Jinamizi Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA: HASSAN O MAMBOSASA
*********************************************************************************
Simulizi: Jinamizi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Hekaheka za uchaguzi zilikuwa zimepamba moto nchini Tanzania,kampeni zenye majigambo zikiwa zimeshika nafasi yake ndani ya ardhi hii yenye amani. Vyama tofauti vilikuwa vikihaha huku na kule ndani ya nchi hii ili viweze kujizolea kura kwa wananchi, wagombea urais,ubunge na udiwani a vyama hivyo walijinadi wawezavyo ili kuwashawishi wananchi wawapigie kura. Hakika zilikuwa ni kampeni za aina yake zilizoleta upinzani katika vyama viwili tofauti, kimoja kikiwa ni chama tawala na kingine kikiwa ni kikuu cha upinzani nchiniTanzania. Upinzani huu ulipelekea hadi wawe wanachafuana kupitia vyombo vya habari, huku wanachama wake wakiwa katika makundi yenye uhasama mkubwa. Hakika hii ilikuwa ni kipato tosha kwa wanahabari wenye tamaa ndani ya nchi hii, wanahabari hawa walidiriki kuandika habari za uongo zilizoleta uhasama baina ya vyama hivi.
Kampeni ziliendelea kuendeshwa sehemu mbalimbali za nchi hii huku serikali ikitoa fungu kwa kila chama ili kiweze kujimudu vyema, kampeni za vyama vyote zilikuwa za kawaida ila chama tawala na chama kikuu cha upinzani kampeni zao zilikuwa zimeimarika zaidi ya vyama vyote.
Chama tawala kilitumia pesa za wanachama wake matajiri waliojitolea kukifadhili chama kipindi cha kampeni ,huku wapinzani wao wakuu wakiwa hawajulikani ni wapi walipopata fedha za nyongeza za kuweza kufanya kampeni zenye gharama kuliko uwezo wa chama chao. Utata wa chama hiki uliwavuta sana waandishi wa kikundi cha kujitegemea kutoka nchi za Afrika ya mashariki kuingia kazini, walianza kulifuatilia suala hili kwa undani sana ili wapate ukweli juu ya chama hiki.
Chama hiki cha wanandishi kinachojulikana kama WAHANGA kiliundwa na waandishi watano wenye roho zisizo na hofu na jeuri ya kupuuzia vitisho , kiliundwa na watu watano kutokana nchi tano za Afrika ya mashariki amboa ni Norbert Kaila wa Tanzania,Davis Elius wa Kenya,Joseph Kiiza wa Uganda,Hilda Alphonce wa Rwanda na Allison Frank kutoka Burundi. Hawa ndio waliojulikana kama vichwa ngumu na baadhi ya vigogo, walikuwa wakitoa jarida lao lenye kuumbua mambo mengi maovu ndani ya Afrika ya mashariki. Hadi muda huo wa kampeni walikuwa tayari wameshaingia nchini Tanzania kwa siri,bwalifanya uchunguzi wa chini kwa chini huku kampeni zikiwa zinanaendelea. Uchunguzi wao ukiwa unaendelea ndio uhasama baina ya vyama hivi ukizidi kushika hatamu nchini, mauaji ya mgombea ubunge wa chama kikuu cha upinzani katika jimbo la Kahama yanatokea katika kampeni za chama hicho wilayani Kahama mkoani Shinyanga. Mgombea huyu aliyeitwa Gerald Geofrey alipigwa risasi ya kichwa akiwa jukwaani akijinadi kwa wananchi , hali ya sitomfahamu ilitokea baina ya chama cha upinzani maarufu kama PTP(people of Tanzania party) na chama tawala RPP (revolutionist political party) . PTP walikuwa wakiishutumu RPP ndio waliohusika na mauaji ya mgombea katika vyombo vya habari, hali hii ilipelekea RPP watumie muda wao mwingi kujitetea katika kampeni huku wenzao wakijinadi kwa wananchi. Hadi uchaguzi unakaribia tayari RPP walikuwa wameshapoteza idadi kubwa ya wafuasi na PTP walikuwa wameshajipatia wafuasi wengi tofauti na ilivyokuwa awali, RPP walijikuta wakipigwa kwenye kampeni zao karibu kila mahali.
Hatimaye uchaguzi ukawadia ukawadia na ikawa ni siku ya mapumziko siku hiyo ya uchaguzi ili kuwapa fursa wananchi wapige,uchaguzi ulifanyika katika hali ya utulivu na amani nchi nzima.
Waandishi wa WAHANGA nao walikuwa tayari wameshafanya uchunguzi na sasa wapo katika hata za mwisho kabla hawajalilipeleka jarida lao mtamboni ili liweze kuchapishwa na hatimaye liingie mitaani, walipolimaliza tayari uchaguzi ulikwisha fanyika na ilikuwa yanasubiriwamatokeo ya uchaguzi kwa hamu kubwa ili mshindi ajulikane. Binti pekee wa WAHANGA Hilda Alphonce ndiye aliyechukua jukumu la kupeleka nakala za jarida lao ili liweze kuchapishwa,alipeleka kiwanda cha EAPL(east africa publishers limited) tawi la Dar es salaam. Kutoka ofisini kwao hadi zilipo ofisi za kampuni ya EAPL hakukuwa mbali kwa mwendo wa miguu ingawa Hilda aliamua kutumia gari la umoja wao ili awahu kurudi aweze kuendelea na kazi kama kawaida,alifanikiwa kufika zilipo ofisi hizo mtaa wa Libya jirani na kituo cha mafuta kisha akaenda kwa mtu wao maalum anayewachapishia majarida yao wakiwa jijini Dar es salaam. Hakuwa na muda wa kukaa tena maeneo hayo baada ya kukabidhi vitu muhimu kwa ajili ya uchapishaji, aliondoka ofisini hapo. Wakati akiwa anatoka nje ya jengo hilo alipishana na kijana mwenye suti nyeusi nadhifu akiingia ofisini humo.
Hakutaka kumtilia shaka yoyote kwa muonekano alionao, alimuona kama mteja wa kawaida kama alivyo yeye ktika kampuni hiyo.
*. Kijana aliyepishana na Hilda aliingia moja kwa mojahadi katika ofisi inayohusika na kupokea nakala zawaandishi , alimkuta mhusika wa upokeaji wa nakalahizo akiwa ameegemea kiti huku miguu ikiwamezani. Aliongea pasipo kuketi katika cha watejakilicho jiranj yake, ” we Daud huyu malaya kaletanini” Daud alijibu bila ya kumtilia maananuanayezungumza naye, “ni nakala za jarida lao ambalo linahitajika kuchapishwa”. Yule kijana aliingiza mkono katika mfuko wa koti la suti yake,alipoutoa ulikuwa na burungutu la pesa ambalo aliliweka juu ya meza kisha akasema, “hizi pesa ni zako zote ikiwa utanipatia hizo nakala kabla hazijafika mitamboni”. Daud alikaa sawa kisha akamtazama yule kijana kwa umakini, alizitazama na pesa pia kwa macho ya tamaa kisha akasema “siwezi kuharibu kazi yangu kisa tamaa”. Yule kijana akatia mkono katika mfuko nyuma wa suruali yake,alipoutoa ulikuwa umeshika pochi ya kuwekea hela iliyotuna mithili ya nyoka mwenye hasira.
Aliifungua zipu ya pochi hiyo kwa majivuno kisha akatoa noti kadhaa na kuzihesabu, aliporidhika nazo aliziweka juu ya meza huku akisema “maisha yako unahitaji uyajenge zaidi ya hapa ulipo rafiki,sasa wewe jifanye mzalendo ukale dona na dagaa”. Daud alizipokea pesa zote kwa pupa kisha akaziweka halafu akaziweka katika mkoba wake wa kazi,alipofunga zipu ya mkoba wake alifungua mtoto wa meza yake kwa funguo. Alitoa karatasi zote alizokuja nazo Hilda na kumkabidhi yule kijana akiwa ametabasamu, “dona na dagaa ni mlo mbaya kwa masikini ila kwa Tajiri ni chakula bora” Daudaliongea kwa mzaha na kupelekea wote wacheke.
Waliagana kwa furaha kisha yule kijana akaondoka ofisini hapo akiwa na nakala hizo za WAHANGA. Mnamo desemba mwaka huohuo matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa katika ukumbi wa tume ya taifa ya uchaguzi,tarehe na saa za kutangazwa kwa matokeo hayo ilitajwa mapema sana. Hatimaye siku ya siku ikawadia na ukumbi huo ukawa umejaa wagombea tofauti huku wagombea wa urais wa kila chama wakawa wamekaa katika viti vilivyo katika safu moja iliyopo mbele karibia na jukwa kuu . Ilipotimu saa nne kamili za asubuhi matokeo hayo yalitangazwa na mwenyekiti wa tume hiyo mhe Ramadhani Gumbo kwa kutaja asilimia za kura kwa kila mgombea,hakika ilikuwa ni shangwe kwa chama cha upinzani PTP huku chama tawala RPP kikipitwa kwa kura nyingi sana. Vyama vingine vilivyobakia vilikuwa na upinzani mdogo hivyo havikuweza kufua dafu kabisa. Mgombea urais aliyeshinda alipeana mikono na wagombea wote kwa tabasami kuu,nao wagombea wengine waliupokea mkono wake kuonesha hawana kinyongo na wamekubaliana na matokeo hayo.
Mwisho akapeana mkono na mpinzani wake mkubwa mheshimiwa Dominic Mtalemwa wa RPP, walipeana mikono wakiwa tabasamu kisha wakakumbatiana kwa furaha yao ya maigizo.
Wakiwa wamekumbatiana mhe Filbert Ole ambaye ni mshindi aliongea kwa sauti ya chini, “bado ni chekechea kwenye siasa usishindane na aliye chuo kikuu”. Maneno hayo ya dharau hayakusikika na mtu yoyote isipokuwa Mtalemwa mwenyewe ambaye hakuhisi kama ipo siku atadharauliwa namna hiyo. Hata hamu ya kukaa eneo haikuwepo ndani ya nafsi yake kutokana dharau aliyooneshwa,kwake ilikuwa ni kuaibishwa ingawa hakuna mtu aliyeiona. Alitoka hadi nje ya ukumbi katika eneo la maegesho akiwa na wapambe wake wote,aliingia ndani ya gari alilokuja kisha akamuamuru dereva aendeshe kurudi nyumbani kwake.
Ukimya wa kampuni ya uchapishaji ya EAPL katika kuchapisha jarida la WAHANGA ulizua hali ya sintofahamu miongoni mwa waandishi hao wa kimataifa, kuzungushwa na mtu aliyepokea nakala zao kuliwashangaza sana kwani haikuwa kawaida kwa jambo kama hilo kutokea.
“nashauri tuifuatilie nakala yetu” alishauri Norbert katika kilichowekwa juu ya suala hilo. “hata mimi naona tufanye hivyo” Davis alimuunga mkono Norbert “hapana tusifanye hivyo ” Joseph alitoa rai ya kupingana na mawazo ya Norbeert na Davis kisha akawaambia “hili suala halijakaa kama mnavyofikiria nyinyi jamani, kumbukeni tulimchezea simba sharubu akiwa amesinzia na sasa amezinduka lakini ametutisha tu pasipo kutung’ata”. Kauli hiyo ilimuacha kila mmoja njia panda, hali hiyo Joseph aliibaini haraka sana na ikamlazimu kuwafafanulia “namaanisha hivi kama jarida lingetoka tungekuwa tumechokonoa mahali pabaya,bsasa ili kutuonesha mhusika anaweza kufanikiwa kufanya lolote ndio amezuia kazi yetu”.
Wote waliafiki kwa kutikisa kichwa kuashiria wamekubaliana na hoja ya Joseph. “jambo ulilolisema Mr Kiiza nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja na sasa inatubidi tusitishe kazi ya kuchunguza tukubali kazi yetu imepotea tu” aliongea Allison kwa mara ya kwanza baada ya kuwasikiliza wenzake. Akaendelea kuwaambia “cha msingi ni kuangalia kazi nyingine baada ya hapa, ila kwa sasa tukubali tumeshindwa kuwazindua wanachi usingizini”.
Baada ya wote kutoa mawazo yao walikaa kimya na kumtazama Hilda, “hakuna kilichoharibika jamanu katika suala hilo mimi nahisi tuwaache wasahau kisha tuwaumbue” Hilda kwa mara ya kwanza aliongea baada ya kuona anatazamwa na kila mmoja.
“unamaanisha nini kusema hivyo?” .Alphonce alimuuliza kwa pupa. Hilda alianza kuifafanua kauli yake kwa kusema “baada ya kukamilisha uchunguzi nakala zile nilivutiwa sana nazo,hivyo nilitoa vivuli vyake kisha picha za ushahidi nikazihamisha kwenye santuri nikavihifadhi mahali ili ziwe kumbukumbu kwangu”. Wote walitoa tabasamu na kufufua tumauni jipya mioyoni mwao….
“aisee we mwanamke sijui una….” Norbert hakumalizia kauli yake hiyo ya kimasihara baada ya kicheko cha ghafla kumshika, hali hiyo ilikuwa kwa wenzake pia waliopo eneo hilo kwa kitendo alichokifanya Hilda. “sasa nimekuwa kikatuni jamani, maana mnavyonicheka ” aliongea Hilda baada ya kuona vicheko vimezidi. Vicheko vya wote vilipotulia Joseph alisema “aisee sikutegemea kabisa kama utafanya hivi, hivi ulioteshwa nini kama kuna tatizo litatokea?”. “labda mzimu wa kitusi ulimfungulia njia” Allison naye alidakia na kusababisha wenzake wote wacheke.
“khaa jamani kuwa mtusi nayo imekuwa mada” Hilda aliongea kwa mshangao baada ya kusikia utani uliotunbukizwa na Allison. Mjadala uliikatika kwa muda na utani ukachukua nafasi yake dhidi ya Hilda, binti wa kitusi aliyeishi Tanzania kwa muda mrefu ingawa makazi yake ni Rwanda. Utani huu ulidumu kwa muda kisha Davis akawarejesha kwenye kwa kusema “sasa jamani suala limeisha au sio?” “hata mimi nadhani hivyo” Norbert naye akaafiki kauli ya Davis. Wote kwa pamoja wakakubaliana wasubiri joto la siasa litulie kisha waitoe kazi yao kwa mara ya pili kwa kutumia kampuni nyingine na sio ile ya awali. Wakitawaliwa nyuso zenye tabasamu baada ya kufufuka tumaini jipya la kazi yao, waliamua wapumzike siku hiyo ili wakaitulize furaha yao.
Januari mwaka uliofuata rais mpya wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania mheshimiwa Filbert Ole
aliapishwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es
salaam, hafla hiyo ya kuapishwa rais Ole
ilihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu
mbalimbali za jijj la Dar es salaam huku wachache
wakitoka mikoani kuja kushuhudia hafla hiyo.
Wanadiplomasia mbalimbali pamoja na viongozi
nao walialikwa katika sherehe hizo, viongozi wa
mataifa mbalimbali barani Afrika nao hawakuwa
nyuma katika uhudhuriaji wa sherehe hizo. Hadi
muda wa kuanza sheria hizo unakribia tayari
uwanja mzima ulishafurika watu walioalikwa huku wasioalikwa wakiwa nje ya geti, hali hiu
iliwalazimu watu wasioalikwa kukaa nje ya uwanja
huo kutokana na kutokana na ulinzi ulio ndani ya
uwanja. Ulinzi wa wanausalama nao haukuwa wa
kulegalega, ulinzi huu ulikuwa imara sana na
wenye kuridhisha sana kwa viongozi wa eneo hilo.
Muda mfupi kabla ya sherehe kuanza rais
anayemaliza muda wake Prof Athumani Kisiga
aliingia uwanjani akiwa katika gari la wazi kisha
akauzunguka uwanja huku akipungia mkono watu,
baada ya hapo alienda kusimama katika jukwa la
kiapo kisha mizinga ishirini na moja ikafuata. Rais
mstaafu alishuka kukagua gwaride la majeshi
yote, alipomaliza alipanda jukwaa na kuketi mahala
pake huku bendera ya rais ikishushwa kuashiria
kuisha kwa utawala wake. Hatimaye shughuli ya
kuapishwa kwa rais Ole ilianza mnamo saa tano za
asubuhi, rais mtarajiwa alipanda katika jukwaa la
kiapo baada ya rais mstaafu kupanda tayari wakiwa
pamoja na jaji mkuu. Shughuli za kuapishwa
ziliannza na kufuatiwa na kuapishwa kwa makamu
wa rais Dk. Hilary Jamadin, ukaguzi wa gwaride
maalum ulifuata kuhitiimisha shughuli hizo. Ratiba
nyingine zilifuata baada ya shughuli hiyo
kukamilika.
Muda huo huo sherehe zikiwa zinaendelea kwenye
mitaa ya jiji la Dar es salaam watu walikuwa
wakishuhudia kupitia kwenye luninga tofauti,
vikundi mbalimbali vya watu vilikuwa vikiijadili
sherehe hiyo ya kitaifa. Mijadala hiyo ilijadiliwa
katika makundi tofauti ndani ya mitaa ya
jiji , wengine walikuwa wamekaa majumbani mwao
wakiendesha mijadala hiyo. Hali hiyo pia ilikuwa imo
ndani ya nyumba moja ya kisasa maeneo ya
mikocheni. Huzuni ya watu humo ndani ilishaanza
kusahaulika
kwa watu wote isipokuwa mama mwenye nyumba
hiyo ambaye ni mjane, watoto wake wakiwa
wanafurahia kuangalia rais wao mpya waliyempigia
kura yeye alikuwa amezama katika dimbwi zito la
mawazo. Hakuwa mwingine bali ni mke wa
aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la kahama
bwana Gerald Geofrey aliyeuawa kwa kupigwa
risasi, mwanamama huyu alionekana ana dukuduku
zito moyoni wake na kila akiangalia sherehe hizo
za kumuapisha rais zilikuwa zinamchefua.
Hakuweza kustahimili kuziangalia sherehe hizo
tena kwani machozi yalishaanza kumtoka, akaingia
chumbani akilia kwa uchungu. Hali hiyo
iliwashangaza sana watoto wake ingawa
hawakuthubutu kumuuliza chochote, walimuacha
kama alivyo hadi atakapokuwa sawa.
Baada ya sherehe za kuapishwa kuisha na hatimaye
rais Ole kukabidhiwa majukumu ya urais na rais
mstaafu, shughuli za kimaendeleo ziliendelea kama
kawaida. Rais huyu aliooingia madarakani aliteua
baraza lake la mawaziri ndani ya muda mfupi tu,
baraza hili la mawaziri lilikuwa na mchanganyiko
wa mawaziri wapya na wa awamu iliyopita. Baada
ya mwaka mmoja tu toka rais Ole aingie
madarakani tayari nchi ilisheheni miundombinu ya
kila aina, pia huduma za kijamii zikaimarishwa
ndani ya muda huo. Hii ilisababisha wananchi
wazidi kumpenda na kumuamini sana rais wao,
hata wale waliokuwa sio wanachama wa chama
chake walianza kuwa na imani nae. Wizara zote
zilionekana zikifanya kazi ipasavyo na kupelekea
awamu hii ya urais iwe ya kipekee.
Ndani ya mwaka huohuo utafiti wa madini ulifanyika
wilayani kondoa katika mji kuu wa nchi hii, kiwango
kikubwa cha madini aina ya almasi kiligunduliwa
ndani ya eneo la kijiji cha Chambalo, madini hayo
yenye thamani kubwa yaligunduliwa ndani ya eneo
hilo na ripoti ikapelekwa kwa waziri wa maliasili na
utalii Dk. Jumanne Mdoe. Habari hizo pia
zilisambaa kwa wananchi wa kawaida ndani ya nchi
nzima, wengi wa wananchi kupitia vyombo vya
habari walitaka mgodi huo utumike kwa manufaa ya
nchi yao tu. Baada ya siku mbili waziri wa maliasili
na utalii alieleza uamuzi uliochukuliwa na wizara
yake juu ya madini. “hakika hii ni bahati ambayo
Tanzania imetuangukia na tunapaswa tuitumie
kama bahati ndani ya nchi yetu. Kumbukeni bahati
haiji mara ya mbili na tunapaswa tusiipoteze bahati
hii bali tuitumie kwa manufaa ya Tanzania yetu,
hivyo mimi na wizara nzima ya maliasili na utalii
tutaitumia bahati hii kwa ajili ya manufaa ya
watanzania na si vinginevyo. Hivyo watanzaniwa
watarajie mazuri kutokana na bahati hii na wawe
na imani ya kupata matunda bora ya bahati hii”
hayo ndiyo maneno ya waziri wa maliasili na utalii
juu ya matumizi ya hayo madini. Maneno hayo
yalimfurahisha kila raia aliyeyasikiliza kupitia
kwenye vyombo vya habari na ikawa ni kama
bahati kuwa na kiongozi kama yeye, watu walikuwa
wanangojea kwa hamu hayo matunda ya maliasili
iliyogunduliwa nchini mwao. Baada ya mwezi mmoja kupita toka hotuba ya
waziri huyo katika mkutano wake na waandishi wa
habari , ajali kubwa ilitokea maeneo ya
msata baada ya gari ndogo aina ya Land cruiser
kugongana uso kwa uso na Fuso lililobeba mkaa
likitokea mkoani Tanga kuja jijini Dar es salaam.
Dereva wa land cruiser alifariki papo hapo huku bosi
wake akiwa ni majeruhi hivyo kulazimika
kukimbizwa hospitali iliyo jirani kwa ajili ya
matibabu, askari wa usalama barabarani walifika
eneo la tukio mapema na kupima ajali. Upande wa
fuso lililobebe mkaa dereva wake hakufahamika
alipo hadi muda huo, ilikuwa ni mshangao mkubwa
sana kwa maaskari hao na walipoangalia gari aina
ya land cruiser ndio walipopata mshango zaidi.
“aisee hii si gari ya mheshimiwa” aliuliza mmoja
wa maaskari hao mwenye V moja begani. “kostebo
una uhakika maana hata majeruhi aliyekutwa
haujamtambua kutokanana majereha yaliyopo usoni
mwake” mwenzake alimwambia huku akitazama namba
za gari hilo pamoja na stika za gari hiyo. “aisee ni
lenyewe na nahisi hata majeruhi aliye kwenye hilo
gari ni yeye maana leo alikuwa anasafiri kuelekea
Tanga kuangalia hifadhi ya mkomazi” aliongea tena
yule askari baada ya kukagua namba za gari lile
kwa umakini. Walipomliza waliamua waliamua
kuwasiliana na wenzao waliongozana na gari la
wagonjwa la hospitali ya tumbi lililofika hapo kwa
ajili ya kuchukua majeruhi na mwili wa dereva
kwenda kuihufadhi.
Joseph Kiiza wa WAHANGA akiwa safarini akitokea
mkoani Kilimanjaro alikuta ajali kubwa iliyotokea
maeno ya Msata mkoani pwani, akiwa kama
mwanishi wa habari mwenye vifaa vyote
alisimamisha gari ya ofisi yake aina ya toyota
harrier na kuanza kuanza kuelekea eneo la ajali.
Hadi muda huo tayari utepe ulikuwa
ushazungushiwa eneo na askari walikuwa wamefika
wengi sana, alipojaribu kuuvuka utepe huo alizuiwa
na askari hali iliyomlazimu atie kitambulisho chake
na kuwaonesha maaskari hao. Maaskari
walimruhusu apite eneo hilo lenye utepe,
alipouvuka huo utepe alianza kupiga picha
mbalimbali kisha akafanya mahojiano na baadhi ya
maaskari wa eneo hilo. Akiwa anaendelea kupiga
picha mbalimbali za ajali hiyo kamba ya kiatu
ilimfunguka na kumlazimu ainame ili aifunge akiwa
jirani na fuso lililopata ajali, alipoinama tu alisikia
mlio wa bati la fuso ukitobolewa eneo ambalo
kichwa chake kilipokuwa wakati amesimama.
Hakuhitaji elimu ya ziada kutambua kuwa alikuwa
amelengwa na risasi ambayo ilimkosa baada ya
kuinama na kufunga kamba za viatu. Alijibiringisha
chini toka pale alioo kuelekea pembeni huku
maaskari wakiwa tayari wameelekeza silaha zao
ilipotokea risasi hiyo.
Hawakuweza kuambulia chochote zaidi ya vichaka
vilivyopo eneo hilo, baadhi ya askari waliamua
kuelekea ilipotoka risasi hiyo wakiwa wameweka
silaha zao kwa namna ya tahadhari. Joseph naye aliinua
kwa tahadhari pale chini alipokuwa amelala baada
ya kujibiringisha pembeni, alikimbia kwa haraka
hadi alipoliacha gari lake kisha akaingia na akakilaza kiti
chake pamoja na yeye kulala akiwa anahema mfululizo kwa tukio
lililomkuta. Hakutaka tena kutoka nje kwa kuhofia
usalama wake, akiwa amejilaza hapo alisikia mlio wa
pikipiki aina ya bajah ukitokea barabara ya vumbi
iliyo jirani na eneo hilo. Pikipiki hiyo ilifuata njia iendayo
Chalinze kwa mwendo wa kasi, mwendo wa pikipiki
hiyo pamoja na makelele yake ulimvuta Joseph na
kumfanya ainue kichwa na kuitazama. Aliiona ikiwa
ina mchoro wa chui katika bango lililokuwa
linaning’inia nyuma, aliipuuzia kisha akarudi na
kujilaza kwenye kiti cha gari yake. Baada ya muda
wale maaskri walirudi pasipo kuambulia chochote
cha ushahidi zaidi ya bunduki aina ya sniper rifle
iliyotelekezwa, Joseph aliinua kiti kisha akaiwasha
gari yake. Maaskari hawakushughulika naye kabisa
hata alipowaambia anaondoka wao walimruhusu
aende, Joseph alifuata barabara iendayo chalinze
kwa mwendo wa wastani kisha akaongeza mwendo
ili awahi aendapo. Alifanikiwa kufika Chalinze ndani
ya muda mfupi tu kutokana na kutumia mwendo
mkali, alifuata njia iendayo Dar es salaam kwa
mwendo ule hadi kibaha . Hapo alifuata barabara iliyo upande wenye kibao
kilichoelekeza mahali ilipo hospitali ya tumbi toka
barabara ya morogoro katika eneo ambalo zamani
lilijulikana kama Tamko. Baada ya kuingia barabara hiyo alienda mwendo mfupi tu
alipishana na ile pikipiki aina ya baja ikitokea mahali
anapoelekea, sasa alimuona dereva wa pikipiki hiyo
alivyo ingawa alikuwa amevaa kofia ya kujikinga
kichwani. Alikuwa ni mtu mrefu na mwembamba
mwenye mavazi yaliyomkaa vilivyo na mikononi
alivaa glovu za kuendeshea pikipiki, kumuona hapo
kwa mara ya pili hakukumshtua Joseph zaidi ya
kuvutika kuuangalia jinsi alivyo. Alipofika hospitali ya tumbi alipitiliza
hadi mapokezi , alijitambulisha kisha akumuulizia
majeruhiwa ajali aliyefukishwa hospitalini hapo.
Joseph alipelekwa kwa mganga mkuu wa hospitali
hiyo kwani manesi na madaktari wengine
hawakutakiwa watoe taarifa yoyote juu ya majeruhi
huyo, alipofika alijieleza kwa mganga huyo shida
yake iliyomleta kisha akaomba ushirikiano katika
jambo hilo.
