SIMULIZI Ajira Toka Kuzimu Episode 04
IMEANDIKWA NA : GEORGE IRON MOSENYA
*********************************************************************************
Simulizi : Ajira Kutoka Kuzimu
Sehemu Ya Nne (4)
TEMBO hakujua kama anaishi kwa kanuni, kanuni ambazo hazikuandikwa mahali zaidi ya ndoto ile ya siku ya kwanza kuingia katika ulimwengu huu wa mauzauza. Tembo alikuwa anajiuliza sana ni kwanini akishafanya zinaa na msichana mmoja hataki wala hajisikii tena kufanya naye kwa mara nyingine.
Hakujua kama hiyo nd’o ajira!!
Lakini kwa Mamamia ilikuwa tofauti, usiku ule ulikuwa wa maajabu sana…. Akautamani ujitokeze tena.
Clara, Lucy Kezi, Maria, Rehema, Brenda na wengineo wengi hakuwahi kuwaza kuzini nao tena….. lakini ladha ya Mamamia akaitamani tena.
Baada ya juma moja akaamua kumtafuta….
Wakapanga kukutana nyumba za kulala wageni!!
Mamamia akakubaliana na Tembo, wakati huo wakiitana ‘mpenzi’.
“Yaani ikiwezekana mi namuoa huyuhuyu kwani nini….” Tembo alijisemea siku hiyo. Na akatarajia kusema na Mamamia juu ya jambo hilo la ndoa.
Laiti kama angejua!!!
***
Hali ya hewa ilikuwa tulivu kmaiwavyosiku zote isiponyesha mvua jijini Dar es salaam. Hasahasa siku za mapumziko.
Gari dogo aina ya vits lilikuwa likatiza mitaa ya Mwenge huku gari jingine aina ya Gx 100 likivinjari mitaa ya Temeke kwa Azizi ally.
Magari yote mawili yalikuwa yanaelekea Kijitonyama. Hoteli yenye hadhi ya juu kiasi Fulani jijini Dar es salaam nd’o yalikuwa makutano ya gari hizi mbili.
Lakini chumba kilichokwenda kwa jina la Paris katika hoteli hiyo ndo alikuwa makutaniko ya miili miwili.
Mamamia Mango na Munyama Mukubwa Tembo.
Wawili hawa walizungumza kwenye simu kabla kila mmoja akaelezea namna alivyomkumbuka mwenzake na hatimaye wakaamua kukutana ili wafurahishane tena.
Majira ya saa kumi na mbili jioni, walikuwa nje ya hoteli ile wakipata mlo wa jioni, Tembo ambaye alikuwa amejaza pweza za kutosha tumboni alishushia na mchemsho wa samaki wakati Mamamia alijipigilia mchemsho safi wa kuku.
Kisha wakatelemshia chakula chao na mvinyo wa zabibu ya Dodoma!!
Naam ila mmoja akafurahi yeye na nafsi yake kutokana na chakula kile ambacho hautakosea ukiita mlo kamili.
Saa mbili usiku walikuwa chumbani!!
Tembo ambaye kama kawaida huwa hana papara alimtuliza Mamamia kabla hajaanza manjonjo yake.
“Mamamia….. nahitaji penzi letu lisiishie hewani kama wengine waliopita….” Kwa sauti nzito ya kiume Tembo alikoroma.
“Unamaana gani kwani?” alihoji yule binti ambaye kuanzia juu hadi chini jinsi alivyovalia halikuwepo la kumkosoa. Aliyapanga mavazi vyema na mwili nao ukayapokea.
“Namaanisha kuwa…. Nataka tuoane Mamamia… nayasema haya kutoka katika nafsi yangu.nitakuwa na amani sana hili likiwa kweli….” Alijieleza Tembo huku akiwa ameinama. Mamamia alijikuta anafungua kinywa chake asijue lolote la kujibu. Akataka kusema neno lakini akakwama.
Tembo akabaki kusikiliza mtazamo wa Mamamia…..
“Mbona mapema sana Hasan.. mapema sana yaani dah!!”
“Unaishi kwako Mamamia nami naishi kwangu ni kiasi cha kubadili makazi tu we uhamie nyumbani kwangu…. Nani wa kukuzuia.. Brenda mkubwa yule sio mtoto mdogo… Mia.. please!!” alisihi Tembo. Sauti ikapenya na kumvuruga Mamamia. Akakosa msimamo thabiti, akaangukia kifuani mwa Tembo…..
Hapakuwa na haja ya kumalizia jibu nd’o lilikuwa lile kuwa na yeye Mia alikuwa tayari.
Wakataka kupongezana… pongezi kwa kufanya ngono!!
Hii ni kuanzisha vyema mahusiano yao……
Kama kawaida yake Mamamia kaanza makeke yake, hii ilikuwa zaidi ya siku ya kwanza.
Safari hii alijipanga zaidi!!!
Kipande cha ndimu, udi na madikodiko mengine.
Tembo akaingoja huduma ile ya maajabu, baada ya kuoga pamoja akalazwa chali binti akaanza uchawi wake wa kitandani. Mara amguse Tembo huku mara amguse kule. Miili ikigusana joto la aina yake linaleta msisimko.
HOFU!!
MAANDALIZI haya yalikuwa yanafurahisha awali, Mamamia alikuwa akimng’ata Tembo kichokozi na wakati mwingine zile kucha zikamtomasa huku na kule mwili wa Tembo ukapata burudani ya aina yake, burudani iliyomfanya kutangaza ndoa mapema.
Maandalizi haya yakabadilika ladha, Mamamia akaanza kung’ata kwa nguvu, Tembo aka anaumia lakini anajikaza akihisi ni bahati mbaya, mara akawa anafinywa kwa nguvu tena makucha yakawa yanampa suluba.
Hapa napo akajikaza lakini akijiuliza kulikoni hali inakuwa vile.
Mara Mamamia akaacha kufinya Tembo akapata unafuu, lakini likatokea jingine la kustaajabisha. Kile kipande cha ndimu ambacho Tembo alingoja kuijua kazi yake kikaminywa kwa fujo.
Tembo hakujua ni kitu gani kinaendelea mpaka pale alipofumbua macho na kuruhusu yale maji ya ndimu kumwingia machoni.
Hapa haukuwepo uvumilivu tena, Tembo akapiga mayowe makubwa sana. Akajirusha upande upande asijue ni wapi atakapotua.
Akajibamiza ukutani!!
Akayapikicha macho yake huku akimzuia Mamamia ambaye alikuwa akihaha huku na kule ili aweze kuminya maji zaidi machoni mwa Tembo.
Hatimaye jicho moja likafanikiwa kuona mbele!!! Mamamia alikuwa amevaa chupi yake aina ya bikini shingoni huku mkononi akiwa na kipande cha ndimu. Sura yake ilikuwa imetaharuki sana!!
“Mamamia… umekuwa…” kabla tembo hajamalizia kauli hii alishangaa kumwona Mamamia akiruka kando na kisha akaanza kuipekua suruali ya Tembo.
Humo akatoka na simu ya Hasan aina ya Samsung Gallaxy S4……. Wacha wee!! Tembo akajaribu kumzuia Mamamia asifanye lolote na ile simu. Lakini alikuwa amechelewa Mamamia akairusha simu ile kupitia dirishani.
Kutoka ghorofa ya tano waliyokuwepo hadi kufika chini. Simu ikasafiri kwenda kukutana na ardhi.
“R.I.P my Phone…..” Tembo akajisemea kwa sauti ya chini.
“Mamamia matani mengine ujue sii mazuri…” sasa akajaribu kumkoromea Mamamia. Akategemea yule binti ataingiwa hofu lakini alijidanganya.
Hapohapo Mia akajirusha na makucha yake yakamparua kifuani Tembo aliyewahi kumkwepa.
Sasa hofu ikamwingia Tembo, jeuri yake ikaishia pale pale ambapo Mia alichukua suruali yake pamoja na shati. Akamshtua Tembo kama anamfuata vile… Tembo akakimbia uchi mle chumbani huku ule mkia wake uliokuwa wima wakati Mamamia akimlamba huku na kule ukiwa umelala chali.
Mia akaingia bafuni, Tembo alipopata ujasiri wa kumfuata alikuta nguo zake zikiwa katika tundu la choo!! Mamamia alikuwa anacheka sasa!!
“We Mamamia wewe….ujue sina nguo za kubadili” Tembo akaita, badala ya kujibiwa akapondwa na sabuni iliyokuwa mikononi mwa Mamamia. Akapiga mayowe huku akitoka nje!!! Mamamia hakumfuata… aliendelea kufanya mambo asiyojua kwanini anayafanya.
Tembo akahofia hali ile na kugundua kuna jambo ambalo haliendi sawa!!
Akachukua taulo akajifunga kiunoni!! Pekupeku akatoka nje huku akijiapiza kuwa akifika nje atatafuta namna ya kutoweka moja kwa moja.
Hatua mbili baada ya kuuacha mlango akakumbuka kuwa ndani ya mifuko ya suruali yake ndiyo kuna kadi ya benki na pesa zake nyingine, ataondoka vipi bila kuwa na pesa???? Hilo lilikuwa swali gumu sana ambalo jibu lake lilikuwa moja tu!! Kurudi ndani ya kile chumba cha Mamamia wa maajabu!!.
Upesi akarejea chumbani akipishana na mteja mwingine wa kike aliyebaki katika mshangao kwa hali aliyokuwa nayo Tembo.
Akanyata hadi mlango wa bafu, uoga ukaanza kumtawala baada ya kukuta bafuni hakuna mtu na zile nguo zake hazipo katika tundu la choo.
“Mamamia…. We mamamia….” Akaita kwa sauti ya chini.. lakini hakujibiwa. Akaangaza pande zote za chumba asione kitu chochote!!
Akaingia tena bafuni mzimamzima!! Mwili mzima ukiwa unatetemeka
Mara akasikia mchakato nyuma ya mlango wa bafu!! Ile anageuka ghafla akanaswa shingo yake akafurukuta lakini haikusaidia kitu, harufu ya mkojo ikamfanya ajaribu kutazama.
Ilikuwa suruali yake iliyokuwa imemkaba. Haikumkaba kimasihara. Ilikuwa inamnyonga kweli. Akajaribu kupiga makelele na kujirusha huku na kule bado hakuweza kuchomoka katika ile suruali.
Hatimaye akaachiwa ghafla akatua chini!!
Akakohoa sana kabla ya kugeuka na kutanabai kuwa Mamamia aikuwa amevaa lile shati alilolitoa katika mikojo na alikuwa anatabasamu.
“Ametoa wapi hizi nguvu huyu dada……” alijiuliza Tembo huku taulo ikiwa imemtoka kiunoni. Yeye na mkia wake wote walilalia marumaru ya bafu lile.
“Nisamehe…nisamehe Mamamia…” kwa uoga Tembo akajikuta akiomba msamaha bila kujua ni kwa kosa gani alilolifanya. Mamamia hakujibu kitu badala yake alimsogelea Tembo, kisha akamruka na kwenda zake chumbani.
Tembo akaipekua upesi na kwa tahadhari kubwa ile suruali. Akitegemea kuambulia walau kadi na pesa zake lakini haikuwa vile akaishia kukutana na maji maji tu ya chooni.
Zimeenda wapi sasa!!! Akajiuliza… mara akamsikia Mamamia anacheka peke yake. Tembo akaitupa mbali ile suruali kwa uoga. Akangonja labda Mamamia atatokea kule ndani lakini kimya kikatanda hakuna aliyetokea.
Tembo akanyata na kuifikia tena suruali yake, akaweka kinyaa kando. Akaingiza mikono kila pande lakini hakuna kitu!!!
“Au huyu mwendawazimu amechukua… eeh Mungu nisaidie mimi…” Tembo akakumbuka kumwomba Mungu…. Na hapohapo akaendelea kuhaha akitafuta kadi ya benki na pesa zake.
Jitihada hazikuzaa matunda hakupata hata kitu kimoja!!
Akaokota taulo ambalo lilikuwa limelowana, akajifunga tena kiunoni. Akanyata hadi chumbani, akamkuta Mamamia akiwa amelala hoi kitandani. Tembo hakutaka kupoteza nafasi zaidi, alikuwa anamuhofia Mamamia na kile kiuno bila mfupa alichokuwa akikiwaza hakikuwa na maana tena…. Huku akiwa anatembelea vidole vya mbele kwa kunyata. Aliufikia mlango akaufungua na kutoka mkuku taulo kiunoni.
Mojamoja kwa moja hadi mpokezi kwa fujo zote akamkuta yule dada ambaye aliwapokea. Ile kukutanisha naye macho akakumbuka kuwa kuna pesa kadhaa waliziacha pale mapokezi.
“:Nipatie ile elfu nane dada…. Tafadhali naomba..”
Dada wa mapokezi alijikuta akimpatia pesa Tembo bila kuuliza chochote, lakini zaidi alikuwa anamshangaa nini kimemsibu hadi anatoka na taulo pekee kutokea ghorofa ya tano hadi mapokezi.
Muhudumu akadhani Tembo atarejea chumbani kwake, lakini haikuwa hivyo. Akaufungua mlango wa kutoka nje akatimua mbio vilevile na taulo lake kiunoni.
Bahati ikawa upande wake akakutana na dereva wa bajaji, Upesi akajirusha ndani ya bajaji. Mwendesha Bajaji akapiga yowe la hofu lakini Tembo akamtoa hofu kwa kumkabidhi pesa yote aliyokuwanayo mkononi..
“Nipeleke Kinondoni kaka… Kinondoni kwa Manyanya pale…..” huku akiwa ametaharuki alimwelekeza dereva.
“Kaka nini tena kwani…. Fumanizi ama……” dereva alihoji.
“Umenifumania wewe ama… hebu acha dharau kijana acha kabisa dharau nasema….” Tembo alikaripia. Dereva akawa mpole.
Akaondoa bajaji upesi!!
****
SALUM Mohamed nd’o aliyeibeba aibu ya Hassan Tembo ya siku hiyo. Tembo hakusema lolote lililotokea aliomba kupumzika kwanza hadi ifike asubuhi ndo anaweza kusema lolote. Salum akamuhifadhi kwa siri kubwa kama Tembo alivyohitaji.
KWELI asubuhi ikafika lakini ule muda wa kuelezana palikuwa na habari nyingine nzito zaidi. Habari iliyomvuruga Salum zaidi kabla hajamshirikisha Tembo. Salum alikuwa haeleweki eleweki, alikuwa amevurugwa haswa na Tembo hakujua kulikoni, na hata alipotulia na kumweleza Tembo vizuri, ikawa zamu ya Tembo kupagawa maradufu!!!
Lakini baada ya kumshirikisha Tembo akachanganyikiwa zaidi.
“Salum.. nipatie nguo zako kaka nijikongoje Mbagala geto aisee….” Tembo alimsihi Salum ambaye akili yake bado ilikuwa haijakaa sawa.
Tembo akajiongeza akaingia chumbani na kuchukua nguo za Salum.
Kituko kingine. Nguo zikamzidi mwili!!!
Akazivaa hivyohivyo!! Akakutana na shilingi elfu kumi mezani akaitwaa!!!
Akaondoka bila kuaga akimwacha Salum akiwa amevurugwa na taarifa aliyoipokea asubuhi hiyo kuwa Mamamia amerukwa akili na ametoka nyumba ya kulala wageni akiwa uchi wa mnyama. Mwanaume aliyekuwanaye hajulikani ni nani?
