyo kwani naye ni mmoja wao katikan sakata hilo lakini alikuwa akifanya kwa siri sana kutokana na wadhifa huo.

“Jamani ee kama Yule kijana niliyemwona yupo katika uchunguzi huu naanza kuhisi tumbo la kuhara. Yule kijana ni nyoka mwenye sumu kali,” Matata akawaeleza.
“Hayo yasiwatishe, hawawezi kutufikisha popote kwa mbwembwe zao si tutaendelea kula kuku kwa mrija,” Nnandi aliongeza kusema huku wakati huo mhudumu alikwishamletea pombe kali aipendayo.

Siku tatu baadae

KATIBU WA BUNGE alishindwa kuchanganyikiwa baada ya kugundua kuwa nyaraka za mswada wa sakata la Escrow hazionekanai ofisini. Alipekua huku na kule lakini wapi. Niliziweka kwenye droo hii, na nilifunga na funguo nilikuwa nazo mwenyewe, zimepoteaje? Alijiuliza akiwa kaweka mikono yake kiunoni. Kila alipojumlisha moja na moja ilikuja nne na sio mbili. Akashika mkono wa droo na kulivuta kwa kulitikisatikisa lakini halikuwa na kitu ndani yake. Akashusha pumzi ndefu na kuketi kitini huku akihisi macho yake kujaa machozi ya dharula.
Alipoona sasa hana la kufanya, aliinua simu yake na kubofya tarakimu Fulani kisha akaiweka sikioni na kusubiri upande wa pili upokee simu hiyo.

“Hello!”

“Ndiyo mkuu, yaani kabrasha zote za lile sakata hazipo kabisa…”

“Sasa zitakuwa wapi? Au ume-missplace…?”

“Hapana mkuu, naijua kazi yangu, hizi zitakuwa zimeibwa,”

“…Zimeibwa!” ile sauti ya upande wa pili ikahamanika kwa jibu hilo, “…haiwezekani… naomba uje ofisini kwangu mara moja!” ikamwamuru Yule Katibu wa Bunge naye muda huohuo akiwa kajawa na hofu akatoka ofisini. Alipofika nje akasimama kidogo na kisha kama asiyeamini akarudi ndani na kuanza upya kupekua.

Dakika thelathini zilizofuata alikuwa tayari kwa mkuu wake wa kazi, mwili wake ulikuwa umetona kwa jasho ijapokuwa kiyoyozi kilikuwa bize kikifanya kazi ya kupoza hewa.

“Unaniambia zimepoteaje?” Yule mwanamama, mwenye wadhifa mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akamwuliza katibu wake wa bunge mwenye mamlaka ya kutunza na kujua dondoo zote za mhimili huo.

“Yaani hata sijui, tangu kikao cha mwisho, kabla ya msiba wa Msesema niliziweka kwenye loka namba tatu lakini sizioni pale”.

“Ina maana mtu kaingia kaiba ofisini kwako humohumo?” Yule mwanamama akuliza huku akionekana wazi kushikwa na hasira kali.

“Ataingiaje?” Yule kijana akajikuta anauliza.

“kama hajaiba mtu kutoka nje basi ni wewe na wasaidizi wako mtakuwa mmekula njama, na hili lazima lichukuliwe hatua mara moja. Nenda nitafanya utaratibu mwingine juu ya hili kisha nitakuita pamoja na wasaidizi wako, hii ni aibu kwetu, kabrasha linapotea vipi kwenye kitengo nyeti kama hiki? Ajabu!” mkuu akaagana na huyo katibu na kubaki peke yake ofisini, sura yake ilisawajika kwa mawazo.

§§§§

ITAENDELEA

SIMULIZI The Escrow Mission Episode 04

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment