SIMULIZI Ajira Toka Kuzimu Episode 02
NEW AUDIO

Ep 2: Ajira Toka Kuzimu

SIMULIZI Ajira Toka Kuzimu Episode 02

IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA

*********************************************************************************

Simulizi : Ajira Kutoka Kuzimu
Sehemu Ya Pili (2)

 “Mambo dada??” sauti kavu iliyotangaza uchangamfu kutoka kwa kijana aliyekuwa kifua wazi ilimsabahi binti huyu ambaye majimaji yaliyokuwa yamemlowanisha kiasi fulani yaliifanya ngozi yake inate kwenye nguo yake sehemu za makalio na mgongo na kumfanya awe katika hali ya kutia matamanio mwanaume yeyote ambaye atajikita kumtazama kwa muda mrefu.
“Safii!!” alijibu kama hataki vile. Alimwangalia yule kaka kwa ncha za macho yake ili kuhakikisha kama alikuwa mpita njia ama alikuwa ana jambo jingine. Dada huyu aliona aibu kuendelea na majaribio yake ya kuogelea kwa kumwonea aibu kijana huyu aliyekuwa na mpira wa tairi ya gari uliojazwa upepo mwingi na kuufanya mpira huu kuunda mduara.
Baada ya kijana mwenye lile boya kuendelea kuwa jirani yake bila kusema lolote yule binti akaanza kuhisi kama anaukosa uhuru. Akaanza kutembea hatua kwa hatua akizifuata njia zake na kwenda mahali alipopajua yeye binafsi. Japo hakuwa amepanga kuondoka.
“Samahani dada, nilikuwa nakuja kwako ujue…samahani kama nitakukwaza..” alianza kujieleza kijana yule mfupi akiwa na nywele chache kichwani. Binti hakujibu kitu, akaendelea, “Utapendeza sana kama ukijua kuogelea, hata bahari hii itafurahia kugusana nawe wakati ukizipiga mbizi kuuburudisha mwili wako”
“Kwani nani kakwambia sijui kuogelea..” alijibu yule dada huku akionyesha kukerwa na maelezo yale ambayo yalikuwa yana ukweli ndani yake.,.
“Tazama wazungu wale na hao waarabu, hawajui kuogelea hao, ukishajua wewe utakuwa unawacheka, waone waone wanayakimbia mawimbi..” Yule kijana hakujali majibu ya yule binti akaendelea na mazungumzo yake akiwa na furaha.
“Jamani si ningetaka huduma zako ningekuita jamani.” Aliendelea kubisha yule binti.
“Halafu kwa jinsi ulivyokuwa mrembo wala hautalipia nitakulipia mimi…..wewe utanilipa siku unayotaka. Cha muhimu wewe ujue tu kuogelea na hii bahari ifurahie mwili wako. Ujue bahari nd’o ndugu na rafiki yangu hapa mjini, sasa kumfurahisha rafiki yako ni vibaya jamani. Mi nataka we ujue kuogelea bahari ifurahie.” sasa yule binti akalazimika kutabasamu, hali hiyo ikamvuta zaidi yule kijana. Akajisogeza jirani yake. Mambo yalishaanza kumnyookea.

“Sasa tutaanzia haya maji mafupi, ukiona tunakwenda sawa tunasogea mbele zaidi, halafu sio lazima ujue leoleo, lakini usipokuwa muoga leoleo utaweza kukata maji mwenyewe. Kuoga ni kitu kimoja chepesi sana sema tu watu ni waoga… naamini wewe sio muoga… hivi unadhani ni wasichana wangapi wanaweza kujifunza kuogelea peke yao kama ulivyofanya wewe…”
“Mh!! Nadhani una nia ya kunizamisha wewe maana dah!! Naogopa maji mie we nisifu bure tu hapo. Mi muoga kuliko hao waoga unaowasema hapa” yule binti hatimaye akatoa jibu ambalo lilimwingiza mtegoni. Tayari alikuwa amevutiwa na somo la yule kaka aliyehitaji kumfundisha kuogelea. Alikuwa amekubaliana na hali ile ya aibu ya yeye kutojua kuogelea.
“Yaani tangu nianze kuwafundisha watu kuogelea hakuna hata mmoja amewahi walau kumeza nusu kikombe maji haya machafu ya baharini…ukimeza matone ya maji niambie na nitajiuzuru kazi hii” yalimtoka kwa upole hayo maneno. Yule binti akajikuta anacheka kwa nguvu kidogo, meno yake ya mbele yalikuwa yameungua kidogo hali iliyomfanya kuvutia zaidi hasahasa alipojaribu kucheka kwa kujificha ili anayemtazama asiligundue hilo. Lafudhi yake kutoka mikoa ya kaskazini lilikuwa jawabu tosha.
Mchaga!!

“Sasa tuanzie pale hivi, nikuonyeshe kwa nini naitwa Hassan Tembo.”
“Unaitwa Tembo heee!!! Makubwa mbona kimwili kidogo hicho halafu jina zito” alishangaa yule binti.
“Twende nikakuonyeshe kwa nini naitwa hivyo, mambo yangu katika darasa hili la kuogelea si ya kiswala swala ni ya kitembo tembo” alijibu kwa kujiamini Hassan.
“Kwani nawe waitwa nani vile….”
“Maria…”
“Nikisema Pretty Maria nitakosea” Tembo akamsifia
“Jamani kuna rafiki yangu huwa ananiita hivyo..hujakosea..”
“Dah!! Na kweli wewe Pretty”
“Nikiweza kuogelea nitakulipa pesa nyingi sawa”
“Usijali utajua na kila wiki utatamani kuja kuogelea”

Hassan Tembo akazama kwenye maji na Maria, somo likaanza, yale maji mafupi waliyamaliza mara moja likafuata somo la maji marefu, huku sasa Maria akaanza kushikwa na uoga, wakiwa wote katika ule mpira uliojazwa upepo, Tembo alikuwa amemshikilia barabara Maria, Maria naye alimkumbatia kwa nguvu zote Hassan, mawimbi yaliwapeleka huku na huko Maria akawa anaifurahia hali ile, hatimaye wakafika mbali kiasi cha kutosha. Miili yao ilikuwa imegusana, Tembo akiwa na kibukta chake chepesi na Maria akiwa na kichupi cha kuogelea kinachofanana na bikini ni kama walikuwa uchi kwani maji yaliunganisha nguo na ngozi zao pamoja. Baada ya muda walibadilisha pozi sasa, Hassan akawa anamwelekeza Maria jinsi ya kujiweka katika maji ili uweze kuelea. Hapa sasa kila Maria alivyoogopa Tembo akawa anamdaka, mikono yake miwili ikawa inakumbatia kifua hichi cha wastani cha Maria. Hali hiyo ilidumu kwa muda kidogo mara Maria akawa hawezi tena hata kuogelea tena mwili ukawa mzito. Tembo akiwa na uzoefu kwenye maji akawa amegundua kuwa tayari Maria alikuwa amehama kiakili hayupo tena pale baharini.
“Aliuliza kwanini naitwa Tembo na sio Swala ok!! Ngoja niwe mstaarabu nimpe jibu lake la kuridhisha..” Tembo alijisemea kimoyomoyo huku akimrejesha Maria katika Boya, miguu yao ikaingiliana wakawa wanaangaliana. Tembo akatumia mwanya huo wa kutazama kulitoa lile jicho lake la huba ambalo wanawake kadhaa lilikuwa linawapagawisha. Lile jicho likamzidi ujanja Maria akajikuta anajibu kwa namna ya ‘nataka’ Tembo huyu asiyejua kusema sitaki akamkumbatia kwa nguvu hapo wakiendelea kuelea baharini.
Hakuna muogeleaji hata mmoja aliyekuwa na muda wa kutazama viumbe hawa walikuwa wapo katika hatua gani za kujifunza kuogelea, kila mtu aliendelea na shughuli zake zilizompeleka pale.
Tembo alikuwa anasaka kitu kimoja tu, alitaka kujua ni wapi Maria akiguswa atalainika moja kwa moja ili aweze kumpa jibu la kwa nini akaitwa Tembo na sio Swala. Mara nyingi sana alikuwa amempapasa kifua chake na hakuna lililotokea.
Tembo akakumbuka kuwa hakuwa amemkamata kiuno chake hata mara moja. Upesi akazamisha mikono na kukikamata kiuno kisha akamgeuzia aangalie mbele kama kwamba ni kweli anahitaji kumfundisha. Alipokiminya kiuno kwa staili isiyosimulika. Maria akatowa yowe kubwa, waogeleaji waliomsikia walijua ni muoga tu wa kuogelea, wakapuuzia na kuachana naye.
Tembo akajipongeza kuwa alikuwa amegusa penyewe.
Maria hoi!! Akaanza kunena kwa kabila lake la kichaga. Tembo akifanikiwa kusikia neno moja tu “Yelewiiii”

Maria hakuwa na kikwazo chochote, kama ni matiti yake Tembo alikuwa ameyashika mara kwa mara na kiuuno tayari amekikamata sasa ilikuwa ruhusa kufanya atakavyo, aidha alete ubishi aachwe ndani ya maji ama afanye kwa kupenda halafu atoke salama. Lakini Tembo hakutumia amri hizi, Maria mwenyewe hajui ilikuwaje kile ki-Swala alichokidharau kabla hawajaingia majini sasa kilikuwa kimepita wanyama mbalimbali na kuwa Tembo. Tembo mwenye nguvu na ujanja wa kila aina, ujanja uliompa raha ambayo kamwe hajawahi kuipata katika ulimwengu wa mahusiano. Raha yenye maajabu, maajabu ya bahari kugeuka kuwa kitanda kikubwa cha kushangaza.
Lile pira jeusi lilitosha kabisa kuhimili mikikimikiki ya wawili hawa, hasahasa Tembo. Maana Maria yeye hakuwa na jipya zaidi ya kupiga mayowe ya huba mayowe ambayo yalimezwa na bahari.

Bahari ya Hindi kwa uaminifu iliitunza siri ya wawili hawa bila kumweleza hata mtu mmoja.
Siri ya kufanya uzinzi baharini!!

“Jeff huyu anaitwa Hassan, alikuwa ananifundisha kuogelea, Hassan huyu ni mchumba wangu ndo anaitwa Jeff kama ulivyosikia” Maria alimtambulisha Hassan kwa mpenzi wake bila kumtazama machoni, aibu bado ilikuwa imemtawala. Hakuamini hata kidogo kuwa alikuwa ametoka kuzini na Hassan Tembo ndani ya bahari ya Hindi!!
Tembo yeye alikuwa na furaha kubwa, hakuwa na wivu baada ya kutambulishwa na Maria. Kazi yake alikuwa ameimaliza tayari, akarejesha lile boya kwa waliomkodisha akavaa nguo zake na kutoweka.

Maria alichukulia jambo hilo kama ajali tu na kamwe halitatokea tena, lakini cha kustaajabisha hakuwa akijutia maana alikuwa amesafirishwa kwenda ulimwengu mwingine kwa dakika kadhaa, ulimwengu ambao aliufurahia sana. Jeff ambaye alikuwa mchumba wake taratibu akaanza kukosa umaana chumbani, Maria hakuwa akifikishwa pale alipopataka, kila siku alikuwa akilia na nafsi yake. Ni hapo sasa akamkumbuka Hassan Tembo na raha za kipekee alizompa wakiwa ndani ya bahari ya hindi.
Walikutana baharini, wakapeana walichopeana lakini hakukuwa na mawasiliano. Maria aliamini kama Tembo aliweza yale basi hata watu wengine wanaojishughulisha na kufundisha watu kuogelea pale Coco walikuwa na ujanja huo. Maria akajaribu bahati yake, japo yule hakuwa amejiandaa lakini mitego yake hatimaye akasafirishwa tena kwenda ulimwengu ule wa Hassan Tembo. Sasa kakawa kamchezo, kila siku za mapumziko ya mwisho wa juma alikuwa anaenda Coco kwa ajili ya burudani hiyo. Yule aliyemkuna wiki iliyopita naye akawa na tamaa za raha hiyo akajikuta anamtega mteja wake mwingine hatimaye wanafanya ya kufanya. Utumwa huu ukazidi kusambaa, waogeleaji wa kike wakazidi kuwa wengi, wafundishaji nao wakazidi kuongezeka. Maria akawa ni mwanafunzi asiyejua kuogelea kila juma, miezi ikazidi kukatika akaendelea kuwa mwanafunzi huku akiamini ni yeye pekee anayeitumia bahari kama kitanda chake cha kujipa raha.
Kumbe bahari hii ya Hindi ilikuwa inazificha siri nyingi, wahindi, waarabu, wazungu na waswahili wengi wakawa katika ajira ambayo kila mmoja aliamini alikuwa anaitendea haki peke yake. Wale watendwa hawakuambiana na hata wale watenda walifichana juu ya kamchezo haka ka kule Coco beach Dar es salaam.
Kila mmoja alitamani kukafaidi peke yake.
Laiti wangejua!!!!
Tembo alikuwa ametapakaza ajira mbaya sana Coco Beach…. Ajira kwa mamia ya waogeleaji!!
Ukiwaona utadhani wanafundishana kwreli kuogelea….kumbee!!

 ********

Rehema Hussein, akiwa katika chumba chake kimoja cha kupanga meneo ya Ubungo External alikuwa akilia na Mungu wake juu ya maisha magumu yaliyokuwa yanamkabili baada kutumia mkopo wake ‘boom’ hovyo hovyo katika starehe na mambo mengine yasiyokuwa na maana.
Kodi ya chumba alicholipia ilikuwa inakaribia kuisha, alikuwa na madeni na pale chuoni alitakiwa kujigharamia matumizi ya chakula, sasa chumba kikawa kimekauka.
Njaa ikawa inasumbua. Akawa mtu wa kushindia mkate mmoja kwa siku na siku anapokosa kabisa huenda kudowea kwa marafiki kwa mtindo wa kuzuga kuwa ameenda kuwasalimia.
Mtindo huo wakaanza kuushtukia baadhi ya marafiki, Rehema akifika ratiba za kupika zinakufa!!

Ile Club maarufu ya Lemambo iliyoko jirani kabisa na mahali alipokuwa anaishi akawa haendi tena. Pombe alizozifanya shibe kila siku akaishia kuinusa tu harufu yake. Maisha ya Rehema yakawa yamebadilika mno na mzee Hussein ambaye ni baba yake hakutaka kusikia lolote juu ya kuombwa pesa na Rehema kwani aliamini kuwa mtoto wake huyu aliyekuwa akisomea masomo ya sheria alipata bahati ya kipekee baada ya bodi ya mikopo kumpatia mkopo asilimia zote.

Mzee huyu aliyekuwa jijini Mwanza alikuwa ni kama amemsahau Rehema. Ndugu zake wachache wa jijini Dar es salaam pia walikuwa wamemchoka kwani alipokuwa hana pesa ndio alikumbuka kwenda kuwasalimia lakini mkopo ukitoka anatangaza kuwa hana ndugu Dar es salaam na hataki kusikia lolote juu ya mtu wa kujiita ndugu. Hayo matangazo aliyafanyia katika kumbi za starehe akiwa amekunywa valeur na mizinga ya Konyagi..
Sasa Rehema au ‘Rey’ alivyopenda kujiita alikuwa katika wakati mgumu zaidi kupata kutokea.
Yale maneno yake kuwa hana ndugu yakaanza kumtokea puani.

Licha ya ugumu wote huu, Rehema alikuwa ni binti aliyefunzwa nyumbani na akafunzika, hakuwa na starehe mbaya ya kupenda ngono, alikuwa na mchumba wake jijini Mwanza na alimuheshimu haswa.
Huyu alikuwa ni Rahim. Maisha ya Rahim yalikuwa ya kubangaiza na kuna wakati alikuwa anategemea Rehema apate mkopo ndipo aweze kumsaidia shilingi mbili tatu. Licha ya hayo yote alimpenda kwa dhati. Na waliahidiana kutimiza ahadi zao walizopanga wakati wakitenganishwa na umbali baada ya Rehema kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar es salaam kuendelea na masomo.

Rehema alivyokosa msaada akili yake ikazidi kufanya kazi mara tatu, sasa akafikiria kuanza kuuza vifaa vyake vya ndani. Jicho likatua katika ‘Sub woofer’ na friji. Luninga ikawa imewekwa pia kwenye orodha huku jiko la gesi likifikiriwa pia iwapo mambo yatakuwa magumu zaidi.
Kitanda chake cha kifahari akaapa kuwa kamwe hatakiuza!!
Jagi la kuchemshia maji nalo akalihesabu katika vifaa vya kuuza.
Rehema alikuwa amekamatika haswa!!
Maisha ya chuo yalikuwa yamempiga.

****

Ijumaa hii Hassan aliiandaa maalum kwa ajili ya mtu maalumu. Hakujua kwa nini alivaa mavazi yale aliyokuwa ameyavaa lakini akili ilimruhusu kuyavaa, hakuwa na nia ya kwenda msikitini kabisa. lakini alifikiria kuvaa kanzu.