“kusema ukweli muda si mrefu tumepokea majeruhi
wa ajali ambaye alikuwa ni mheshimiwa, ninasikitika
kukutaarifu kuwa hatunaye tena duniani hadi sasa”
aliongea mganga mkuu Joseph akinakili maelezo
hayo, alimsaili mganga huyo kwa maswali
machache kisha akaondoka eneo hilo baada ya
kuwaaga wenyeji wake.
Taarifa za kifo cha waziri wa maliasili na utalii
zilisambaa kama moto wa kifuu, karibu sehemu
zote za jiji la Dar es salaam na majiji mengine
yalishazipata taarifa hizo kabla hata vyombo vya
habari havijaitangaza. Maelfu ya wananchi
walihuzunika na kifo cha mtumishi wa umma
mwenye kuijali kazi yake, taarifa hizo zilipofika ikulu
zilipokelewa kinamna nyingine ingawa rais Ole alitoa
salamu za rambirambi kwa familia ya waziri wake.
Ilikuwa ni huzuni isiyoelezeka kwa familia ya
marehemu, hata watu wa karibu waliomjua vizuri
waziri huyo. Siku iliyofuata mwili wake uliletwa jijini
Dar es salaam kisha ukaenda kuhifadhiwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili, hadi mwili
unaingizwa katika chumba cha kuhifadhiwa maiti
tayari hospitali hiyo ilifurika waandishi wa habari
waliokuwa wakisaka habari na utbibitisho juu ya hilo
suala. Joseph na Nobert wakiwa miongoni mwa
waandishi hao, walitumia taaluma yao vizuri jambo
lililowawezesha wapate picha za uthibitisho wa tukio
hilo. Waliporidhika waliondoka hadi walipoacha gari
ya kikundi chao aina ya toyota Noah ya rangi nyeupe, walipanda
wote huku Norbert akiketi nyuma ya usukani kisha
wakaondoka hospitalini hapo. Walifuata njia iendayo
kituo cha zimamoto, wakiwa wanamalizia kona ya jengo la Swiss kuingia
katika barabara ya umoja wa mataifa Joseph aliangalia
nyuma kupitia kioo cha pembeni kilicho upande
wake. Hapo ndipo alipoingiwa wasiwasi kwa kile
alichokiona aliiona pikipiki aina ya baja ikiwa nyuma
yao baada ya magari mawili, alipomtazama dereva
wa ile pikipiki alikuwa mrefu na mwembamba kama
aliyekutana nae jana msata na hospitali.
“Norb huyo jamaa mwenye pikipiki huko nyuma sina
imani nae” alimwambia Norbert
“yupi? huyo kwenye baja au boxer maana wapo
wawili huko nyuma na wote wamevaa suti nyeusi”
alisema Norbert na kumfanya Joseph ageuke
aangalie vizuri, alipoangalia aliona pikipiki ya tatu
ain ya suzuki ikija kwa kasi kisha ikaungana na wale
wawili hali iliyofanya waonekane wapo watatu
kiidadi. Alipowatazama vizuri aliona wote ni
wembamba na warefu tena wamevaa mavazi
yanayofanana.
“wapo watatu Norb inabidi tufanye kitu aisee ili
tuwakwepe” aliongea Joseph.
“punguza uoga Jose” aliongea Norbert.
“Norb niliwaambia jana nimekoswa na risasi kisha
nikaiona pikipiki aina ya baja ikiendeshwa na mtu
mwembamba na mrefu baada ya kukoswa na risasi
na nilipokuwa naenda hospitali ya Tumbi, sasa mimi
sina imanu nae huyo” alifafanua Joseph na
kumfanya Norbert aifuate barabara ya morogoro kwa
mwendo wa kasi punde tu alipofika katika makutano
ya barabara yaliyo jirani na kituo cha zimamoto
maarufu kama fire, aliifuata barabara hiyo kwa
mwendo wa kasi huku akiangalia nyuma. Zile
pikipiki tatu nazo bado zilikuwa zinawafuatilia kwa
mwendo wa kasi lakini hazikuwapita wao, hali hiyo
ilimsababisha Norbert aifuate barabara iendayo Ilala
baada ya kufika makutano ya barabara yaliyo jirani
na msikiti wa kichangani maeneo ya magomeni
mapipa. Akiwa katika mwendo uleule huku akiyapita
baadhi ya magari, aliifuata barabara hiyo hadi
mzunguko wa kigogo kisha akafuata barabara ya
mkato iendayo ubungo kupitia kigogo. Hadi muda
huo tayari ilikuwa ni muda wa saa saba muda huo
watu walikuwa wakiswali swala ya
adhuhuri katika misikiti. Norbert alifuata njia hiyo ya
mkato iendayo ubungo kisha akaingia katika
maegesho ya magari ya msikiti mmoja wa ghorofa
uliopo upande wa kulia mkabala na dhule ya msingi ,maegesho hayo ya msikiti yalikuwa
yana magari ya waumini wachache. Kulikuwa kuna
gari aina ya Noah zenye kufanana na gari la akina
Noerbert, hakika huo ulikuwa mwanya kwa akina
Norbert kwani nao waliegesha gari kisha wakalaza
siti walizokalia. Baada ya muda walisikia milio ya
pikipiki tatu tofauti huku makelele ya pikipiki aina ya
baja ikiwa inavuma zaidi, pikipiki hizo zilisimama
kwa muda mfupi kisha zikaondoka kuendelea mbele.
Vijana watatu wa kundi hatari la three devils kutoka
Marekani walikuwa wapo maeneo ya hospitali ya
taifa ya muhimbili, walikuwa hapo kuhakikisha kama
mwili ulioingizwa hapo ni wa mheshimiwa waziri
aliyepata ajali siku iliyopita. Wakiwa na vitambulisho
feki vya usalama wa taifa, waliweza kuiona maiti
baada ya kujitambulisha wao ni usalama wa taifa na
walikuwa kwenye uchunguzi. Walipotoka mmoja wao
alipiga simu na kuongea, “ni yeye bosi” kisha
akakata simu na kuwaashiria wenzake waondoke.
Wakiwa wanatoka waliwaona Norbert na Joseph
wakiwa pamoja, walipotaka kuondoka kuondoka
mmoja wao akawaambia wenzake wawili, “ni
sehemu ya kazi yetu, au mmesahau”. Walitazamana
kisha wakaenda kuziegemea pikipiki zao huku
wakiwasubiri wakina Norbert, baada ya muda
Norbert na Joseph waliingia ndani ya gari lao na
kuondoka hospitalini. Three devils nao waliingia
kwenye pikipiki zao na kuanza kuwafuatilia wakiwa
katika namna ya kufuatana katika mstari ulionyooka,
mwenye pikipiki aina ya bajah akiwa mbele kisha
akafuata mwenye pikipiki aina ya boxer na mwisho
akaja mwenye pikipiki aina ya suzuki. Kwa
walivyopangana ilikuwa ni vigumu sana mtu kujua
kama wapo watatu kwa muonekano wa mbele,
walitembea hivyohivyo hadi walipofika jirani na
makutani ya kituo cha kuzimia moto jirani na shule
ya jangwani. Hapo mwenye boxer alitoka pembeni
kisha mwenye suzuki akafuata na kukaa nyuma ya
mwenye bajah kwa upande wa kushoto na kulia.