Salum alikuwa amemtaka kimapenzi Mamamia kwa muda mrefu sana bila mafanikio lakini aliposikia ameachana na aliyekuwa mpenzi wake akaamua kuanza upya mashambulizi.
Sasa anaambiwa Mamamia amekuwa kichaa!!!
***
Taarifa za Mamamia kupata wazimu hazikuyafikia masikio ya Brenda kwa upesi.
Hii ni baada ya kuwa na usiku mgumu kupita yote aliyowahi kuwanayo. Alihangaika kuutafuta usingizi kwa masaa kadhaa bila mafanikio. Alijaribu kulala kwenye sofa akajaribu kulala katika zulia bado hali ilikuwa ileile.
Hakujisumbua kujiuliza mara mbilimbili nini kilikuwa chanzo cha yote haya. Alijua hakika kuwa ni wivu ulikuwa unamsumbua, wivu dhidi ya dada yake mpenzi.
Naam!! Aliamini kuwa ukimya wake unasababishwa na penzi zito analolipata kwa munyama mukubwa kamba fedha Hassan Tembo.
Majira ya saa tatu usiku alijaribu kupiga simu ya Mamamia, ikaita pasi na majibu, akajaribu kupiga simu ya Tembo ili kujihakikishia hii nayo haikuwa inapatikana.
Brenda kashindwa kuyazuia machozi yake!
Alikuwa analilia penzi la Tembo.
Kilio cha Brenda kilikosa maana pale alipokosa mtu wa kumbembeleza akaamua kuyafuta machozi na kuyakodoa macho yake kwenye kioo kikubwa kilichokuwa pale sebuleni, akajitazama vyema jinsi macho yake yalivyokuwa mekundu. Kisha akachukua kiti akakiweka jirani na ukuta akapanda na kubandua picha iliyokuwa ukutani. Halafu akarejea katika kioo.
Akaielekeza picha ile katika kioo na kuanza kujifananisha.
“Hata hanidhidi kwa lolote huyu…” Brenda akajisemea huku akijilinganisha yeye na ile picha ya dada yake ambaye hakuwepo wakati huo,.
“Yaani Tembo na ujanja wake wote ameona huyu nd’o mdhuri kushinda mimi ama…” akazidi kujiuliza. Kisha kwa hasira akaitupa chinbi ile picha.
Brenda akajiona mjinga kuendelea kubishana na picha, akachukua simu yake akatafuta namba aliyoifahamu yeye akabofya na kulipata jina alilokuwa anahitaji.
Akaipiga ile namba!
Alikuwa ni rafiki yake.
Wakazungumza kwa kirefu Brenda akazieleza hisia zake waziwazi juu ya Tembo akasema sana kwa huzuni.
“Kwa hiyo unataka tumfanye kama Lameck….” Rafiki yake Brenda alimuuliza Brenda. Kwa sekunde kadhaa Brenda akafikiria juu ya Lameck na kisha akakubaliana na rafiki yule.
“Asubuhi na mapema tukutane si unajua anavyokuwa na foleni ndefu yule…”
Brenda akakubali na kisha akakata simu!!
Sasa hakuwa anamuwaza Mamamia tena na kumwonea wivu, badala yake alikuwa akiwaza jinsi Tembo atakavyogeuzwa kuwa kama Lameck.
Lameck ni shemeji yake ambaye hana la kusema wala hawezi kukohoa lolote mbele ya rafiki yake huyo aliyempigia simu. Alipomuuliza siri ya mafanikio akamweleza kuwa watu kama hao lazima watengenezwe kwa wataalamu.
Sasa anataka kumtengeneza Tembo na yeye asiwe na la kusema wala kukohoa mbele yake.
“Yaani akishatengenedhwa thatha, nikitaka kwenda Mlimani thity namwambia ananipeleka mara moja, nikitaka kwenda kwake naenda muda ninaotaka, nikitaka aje kunichukua napiga thimu anakuja…. Mamamia atanunajeee!!” Brenda alijipa moyo huku akirusharusha miguu na mikono huku na kule, hatimaye akasinzia kichwani mwake akiamini kuwa wakati wa kumkera Mamamia umewadia!!!
Hakujua kuwa muda huo wawili hao anaowawaza walikuwa kwenye hekaheka za kutisha!!!
***
Majira ya saa mbili asubuhi tayari Brenda na monica ambaye ni rafiki yake walikuwa katika kijumba cha mzee mwenye kipara, Monica kwa sababu alikuwa mzoefu alizungumza kwa niaba ya Brenda.
“Anaitwa nani huyo mtu wenu…”
“Hathani…” Brenda kithembe akajibu.
“Hathani… Hathani jina la mtu hilo…”
“Hamna sio Hathani ni Hathani…” Brenda akasababisha monica acheke kabla ya kumsaidia, “Anaitwa Hassan babu, huyu ana kithembe….”
“Hassan nani… kuna akina Hasan wengi duniani…”
“Tembo….” Akamalizia Brenda.
Yule mzee mwenye kipara akaanza kupiga makelele yake hapa na pale. Mara apulize hiki mara anuse kile na kisha akapiga chafya, mara acheke. Ilimradi tu varangati.
“Ohhh! Tuntu… Tuntu ndani ya jiji…. Tuntufyeeee!! Tuntu weeee..” mganga akaanza kuzungumza huku akitazama katika maji yaliyokuwa katika sufuria dogo.
“Ajira.. unasaka ajira wewe….mbona umeajiriwa tayari ama haujaridhika na kazi yako…” mganga akamuuliza Brenda.
“Hamna babu mi thitafuti ajira namtaka Tembo…” akajitetea Brenda. Monica naye akahisi mzee wake ameingia chaka kwa kubashiri uongo.
“Hakipo kingine unahitaji zaidi ya ajira binti, unaitafuta ajira ambayo unayo tayari….unamtaka Tembo….. unamtaka Tutufye Kanyenye… Tuntu!!” Mganga akawa kama anazungumza peke yake hivi.
“Ni kweli unamtaka Tembo!!!”
“Ndio babu…”
“Basi nenda ukamlete kamlete nijue namna ya kumsaidia, amemkosea Tuntu tayari na Tuntu hajui maana ya kusamehe…. Kamlete Tembo… maana kinyume na hapo atazua janga kubwa sana kwa waajiriwa wake, mmojawapo ni wewe… tena wewe wa hivi karibuni ndo mtaanziwa…” Mganga alizidi kuropoka.
“Huyu mzee wako vipi Monica eeeh!! Mara natafuta ajira mara nimeajiriwa, mara nimlete Tembo…. Mambo gani sasa haya jamani… naomba tuondoke kwa kweli…” Brenda akiwa amehamaki na kutangaza hasira zake nje nje alikuwa amesimama tayari.
Ghafla yule mganga akamdaka gauni lake akamvutia ndani kisha akambana vyema asiweze kutikisika. Wakati huu aliendelea kuzungumza lugha alizozifahamu yeye mwenyewe.
Baada ya Brenda kutulia, yule mganga alimfunua paja likabaki nje kisha akamnyunyuzia maji kutoka katika kibuyu. Kisha akamvuta kichwa chake akamuinamisha aweze kuona maajabu.
Brenda akisaidiana na Monica wakatazama kilichopo katika paja la Brenda. Ilikuwa ni alama mfano wa fuvu la kichwa. Brenda akapiga mayowe yule mganga akawahi kumziba mdomo.
“Hii nd’o ajira niliyokwambia…. Umeajiriwa na Tuntu kupitia kwa kibaraka wake aliye matatani.. Tembo!! Unatakiwa kumleta Tembo upesi kwangu na hapo ndipo utapata muafaka wa hili jambo, vinginevyo ndani ya siku mbili sio paja tu, mwili wako wote utakuwa uchi ukizurura huko mtaani.” Mganga sasa alikuwa amemuachia Brenda huru.