Majira ya saa sita mchana aliingia ndani na kutoa kanzu yake maridadi nyeupe, kwa kuwa ilikuwa haijakunjwa bali ikiwa imetundikwa ilikuwa imenyooka sana, kibalaghashia pia kilikuwa cheupe cha kupendeza pia, miguuni alivaa viatu vya wazi yaani makubadhi.
Alipiga hatua chache kabla ya kulifikia gari lake dogo ambalo lilikuwa limepigwa rangi na kuwa kama jipya tena.
Alitembea kwa madaha yote na kuonekana kama muumini safi wa dini ya kiislamu tena anayeiheshimu sana siku ya ijumaa.
Akalitazama gari lake kisha akatabasamu.

Simu yake iliita, alikuwa ni rafiki yake wa jijini hapo. Alikuwa ni rafiki wa kitambo lakini kadri majukumu yalivyochukua nafasi yake na urafiki wao ulizidi kufifia.
Majukumu yenyewe ni ajira, ajira asiyoijua.

“Niaje kaka…”, maongezi yao yalianza baada ya salamu mbili tatu. Robert alimweleza Tembo shida yake, shida yenyewe ilikuwa shida ya pesa kwa ajili ya kununua vitu ambavyo vilikuwa vinauzwa kwa bei nyepesi sana.
“Kaka kuna demu ameuwawa huku anauza ‘Woofer hiyo kaka daaah!! Sub woofer ya maana kaka ” Robert alimweleza Tembo. Tembo kusikia neno demu, akasisimuka, hapo palikuwa ndio alipopataka sasa.
“Bei gani sasa anataka??? We naye kwa kupenda vitu used”
“Bei amenitajia lakini tutaongea naye vizuri najua atalegeza zaidi si unajua ”
“Poa basi mpange kama yupo mi nakuja huko tucheki ubora wa hivyo vitu pesa sio tatizo kabisa”
“Poa sana jembe langu!!!”

Maongezi yaliishia hapo baada ya muda Hassan akiwa anaendesha uliingia ujumbe, muuzaji alikuwepo muda wowote baada ya kutoka msikitini kuswali. Tembo akaitazama saa yake zilikuwa bado dakika chache swala ya ijumaa iweze kumalizika.

“Kumbe ndo maana nimevaa mavazi haya….safi kabisa labda asinivutie lakini akijiroga anivutie amekwisha…” Tembo alijiaminisha huku akiitupa simu katika siti ya kushoto kwake, akaendelea kuendesha akiitesa Mandela Road kuelekea Ubungo kwa Robert.

****

Mlango wa chumba cha Rehema uligongwa, akajifunga upesi upesi kanga kiunoni akauendea mlango, akauliza ni nani lakini kabla hajajibiwa akabaini sauti ya Robert akakoma kuulizia akaufungua mlango, Robert hakuwa peke yake alikuwa na kijana ambaye alionekana kuyafuata maadili ya dini ya kiislam kwa juhudi zote, mavazi ya kijana huyu yalimvutia Rehema akajikuta katika nafsi yake akijutia kitendo chake cha kutokwenda msikitini kuswali siku hiyo ya ijumaa lakini alipokumbuka chanzo cha kutokwenda msikiti kuwa ni kupungukiwa nauli alijipuuza. Kwani hata angetaka kwenda bado asingeweza

“Asalaam Aleykum” sauti yenye ukarimu ya kijana Hassan Tembo ilimjulia hali Rehema.
“Aaleykum-salaam” Alijibu kwa nidhamu ya hali ya juu kwa lafudhi nzuri ya kiswahili iliyochanganyikana na upemba na uarabu kwa mbali. Sauti hiyo ikampa ladha Fulani Tembo, akatoa tabasamu hafifu.

“Khaifa….” Tembo akaupima ujuzi wa Rehema kama alikuwa kweli ameiva kidini ama alikuwa anarashia rashia. Rehema akashindwa kujibu, Tembo akajipa majibu yake kichwani.

Robert alimtanguliza Tembo akaifikia sofa nyekundu iliyoanza kupoteza ubora wake wa awali. Laiti kama kingekuwa kipindi cha nyuma basi huenda sofa hii ingekuwa ya kuitazama mara mbili. Huenda aliinunua kwa mtu ambaye alikuwa ameanza kuichoka au alikuwa katika kununua sofa nyingine akaamua kuiuza hii.
“Roby mambo?!”
“Poa ndugu za siku kadhaa, hatuonani” Rehema hakujibu badala yake akacheka kwa kujilazimisha. Sura yake ilitangaza dhiki ya hali ya juu.
“Naona upo na mtu mkubwa sana kama shehe vile, kaka umependeza sio siri” Rehema alimsifia Hassan kupitia mazungunmzo yake na Robert.
“Huyu Mufti kabisa mbona…” Roby alikolezea kikatoka kicheko kidogo kutoka kwa Rehema, safari hii aliufumbua mdomo wake, Tembo akauona mwanya. Moyo ukamdunda sana kana kwamba ameona kitu cha kutisha ama kushangaza sana.
“Kaka unatumia kinywaji gani?” Rehema alimuhoji Tembo huku akiwa wima wima, akajibiwa kwa kichwa. Tembo hakuhitaji kinywaji.
“Jamani kaka, hata maji tu…”
Anazuga huyu hana pesa wala nini! Tembo aliwaza kisha akausimamia msimamo wake ili asije kumwaibisha Rehema.
“Mimi niletee maji yanatosha” Robert aliomba. Rehema akatoka nje, Tembo hakuona dalili ya pesa katka mikono ya Rehema.
Akaduwaa!

“Oya kaka, mzigo wenyewe ndo huo hapo sasa,..ona!” Robert alimnong’oneza Tembo. Tembo hakujibu kitu zaidi ya kuitazama subwoofer iliyoketi kipweke katika stuli ndogo yenye mguu mmoja mbovu. Ilikuwa inavutia sana, lakini kwa Tembo ilivutia zaidi, sio kuwa hakuwa na uwezo wa kununua mpya tena yenye ubora kupita ile bali aliiona kama vile ni chambo ya kumnasa Rehema. Tayari Hassan Tembo alikuwa amevutiwa na mwanya wa Rehema pamoja na ile mitikisiko aliyoishuhudia ikipenyeza kutoka katika kanga moja nyepesi.
Kabla Tembo hajajibu lolote, aliingia msichana mwingine bila kugonga mlango. Bila shaka yalikuwa ni mazoea yake kufanya hivyo!!
Au huenda alijisahau!! Nani anajua?

“Rehema yuko wapi?” Aliuliza kibabe huku akiwa amekunja ndita. Hakuna aliyemjibu bila shaka wote walikuwa wamekereka na kitendo hicho cha kuingia bila hodi pale ndani halafu mbaya zaidi hata salamu pekee hakukumbuka pia!!!

Yule binti hakuonyesha kukerwa na jambo hilo la wawili hawa kukaa kimya badala yake aliendelea kubwatuka.
“Aisee akija mwambieni Hawa kaibuka hapa…mkimwambia atajua nilifata nini…” alimaliza kutia mkwara huo akatokomea zake huku akiipa tabu ardhi kwa vishindo alivyokuwa akikanyaga. Tembo alimtazama Robert akagundua kuwa hakuwa akimtazama akahamisha macho kwenye simu yake. Kichwani akajiongeza kuwa yule Hawa alikuwa anamdai Rehema.
“Maisha ya chuo bwana!!!!!” alijisemea Tembo huku akibetua midomo yake kisha akajikuna kichwa chake kisichokuwa na nywele.

Bila kuzungumza lolote na Robert mara Rehema akaingia ndani. Alikuwa amemletea maji kopo dogo kupita yote yanayotengenezwa na kiwanda cha tajiri maarufu ambaye sura yake haifahamiki kwa watu wengi hapa nchini, Maji ya uhai. Na bei yake ilikuwa ya chini sana kupita yote, ondoa yale maji ya ‘Kandoro’ ambayo huuzwa bei chee zaidi.
“Mh!! Huku kwetu aisee maji makubwa hamna nimezunguka mpaka basi!!!” Rehema alijisemesha bila kujiamini. Robert na Tembo wote wakajilazimisha kucheka.

Anazuga tena maskini!!! Tembo aliwaza huku akiibia kumtazama Rehema, aliyekuwa amekaa mkao Fulani wa kuinama. Macho ya Tembo yakatua katika kifua chenye rangi ya dhahabu mpauko, kifua hicho kikiwa kimebeba matiti mekundu, hakuwa amevaa ‘kinyanyua matiti’ bila shaka yalikuwa yamesimama peke yake!!!!
Wacha wee!!