Hapo ndipo gari ya akina Norbert iliongeza mwendo
kuifuata barabara iendayo magomeni,
“wamegundua
hawa,tuwafuate hivihivi hakuna kuwaacha” aliongea
mwenye bajah kuwataarifu wenzake kupitia simu zao
ndogo zilizokuwa ndani ya sikio. Waliwafuata
wakiwa na mwendo wa wastani ili kuwaondoa hofu
wakina Norbert, walipofika magomeni walifuata njia
iendayo Ilala kisha wakapunguza mwendo ili
kuwapumbaza wakina Norbert na kuhakikisha
hawawapotezi. Hadi wakina Norbert wanaingia
mzunguko wa kigogo na kuelekea upande wa kulia wao walikuwa
wamewaona ila walikuwa mbali kidogo, hapo ndipo
walipokuja kupigwa chenga ya mwili na Norbert
baada ya Norbert kuegesha gari jirani na msikiti
kwenye magari yanayofanana na gari lao. Three
devils walipofika hapo kwenye kona yenye barabara
inayopita msikitini hapo, walisimama kwa muda
kisha wakayaangalia magari hayo kwa umakini
halafu wakaondoka.
Walienda hadi ilipo shule ya sekondari ya Loyola
kwa mwendo wa kasi, hapi ndipo walibaini
wamepigwa chenga ya mwili. Baada ya kubaini
wamepigwa chenga ya mwili, waligeuza pikipiki zao
kisha wakatazamana kila mmoja halafu wakarudi
kule walipotokea. Walipofika kigogo kwenye msikiti
mkabala na shule ya msingi, walikuta bado watu
hawajamaliza kuswali swala ya adhuhuri na moja ya
magari haikuwepo eneo lile. Hali hiyo iliwafanya
wamuite kijana mmoja muuza maji aliyepo jirani,
“hey njoo mara moja!” alipaza sauti mwenye pikipiki
aina ya bajah. Kijana huyo alifika mara moja akiwa
na deli lake la kuuzia maji baada ya kusikia wito
huo, “mambo vipi?” alimsabahi huku akitoa noti ya
shilingi elfu moja kisha akampatia yule kijana. “safi
braza unataka ya shilingi ngapi?” muuza maji
aliitikia salamu kisha akamuuliza maji anayoyataka.
“nipe ya mia saba, halafu samahani naomba
nikuulize” aliongea huku akiweka stendi ya pikipiki
halafu akashuka.
“usihofu braza uliza tu” aliongea muuza maji huku
akimpatia maji.
“eti hujaona gari yoyote aina ya Noah ikija kuegesha
hapa msikitini wakati watu wanaswali”.
“nimeiona braza sema imeondoka kitambo kidogo bila
hata kutoka mtu”.
“poa poa kaka ngoja sisi tuwahi” aliongea huku
akiuma meno yake kwa hasira. Alichukua maji hayo
pasipo kuyanywa kisha akaenda kwenye pikipiki
yake, alipofika akaiwasha kisha akawaashiria
wenzake waondoke, alitia gia kisha akaondoa
pikipiki hiyo huku mkono mmoja akiwa ameshika
maji aliyoyanunua. Alienda hadi kwenye mzunguko
wa kigogo kisha akayatupa maji hayo kwenye mtaro
halafu akavuta mafuta kuelekea njia iendayo Ilala.
Jim ndio jina lake na ndio anavyotambulika hata
kwa wenzake, ni mmarekani aliyeingia Tanzani
miaka miatu iliyopita kwa agizo maalumu la mkuu
wake anayejulikana kwa jina la Eagle kutoka Miami
jijini Marekani. Kijana huyu ni muuaji wa hatari na
wakuaminika wa kundi la Three devil , yupo nchini
Tanzania kwa miaka hiyo ili aweze kutimiza lengo
maalumh aliloamriwa kulitimiza. Jim ameingia
Tanzania kama mfanyabiashara aliyeamia Tanzania
kwa ajili ya kuwekeza, akiwa nchini kwa muda wote
huo amefanikiwa kujifunza lugha ya kiswahili kama
inavyozungumzwa na makundi tofauti ya watu
nchini kulingana na umri na kazi zao. Hadi mwaka
wa tatu ndipo alipoongezewa wenzake wawili wa
kundi lake wakiwa tayari wameshajifunza kiswahili,
sasa wapo kazini na wameshafanikisha sehemu ya
kazi waliyotumwa. Akiwa peke yake amefanikisha
mauaji ya waziri kwa kutengeneza ajali dhidi yake,
pia alijaribu kumuua mwandishi wa habari ingawa
mpango huo ulifeli. Michael na Morris ndio
wamarekani wengine wanaounda kundi la Three
devil wakiwa chini ya Mr Eagle wa Marekani.
Mpango wao wa kwanza toka waanze kufanya kazi
pamoja umefeli baada ya kupigwa chenga ya mwili
na Norbert, sasa wana hasira na wanaelekea yalipo
maskani yao kujipanga upya.
Norbert aliinua kiti cha gari kisha akawasha gari
baada ya zile pikipiki kupita na milio kufifia, alirudi
hadi kwenye mzunguko wa kigogo kisha akafuata
barabara iendayo ilala. Alipofika mataa ya Ilala boma
alikuta taa za upande wake zikiwa zimeruhusu na
kumlazimu kunyoosha moja kwa moja hadi yalipo
mataa ya keko, hapo napo ikawa ni kama bahati
baada ya kukuta askari wa usalama barabarani
akiwa ameruhusu magari ya upande wake. Alikata
kona kuingia barabara ya mwalimu nyerere iendayo
Tazara halafu akaongeza mwendokasi wa gari,
walipofika yalipo mataa ya makutano ya barabara
maarufu kama Tazara aliamua kufuata barabara ya
Mandela iendayo vetenari. Alitumia dakika takribani
tatu akawa ameshavuka vetenari na sasa alikuwa
anakata kona kuingia upande wa kulia kufuata
barabara iendayo mtoni kwa azizi ally kupitia
temeke. Hapo alienda kwa mwendo wa kasi
kutokana na uchache wa magari hadi usalama kisha
akaingia upande wa kulia kwenye barabara ya vumbi
ipitayo shule ya msingi Muungano eneo la temeke,
aliendelea hadi alipoivuka shule ya msingi
muungano kuingia
kushoto kisha akaenda moja kwa moja hadi katika
nyumba moja yenye geti kubwa jeusi kisha akapiga
honi. Ndani ya dakika moja geti lilifunguliwa kisha
akaingiza gari hafi kwenye maegesho ya nyumba
hiyo, alikanyaga breki kisha akazima gari halafu
wote wakashuka kwa haraka huku wakihema kama
wamekimbia mbio ndefu. Wakiwa na mwendo wenye
papara kama wamekuja kwa shari, waliingia ndani
ya nyumba hiyo kupitia mlango wa uani hadi katika
ukumbi wa nyumba hiyo unaopendeza kuutazama.