Brenda hakuwa na namna zaidi ya kufuata maelezo aliyopewa, ni hapa ambapo Monica aliamua kujiweka mbali naye!!
Urafiki wa kinafiki!!
****
HABARI ya Mamamia kurukwa akili ilikuwa imemvuruga sana tembo. Kuna maswali alihitaji sana apatikane mtu wa kumjibu lakini bahati mbaya hakuwepo mtu huyo.
Yawezekana Mamamia huwa ana kichaa? Au ana majini? Au ni Malaria ilimpanda kichwani?
Hakupata jibu!! Akaamua kulichukulia jambo lililotokea kama bahati mbaya tu. Akanyanyuka na kwenda kuangalia uwezekano wa kutengeneza namba yake ya simu ambayo Mamamia aliitupilia mbali ikiwa katika simu yake.
Zoezi halikuchukua muda mrefu sana!! Akaipata namba yake, akachukua simu ya ziada iliyokuwa ndani akapachika ile kadi ya simu.
Tembo akarejea hewani!!
Baada ya pale akakumbuka gari yake aliyoiacha kule hotelini.
Naifuata vipi sasa wakati yule bwege sijui aliutupa wapi ufunguo, si nd’o mwanzo wa kushikwa uchawi wakasema nimemtupia msichana wa watu majini mimi Tembo nikaaibika!! Tembo alijisemea huku sasa akiwa muoga waziwazi tofauti na zamani.
“Hapa ngoja nimpigie Kithembe nimuulize” Tembo akaitwaa simu yake….
Shit! Namba ya Kithembe haikuwa katika simu yake, kila jina lilikuwa lilibaki katika simu yake iliyotupwa mbali na Mamamia.
Wakati Tembo akizidi kughafirika mara alianza kukerwa na sauti za watoto waliokuwa wakipiga kelele nyingi sana.
“Hapo washamkamata kikojozi basi leo hapakaliki hapa, yaani uswahilini bwana.. hapa nifanye nihame!!” Tembo alizungumza peke yake.
Zile kelele zikazidi kusogea karibu!! Tembo akaliendea dirisha lake ili aweze kumwona huyo kikojozi aliyeandamwa na wenzake!!
“Yaani vitoto bwana, unakuta na vingine hapo vinakojoa kitandani lakini vimeshupalia kumwimbia mwenzao duh!!” Tembo akacheka mwenyewe kisha akazikumbuka enzi alipokuwa mtoto, hata yeye alipenda kuwaandama watoto wanaokojoa kitandani.
Umati ukazidi kusogea na kelele zikazidi, Tembo katika dirisha lake akazidi kuhangaika ili amwone huyo kikojozi!!
Mh! Mbona kikojozi mwenyewe mkubwa hivi!! Tembo alijiuliza baada ya kumwona yule anayekimbizwa na watoto lukuki.
He! Halafu lipo kama uchi lile au ni nguo ile…. Au chizi jamani mbona hee!!….. maajabu…. Halafu.. halafu lile shati kama, kama shati langu vile au nalifananisha!!
Alipoimnalizia ile kauli yule aliyedhania kuwa ni kikojozi mkubwa sasa alikuwa anatazama mbele….
Tembo akaishiwa nguvu miguuni, akataka kukimbia lakini akajihisi amenasa!!
Jicho lilikuwa limemuona Mamamia Mango.. yule aliyemzulia tafrani nyumba ya kulala wageni huko walipokutana.
Sasa ana kundi la watoto zaidi ya mia moja… wanajongea katika nyumba yake.
Amevaa shati lake lilelile la siku ya tukio!!
Tembo akaanza kulia kama mtoto mdogo!! Mkojo ukaomba ruhusa kupenya Tembo akauzuia, mkojo ukalazimisha kupita…
Nguvu zilizidi kumwishia Tembo huku akiiona aibu ikimfuata kwa kasi. Alikuwa na heshima kubwa sana pale mtaani kwao, mama yake mzazi pia alikuwa mtu maarufu hadi mtaa ukafikia kuitwa kwa Mama tembo!!
Sasa anakumbana na aibu ya mwaka!!
Tembo akakumbuka ule usemi wa heri nusu shari kuliko shari kamili.
Akajikongoja hadi mlango wa kutokea nyuma ya nyumba… mlango wa dharula ambao huwa unatumika mara moja moja sana!! Akaufungua na kutokea pande zile, upesi bila kutazama kushoto na kulia alijichanganya katika kundi la watu waliokuwa wakimshangaa Mamamia, akajipenyeza humo ili aweze kutoka kwa usalama.
Ile hali ya kuwa nje ya nyuma ile ambayo kwa namna yoyote ile Mamamia alikuwa amenuia kuingia… walau amani iliishi naye kidogo.
Kama mamamia ataamua kuvamia nyumba na yeye hayupo ndani ilikuwa njema zaidi kuliko yeye kufumaniwa ndani.
Kwanza akithubutu kufanya hivyo lazima watamshika na kumpiga ikiwezekana, hakuna hata mtu mmoja awezaye kumwamini mwendawazimu.
Tembo akajipa moyo kisha akajichanganya katika kundi la watu na kujiweka mbali kabisa na lile tukio.
Bado hakuwa na amani timilifu kwa sababu ya umaarufu wake pale mtaani akahofia huenda anaweza kutokea mtu akamuuliza kulikoni yule dada achague nyumba yake na kuweka kambi pale.
Upesi Hassan akakatiza mitaa kadhaa na kufikia nyumba fulani, akatabasamu baada ya kuona alichokuwa akikihitaji kilikuwepo.
Gari!!
Na mwenyewe ambaye ni rafiki yake naye alikuwepo. Hassan akamweleza juu juu huku akimdanganya kuwa gari yake imeharibika. Yule swahiba wake akakubali kumwazima gari yake.
Tembo akatokomea kuelekea kariakoo, alipoufikia mji akiwa hana kitu cha ziada cha kufanya akaamua kuingia msikiti ambao alikuwa akifahamiana na watu kadha wa kadha. Alifahamiana nao kwa sababu mara kwa mara alikuwa akitoa misaada kila inapotakikanika, hivyo alikuwa akiheshimika pia kama kijana mdogo lakini mwenye mambo makubwa!!
Siku hiyo akaamua kujituliza pale ili tifutifu la nyumbani kwake Mbagala liweze kupoa.
****
Kabla Brenda hajaondoka kwa mganga aliongezewa sharti jingine ambalo lingemwezesha kumrejesha Tembo ama akimkosa basi anaweza kupoteza uhai wake katika namna ya kusikitisha sana.
Mganga yule alizidi kumtisha Brenda na hatimaye akamshauri ayahamishie maswahibu hayo kwa kiumbe mwingine ili apate muda mzuri wa kumsaka Tembo na kumfikisha kwa mganga yule kwa ajili ya tiba.
Mganga akampa Brenda kioo na kisha kumshauri ataje jina lolote ili waweze kuangalia uwezekano wa kuhamisha maswahibu ambayo yangeweza kumkabili kwa sababu ya kuajiriwa na Tembo.
Brenda huku akitetemeka akaijiwa na jina kichwani… akalitaja!!
Mganga akacheka kicheko kifupi kisha akawaruhusu wawili wale kuondoka zao.
Brenda akaanza kuhaha akitafuta namna ya kumpata Tembo huku Monica akijitafutia visababu na kujiweka mbali.
****
ASIA DIGITALI
Neno msikiti, lilimjia akilini mwake katika namna ya kushtukiza. Akafanya tabasamu pana na kujishangaa, imekuwaje hadi akauwaza msikiti ilihali hakuwa mtu wa swala tena.
Tabia zake mbovu za kuwalaghai wanaume na kuwaibia mali zao, leo hii anawaza msikiti.
“Au nd’o shetani kuzeeka anakuwa malaika…” Asia alijiuliza huku wazo la msikiti likiwa palepale. Na hapo ndipo alipokumbuka juu ya kijana wa kuitwa Hassan Tembo!!