Kikohozi kikamkaba Tembo, ila akafanikiwa kukikabili!!! Hakukohoa.
Kama vile Rehema aliendelea kufanya mambo hayo makusudi. Sasa alikuwa amekaa vibaya. Paja lenye rangi kama ya kifua chake likachungulia nje. Ule mfanano wa rangi ulithibitisha kuwa alikuwa na ngozi ya asili hakuwa akijichubua. Akili ya Tembo haikuwa pale na wala hakumsikia Robert alivyomnong’oneza mpaka alivyorudia tena!!!!
“Kwa hiyo inakuwaje bosi!!!”
“Aaaah!!! Hebu ngoja nifike kwanza ofisini feri kuna ishu imetokea ‘then’ ntakupigia tuje kumaliza biashara” alijibu Hassan Tembo huku akiwa nusu amekaa nusu amesimama.
“Basi poa utanishtua!!!” alijibu Robert. Wakasimama wakamuaga Rehema mtoto wa Hussein, wakatokomea garini.
Walipofika garini, Tembo akaingiza mkono wake katika suruali na kurekebisha ustaarabu ulioanza kuvurugika.

Rehema aliwasindikiza kwa macho yaleyale yaliyotangaza dhiki. Laiti kama wangeweza kumsoma vizuri macho yale yalisema, “Jamani maji yenyewe pia nimekopa nilitegemea mtanipatia pesa nilipe…..na Hawa naye aaah!!”
Bahati mbaya kwake!!!!

Rehema aliufunga mlango akakimbilia kitanda chake akajirusha na kuanza kumlaani Tembo kwa kupewa taarifa kisha kuondoka bila kumaliza biashara. Wazo la kutafuta mteja mwingine likamuingia. Akaitwaa simu yake, akajaribu kupiga, yule mwanamke anayekera kwa lazima akamjibu kuwa ‘Huna kiwango cha kutosha katika simu yako tafadhali ongeza salio…….” Rehema akaikata simu na kufura kwa ghadhabu.
Njaa nayo ilikuwa inamtafuna!!!!

 Hodi ya kwanza ilikuwa na heri na ilileta tabasamu kidogo japo ilimalizikia kwenye machungu, alichokitarajia hakukipata kwa wakati. Mlango ukagongwa tena Rehema akaenda kuufungua safari hii hakuulizia chochote.

Moyo ukampasuka Rehema, alikuwa ni Hawa. Wiki mbili zimepita akiwa anachengachenga kumlipa pesa yake sasa yupo mbele yake, sura yake ikiwa imetawaliwa na shari tupu..
“Sihitaji maelezo aisee nipatie pesa yangu nadaiwa huko…yaani nilikupa kiistaarabu kunirudishia ndo tunasumbuana hivyo???” alikoroma Hawa huku akiwa ametega mkono kusubiri chochote na sio maelezo, mkono mmoja kiunoni mwingine ukiwa umetega ukingoja pesa. Rehema akakosa la kuzungumza, akajilazimisha kutabasamu. Hawa hakuwa pale kimzaha alimaanisha.

Hawa akazidi kupayuka, neno ‘nivumilie’ hakutaka kulisikia kabisa. Rehema aibu zikamtawala na kuanza kujilaani kwa starehe alizofanya kwa pupa hadi kufikia hatua ya kumaliza pesa zote.

Wakati sakata hili likiendelea mara akaongezeka mdada mwingine huyu alikuwa rafiki yake na Hawa, wote wakaanza kumsimanga Rehema. Rehema akahisi anaonewa na hana mtetezi.
Machozi yakamlengalenga huku moyo ukiwalaani Tembo na mwenzake kwa kushindwa kumpa pesa awapatie Sub woofer.
Laiti wangempa basi angeikwepa aibu hii kwa kulipa deni.

Wakati akimlaumu Mungu kwa kumpa adhabu hii ya aibu mara akatokea mtu mwingine huyu sasa alikuwa upande wa Rehema. Hakuwa akimfahamu yeyote pale bali Rehema. Huyu naye hakugonga hodi kwani mlango ulikuwa wazi!!!!!
“Karibu …….” Rehema alijitutumua akasema, kisha akawakonyeza akina Hawa ili wasiendelee kumdai kwa sekunde kadhaa ili yule mtu aliyeingia asijue lolote.
.
“Oya!!!! Hebu mwambie bwanako atulipe chetu tusepe!!!!” Hawa akarusha kombora. Kombora hili likamshinda nguvu Rehema, likapokelewa na Munyama Mkubwa, Mnyama asiyeunguruma lakini akitembea anatikisa pori. Tembo!!!!!!
Hassan Tembo kijana asiyekuwa na mbwembwe nyingi lakini anaamini kuwa hakuna kamba nzuri na imara zaidi ya pesa. Tembo akajikoholesha kidogo kisha akamsogelea Rehema, akamdaka kiuno.
“Baby!! Hebu kaa nitamalizana nao!!!” Tembo akatupa chombezo. Ikawakera akina Hawa.
Lilikuwa lengo lake!!!

“Mnadai nini labda samahani!!!! Na mnaonaje mkiongea sauti za chini kidogo, maana si mimi hata wewe umewahi kukopa. Utajisikiaje ukidaiwa kwa shari kiasi hiki?” maneno yake na kujiamini vikawakata mzuka waliokuwa wamepandisha.

“Sikia shem nilimwazima Rehema elfu hamsini yangu….hadi leo ananizingua mwezi umepita sasa, hata ungekuwa wewe ungetoa wapi uvumilivu?”
“Aaaah!! Samahani sana na poleni, ni mimi wa kulaumiwa sio Rehema naombeni mnisamehe, nilichukua pesa hiyo nikaitumia kama nauli kwenda visiwani ndo nimerejea na alikuwa hataki kuzungumza na mimi najua zilikuwa ni hasira..” Hassan Tembo akazungumza maneno ambayo hata yeye hajui aliyatolea wapi, Rehema akabaki kuduwaa.

“Mamii…..nisamehe mie…” sauti ya upole ya Tembo ikapenya katika masikio ya Rehema, ikasafiri mpaka moyoni, ikamwambia Tembo anakupigania…..Machozi yakaanza kumtoka, Hawa akawa wa kwanza kumbembeleza. Baadaye Tembo akachukua jukumu, akampakata Rehema!!!!
Wivu ukapenya na kuwasurubu akina Hawa. Mara mikono ya Tembo ikapenya na kukumbatia tumbo dogo la Rehema, bila kujua wapo katika mchezo wa kuigiza Rehema naye akajibu mapigo, akaanza kupapasa kifua cha Tembo. Tembo akacheka kimya kimya kisha akajitoa katika mikono ya Rehema akasogelea kochi alilokuwa amekaa awali. Akaitwaa ‘pochi’ yake. Hapo ndipo Rehema akatambua kwa nini Tembo amerejea, kumbe alikuwa amesahau pochi yake.
Pochi ikafunguliwa kwa kujiamini, noti ambazo hazijapita katika mikono ya watu wengi zikatolewa bila kuhesabiwa kwa umakini. Hawa akakabidhiwa akazihesabu. Zilikuwa zimezidi mara tatu. Yaani laki moja na nusu.
“Baby…si ananidai elfu hamsini tu!!!” Rehema akajikuta anamwita Tembo baby…
Ajabu!!
“Usijali na ya usumbufu!!!” alijibu Hassan Tembo kwa sauti ya gharama, sauti nzito lakini ya kuvutia.
Rehema alionekana kutopendezwa na uamuzi huo wa Tembo, labda alidhani kuwa Tembo hana pesa nyingine tena zaidi ya hizo alizotoa. Mawazo yake hayakuwa sahihi hata kidogo. Tembo alikuwa kifaa kingine!!!!!
“Mh!! Baby mbona kama hujaridhika vile mpenzi wangu!!!”
“Hamna nimeridhika…”
“Kama umeridhika kweli sogea hapa…” Rehema akasogea.
“Mbele ya rafiki zako naomba unichumu..” Tembo akamwambia Rehema huku akiwa amemtazama usoni.

Rehema akaingiwa kigugumizi, waliopo mbele yake wanajua kuwa Tembo ni mpenzi wake tena wa siku nyingi, kama hiyo haitoshi amemsaidia kulipa deni kubwa kama lile tena kwa kiwango mara tatu. sasa Tembo anataka apewe busu tena hadharani. Kama akikataa kumbusu basi ana kinyongo moyoni, jambo ambalo hakuwa tayari litokee, na kama akikubali basi amemsaliti mpenzi wake masikini wa jijini Mwanza. Rahim!!!!!