Waliwakuta wakina Hilda, Davis na Allison wakiwa
wapo kwenye meza ya inayotumika kwa chakula
iliyopo katika ukumbi wa pili jirani na ukumbi wa
sebule wa nyumba hiyo, Joseph alijitupa kwenye
kochi huku akihema mfululizo na Norbert alibaki
kasimama huku mikono yake ikiwa imeshika kiuno
chake na kichwa akiwa anakitikisa kwa masikitiko.
“nyie wanaume vipi kwema?” aliuliza Hilda baada ya
kuwaona wakiwa katika hali hiyo.
“ni kinyume cha kwema” alijibu Norberr huku
akintoa kitambaa mfuko wa nyuma wa suruali yake
kisha akajifuta jasho katika uso wake.
“kulikoni” aliuliza Hilda huku akigeuza kiti
kuwatazama Norbert na Joseph.
“yule jamaa niliyemuona msata na kibaha
tumuona tena muhimbili leo akiwa na wenzake
wawili” aliongea Joseph halafu akajiweka sawa
kwenye huku
akihema kisha akasema ,”walikuwa wanatufatilia
pasipo sisi kujua, na hata tulipojua Nor aliongeza
mwendo wa gari na wao wakaongeza mwendo wa
pikipiki zao kutufualia hadi sehemu moja yenye
msikiti wa ghorofa. Hapo ndipo Nor akawapiga
chenga wakapotea”.
“pongezi kwako mr Transporter kwa kucheza na
usukani kama unamkimbia aduo kuu” aliongea Allison kumfananisha Norbert na
muigizaji Jason Statham wa Uingereza aliyeigiza
filamu ya The transporter. Wote walicheka humo
ndani kasoro Joseph.
“yaani nyie sisi tumekimbia umauti mnatucheka, na
wewe Nor unacheka wakati ulikuwa unawindwa”
alipngea Joseph huku akijigeuza kwenye kochi kisha
akalala chali kuangalia dari la nyumba hiyo.
“Jose na wewe umezidi uoga” Davis alisema huku
akicheka
“ndugu kifo kitu kingine kabisa msilete mzaha”
Joseph alisema akiwa anajiinua kivivu kwenye kochi
huku wenzake wakicheka, aliposimama wima alienda
moja kwa moja hadi kwenye jokofu lililopo jirani na
meza ya chakula. Alitoa pombe kali kisha
akaifungua halafu akaipeleka kichwani, alikunywa
funda moja halafu akawatizama wenzake na
kuwaambia “mimi leo wacheni nipumzike mpaka
kesho, mnaweza mkaendelea”. Joseph alifuata
ukumbi mwembamba
unaotenganisha vyumba vya humo ndani kisha
akfungua mlango mmoja wa vyumba halafu akaingia
ndani na kuufunga. Huku katika ukumbi wa
unaotumika kama sehemu ya chakula Norbert
alivuta kiti kilicho jirani na Hilda kisha akakaa karibu
ya Hilda, “mahaba niue hao wapo pamoja” aliongea
Davis kuwatania Norbert na Hilda.
“we ulitaka tuwe mbalimbali kwani?” Hilda alisema
akiwa
ameweka mkono wake katika bega la Norbert.
Waliendea kuongea huku wakitaniana kwa muda
mfupi kisha ukimya ukatawala huku Norbert na Hilda
wakiwa wanakumbatiana na kupigana na mabusu
hapo mezani.
“ngoja tuwapishe nyie mahaba niue”
aliongea Davis akivuta kiti nyuma kisha akasimama
halafu akaondoka eneo hilo, Allison naye alisimama
akaondoka kumfuata Davis. Wakiwa wamebaki
wenyewe hapo ukumbini Hilda alinyanyuka katika
kiti chake kisha akaenda kukaa katika mapaja ya
Norbert miguu yake akiipitisha kiunoni mwa kijana
huyo. Hapo waligusanisha mapaji yao uso wakawa
wanatazamana kwa ukaribu, hakika walionekana ni
watu waliozama kwenye mapenzi mazito sana kwa
mkao huo waliokaa.
“kuna simu leo kutoka kwa CE imeingia leo
asubuhi” aliongea Hilda kwa sauti ya chini
“mh! huyo kibabu anasemaje?” aliuliza Norbert kwa
sauti ya chini.
“anataka kuongea na wewe, amesema ukirudi
nimpigie”
“mh! Kuna jipya limezuka nini?” Norbert aliuliza
swali hilo kisha akamnyonya ndimi Hilda huku
akimpapasa mgongo baada ya
Joseph kutokea eneo hilo.
“wa mahaba subirini kwanza nichukue kinywaji ndio
muendele”
Joseph aliwaambia kwa sauti iliyochangamshwa na
pombe halafu akafungua jokofu, alitoa
pombe kali ya pili kisha akaondoka..
Hapo Norbert aliacha kunyonya ndimi ya Hilda huku
akiwa amegusanisha paji la uso kama alivyokuwa,
alihema kwa nguvu kisha akasema, “hizi kazi hizi
aisee ni tabu kila siku kama wacheza filamu”. Kauli
hiyo ilimfanya Hilda acheke kwa sautu ya chini
akiwa tayari ameshaingiwa na aibu zake za kike.
“Nor inabidi umpigie CE leo hii maana unamjua yule
mzee akisema ujue kuna jambo” Hilda aliongea
huku ameelekeza macho yake pembeni kwa aibu.
Norbert alimshika kidevu halafu na kumfanya Hilda
amuangalie kwa macho malegezo. Walitazamana
kwa muda mfupi kisha Norbert akambusu Hilda
mdomoni jambo lililosababisha binti huyo afumbe
macho kwa hisia.
“Nor bwana ushaniweka katika wakati mgumu
mwenzio kumbuka tupo kikazi acha tafadhali” sauti
ya kudeka na yenye kubembeleza ilitoka kinywani
mwa Hilda, muda huo tayari Hilda alikuwa ameibana
miguu yake kwa nguvu katika kiuno cha Norbert.
“najua mama ila hapa imebidi tuwe hivi” aliongea
Norbert huku akinyanyuka na Hilda pamoja akiwa
amembeba kama anampeleka mtoto aliyelala
kitandani. Hilda naye alikuwa amepitisha miguu
kiunoni mwa Norbert na mikono ikiwa shingoni kwa
Norbert huku vifua vyao vikiwa vimegusana. Norbert
alitembea kuufuata ukumbi mwembamba
unaotenganisha vyumba vya kulala katika nyumba
hiyo, alipofika katika mlango wa chumba ulio
mkabala na chumba alichoingia Joseph alinyonga
kitasa huku mlango ikikaidi amri ya kufunga na
ukatii amri ya kufunguka. Alimuingiza binti huyo
ndani kama anaenda kumlaza mtoto, alienda hadi
kwenye kitanda kisha akamuachia kitandani ili arudi
kufunga. Hadi muda huo Hilda alikuwa yupo
amelazwa kitandani ila hataki kutoa miguu kiunoni
mwa Norbert wala mikono shingoni.