Ni muda mrefu sana alikuwa ameelezwa sifa zake na uwezo wake kipesa.
Asia hakutaka kitu kingine cha ziada kwa mwanaume zaidi ya pesa. Hakujali juu ya utu wake, lakini zaidi ni kwamba Asia alikuwa akijiuza katika namna ya kidigitali. Hayajui mapenzi wala hajui nini maana ya kupendana…. Anachoamini ni kuwa anatoa penzi nawe umpatie pesa. Tena sio pesa kidogo!!
Anachuma mamilioni.
(MIKASA ZAIDI YA ASIA NI KATIKA SIMULIZI YA ASIA DIGITALI kama hujaisoma wasiliana nami inbox)
Alikuwa anamiliki gari yake, na nyumba nzima ya kupanga….. pesa yote aliitoa kwa wanaume katika njia za ki-digitali.
Asia akiwa na rafiki yake Husna wakaongoza njia kuelekea msikitini Kariakoo…
. . Jua lilikuwa kali, kilammoja alifanya jitihada za kupambana na joto la jijini Dar es salaam.
Hekaheka za hapa na pale Kariakoo ziliufanya mji kuonekana mdogo sana.
Kanzu nyeupe na mabaibui meusi yalitapakaa huku na kule ishara ya sala ya ijumaa.
. . Asia naye alikuwemo katika hekaheka za siku hiyo.
. . Muda wa sala ulipowadia kila mtu alikuwa mahala pake akiswali.
. . Asia naye alikuwa mmoja kati ya waliojumuika kuswali katika msikiti ambao hajawahi kuswali hapo kabla.
. . Asia aliswali huku mahesabu yake yakienda sawa kabisa juu ya mipango yake madhubuti kichwani.
. . Muda wa swala ulipomalizika Asia alitoka nje ya msikiti.
. . Akaangaza macho huku na kule.
. . Aliyategea mawindo yake yaweze kunasa.
. . Hatua kwa hatua Asia alijitembeza, kwa kasi huku akipigia mahesabu makali ya tukio ambalo litatokea.
. . Asia alikuwa akimtazama mwanaume mfupi mweusi ambaye huenda alikuwa amependeza kuliko wote ndani ya kanzu yake yenye thamani ya juu.
Asia alimtazama jinsi alivyokuwa amejikita katika kutumia simu yake. Asia akatumia upenyo ule.
. . Akajipitisha mbele yake, bwana yule pasipokumwona Asia akajikuta amemkanyaga. Asia akajilegeza akatua chini.
. . Aliyemgonga alikuwa ni Hassan Tembo, Munyama mukubwa kamba fedha ambaye alikuwa amevurugwa haswa na tukio lililotokea kwa Mamamia.
Hassan alikuwa anajulikana sana maeneo yale ya msikitini, asingeweza kumkimbia Asia ama kumpuuzia, aliheshimika kutokana na moyo wake wa kujitolea huku akiwa kijana mdogo.
. . Tukio la Asia akalitumia kama nafasi nyingine ya kuthibitisha kuwa ana pesa japo kwa wakati huo alitumia gari la kuazima na hakuwa na kadi yake ya benki japo alikuwa na kiasi fulani cha pesa alichokuwa amehifadhi ndani ya nyumba yake.
Akaamuru apelekwe katika gari lake binti yule.
Wafuasi wakambeba Asia hadi ndani ya gari la Tembo.
. . Akisindikizwa na wanaume wawili Hassan alimchukua Asia hadi katika hospitali ya watu binafsi maeneo ya mnazi mmoja.
Hapa sasa hakuwahitaji wale watu tena, akabaki peke yake.
Uzuri ni kwamba alikuwa na bima ya afya hivyo alifanya utaratibu na pesa kiduchu ikaongea Asia akatibiwa bure kwa kutumia kadi yake.
. . Hassan baada ya kuelezwa kuwa binti yule hakuwa amepata majeraha makubwa sana aliamua kuondoka naye aweze kumrejesha nyumbani.
Wakiwa ndani ya gari Hassan Tembo akakumbuka kuwa alikuwa matatani, na kilichochokonoa kichwa chake ni kisa cha Mamamia, akajiuliza ni lipi lilisababisha yale mambo kutokea. Akakumbuka na kujisahihisha kuwa haukuwa utaratibu wake kulala na msichana mmoja mara mbili.
Mh! Yawezekana ndo tatizo kweli ama?? Alijiuliza bila kupata jibu.
Akilini mwake sasa aliingiwa na ujasiri wa ajabu sana, hakutishika na kilichotokea chumbani akiwa na Mamamia, ile akili yake ya zamani ikarejea tena kwa kasi akaona Asia alikuwa mtu sahihi kabisa wa kumfanyia majaribio.
. . Dini ya shetani.
Hassan alitakiwa kumwongezea wafuasi shetani. Na wafuasi waliokuwa wakihitajika ni wasichana.
. . Hassan alitakiwa kuwa anawaingiza wasichana katika utumwa ambao utawaweka dhambini. Na dhambi ile wataigawa kwa wanaume wao!
Tayari alikuwa amewavuruga wasichana zaidi ya sita. Wasichana hawa sita kadri walivyokuwa nao wanaunda cheni kubwa zaidi ndivyo Tembo alivyozidi kutajirika.
Hii iliitwa biashara ya mtandao ambayo Tembo alijiunga bila kujua ili aweze kujikwamua kutoka katika umasikini. Na kweli ikawa!!
. . Mitindo yake ya kizaramo, ujanja katika mapenzi ulimuwezesha kuwakamata wasichana wengi sana.
. . Sasa aliona hata Asia alikuwa msichana sahihi sana kwake.
. . “Binti..unaishi wapi kwani?” Tembo alivunja ukimya.
. . “Mbagala rangi tatu..” Asia alidanganya.
. . “Ok..naomba tupite mahali nimesahau kifaa changu halafu nikupeleke nyumbani.” Tembo akaingiza ujanja.
. . Asia hakupinga, kwani hata yeye alikuwa anataka Tembo ajilengeshe aweze kumtapeli kidigitali.
. . Tembo aliendesha gari hadi akaifikia hoteli maarufu na ghali kiasi mitaa ya Kinondoni.
Akamuacha Asia garini, upesi upesi Tembo akachukua chumba kwa senti alizokuwa amebakiwa nazo.
. . Akamwendea Asia garini.
. . Akamsihi wapate chakula kabisa. Asia hakupinga akakubali.
Moyoni kila mmoja alikuwa akifurahia kuwa na mwenzake zaidi na
zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa akiwaza la kwake lakini lililofanana na la mwenzake. Asia alikuwa akiwaza namna ambavyo atamuingiza mkenge Hassan Tembo na kisha kujipatia pesa za bwelele, Hassan Tembo naye alikuwa akiwaza na kuwazua namna ambavyo atamtumia Asia kupata pesa nyingi zaidi huku akiamini lile gundu la Mamamia litakomea hapo.
. . Kila mmoja alikuwa kidigitali zaidi. Pagumu hapo…
. . Tembo hakuwa na wasiwasi kuhusu kufanikiwa kwake kwani alikuwa anaamini kuwa yupo ambaye alikuwa akifanya kazi badala yake.
. . Asia alilazimika kutumia akili zaidi.
. . Baada ya kupata chakula Tembo nd’o alizuga kukumbuka kitu ambacho alikuwa amekisahau katika chumba kimojawapo katika hoteli hiyo.
. . “Vipi nikusindikize?” Asia aliingiza ujanja wake. Tembo akafurahia ombi lile.
Asia digitali na Hassan Tembo wakaongozana hadi chumbani.
Kama ilivyokawaida ya Asia akazuga hapa na pale mara ajikalishe vibaya.
Tembo akatabasamu kisha akafanya kitendo cha ghafla ambacho Asia hakukiona lakini taratibu hali ikabadilika.
. . Matiti ya Asia yakaanza kumwasha taratibu, akayakuna kidogo. Mara yakaendelea kumwasha tena.
. . Hali hii ikamshangaza kidogo, muwasho huu ulikuwa wa aina yake. Haukuwa katika namna ya kukera lakini ulikuwa wa kusisimua.
. . Asia anasisimka? Maajabu.
Matiti yakaendelea kuwasha kwa fujo.
. . Asia sasa alikuwa anamuhitaji mkunaji.
. . Nani zaidi ya Tembo?
. . Tembo alielewa ni nini kinaendelea. Alimsikitikia sana Asia kwani alikuwa anaenda kuingizwa katika mtiririko wa aina yake ambao una maana moja tu. Kumtumikia shetani.
Ni kweli Asia alikuwa amemtumikia shetani kwa kipindi kirefu, lakini hii ya sasa ilikuwa ni utumikiaji wa kilazima.
. . Tembo alikuwa anamuingiza katika ajira mbaya.
Asia akiwa pale kitandani jicho limemlegea hakuelewa ni nini kinaendelea lakini hakika alikuwa anahitaji huduma kutoka kwa Tembo.
Hassan Tembo akajawa na huruma akamvagaa Asia pale kitandani.
. . Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa Asia alikuwa akifurahia penzi. Hisia zilikuwa juu mno na alionyesha ushirikiano wa hali ya juu.
Wazo la kutumia upenyo ule kumwibia Tembo lilipotea, Asia alikuwa katika dunia nyingine.
. . Laiti kama Asia angekuwa anamtambua Tembo vizuri, asingethubutu kujiingiza katika jaribio la kumdhulumu.
. . Tembo alikuwa mwanaume kama wanaume wengine kwa sababu anavaa suruali kama wengine lakini Tembo hakuwa mwanaume wa kawaida.
Alikuwa anasambaza ajira ya kutoka kuzimu. Ajira ya kumtumikia shetani.
. . Baada ya tendo Asia alikuwa amechangamka sana. Alikuwa amepata faraja ya mwili wake.
Asia akaijiwa na wazo la kuzungumza zaidi na Tembo ikiwezekana wawe wapenzi.
Akapanga kusema haya kwa Tembo baadaye wakiachana.
. . Tembo kama alivyoahidi alimwendesha Asia hadi Mbagala akamwacha kituo kikuu. Wakapeana namba na kuagana. Asia akiwa anashangaa Tembo ni mwanaume wa aina gani hadi ameweza kumpagawisha namna ile.
BALAA KWA ASIA ALIYETOLEWA KAFARA
. . Siku iliyofuata kizungumkuti kikaanza.
. . Asia akiwa peke yake chumbani, alianza kupatwa na hisia za maajabu.
Zile hisia za kuwashwa matiti na kupata hamu ya kufanya ngono.
. . Asia alizipuuzia lakini mara zikaendelea kumnyanyasa.Asia alihitaji kukunwa, lakini mkunaji angetoka wapi?
. . Mkusanya uchafu alisikika akiugonga mlamgo wa Asia.Kinyume na siku zote Asia alimkaribisha ndani. Mkusanya uchafu akaingia, Asia akafika hadi sebuleni akiwa na kanga moja.
. . Mkusanya uchafu akashangaa lakini hakuweza kufumba macho.
. . Asia alikuwa katika mateso makubwa.
. . Mkusanya uchafu naye mwanaume anajua mwanamke akiwa katika uhitaji anakuwaje.
. . Mkusanya uchafu akaona hii ilikuwa nafasi ya kipekee ya kutuliza hamu zake. Akamvamia Asia akaitupa kanga mbali naye.
. . Kilichofuata Asia hawezi kukisimulia zilikuwa ni raha za kipekee.
Baada ya tendo Asia akakimbia chumbani kwa aibu kubwa. Mkusanya uchafu akaondoka zake huku akistaajabu nini kimetokea.
. . Hali hii ya utumwa iliendelea tena siku nyingine.
Siku hii mwili wa Asia ukawa mali ya ‘Mr. kucha’…….
. . Hii nayo ikapita. Asia hakuwa kibiashara tena bali alikuwa analiwa bure tena alikuwa akipata faraja ya hali ya juu.
. . Asia yule wa digitali akajikuta amaewingizwa mkenge. Sasa akawa mfuasi wa mapenzi.
Hakujua kama mapenzi hayo alipachikwa na Hassan Tembo ili amsaidie kuongeza idadi ya waumini katika kontena lake la kishetani.
Kila muumini mpya mmoja, pesa ya Tembo ilikuwa inaongezeka.
Asia hadi kufikia wakati huo alikuwa amevuta wateja wapya sita na alikuwa anaendelea kuvuta wengine.
. . Fedheha na aibu zikamtawala na kumpelekesha Asia, akajikuta katika maamuzi mabaya sana.
Maamuzi ya kukataa kurejea alipotoka.
. . Asia alikuwa mfuasi wa mapenzi hapo zamani, alikuwa akipenda amependa kweli lakini baadaye akayageuza mapenzi hayo kuwa biashara. Akapata pesa nzuri. Lakini tangu akutane na Hassan Tembo basi mambo yakabadilika, hazikuwa zikipita siku tatu, Asia alikuwa anahitaji mwanaume wa kukidhi haja zake.
. . Alikuwa anawashwa sana matiti yake, ni mwanaume pekee alihitajika kwa ajili ya kumkuna.
Kila alivyokunwa akajikuta akitoa na utupu wake.
Hii kwake ilikuwa dharau isiyostahimilika.
. . Asia akaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Hawa nao wakamtaka kimapenzi.
Akawapa huduma bila mafanikio.
. . Baadhi ya waganga wakampa maelekezo kuwa kila anapowashwa awe anawatembelea wampe tiba. Huu akaona ni upuuzi.
. . Waganga wa jadi hawakumsaidia chochote.
. . Hospitali napo walisema lugha zao ngumu ambazo Asia hakuzielewa, wakampatia vidonge lakini bado hali ikawa tete. Hamu kwa Asia ikadumu. Na alipoipata haikupoa hadi pale alipopata wa kumpooza. Leo akipoozwa na huyu kesho anapoozwa na yule.
. . Wanaume wakahadithiana na sasa wakawa wanamlia ‘taiming’ akiwashwa wamkune.
Hali hii ikamdhoofisha Asia. Na kumweka katika hali ya kukata tamaa.
Hakuwa mchakarikaji tena. Hakuwa kidigitali tena.
Asia hakungoja ukurasa ujifunge wenyewe akaamua kuufunga kwa nguvu.
. . Ilikuwa siku kama siku nyingine, wanaume kadhaa walikuwa wakiranda randa jirani na nyumba ya Asia wakingoja akumbwe na muwasho.
Walingoja sana kwa siku hiyo lakini hapakujiri chochote. Hali ambayo iliwakera sana, kwani waliufanya mwili ule kama mali yao halali.
. . Wengine waliendelea kuvuta subira hadi usiku lakini cha kustaajabisha Asia hakusikika walau kujishughulisha katika chumba chake.
Ajabu na kweli.
. . Siku nzima bila kutoka kitandani.
. . Wanaume wenye uchu wakaamua kuingia ndani, kutazama kulikoni.
. . Wakatumia tochi zilizo katika simu zao.
. . Wakapekua huku na kule, hawakuona mtu.
Mwisho wakalifikia jiko.
Ni huku walipoukuta mwili wa Asia ukiwa unaning’inia juu.
Ulimi nje.
Asia hakuwa hai tena. Alikuwa ameamua kujiua
. . Alizaliwa kianalojia akaishi kidigitali na hatimaye anakufa kianalojia akiwa na upande wa kanga shingoni kwake, ulimi nje. Miguu ikining’inia.
. . Wale waliokuwa marafiki zake walikana kumjua. Wale walioshiriki naye kuzitumia pesa alizochuma kidigitali wote wakajiweka mbali na mwili ule.
Serikali ikachukua maamuzi baada ya kutangaza na ndugu kukosekana.
Asia akazikwa na serikali.
Huu ukawa mwisho wa simulizi yake ya maisha. Lakini mwisho huu ukaibua makubwa!!
ASIA alikuwa ametolewa kafara na mganga yule kupitia Tembo ili kumpa nafasi mteja wake yaani Brenda aweze kupambana zaidi kumfikisha Tembo kwenye tiba.
Kifo cha Asia kikaondoka na nguvu nyingi za Tutufye Kanyenye yule mtumikia shetani aliyemuajiri Tembo.
Kilichobaki ili kuleta amani zaidi na kila mmoja kurejea katika hali yake ya kawaida kikawa kimoja tu!!
Hassan Tembo apatikane kisha aongozane na Brenda katika kitanda ambacho kwa mara ya kwanza Hassan aliota ile ndoto na alipoamka akaamka na utajiri huku akifanya mambo ya ajabu bila akili yake kutambua.
Mganga alimweleza Brenda kuwa mzimu ule wa Tutufye unatakiwa kuzikwa moja kwa moja. Kwani baada ya siku saba unaweza kuamka tena huku ukiwa na hasira.
“Umtafute Tembo umweleze ninayokueleza, baada ya siku saba akinyanyuka mimi, wewe, yeye na wote walioajiriwa naye tutakuwa matatani, tutakufa vifo vibaya sana…. Tuntu hajui kusamehe.., narudia tena Tuntu hajui kusamehe….” Mganga alimsisitiza Brenda juu ya hilo, na kisha kumsihi afanye juu chini aweze kumpata Tembo.
WAKATI Tembo anatafutwa kwa udi na uvumba, tayari alikuwa amebadili namba ya simu. Biashara yake ilikuwa imezorota sana hivyo akabaki kuwa mtu wa kujifungia tu nyumbani kwa rafiki yake.
Mamamia naye alikuwa amerejea katika hali yake ya kawaida na asikumbuke kitu gani kilitokea katika maisha yake.
Kifo cha Asia kilikuwa kimeondoka na utawala wa Tuntu… lakini kama alivosema mganga… ilikuwa kwa siku saba tu na baada ya hapo yanafuata maafa. Asia anainuka tena ndani yake akiwa amemvaa Tuntu!!
Siku tatu zikakatika na hatimaye kubaki nne, mganga hofu ikatawala na Brenda akakiona kifo kikiwa jirani naye.
****
MGANGA alijaribu kurusha matunguli yake lakini hakuna kilichoonekana kuleta uelekeo wa wapi alipo Tembo. Hii ilikuwa ni siku ya nne, mganga akamlaumu Brenda kwa kumwingiza katika tatizo lile, Brenda hakujua nini cha kujibu, tamaa zake za kutaka kuolewa na Tembo zikamtokea puani….
Dar es salaam ni ndogo kwenye ramani tu, lakini kiuhalisia ni jiji kubwa sana, utaanza vipi kumsaka Tembo mtaa kwa mtaa.
Brenda alikonda haswa.. huku nyumbani kwao alitakiwa kumuhudumia Mamamia ambaye licha ya kuwa timamu tena alitakiwa kuwa chini ya uangalizi wa karibu sana. Wakati huohuo Brenda alitakiwa kushirikiana na mganga wa jadi kuweza kutatua lile jambo ili watetetee uhai wao.
Akili ya Brenda ilitanuka haswa!! Hakuwa na mahali pa kupata ushauri, kikubwa alitakiwa kummpata tembo.
SIKU YA TANO.
Brenda akaona ni upuuzi kufa huku ukikiona kifo ukashindwa kukikwepa. Akaamua kumshirikisha Mamamia juu ya jambo lile, Mamaia akataharuki haswa lakini akakiri kupafahamu nyumbani kwa Tembo. Akamuelekeza Brenda vyema namna ya kufika katika nyumba ile.
Mamamia ambaye alikuwa mnyonge aliyekonda, macho yakamtoka pima. Akapagawa haswa na kumuhimiza mdogo wake afanye kila namna aweze kupapata nyumbani hapo na kisha kumsisitiza Tembo afanye kama mganga alivyowaagiza.
Brenda alikodi pikipiki hadi nyumba aliyoelekezwa na dada yake.
Alipoifikia nyumba akapagawa alipoelezwa kuwa Tembo ameshindwa kulipa kodi yake na haonekani alipo…… na mwenye nyumba alikuwa amemchukua mjumbe tayari kwa zoezi la kuhamisha vitu vya Hassan ili ndani ya nyumba ile aingie mtu mwingine.
Brenda alijikaza asiionyeshe hofu yake waziwazi, lakini alipofika chini ya mti mbali na nyumba aliyokuwa anaishi Hassan Tembo, aliketi chini kisha akaanza kulia na kujuta huku akilini akikumbuka kuwa bado takribani masaa ishirini tu!!
Masaa ishirini Tuntufye Kanyenye ainuke tena akiwa na hasira kali….
Harufu ya kifo nje nje!!
***
Tembo alikuwa amejikunyata katika kochi, miguu yake ikiwa imekunjwa kwenye sehemu ya kukalia kichwa chake kikitazama dari.
Tembo alijipapasa katika mabega yake akavipapasa na vishimo juu ya kifua chake akakiri kweli kuwa amekonda sana. Hakuamini hata kidogo kuwa yupo katika msoto mkali ghafla kiasi kile.Lakini licha ya msoto huo kuna jambo la ziada aliligundua katika mwili wake!!
Tembo hakuwa na hamu na wanawake kama ilivyokuwa awali na pia akili yake ilikuwa ikifikiri kwa mapana zaidi. Akajiuliza, ilikuwaje hata akafanya zinaa na wasichana wengi kiasi kile, hakupata jibu la moja kwa moja.
Mlango ulipofunguliwa ndipo akafikia ukomo wa kuwaza kwake, alikuwa ni rafiki yake ambaye alikuwa amemuhifadhi….. Alikuwa anatokwa jasho na shati lake jeupe likiwa shaghalabaghala!
Tembo akaduwaa kumwona yule bwana katika hali ile, haikuwa kawaida yake hata kidogo. Kukosa unadhifu!
“Yupo wapi huyo mwenzako!?” swali lilisikika kutokea nje…. Tembo akataka kusimama na hapo wakaingia wanaume wawili. Sura zao na lafudhi yao ikawatambulisha kuwa ni watu kutoka mkoa wa Mara.
“Wewe nd’o wa kujifanya kidume sivyo…” swali likamuelekea Tembo. Akaanza kubabaika, mara akaongezeka mtu mwingine ndani ya kile chumba. Huyu alikuwa ni mwanamke, mimba yake ikionekana waziwazi. Sura ile haikuwa ngeni sana kwa Tembo lakini hakujua ni wapi aliiona mara ya kwanza.
“Ndiyo huyu mwenzako eeeh!” mzee aliyekuwa na jazba alimuuliza yule binti…
Binti akatikisa kichwa kukubali.
“Kijana nisikilize kwa makini maamuzi ni mawili tu hapa… Utamlea mwanangu na mimba yenu hii… Ama hii RB nikupeleke kituoni sasa hivi…” mzee akazungumza kwa sauti ya chini akijaribu kuidhibiti jazba yake. Lakini mikono yake ilikuwa ikitetemeka kumaanisha kuwa alikuwa ana hasira kali.
Baada ya kusikia kuhusu mimba Tembo akamtazama tena yule binti safari hii akamwangalia mikononi, akakutana na kicheni kilichoandikwa maneno kadhaa, akamkumbuka Beatrice binti wa kwanza kabisa kukutana naye akiwa ameianza ajira asiyoifahamu, akamnunulia chipsi kuku mwishowe wakazini.
Kumbe alimjaza mimba.
“Tembo eeh ulichoniletea ni aibu mshkaji wangu, mimi nimekabwa ka’ mwizi yaani, cha msingi kaka ili heshima iendelee kuwepo ni heri tu hapa kwangu uondoke… Na hilo sio ombi ujue… we una kwako kabisa naomba urejee tu huko.” Rafiki yake Tembo aliyekuwa amemuhifadhi alitoa amri hiyo.
Tembo hakuwa na la kufanya, kila jambo baya lilikuwa limegeukia upande wake. Beatrice akaachwa pale na wazazi wake. Tembo akatakiwa kuhudumia tumbo na mama. Wakati huohuo aliyekuwa anamuhifadhi naye akakifunga chumba chake na kuondoka akimwacha Tembo nje akiwa hana la kufanya!!
***
Masaa yalizidi kuyoyoma na ahadi ya mganga yule ikiwa ni moja tu. Kama Tembo hapatikaniki hadi muda alioukadiria kupita basi kifuatacho ni maafa makubwa!!! Wote ambao wapo katika orodha ya kupitiwa na Tembo basi kifuatacho ni hasira ya Tuntu kukaa juu yao.
Vifo vibaya, nd’o mganga alichowaeleza!!
Mamamia akiwa bado dhaifu kiafya akaona ni heri nusu shari kuliko shari kamili, akaamua KUINGIA RASMI KATIKA OPERESHENI MSAKO WA Tembo.
Mguu kwa mguu na mdogo wake wakaandamana huku na kule, wakati huo yakiwa yamesalia masaa kumi na ushee ili Tuntufye aweze kunyayuka tena kutoka katika kaburi ambalo alikuwa amezikwa na serikali ndani ya mwili wa Asia Digitali.
Wakahaha huku na kule jitihada zikagonga mwamba.
Hatimaye wakaamua kurejea tena nyumbani kwa Tembo ambapo hakuwa akiishi tena.
Huku wakitumia usafiri wa pikipiki ya kukodi hawakuweza kuhangaishwa na foleni, wakafika yakiwa yamebakia masaa manne tu kabla ya kutokea hayajatokea.
Kila mara mganga ambaye alikuwa na hofu tele alikuwa anapiga simu kuuliza mafanikio. Uoga wa mganga ukazidi kuwapagawisha akina Mamamia na Brenda. Kifo wakakiona kikiwapungia mkono wa kuwaita. Ile kauli ya Tuntu hajui kusamehe nayo ikazidiu kuvitawala vichwa vyao.
Ilikuwa kama bahati ya mntende kuota jangwani!!
Walipofika nyumbani kwa Tembo wakapewa taarifa kuwa ameenda nyumbani kwa mjumbe ili aweze kupewa mizigo yake iliyotolewa ndani baada ya kuonekana kuwa hawezi tena kulipa kodi yake.
Mamamia na Brenda wakiongozwa na mtoto mdogo wakaelekea nyumbani kwa mjumbe.
Huku likazuka timbwili la aina yake!
Tembo alikuwa wa kwanza kumuona Mamamia, msichana yuleyule aliyemtaabisha ndani ya kile chumba na kumsababisha aondoke akiwa amevaa taulo pekee.
Tembo akabaki kutetemeka, mjumnbe hakujua nini tatizo. Mamamia na Brenda wakazidi kumsogelea, Tembo akiwa amekodoa macho yake alihamanika haswa!!
Wakati huu hakutaka tena kuaibika kama ilivyokuwa awali, akahesabu mita kadhaa kutoka lilipokuwa geti akaona zinamfaa kabisa kuukwepa mkasa huu wa hatari, Tembo alikywa akimuogopa Mamamia.
Laiti kama angejua jambo aliloitiwa ni kwa ajili ya usalama wake. Wala asingediriki kufanya alilofanya.
Tembo akaamua kutimua mbio ghafla, akimwacha nyuma Beatrice na tumbo lake pamoja na Mamamia na Brenda.
Labda Brenda alikuwa hakiogopi kifo sana kuliko Mamamia nd’o maana akabaki kuduwaa.
Mamamia hakutaka kuipoteza nafasi hii, upesi akalikunja gauni lake, urembo akaweka kando akaanza kutimua mbio kumfuata Tembo. Na kosa kubwa alilofanya Tembo ni kukimbilia sehemu tambalale ambapo anaonekana. Mamamia akaamua kuifanya hii kuwa nafasi yake ya mwisho kumpata Tembo na nafasi yake ya mwisho kuutetea uhai wake ambao upo mikononi mwa Tembo bila yeye kujua.
Tembo hakuamini alipogeuka nyuma na kushuhudia Mamamia akimfuata kwa kasi.
“NBaabika mtaani kwangu leo hii…” Tembo akajisemea huku akiendelea kutimua mbio.,
Alichoendelea kuamini Tembo ni kwamba Mamamia alikuwa amepandwa na mashetani yake bado. Tembo alipokaza mwendo zuali yake ikafunnguka mkanda na kum legea, akajaribu kuipandisja lakini jitihada zile zikagonga mwamba. Suruali ikatelemka na kumnasa miguu, Tembo akaanguka mchangani, na ndani ya sekunde kadhaa Mamamia akawasili…… akamwangukia pale pale mchangani.
Tembo akaanzaq kupiga mayowe!! Mamamia akiwa anahema juu juu akawa anamshangaa kijana huyu, kumbukumbu kuwa aliwahi kuimletea puruykushani walipokuwa nyumba ya kulala wageni hazikuwepo kabisa.
“Hassan…. Ha….Tembo… tupo hatarini Tembo, tuokoe tafadhali tuokoe tunakufa..” Mamamia akajikaza huku akihema juu juu vilevile akazungumza. Kauli hiyo ikamzidishia Tembo imani kuwa Mamamia bado ana mashetani kichwani.
“Tembo, yaani mimi,wewe, Brenda, na mganga.. wote tutakufa huyo Tuntufye akiamka.. tunakufa Tembo..” alilalamika zaidi. Tembo akasikia jina ambalo aliwahi kulisikia mahali.
“Tuntu ndo nani..” akauliza.
“Alikupa ajira toka kuzimu.. alikuajiri wewe nawe ukatuajiri sisi.. Tembo hakuna muda wa kupoteza hapa. Muda umekwisha Tembo tutakufa.”
“Sasa nafanyaje mimi, nani kaniajiri umesema..aah huyu Tuntu ye yukwapi?” akaanza kuuliza maswali ya kipumbavu Tembo…
Mamamia akamnyanyua, na hapo akina Brenda na Beatrce wakawasili. Brenda akamweleza Tembo kwa kifupi kisa na mkasa na nini hatma yao!!
Tembo akapagawa!!!
Hofu ya kifo ikamwingia na yeye…
Upesi zikachukuliwa pikipiki na kuelekea nyumba aliyokuwa akiishi Tembo zamani, nyumba ambayo Tuntu alimpatia ajira kewa mara ya kwanza. Kwenye kile kitanda alitakiwa akatoe vitu ambavyo vcinatakiwa kuchomwa moto, likiwemo na lile godoro alilokuwa amelilalia siku hiyo.
Tembo akaongoza msafara… wakaifikia nyumba yakiwa yamebaki masaa mawili tu Tuntu ainuke tenma na kuwapa adhabu kuu.
“ANAYEISHI HUMU AMEFIWA AMESAFIRI KWENDA MSIBANI….” Wakapewa jibu hilo na mpangaji mwingine.
Wote kwa pamoja wakachoka, na lilikuwa limebaki saa moja na dakika kadhaa!!!
ITAENDELEA
SIMULIZI Ajira Toka Kuzimu Episode 05
Also, read other stories from SIMULIZI;