Macho ya Tembo yakatazamana na Rehema. Rehema akajaribu kukwepesha alipoyarudisha bado alikuwa anatazamwa. Hawa na mwenzake huku wivu ukiwashambulia walikuwa watazamaji. Ile pesa iliwafanya wawe mabwege, walibaki kama matahira bila kujua yale hayawahusu.

Sura ya Tembo ikauvaa upole wa Rahim wa Mwanza, kanzu aliyovaa pia ikamkumbusha Rehema uvaaji wa Rahim siku kama hiyo ya ijumaa. Japo Rahim hakuwa nadhifu kama Tembo lakini waliendana. Tembo hakuwa mrefu lakini kwa kuwa walikuwa wamekaa hilo halikuleta shida. Kosa kubwa alilofanya Rehema ni kufumba macho.

Ikajengeka taswira ya Rahim wa kweli. Akafungua midomo yake yenye njaa, Tembo akasikia maneno yakimwambia karibu. Akamvagaa Rehema, kwa dakika moja ndimi zao zikawa katika mpambano wa kufurahisha. Hawa na mwezake wakawa watazamaji, huku roho zikiwauma.
Walipomaliza Rehema akakimbilia kitandani. Hawa na mwenzake wakaaga.
Akiwa kitandani Rehema akawa anajipa matumaini kuwa ‘hata hivyo ni busu tu!! Kwani nini??’…..
Laiti kama angejua kuwa lile halikuwa busu la kawaida kama linalotoka kwa mpenzi wake wa Mwanza basi angesita kulipokea.Lakini ndio tayari alikuwa amelipokea………………………………..

amelipokea………………………………..

“Mimi natoka Rehema…..naitwa Hassan Tembo, marafiki zangu huniita Munyama Mukubwa…….” Alijitambulisha Tembo. Rehema akashukuru bila kugeuza shingo yake kumtazama Tembo.
“Sasa kuna hii hapa….” Alizungumza Tembo huku akifungua wallet yake maksudi ikapiga kelele…Rehema akasikia akageuka upesi upesi. Tembo akamtazama kwa ncha za macho, Rehema wa Hussein akushtukia tego hilo, Tembo akatumia nafasi hiyo kufanya shambulizi, noti zaidi ya kumi zenye rangi nyekundu na harufu ya kipekee zilipita katika viganja vyake kisha zikatua mezani katika mfumo wa kusambaa.
“…….Utaangalia basi chakula kidogo!!” alimalizia kauli yake Tembo kisha akatokomea bila kuaga mara nyingine. Rehema mapigo ya moyo yalikuwa juu sana.
Shambulizi alilofanya Tembo ni wasichana wachache sana wanaweza kupindua!!! Wachache sana!!

Pesa ya chakula!!!!! Alijiuliza, kama hii ni ya chakula je ya matumizi ya wiki itakuwaje sasa. Tamaa ikamkonyeza kidogo!!!
Rehema kwa kunyata kama vile akitembea upesi upesi zile pesa zitapeperuka alisogea na kuzifikia zile pesa, akataka kuzigusa akasita. Akauendea mlango na kuufunga vyema na kitasa. Akayashusha mapazia halafu akawasha taa, chumba kikawa kama usiku. Hali hiyo ikamfanya Rehema ajione kama vile yu ndotoni!!!
Hakika yale yalikuwa mauzauza. Siku iliyoonekana mbaya kupita zote sasa ilikuwa imegeuka ya kupendeza. Rehema akazikusanya zile noti, zote zilikuwa na rangi nyekundu kasoro noti moja tu ndo ilikuwa haieleweki eleweki. Alipoitazama vyema akagundua kuwa ilikuwa ndogo kuliko zote. Akaisogeza kwenye upeo wa macho yake, akaisoma kidogo akagundua ilikuwa ni ‘Business card’ hakuitilia maanani akaiweka katika moja ya viti vilivyokuwa pale ndani.
Laki moja na elfu ishirini!!!!!
Pesa hii ilikizunguka kichwa cha Rehema. Tayari alijisahaulisha shida iliyokuwa inamkabili na pia alikuwa hana wakati wa kuwaza juu aibu ambayo almanusura imkumbe na kisha kupata msaada wa aina yake kutoka kwa mtu wa aina yake. Kibaya zaidi Rehema akamsahau mtu huyo kuwa ni Hassan na alihitaji kupewa walau neno moja kuu ‘Asante’….Rehema hakuwa ametoa shukrani.
Sasa alikuwa katika ki-bar cha jirani akipata bia mbili tatu ambazo alikuwa akizinywa kwa fujo sana kwani ni siku nyingi alikuwa hajazigida. Mara akaagiza huduma kutoka jikoni. Aliyekuwa mbele yake ni muhudumu wa vinywaji. Kwa kumjali mteja wake huyu akaamua kumuita muhudumu wa jikoni, “Hassan…we Hassan!!!!” muhudumu akaita kwa sauti ya juu kidogo. Akili ya Rehema ikashtuka akakumbuka hizo pesa alizokuwa anatumia zilitoka kwa kijana aliyeitwa Hassan hakukumbuka jina la pili. Hapo hapo akakumbuka pia kuwa alikuwa hajatoa shukrani kwa yote aliyofanyiwa na Hassan. Sasa akalikumbuka na lile busu motomoto. Akakunja sura kama vile mtu aliyepatwa na kichefuchefu cha ghafla.

“Ngoja nimpigie simu..yaani namwambia asante halafu nakata simu hakuna la ziada hapa!!!” alijisemea Rehema kisha akaitoa simu yake. Akabaki anajishangaa kumpigia mtu simu wakati hana namba yake. Akataka kuifuata ‘Business card’ ya Hassan lakini ile harufu nzuri ya kuku wa kuchoma ikamshawishi kubaki. Tabia Fulani ya ulafi ikawa inamtawala na kile kimuhemuhe cha kuwa na pesa za ghafla mfukoni kikawa kinampelekesha.
Akiwa anairejesha simu yake mara ikaingia simu, alikuwa ni Robert kumbukumbu zikamjia kuwa Robert alihitaji kununua vifaa kadhaa kutoka kwake tena kwa bei poa sana. Rehema akaitazama ile simu kisha bila kuipokea akapiga mafunda mfululizo ya bia iliyokuwa mbele yake katika mfumo wa tarumbeta huku akijisahau kuwa ndani ya glasi pia alikuwa amemimina kiasi cha pombe yake. Robert aliyekuwa Lulu masaa machache yaliyopita akakosa maana tena, ile subwoofer iliyokuwa iuzwe kwa bei poa sasa haikufikiriwa kuuza. Rehema alikuwa katika starehe zake, starehe alizozilaani wakati akiwa na matatizo chungu nzima. Akaipokea simu!!!
“Roby kakangu nitakupigia nipo diskasheni” Rehema alijieleza upesi upesi kisha akakata simu. Robert akapiga tena, Rehema akaanza kuhisi kero. Akaacha kuipokea.
Ilipokatika ikaita tena safari hii aliichukua kwa jazba, akaipokea bila kuangalia mpigaji alikuwa nani.
“Jamani Ro…….”, kabla hajaendelea akakatishwa na sauti nyingine, haikuwa ya Robert.
“Mambo vipi…..”, ilikuwa sauti ngeni sana masikioni mwake. Akaitoa simu sikioni na kuitazama, ilikuwa namba mpya.
“Nani mwenzangu, samahani lakini simu yangu ilijiblock, nikawa nimerinyuu laini…..”
“Usijali usijali naitwa Tembo….”
“Temboooo….Tembo yupi??” Rehema aliuliza huku akiichukua bia yake na kuisogeza karibu na mdomo tayari kwa shambulizi.
“Hassan…..”
“Oooh!!! Jamani Kaka Hassan mambo vipi za mida”
“Poa vipi upo wapui??”
“Nipo kwangu hapa nimejipumzisha tu!!!”
“Poa napita baadaye kidogo” alisema Tembo kwa kujiamini. Rehema alitamani kukataa na nafsini mwake hakupenda Tembo arejee nyumbani kwake usiku huo. Lakini mdogo ulishindwa kutamka hadi pale Hassan alipokata simu.

Hapa akija asitegemee mtelemko, eti visenti alivyonipa nd’o atanipa kirahisi.. mimi namba nyingine aisee.
“Naitwa Tembo, rafiki zangu wananiita Munyama mkubwa nyooo…” Rehema akazungumza huku akibana pua yake.
Hatua kwa hatua akarejea nyumbani kwake kwenda kumngoja Hassan Tembo.