“no Hil wacha nifunge mlango kwanza” aliongea
Norberr na kupelekea Hilda amuachie, Norbert alienda
kufunga mlango kisha akarejea kitandani hapo
alipomuacha Hilda. Muda huo tayari Hilda alikuwa
amelala chali akiwa amejiweka huru kabisa, Norbert
alipanda juu ya kifua chake kisha wakagusanisha
ndimi na kupelekea wote waingie kwenye
ulimwengu mwingine tofauti na sayari hii ya dunia.
Hakika kila mmoja alionesha kumuhitaji mwenzake
na hakuna aliyekuwa kumuacha mwenzake kwa
muda huo, kazi yao waliiweka pembeni kwa muda ili
kuhitimisha kazi hiyo isiyo rasmi. Baada ya masaa
mawili walikuwa wameshakamilisha kazi yao na
sasa wamepitiwa na usingizi mzito wakiwa
wamejifunika shuka moja, ilipotimu saa kumi na
moja jioni usingizi wao ulikatika baada ya simu ya
mkononi inayotumiwa kwa ajili ya kazi kuita.
Norbert aliinuka kivivu huku akiangalia mpigaji wa
simu hiyo akiwa na uchovu mwingi, jina la mpigaji
lilimuondoa uchovu kisha akaipokea simu hiyo kwa
pupa kisha akaongea ,”N001 hapa naongea”.
“njoo ofisini haraka ukiwa na HI002” ilisikika sauti
ya mpigaji ikitoa amri kisha simh ikakatwa. Norbert
akaiweka simu kwenye mtoto wa mtanda kisha
akampiga Hilda kibao katika kalio lake halafu
akamwambia, “CE katuita sasa hivi, jiandae twende
ofisini kwake”, kisha akaokota kaptula yake
aliyoitupa wakati wanaanza kasheshe na kuivaa
mwilini. Hilda naye alishaamka na alikuwa
anajinyoosha akiwa hana nguo yoyote mwilini.
“aisee kama siyo kazi tungekesha leo, maana
nikikutazama mh!” aliongea Norbert na kusababisha
Hilda amtizame jicho la upande kisha akasema
“looh! Lionee”. Hilda alijifunga taulo kisha
akamshika Norbert mkono, alimuongoza hadi bafuni
pasipo Norbert kuleta pingamizi lolote. Huko
walioga kisha wakatoka baada ya kumaliza,
walijiandaa kisha wakatoka humo chumbani hadi
sebuleni wakiwa wameshikana mikono kiupendo. Sebuleni waliwakuta Allison na Davis wakiangalia luninga na kuwaaga kisha wakatoka hadi nje kwenye banda la
gari lililopo jirani maegesho ya gari ndani ya
nyumba hiyo, walifungua milango ya banda hilo
halafu wakaingia ndani kulifuata gari aina ya suzuki
ya rangi nyekundu. Waliingia wote kwa pamoja huku
Norbert akiwa ndio dereva wa gari hilo, mlio wa
kuwashwa kwa gari hilo ulisikika kisha matairi yake
yakaanza kujongea taratibu na kusababisha gari
litoke kwenye banda la gari na kufuata uelekeo wa
getini. Geti lilifunguliwa na mlinzi kuruhusu gari hilo
litokee nje ya nyumba hiyo kwa mwendo wa
taratibu, mwendo uliongezwa baada ya kuingia
katika barabara ya vumbi inayopita shule ya msingi
muungano kuelekea usalama kwenye barabara ya
lami.
Ndani ya nyumba ya ghorofa iliyopo maeneo ya msasani kwenye moja ya mitaa ya msasani ambayo huwa wanaishi watu wenye kipato cha juu, kulikuwa na kikao cha dharura katika moja ya chumba cha mikutano cha nyumba hiyo na wahudhuriaji wake walionekana ni watu wenye kujiweza kiuchumi na wenye kauli.
Mmoja akiwa ni kigogo maarufu wa Tanzania anayetumia jina KL akiwa sehemu kama hizo, mwingine akiwa ni kiongozi maarufu anayejiita FI na wengine ni vijana wa kundi la Three devils. Suala lililokuwa linajadiliwa katika mkutano huo ni kuhusu mpango wao madhubuti wa kupunguza vikwazo katika mambo yao. Hadi muda huo wote walishapeana salamu na sasa walikuwa ndio wanaanza kujadili, “wakuu napenda mjue kuwa tushapunguza moja ya magugu katika kubakikisha shamba letu linastawisha mazao yetu” Jim aliongea kwa kutumia lugha ya mafumbo kutokana na uwepo wa wafanyakazi waliokuwa wakiwahudumia wahudhuriaji wa mkutano huo.
“vizuri Jim sasa naona kuna gugu jingine nitaliweka katika anga zenu ili muliondoe upesi kama ilivyokuwa kwa gugu la kwanza mtindo ni uleule” aliongea FI kumpongeza Jim kisha akampa kazi nyingine hapohapo.
“pia ningependa ningependa wale kenge watano waondolewe haraka maana ni hatari sana” KL alitoa wazo hilo kwa kutumia lugha ya isiyo ya mafumbo baada ya wafanyakazi wote kutoka katika chumba cha mkutano. “hao ni kiporo kwanza kwa sasa tushughulikena hawa wenye kauli huku tukifunga midomo kupitia kwa wachapishaji” aliongea Michael kwa mara ya kwanza.
“wazo zuri hilo Michael sasa baada ya huzuni kutulia nitaweka gugu jingine jirani na jembe ili liweze kulimwa haraka” FI aliongea kisha akavuta bilauri yenye kinywaji iliyopo halafu akapiga funda moja. “sasa huko tumemaliza ila kwa sasa inabidi tufanye juu chini tuwajue wanausalama wa kampuni ya upelelezi ya EASA walioingia nchini kwa kazi maalum ambayo bado hatujaijua mpaka saea , yaani siba imani nao kabisa” KL alibainisha jambo geni ambalo halijukani kwa wenzake waliopo haoi kwenye mkutano.
“KL hiyo ni habari nyingine ila hawa vijana nina uhakika wataimaliza,sasa mimi na KL tunawahi sehemu mra moja. Tutakuja siku nyingine kuwapa maelekezo kama yakihitajika” FI aliongea baada ya simu yake kuita kisha akanyanyuka akiwa na KL ambaye alishanyanyuka tayari. Walitoka ndani ya chumba hicho cha mkutanina kuwaacha Jim,Michael na Morris wakiwa wanajadiliana mamboyao mengine.
ITAENDELEA
Jinamizi Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;