******

Hakuwa tena katika vazi la kanzu ila sasa alikuwa katika vazi la fulana na suruali ngumu aina ya cardet. Machoni alikuwa na miwani nyeusi, kiatu chake kilitangaza bei kwa ubora wake. Marashi makali yasiyokera yalikitawala chumba cha Rehema. Mbele yake alikuwepo Hassan Tembo. Ilikuwa tayari saa nne kasoro dakika kadhaa usiku. Ilikuwa mara ya kwanza kwa mwanaume kuwa katika chumba cha Rehema hadi muda huo wa usiku, Rehema alitamani kumwambia Tembo aondoke mdomo ukawa mzito.
Rehema hakuwa na uoga wa kuzungumza pale alipojisikia kuzungumza lakini sasa mbele ya huyu Tembo akawa na mdomo mzito.
“Rehema naweza kuungana nawe hapo kitandani….” Hassan kwa kujiamini na bila kumtazama machoni Rehema alimwambia. Rehema akashtushwa na kauli hiyo, akatamani kukataa mdomo ukawa mzito sana. Nafsi ilipinga vikali ombi hilo lakini mdomo haukusema lolote.
“no..no nooo…” akili ilisema lakini mdomo haukutoa sauti yoyote ile. Ulikuwa mzito.
Sasa Hassan alisimama kwa madaha, hatua kwa hatua akakifikia kitanda akaketi pembeni ya Rehema.
“Vipi mbona kama hujiamini au kuna mtu anakuja baadaye” Rehema akajichekesha lakini haikusaidia kuificha hofu yake.
“Najiamini.. najiamini sana na haunifanyi chochote nakuapia..” akili ilisema lakini mdomo ukawa mzito kutoa maneno haya… hivyo Tembo hakusikia lolote.

“Rehema…” Tembo aliita…..Rehema akaitika kwa kutikisa kichwa, “Asante kwa busu lako la muda ule” Tembo aliongea kwa sauti ya chini. Rehema akawa msikilizaji. Maneno ya Tembo ya kukumbushia busu alilopewa mchanaq yalimkera na kuona kama anadhalilishwa lakini hakuwa na la kufanya.
Akiwa bado hajajua nia ya Tembo ni nini mara aliusikia mkono wa Tembo ukimgusa begani, kisha ukahama kutoka bega hili ukaenda lile, Rehema akawa ameganda kama gogo. Hakuwa na ujasiri tena.
“Sitaki.. sitaki niache.. nasema niache!!” bado mdomo haukutoa sauti, haya ni maneno aliyoyawaza akilini na hayakumfikia Tembo.

Maskini Rehema hakujua lile busu limemletea madhara gani, madhara ya kuisikia akili ikisema lakini mdomo kushindwa kufunguka. Sasa tatizo hili likayazua haya.
Rehema hakuwa na kiguo chake cha juu, akawa kama zezeta, hakuelewa kama alikuwa anaota ama ni kweli yanatokea. Muda si mrefu wakawa katika mapenzi mazito. Bado Rehema akawa anajiuliza ni kweli yanatokea???
Hakuweza kuzungumza, alifuata vile Tembo alivyotaka. Akili ilikataa kabisa, lakini ajabu mdomo haukutoa ushirikian kusema hapana….
Hakuna neno la ‘ninakupenda’ lililotamkwa na Hassan Tembo hadi walipomaliza na kusinzia wakiwa wamekumbatiana. Boxer ya Tembo ilikuwa imechanganyikana na skin taiti ya Rehema na kichupi, gauni lilikuwa uvunguni huku suruali ikiwa sakafuni, hakuna aliyekuwa na nguo ya ziada.

Suala la kuwa na mdomo mzito lilikuwa moja lakini likazuka jingie. Tembo alikuwa na ujuzi maradufu zaidi ya Rahim, mpenzi wa Rehema aliyeko Mwanza. Kutokana na maisha magumu aliyoishi Rahim, pia hata uwezo wake chumbani ulikuwa chini.
Rehema alikuwa hajawahi kujaribu ladha nyingine lakini leo hii alikuwa katika ulimwengu wa Hassan Tembo, kijana machachari aliyemgalagaza Beatrice kwa mtego wa Chipsi kuku, Clara wa Mwanza kwa kumzuga na hadithi za kubuni, Tembo aliyemkanyagakanyaga Lucy Kezi bila kujali amemzidi miaka kibao, Tembo yule yule aliyegeuza bahari kuwa uwanja wa malavidavi akamchinja binti wa watu huko. Sasa Tembo alikuwa anashughulika kwa Rehema. Rehema akapagawa!!!!! Tembo mwenye afya njema alikuwa ametenda kile alichokikosa kwa Rahim Mwanza.

Alfajiri Tembo alikuwa ndani ya gari yake akirejea nyumbani kwake. Alikuwa ametimiza wajibu wake. Wajibu asiojua kwa nini anautimiza
Rehema alibaki peke yake akijilaani kwa kumsaliti Rahim wake, lakini mdomo wake haukuzungumza kitu. Huku akiamini pia hiyo ilikuwa bahati mbaya, mlolongo ukaanza, siku hii akiwa na mwanafunzi mwenzake wa kiume wakiwa nyumbani kwake, ikaanza kama utani yule kijana akamtaka Rehema, huku akiamini kuwa Rehema ana msimamo sana alifanya kama kubahatisha tu.
Maajabu!!!! Rehema hakupinga wala hakukubali. Raymond akajaribu kumsogelea, Rehema hakupinga wala hakukubali, mara akaanza kumpapasa. Bado Rehema hakupinga wala hakukubali.
“Vipi nifunge mlango??” Rehema hakujibu. Ray akajiongeza ukiona kimya ujue kakubali. Mlango ukafungwa.
Sasa tayari alikuwa kama alivyozaliwa akiwa mfano wa zezeta. Raymond akachangamkia dili.
“Baby….nitumie mpira au upo safe” Rehema alikuwa hajitambui wakati swali hilo linaulizwa. Raymond akajipa jibu ‘yupo safe huyu’ akafakamia na kuukamia mchezo. Kwani mimba kitu gani bwana?
Baada ya hapo kila mtu akawa anamtazama mwenzake. Mwisho Rehema aliaga na kuondoka.
Alipofika nyumbani kwake akaanza kujutia, lakini mdomo haukusema lolote. Ajabu kweli!!
Mvulana ni mvulana tu….Rayumond akafuata mkondo wa tabia za wanaume wengine. Akawatangazia wenzake alivyopata tunda kwa wepesi. Walimsifia huku wengine wakijiapiza kimoyomoyo kuwa watajaribu.
Kweli waliokuwa na nia ya dhati wakajaribu. Maajabu tena!!!! Wakafanikiwa.
Rehema aliyekuwa na msimamo mkali sasa hajui kusema ‘NO’. kila aliyejaribu akawa anapata. Baada ya kuridhika na majaribio sasa akapewa jina rasmi la ‘MAMA HURUMA’ na wale wasiokuwa na haya wakawa wanamwita ‘CHA WOTE!!!’. Masikini lile busu kutoka kwa Hassan Tembo likamkata kabisa msimamo wake. Busu kutoka kuzimu!!!!!

Wanaume wakapangana kwa foleni bila kujijua ni wangapi wanapita katika njia moja wajanja walitumia kinga na walio wajinga hawakutumia kinga. Ajira hii ikawatumbukiza katika mkondo wa kushindana kwa kila namna kuusaka UKIMWI. Tembo alishatimiza kazi yake na kuwaachia wafuasi wake!!!!
Uzuri ama ubaya wa Tembo, akionja mara moja harudi nyuma tena….

*****

Taarifa za juu juu zilimfikia Hassan Tembo akiwa katika mawindo yake kwenye saluni moja ya kike. Akiwa anajidai hasikii lolote linalozungumzwa huku akiwa bize na simu yake na mwanamama mfanyakazi wa pale akiendelea kuzitengeneza nywele za Tembo kama alivyotaka yeye. Stori iliyokuwepo ni kuhusu mcheza shoo maarufu jijini ambaye inasemekana alifikisha lawama kwa shoga zake kuwa mpenzi wake yuko bize sana na anashindwa kumpa vyema pendo analolihitaji yeye. Wanawake wale waliendelea kupiga stori. Tembo akawa anaburudika maana walitaja hadi mahali anapokaa yule mwanadada.
Kwa kuwa alikuwa anajulikana basi Tembo alimfahamu kwa wepesi sana. Ile stori ikamkolea akaanza kukijengea picha kile kiuno cha mwanadada yule akiwa stejini anavyozungusha, laiti kama angeanza kuwika kabla ya Ray C huenda lile jina la kiuno bila mfupa angepewa yeye.
Hassan Tembo akaanza kutamani kuijua kwa vitendo ladha ya kiuno bila mfupa. Pia akakumbuka sifa wanazopewa wacheza shoo kuwa wana habari kubwa chumbani. Tembo Hassan akamweka katika mahesabu yake Mamamia Mango!!!!
Ni huyu ndo alimuhitaji, ni huyu alikuwa na kiuno kisichokuwa na mfupa. Lini na nitampata vipi??? Tembo alijiuliza!!!!!
Hakuwa na jibu la haraka haraka. Alihitaji muda wa kufikiri!!!!
Lakini wakati wa kufikiri akashangaa yeye na akili zake. Baada ya muda mrefu wa kurukaruka na wasichana leo hii anawaza juu ya ladha ya msichana? Kulikoni!!
Huyo Mamamia na kiuno chake asichokijua ndo anakiwaza ama?
Alistaajabu lakini akajiapiza kuwa kwa hali na mali lazima amsake Mamamia!!
Laiti kama angeijua safari anayoiwaza ilivyo.. ni heri asingelisikia lile jina tena!!!

 Mamamia Mango kama jina lake lilivyokuwa maarufu jijini Dar es salaam na pande nyingine ndani ya nchi . Alizaliwa miaka ishirini na sita iliyopita na kupatiwa jina la Lulu kutoka kwa wazazi wake, alikuwa na thamani ya lulu kweli kama wazazi wake walivyompa jina hilo. Akiwa na miaka kumi tu, tayari ule urembo wake wa asili ukachomoza machoni pa watu. Hakujijua kama ni mrembo hadi baadhi ya watu walipoanza kumwita mrembo. Kitotototo aliamini kuwa ni utani. Mama yake mzazi akaona kuwa mwanaye alikuwa na thamani kupita hiyo lulu yenyewe, taratibu akaanza kumwita mtoto wa mama, baadaye bwana mmoja aliyejifanya mjuaji sana akamtonya mama yake Lulu kuwa mtoto wa mama kwa ki italiano anaitwa mamamia, mama Lulu akapuuza lakini yule bwana mara moja akaanza kumwita Lulu: mamamia, jina hili likaanza kunoga hatimaye Lulu likasahaulika akawa anaitwa Mamamia. Yeye binafsi alilipenda.

Kasoro moja tu, Mamamia hakuwa mwelevu darasani hivyo alijikuta mara kwa mara akifeli masomo yake. Hali duni ya wazazi wake ikamsukumia katika kucheza ngoma za kiasili, kiuno chake kilizimudu haswa ngoma hizo. Baadaye kiuno kile kikahitaji mambo ya kisasa zaidi. Bendi ya Twanga pepeta ya jijini Dar es salaam ilipohitaji madensa wapya ilifanya shindano dogo katika ukumbi maarufu na wa muda mrefu wa Mango Garden maeneo ya Kinondoni.
Mamamia alikuwa mmoja kati ya washiriki katika mashindano haya. Hakuwa na kipingamizi chochote alishinda kwa kura nyingi sana. Akawa Mamamia wa Mango Garden, baadaye akafupishwa kuwa Mamamia Mango, likavuma sana hatimaye likawa jina lake. Wale waliomjulia ukubwani wakisikia unamuita Lulu wanadhani umekosea. Jina hilo lilisahaulika kabisa!!

Mamamia akaweka heshima mbele. Alikuwa mgumu sana kuukabidhi moyo wake kwa mwanaume lakini hatimaye akanasa kwa mtengenezaji wa muziki, aliyeitwa Romeo, urembo wa Mamamia haukuwa tiba tosha kwa Romeo aliyezoea kujibadilishia wanawake kila anapowachoka. Mamamia alivumilia kwa kila hali alimpenda Romeo kwa jinsi alivyoweza. Hakuitaka orodha ya wanaume wengi katika maisha yake ya usichana.
Ni hapa mnyama mwenye nguvu za ajabu. Hassan Tembo alikuwa amepatamani. Swali likabakia anaingia vipi??

****

Ukumbi wa Mango Garden uliopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam ulikuwa umesheheni watu kadha wa kadha waliofika pale kwa nia ya kujipatia vinywaji na kutazama burudani kutoka kwa wakali wa muziki wa dansi.
Katika meza ndogo iliyotosheleza watu wawili alikuwepo kijana ambaye alifika mapema kuliko wateja wengine, meza yake ilikuwa imebeba chupa tupu tatu za bia aina ya ‘castle lite’…… hapakuwa na dalili ya kumsubiri mtu. Alikuwa ameridhika sana na kuwa peke yake.

Majira ya saa nne usiku umati ulikuwa mkubwa na kila mtu alikuwa katika pilika pilika zake huku na kule. Bendi ya Twanga pepeta ilikuwa imejikita katika kutoa burudani. Sasa macho ya kijana huyu yalikuwa yapo makini kabisa yakilitazama jukwaa, kuna kitu alihitaji kukiona lakini hakukiona. Akahama kutoka alipokuwa akasogea karibu zaidi, bado hakuonekana kuridhika. Baadaye akawa kama aliyekata tamaa lakini kelele za ghafla kutoka kwa wateja waliofika pale zilimgutusha akageuka nyuma. Macho yake yakampa jibu la kwamba hizo kelele zimesababishwa na nini. Mbele yake kilionekana kiwiliwili kikijiviringisha huku na kule katika namna ya kipekee, kiwiliwili kile kilikuwa kimejigeuzia nyuma na kuwaachia wateja wajionee mgongo na makalio yanavyotikisika kiufundi. Na hicho ndio kikubwa wateja walipendelea. Huyu alikuwa ni Mamamia Mango akijishughulisha jukwaani. Tembo akatahamaki, alikuwa hajawahi kuonana na Mamamia ana kwa ana. Moyo ukapiga kwa mshindo mkubwa. Akakaa kwenye kiti. Akajitokeza mteja mmoja kwenda kumtuza Mamamia, Tembo naye akaunga tela. Alipofika pale nia yake ilikuwa kumtumbukizia Mamamia pesa kwenye matiti yake ili aweze kumpakaza miujiza yake.
Alipomfikia Mamamia ilikuwa ni aibu ya mwezi, hakuwa na pesa hata kidogo. Kumbe katika kushangaa wajanja wa mjini walikwishajichukulia vilivyo vyao. Tembo akapatwa na mshituko.
Walinzi wakawahi wakamtoa walijua ni mlevi!!!!

Taharuki iliyomkumba Tembo ikamfanya atoweke eneo lile akafika nje na kupiga simu kwa rafiki zake waweze kumpatia pesa, bahati nzuri walikuwa na pesa lakini pesa hizi zilikuwa katika mfumo wa Tigo pesa na Mpesa. Haraka haraka wakamtumia, sasa sita hii Mpesa na Tigo pesa wapi na wapi??? Tembo ambaye hakuja na gari siku hiyo kwa simanzi kubwa akaondoka kwa miguu kurejea nyumbani. Mbagala!!!

Kila hatua aliyotembea alijikuta akihamishia hasira zaidi kwa Mamamia kama ni yeye aliyemtuma kuja hapo Mango Gardern.
Kinondoni Studio, Mkwajuni, Morocco hoteli, Magomeni, Kigogo, Msimbazi, Ilala, Veta, Keko, Taifa, Uhasibu, Sabasaba, Kwa Azizi Ally, Mtongani, Mission, Sabasaba ya pili, Kipati hapa ndo akapata lifti ya kumalizia safari yake.
Alifika hoi sana. Hakupata hata muda wa kuingia bafuni akajitupa kitandani akalala.
Hasira ikiwa imemtawala

Kesho yake alizinduka majira ya saa sita mchana. Karaha ya siku iliyofuata ilikuwa haijaisha. Mamamia Mango, jina hilo likakiteka kichwa chake. Akaingia bafuni kuoga. Alipotoka akawasha gari lake, safari ya kwenda Kinondoni!!!!!
Hakuwa na uhakika ni wapi hasa anaelekea na ni nini hasa atamwambia Mamamia lakini alichoamini kuwa lazima aonane na Mamamia.
Hapakuwa na foleni sana hivyo alifika kwa wakati ambao aliufurahia. Saa kumi alasiri mida ambayo wapenzi wengi hupenda kukutana. Ilikuwa ni siku ya mapumziko.
Tembo akaanza kuichora ramani ya wapi nyumbani kwa Mamamia. Alipoona haichoreki akaamua kuulizia, haikumchukua watu watatu kuweza kuliona geti la nyumba iliyosemekana kuwa ni makazi ya Mamamia.
“Naenda kumwambia nini sasa???” alijiuliza Tembo. Kwa mara ya kwanza akajihisi uoga kumvaa msichana.
Akastaajabu!!

Akapiga moyo konde akaisogeza gari taratibu akapiga honi getini. Baada ya muda akatoka ndani msichana, kiumbile alirandana na Mamamia lakini tatizo moja tu hakuwa na kiuno kisichokuwa na mfupa.
“Samahani kaka….unamuhitaji nani??” aliuliza Yule dada baada ya kumjulia hali Tembo.
“Mamamia….sijui yupo”
“Una ahadi naye??” aliulizwa.
Aaaah!!! Washaanza uzungu wao!!!! Tembo Hassan alilalamika kimoyomoyo.
“Hapana kwa kweli ila nahitaji sana kumwona!!!! Mimi ni shabiki wake namba moja” alijibu Tembo.
“Mh!! Hebu ngoja nimuulize…nimwambie nani??”
“Hassani!!”
Yule binti akaitwaa simu yake akabonyeza namba kadhaa.
“Dada kuna mgeni wako anaitwa Hassani”
“……..Hapana….haya….” alimaliza mazungumzo.
“Msubiri anakuja….”
Tembo akakubali kwa kutikisa kichwa Yule binti akaingia ndani kisha akalifunga geti akimwacha Hassan nje. Kitendo hicho kikamkera Hassan akahisi amedhalilishwa.
Alisubiri dakika kumi mara zikawa ishirini na hatimaye nusu saa….hasira zikaanza kujiunda kooni. Akachukizwa na dharau hiyo. Akataka kupiga honi tena, akajikuta katika kusita akaacha. Akashuka kutoka ndani ya gari yake. Akaliendea geti ili aweze kuingia ndani na kuulizia kulikoni.

Ile anataka kugonga hodi akakatishwa na geti kufunguliwa, alikuwa ni yule yule aliyelifunga awali.
“Amesema samahani anakuja sasa hivi” alimaliza kutoa taarifa na kufunga tena geti. Hakumkaribisha Tembo ndani. Tembo akajiuliza kulikoni, hakupata majibu. Kitendo cha Mamamia kutuma maombi ya samahani kidogo kikamfariji Tembo. Akarejea ndani ya gari akaketi, akauacha mlango wazi akazima kiyoyozi.

Hatimaye geti kubwa lilifunguliwa. Tembo akadhani ilikuwa ni zamu yake kukaribishwa na kuliingiza gari lake ndani. Akazama garini akajiweka sawa kwa ajili ya kuendesha, tofauti na mawazo yake mara akasikia honi, ilikuwa inatoka gari nyingine. Gari mfano wa mpya, aina ya Grand Vitara.
“Kama ni ya kwake amenipiga bao la kwanza!!!” Tembo alijisemea. Na baada ya muda akalipata jibu la uhakika. Kioo kiliposhushwa kikachomoza kichwa cha mwanadada ambaye hakuwa Yule anayekata viuno mbele ya umati, huyu alikuwa Mamamia mwingine.

Tembo akataharuki. Kisha akajaribu kujiweka sawa. Mamamia akamwita Tembo, kwa ishara ya vidole viwili, Tembo akatii. Akasogea hadi karibu na gari aliyokuwa anaendesha Mamamia.
“Nisamehe kwa kukuweka sana…..”
“Aaaah!! Usijali dadangu”
“Naitwa Lulu….niseme Mamamia huenda ndio utanielewa vyema, sijui mwenzangu”
“Hassan….Munya…..aaah!! niite Hassan” Tembo akaogopa kuweka mbwembwe, nidhamu ya uoga mbele ya Mamamia ikawa inamshambulia bila kutarajia.
“Ehe!! Nambie…” Mamamia akamwachia uwanja Tembo ajieleze.
“Nilikuwa na maongezi na wewe”
“Ndo hapa sasa nipo zungumza…” alijibu Mamamia. Bila kushuka garini.
“Mamamia nahitaji kuzungumza kirefu na wewe.” Alijiumauma Tembo.
“Hebu sema kwa kifupi halafu kama yana maana nitakuambia unieleze kwa kirefu.” Mamamia akajibu huku akiiweka miwani yake vyema machoni pake.
“Aaaah!! Mamamia bana….haya…..”, alijichekesha kimtindo kisha akaendelea. “Mamamia ni masuala Fulani kuhusu mahusiano”
“We ni mwandishi wa habari????” Mamamia hakushtushwa na kauli ya Tembo juu ya mahusiano. Badala yake akazua mengine.
“Hapana sio mwandishi kwani vipi….”
“Nilijua unaandaa makala kuhusu mahusiano….” Mamamia akatoa kijembe. Kikamkera Tembo akajichekesha huku akiumia moyoni.
“Na pia kama ungekuwa mwandishi huu mzigo wa mahusiano wangekuwa wamekuonea, mbona we kadogo hivyo?” Mamamia alizungumza hayo huku chembechembe za dharau zikichomoza.
Kadogo!!!!!!! Amenidharau @Q#$4%….Tembo akamtukania Mamamia mama yake kimya kimya.
“Ehe!! Au sijaelewa mahusiano kivipi??”
“Nahitaji kuzungumza na wewe Mamamia…ni maongezi kuhusu mimi na wewe”
“Na hapa tuko mimi na wewe, Hassan!!!” Alisisitiza.
Tembo akakosa la kujitetea, akaamua kuachana na mada hiyo.
“Basi tutaonana siku nyingine Mamamia…ila nakupenda”
“Asante karibu home!!!” neno la mwisho halikusikika vizuri, gari ilikuwa mita kadhaa ikiondoka.

Tembo akatazama kushoto na kulia kuangalia kama kuna mtu alikuwa anawatazama. Aibu kama zingekuwa zinapimwa kwa mzani, hii ya leo ilikuwa haipimiki, isitoshe Tembo alikuwa anajiamini sana. Kushindwa huku kukamfadhaisha.
Tembo akiwa katika bumbuwazi, mara geti likafunguliwa.
Akashtuka!!!! Kutazama akatoka yule binti ambaye ndiye alimkaribisha.
“Ahh!! Kaka umeonana naye eeeh!!”
“Yeah!! Nimeonana naye alikuwa na haraka huyo, lakini tumeelewana” alidanganya Tembo.
“Mh!! Yukogo bize huyo we acha tu!!!” aliongezea yule mwanadada.
“Haya mi ngoja niondoke tutaonana siku nyingine.”
“Thamahani kaka, unapitia njia ipi…”
“Vipi na wewe unatoka, naweza kukusindikiza sina haraka”
“Naelekea Mlimani City hapo….magari ya kwenda Ubungo taabu kweli”
“Kama umeshajiandaa twende zetu”
“Mi nipo tayari”
Tembo akashuka garini akamfungulia mlango yule binti, akaingia kwa madaha akakaa siti ya mbele.
Kinguo chake kilichokuwa kimevuka magoti kidogo kikavuka zaidi na kuacha mapaja yake meupe kwa nje.
Tembo akachungulia kidogo!!!
Safari ikaanza.
“Mimi nilikwambia naitwa Hassan, na wewe je?”
“Mimi??” aliuliza kama vile ndani ya gari wapo sita.
“Naitwa Brenda Brendson shothti dhangu wananiita BreBre…”
“Kwa hiyo mi nikiita yote nakosea…”
“Aje?”
“Brenda BreBre” Tembo akatamka kiufasaha, jina lile likampendeza Brenda na yeye akalitamka huku akiliwekea nakshi za kimjini mjini, “Brenda BreBre” kisha akacheka kizungu huku akijiziba mdomo, Tembo akawa makini kwenye kioo cha ndani akimtazama.
“Hathani jamani nimelipenda hilo jina!” Brenda akamwambia Hassan. Tembo akasikia kitu akaanza kujiuliza ni nini hicho, mara akatanabai kuwa ni KITHEMBE!!!!!
Brenda alikuwa na kithembe, badala ya kusema Hassan maskini Brenda anaita Hathani. Hali hiyo haikumkera Tembo akafurahia na kujikuta akianza kumsahau Mamamia. Mwili ukamsisimika, akaanza kufikiria kumtoa Brenda kafara ya Mamamia, yaani ajichinjie Brenda kupunguza machungu ya kuaibishwa na Mamamia.
Halmashauri ya kichwa chake ikapitisha uamuzi huo.

ITAENDELEA

SIMULIZI Ajira Toka Kuzimu Episode 02

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment