SIMULIZI The Escrow Mission Episode 02
NEW AUDIO

Ep 02: The Escrow Mission

SIMULIZI The Escrow Mission Episode 01
SIMULIZI The Escrow Mission Episode 02

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi : The Escrow Mission
Sehemu Ya Pili (2)

“Kama ni kweli,” Madam alidakia.

“Ee kama ni kweli,” Chiba akamalizia.

“Mi sina uhakika,” madam akaongeza.

“Hata mimi pia, sina uhakika,” Chiba akamalizia.

“Kamanda mimi nimemaliza,” Dr. Jasmine alimwambia Amata huku akishuhsa glasi yake iliyokuwa tupu.

“Najua, na asante sana, lakini inabidi uwasilishe taarifa hiyo kunakohusika haraka sana ili taratibu nyingine zichukue nafasi,” Kamanda alieleza.

“Sawa boss.”

Wote wakanyanyuka na kuiacha meza wazi, wakatembea taratibu kuifuata barabara inayoelekea ukumbi mkubwa wa Bunge huku wakiendelea kuongea na vicheko vikitawala. Wakiwa wanatembea kandokando ya barabara eneo la Jamatini, mara ghafla bahasha iliyokuwa katika mkono wa Jasmine ambayo ilibeba taarifa ya vipimo vile ilinyakuliwa na mtu mwenye mkono mwepesi kama Kipanga. Jasmine hakuelewa kilichotokea wakati ile pikipiki ikipita kasi juu yake kukiwa na watu wawili ikielekea barabara ya Dar es salaam. Kamanda Amata akili yake ikalielewa vyema tendo hilo, akatazama kushoto na kulia, akakuta kuna pikipiki zilizoegeshwa pembeni, akaivuta moja na kukaa juu yake, akachomoa pini iliyobana tai yake na kuipachika katika tundu la ufunguo, akapiga stata na kuingia barabarani, waendesha bodaboda wote wakaanza kushangilia.

“Kamandaaaaaa!!!!” Jasmin aliita, Kamanda Amata akaweka mguu chini na kusubiri mwanadada huyo aliyeirukia pikipiki hiyo aina ya boxer kwa usatdi wa hali ya juu; kisha wote wakaondoka kwa kasi. Walifika kwenye mzunguko wa stendi kuu, Kamanda Amata akapepesa macho kutazama watu wale wameelekea wapi, akawaona wakipotelea kwenye barabara kuu ya kwenda Morogoro, naye akawafuata. Ulikuwa ni mfukuzano wa aina yake. Kamanda vAmata alihakikisha hawapotezi watu hawa, “Jishike Jasmin !” alipiga kelele, na Jasmin akalikamata tumbo la Amata barabara akivishakanisha kiganja vya mikono yake kwa mbele, Amata alionesha umahiri wake katika kuiongoa pikipiki hiyo akiyapita magari makubwa na madogo. Lorikubwa la mizigo lilikuwa mbele yao, wale jamaa wakawa wanalipita lile lori ili wapate nafasi ya kuendelea na safari yao, Kamanda Amata aliuona uzembe wao wa kuamua kunyoosha na barabara hiyo. Walikuwa wakikaribia mataa ya njiapanda ya Area C mbele kidogo ya chuo cha CBE.

“Jishike vizuri Jasmine, nafanya manuva,” alimpigia kelele Dr. Jasmine aliyekuwa nyuma naye akamshika sawasawa; Kamanda Amata aliyumba ghafla na kuingia upande wa kushoto wa lile lori wakati wale jamaa wakiwa upande wa kulia wa lile lori, pikipiki aliyokuwa nayo Kamnda Amata ilikuwa ikiongeza mwendo kulipita lile lori na wakati huo huo upande wa pili wa lori wale jamaa nao walikuwa wakiongeza mwendo kuwahi taa za kijani. Amata alipolimaliza lile lori tu akarudi kulia na kusababisha mtafaruku, maana dreva wa lori alifunga breki kali na kusababisha kelele na harufu kali ya mipira kusambaa eneo hilo, nukta hiyo hiyo Jasmine alikuwa kama aliyezinduka, aliutoa mguu wake kwenye pedo maalumu ya kuegeshea mguu upandapo pikipiki na kumpiga teke la kukanyaga yule dereva wa ile pikipiki nyingine, yule bwana akayuba vibaya, alipojaribu kuiweka sawa pikipiki akarudi tena upande wa Amata, na wakati huo kamanda Amata alikuwa katika uelekeo wa kukatisha barabara, akamgonga kwenye tairi la mbele na ile pikipiki ikaanguka barabarani, gari zilizokuwa zikipita hapo zililazimika kufunga breki kali na kusababisha mtafaruku mkubwa, kizaazaa.

Dr. Jasmin tayari alkikuwa amekwisharuka chini na kusimama imara, alivuta teke kali lililotua usoni mwa dereva wa ile pikipiki, akarudi chini kinyumenyume, yule aliyekuwa kama abiria akiwa anajiokotaokota alipata teke la mbavu na kabla hajatulia alikanyagwa mgongoni, Dr. Jasmine alikuw amefura kwa hasira, mishipa shingo ikiwa imemdinda, aliinama na kuiokota ile bahasha. Amata aliicha pikipiki ile, na kusimama chini kwa miguu yake miwili, almkamata yule jamaa aliyekuwa dereva ambaye alikuwa kainuka kwa minajiri yan kukimbia, alimkwida shati lake na kumtazama huso, alimshushia ndosi mbili za katika paji la uso.

“Wewe ni kibaka ee?” akamuuliza.

“Ha- ha- hapana,” yule jamaa akajibu huku akionekana wazi kuwa kichwa chake kilipoteza mtandao.

“Sasa nani aliyekutuma ufanya hili mlilofanya?”

“Tajiri mmoja, tajiri katupatia pesa tumpelekee hiyo bahasha,” akajibu huku bado akiwa katika himaya ya Kamnda Amata.

“Unajua ndani ya bahasha hiyo kuna nini?”

“Si – si – juuuiiii,” alijibu huku kamasi lililochanganyika na damu likimdondoka. Kamanda alimtikisa kwa nguvu na kumuachia akajibwaga chini kama mzigo na wakati huohuo gari ya polisi ilifika eneo lile.

“Afande, kamata hawa niwakute kituo cha kati, msiwahoji lolote mpaka nifike,” akatoa amri huku akimuonesha yule afande upande wa ndani wa koti la suti yake ambapo macho ya afande huyo mdogo police constable yalikutana na nembo ya dhahabu ya usalama wa taifa. Alimgeukia Gina ambaye tayari alikuwa kamuacha yule bwana nusu mfu kwa kichapo cha maana.

“Vipi?” Amata alimuuliza Gina.

“Nilishakwambia sipendi kupiga maana mi nikipiga huwa nakuua au nakuacha kwenye coma,” alimjibu Kamanda Amata huku wakitoka nje ya barabara akiikokota ile pikipiki.

KITUO CHA POLISI DODOMA
“Nani aliwatuma kuchukua ile bahasha?” lilikuwa swali kutoka kwa polisi mmoja aliyekuwa akiwapa kichapo wale jamaa ndani ya chumba maalumu cha kuhojiana kwa shuruti. Hali za watu hao zilikuwa taabani kwa kutotoa ushirikiano na jeshi la polisi.

“Unawaonaje hawa?” Jasmine alimuuliza Amata kutoka chumba cha pili.

“Hawa ni majambazi, sio madereva bodaboda, tazama walivyo majeuri kujibu,” Kamanda Amata akajibu huku akiishusha mikono yake kutoka kifuani alipoikutanisha, “Wanaleta mchezo.” Akazunguka na kuingia katika kile chumba alichokuwa yule mtuhumiwa, akamwomba yule askari asogee pembeni. Amata akamtazama yule jamaa kwa jicho baya.

“Sasa ongea na mimi na kama hutaki basi hapa utataka tu,” akakohoa kidogo, “ Naimbie nani aliwatuma kuipora ile bahasha?” akamtazama lakini yule mtu hakuonekana kujibu.

“Unajifanya sugu si ndiyo?” Amata akasimama na kumpa ishara yule askari, akatoka nje na kuja na kitu kama banio lililobana jiwe la mviringo katika miisho yake, Kamanda akamwambia yule mtu aoneshe viganja vya mikono yake, avifungue, naye huku akitetemeka akafanya hivyo, lile jiwe likawekwa katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, lilikuwa ni jiwe la moto sana lililotoka kwenye jiko la mkaanga chipsi.

“Aaaaaaaiiiiigggghhhhhrrrrr!!!! Nasema afande, nasema,” alilia kwa uchungu huku mkono wake ukiwa umeshikwa kwa nguvu na mkono wa Amata.

“Sema!”

“Ni tajiri, ni tajiri, ni tajiri!” alilalama.

“Tajiri nani?”

“Tajiri mgeni, uuuuiiiii mama, simjui, simjui jina lake,” alilia kama mtoto. Baada ya kibano cha maana kutoka kwa Kamanda Amata yule bwana, akaeleza tu kuwa alikabidhiwa hiyo kazi na mtu asiyemjua, ambaye alimkuta kijiweni kwake. Zaidi ya hapo hakuwa na maelezo yoyote zaidi ya kulia kama mtoto, mkono wake ulikuwa umeungua vibaya kwa moto wa lile jiwe.
Kamanda Amata alitoka nje ya chumba kile, “Mpakieni kwenye gari huyo, akatuoneshe mtu aliyemtuma,” akamwambia askari aliyekuwa eneo hilo la mapokezi. Yule bwana akachukuliwa akiwa na pingu mikononi na kupakiwa kwenye gari ndogo yenye vyoo vya giza, gari inayotumiwa na polisi kitengo cha upelelezi katika kutimiza majukumu yao.
Dakika chache baadae walikuwa tayari katikati ya mji wakielekea kijiweni kwake, kijiweni anakoegesha pikipiki yule bwana. Walipofika na kuonesha kuwa ni hapo, nje tu ya lango la hospitali ya mkoa, Dr Jasmine aliteremka na kuwaendea wale waendesha bodaboda, akasimama kimya akiwaangalia wale vijana waliojipanga wakisubiri abiria.

“Dada hii hapa!” mmoja aliita huku akiwa tayari amemfikia.

“Hii huku ina muziki dada ‘angu,” mwingine alidakia.

“Hapana, kuna mtu namtafuta mnamjua Kaduma?” akawauliza.

“Ndiyo tunamjua, lakini hayupo hapa katoka kama saa hivi imepita,” wakamjibu.

“Kaenda wapi?”

“Alipata mteja akaondoka naye,” Yule kijana akaeleza.

“Kaduma leo kawini maisha, wale jamaa walikuwa na mahela bwana, mmoja akaenda naye mwingine akabaki,” kijana mwingine akadaki.

“kwa hiyo atarudi kumchukua aliyebaki?” Jasmine akauliza.

“Hapana, Yule mwingine alimleta mwenzake yeye aliingia hapo café” Yule kijana akaeleza.

Wakati wote wa mazungumzo hayo; Kamanda Amata alikuwa akisikiliza ndani ya ile gari, aliposikia tu kuwa huyo mtu kaingia hapo café, akashuka kwenye ile gari na taratibu akapita palepale walipo wale vijana na kuvuka barabara hadi kwenye café hiyo iliyotajwa. Akazikwea ngazi na kuingia ndani ya mgahawa huo, akavuta kiti na kuketi nyuma kabisa karibu na mlango akisikiliza maelekezo wanayoampa Jasmine.

“Alivaaje huyo mtu? Unaweza kukumbuka,” jasmine aliendelea.

“Shati kama la kitenge Fulani hivi, yale mashati ya kisasa, kama kitenge hivi lilikuwa la rangi nyeusi na maua meupe, chini alikuwa na suruali nyeusi,”

“Sio nyeusi ni kijivu ya kitambaa,” mwingine akadakia.

“Basi asanteni nilitaka nijue tu kama aliondoka nae au la, asanteni,” Jasmine aliwashukuru.
Kamanda Amata aliangaza macho na kuona mtu aliyevali kadiri ya maelekezo hayo, akainuka na kukiendea ile meza ambayo Yule bwana alikuwa ameketi akipata sharubati.

“Naomba Coke baridi na bilauri tafadhali,” Amata alimwambia mhudumu. Uso kwa uso alikuwa ameketi na Obobo aliyevalia kofia pana kichwani mwake. Aliinua uso wake na kukutana macho na Amata aliyeonekana kuwa na utulivu usio na waa lolote.

“Habari,” Amata akamsalimia mwenyeji wake, lakini Yule mtu hakujibu kasha akaendelea na hamsini zake huku Kamanda Amata akinywa taratibu kinywaji alicholetewa muda huo. Obobo alionekana kutazama saa yake kila wakati, na kugeuka geuka nje mara kadhaa, alikuwa mwenye wasiwasi Fulani.
Baada ya dakika kadhaa alisimama na kulipa chakula chake kasha taratibu akatoka ndani ya mgahawa ule huku mkononi akiwa na  gazeti la The Citizen.

“Mfuate anakoelekea, niko nyuma yako,” Kamanda akajisemea na Jasmine akaupata ujumbe uloe moja kwa moja kupitia heleni yake aliyokuwa ameivaa sikioni mwake. Akajitoa pale kwa waendesha boda boda na kuingia katika taksi mojawapo iliyokuwa maegeshoni.

“Ifuate ile gari, ileee ya njano,” Jasmine alimwambia dereva. Wakatoka maegeshoni na kuifuata hiyo gari.

“Unamjua Yule mtu?” dreva akauliza.

“Ndiyo, tupo pamoja,” Jasmine alijibu wakati ile gari ikichukua barabara kuelekea upande wa sokoni.

“Hakikisha hapotei machoni pako. Niko nyuma yenu nakuja,” sauti ya Amata ikalifikia sikio la Jasmine.

“Vipi bado au tayari, maana naona ukimya unaingia,” Yule dereva sksmwuliza Jasmine.

“We nimekwambia ifuate. Dhida yako nini!” Jasmine alimjibu kwa hasira.

§§§§§

HOTELI YA BAHI ndipo Yule mtu aliposhuka na kuingia ndani yake. Amata aliegesha gari yake jirani na zingine alizozikuta. Akateremka na kuuendea mlango wa hoteli hiyo kabla hajaamua kuingia ndani yake. Akaufunga taratibu, akavuta hatua kuingia na kujongea katika meza ya mtu wa mapokezi aliyeonekana katingwa na kusajili wageni wapya.

“Habari, karibu Hoteli ya Bahi, nkusaidie nini?” Yule mhudumu akaanzisha mazungumzo na Amata akiwaacha wale wageni waliokuwa wamemzingira pale. Amata akamsogelea na kumwinamia karibu na sikio lake.

“Katika hoteli yako kuna mgeni yoyote ambaye si raia wa Tanzania?”

“Ndiyo; na si mmoja,” akajibu.

“Yuko chumba namba ngapi?”

“Samahani kaka, huwa hatutakiwi kutoa siri za wageni wetu, ni kinyume na taratibu za kazi,” Yule mhudumu akamjibu Amata huku akianza kuendelea na zoezi lake la awali.

“Hey!” akamshtua, “Najua una kazi nyingi lakini mimi pia nipo kazini,” akamwonesha kitambulisho chake cha upolisi ihali alishaachana na kazi hiyo kipindi kirefu. Yule Mhudumu akaonekana kugwaya baada ya kukisoma na kukielewa.

“Nipe leja yako,”

“Hii hapa!”

Kamanda Amata akapokea kitabu kikubwa cha kusajilia wageni na kukichambua tarehe za siku nne nyuma, akafuatilia jina moja baada ya jingine. Macho yake yakatua kwenye jina la kigeni na kidole chake kikagonga gonga hapo, kingine kilichomvutia zaidi na hasa kilichoimpa uhakika wa kuwa windo lake limeweka kambi hapo ni jina la Kigogo marehemu, Msesema.

“Kumbe naye alikuwa hapa!” akawaza. Jina la Msesema lilionekana kuandikwa siku mbili nyuma ya lile la Obobo, na hata vyumba vyao vilionekana kufuatana milango. Akatikisa kichwa kwa ishara kuwa ameelewa kitu. Akakifunga kitabu na kumrudishia Yule mhudumu, na kasha baada ya kumshukuru na kumbania jicho binti huyo wa Kinyaturu, akazikwea ngazi na moja kwa moja aliufikia mlango wa chumba kilichokuwa cha Mheshimiwa Msesema, Marehemu. Akataka kupita kuelekea kile cha Obobo lakini akasita, akatazama huku na kule, yuko peke yake, kama kawaida, akacheza na kitasa, sekunde kadhaa akajikuta tayari yuko ndani ya chumba hicho ambacho hakikuwa kwenye utaratibu, vitu vilikuwa vimetawanywa huku na huko.

Ilionekana kuna mtu aliyeingia ndani ya chumba hicho na kufanya upekuzi huo wa harakaharaka lakini usio na utaratibu. Juu kijimeza kidogo kulikuwa na begi la laptop lakini ndani halikuwa na kitu,
 “Ameichukua!” akafikiri, akatazama hapa na pale na kuiendea briefcase akaifungua, na ndani yake kulikuwa na makabrasha ya Ki-bunge, miswada na ajaenda nyingine nyingi za kujadili na kuandika. Katika mfuko wa koti lililoonekana lilivaliwa siku hiyohiyo, Kamanda alihisi anashika kitu kigumu mfano wa simu ya mkono, akaitoa, kweli ilikuwa simu, tena bado ilikuwa inawaka lakini ikiwa ‘Silence’.

Akaiperuzi jumbe tatu nne za mwisho.

“…nitakupitia palepale mpenzi…”
“…sawa utanikuta, mi ni wako tu, nimefunga biashara kwa ajili yako siku zote za Bunge…”
“…sawa Cheupe wangu, leo unipe mambo ya kwenye video…”
“…hara hara usimsahau mkeo…”
“…Kazeeka Yule…”

Kamanda Amata akacheka kwa kukenua tu, “Wazee wana mambo, badala pesa wapatayo wapeleke majimboni wanahonga machangudoa,” akawaza huku akiitia ile simu mfukoni mwake. Akiwa katika kujiandaa kutoka mle ndani, akasikia sauti za watu wakiongea mlangoni mwa chumba hicho. Mara kitasa kikaanza kuchokonolewa, Kamanda akatulia kwanza akiangalai wapi ajipachike. Upande wa dirishani palikuwa na pazia kubwa sana, akaenda haraka na kutazama kwa nje, akagundua kuwa kuna kijiukuta cha kuzuia maji au mwanga nyakati Fulani kwa mtu wa chumba cha chini, akaichukua simu ya Msesema, akajipigia namba yake kasha akaipokea upande wa pili, akaitumbukiza kwenye kopo la maua kasha akasukuma kioo kilichoshikwa kwa aluminiam na kutoka nje, akatazama kiukuta cha pili kilikuwa na umbali kama wa mita moja na nyusu hivi, akajikunja na kujikunjua akaruka kwa ustadi na kutua juu ya kiukuta cha pili, akatulia huku simu yake ikiwa tayari sikioni.

Akasikiliza mazungumzo yote yaliyokuwa yakizungumzwa na wale watu, akang’amua kuwa walikuwa ni polisi na mwingine ilionekana kama ni motto au ndugu wa karibu wa marehemu. Baada ya dakika kama kumi na tano au ishirini waliondoka wakikubaliana kurudi tena kuja kuchukua vitu vya marehemu kwani mara hiyo walikuja tu kwa uchunguzi. Alipohakikisha wameondoka, akarudi kwa jinsi ileile na kuichukua ile simu kasha naye akaondoka.

§§§§§

Jasmine alitulia tuli kwenye moja ya kibanda cha muuza vibanzi akijipatia chakula hicho kinachopendwa na wasichana wengi hasa wanafunzi. Alimwona Kamanda akitoka ndani ya hoteli ile na kasha kuingia katika moja gari za kukodi zilizoegeshwa hotelini hapo na kuondoka.

“Wapi sasa?” akmwuliza kupitia simu ndogo iliyokuwa katika pete yake ambayo ungeiona hiyo pete ni kama pente ya uchumba. Kasha kupitia katika heleni yake akapata jibu.

“Kitalani,”

Jasmine akainuka haraka.

“Dada, mbona hujala kabisa?” muuza vibanzi akamuuliza.

“Asante, nina haraka nifungie nizibebe,” akamjibu. Yule kijana akafunga na kumpatia.

Jasmine aliteremka ngazi za kibanda hicho na kuiendea gari ya wale polisi waliokuwa wakifuatana tangu kule hospitali.

“Sasa ninyi, mumrudishe huyu jamaa lokapu, kasha muendelee na uchunguzi mwingine,” Jasmine akawaambia wakati tayari wamefika katika mzunguko wa barabara unaotenganisha njia za kwenda Kondoa, Singida, Iringa na ile inayoingia mjini, akashuka na ile gari ikaondoka. Kutoka hapo akachukua taxi mpaka ofisi za basi la Kimbinyiko na kuteremka kasha akatembea kwa barabara ipitayo nyuma ya jingo la Bunge na kwa kutumia mlango ulio upande huohuo akaingia katika himaya hiyo.

§§§§§

Obobo alitulia kimya ndani ya chumba kipya katika lodge ya Mwendapole maeneo ya Isanga, lodge mpya tu ambayo vyumba vyake bado vilikuwa vikinuka rangi; mkononi mwake alikuwa ameshika kisu alichokuwa akigusa pande za makali yake kwa vidole vya mkono wa pili, akatabasamu, na weusi wa mwili wake kama angekuwa gizani ungeona meno tu.

Obobo mara tu baada ya kukamilisha zoezi la kwanza aliamua kubadilisha hoteli kimyakimya na kuhamia Isanga ili kujipanga tayari kwa kazi ya pili ambayo kwake aliiona ngumu zaidi, kuhakikisha anazipata kabrasha za mjadala wa pesa za Escrow kabla haujapandishwa kitalani na watu hao waliokuwa ‘mwiba’ kwa wale ‘tatu supa’. “Nitazipata tu hata zikiwa Ikulu, naanza na huyo Kibanio ambaye ndiye kidomodomo kama nilivyoelekezwa, nitambana Kibanio kwa kibanio changu mpaka ataeleza kila nakala ilipo,” akajiwazia kasha akatabasamu tena na kuendelea kukata kinywaji chake akisubiri giza lichachamae ili afanye yake.

4
BAR YA CHAKO NI CHAKO
KAMA KAWAIDA madada poa na Makahaba waliokubuhu walikuwa katika eneo hilo wakiendelea na kazi yao ya uwindaji wa usiku, waliokuwa hapo walikuwa ni wale ambao hawana watu maalumu, wenyewe walidandia kila apitaye kwa bei yoyote wanayoahafikiana kutokana na hali halisi ya mteja mwenyewe. Wale wanaoitwa ‘matawi ya juu’ walikuwa na wateja wao tena kwa muda maalum, walikuwa na uhakika kuwa kesho nitaingiza shilingi ngapi au dola ngapi, hawakupenda kujianika nje usiku wa giza wang’atwe na mbu, la; wao walisubiri simu zao ziite tu na tax isimame nje wapelekwe kutoa huduma.
Jioni hii ya siku ya pili tangu kutokea kifo cha Msesema, Cheupe alikuwa kajifungia chumbani kwake akijaribu kuganga majeraha kadhaa mwilini mwake na kuuguza maumivu yaliyotokana na ajali ya jana yake. Alimpoenda Msesema, ‘buzi’ lake la muda mrefu, kila mara alijikuta akilia pale alipokumbuka kuwa sasa hatomwona tena, aliiweka picha yake kwenye kijimeza kidogo na kuiwekea mshumaa uwakao akiomboleza moyoni; alijiona mjane. Akiwa ndani ya kanga moja tu isiyotanguliwa na chochote, huku kajilaza kihasara hasara katika kitanda kidogo cha futi tatu na nusu, Cheupe alihisi nyayo za mtu anayetembea nje ya mlango wake, akatulia kimya na kupunguza muziki wa dini uliokuwa ukipigwa katika simu yake kama moja ya maombolezo yake kwa bwana wake.

Ile sauti ya zile nyayo ikatulia, akahisi mtu huyo kasimama mlangoni pake, moyo ukamlipuka kwa hofu, akahisi kijiubaridi kikipanda kutoka unyayoni kuelekea utosini huku koo likikosa mate kwa nukta kadhaa.
Ngo! Ngo! Ngo! Mlango uligongwa kwa mbisho wa hodi mara kadhaa, hakuitika, aliendelea kutulia palepale, kimya kabisa. Hodi ile ikagongwa tena na taena, kasha Yule mtu aliyekuwa akigonga akaondoka eneo lile. Baada ya dakika kama kumi hivi, kigiza cha nje kikiwa kimeanza kuifukuza nuru ya nje akasikia sauti ikimwita.

“Cheupe! Cheupe!” ilikuwa sauti ya mtu aliyekuwa akimfahamu, mwanadada mhudumu wa Bar ya Chako ni Chako.

“Bee, Suzi unasemaje?” akaitikia kutoka ndani.

“We mtu umelala au umekufa? Unatutia wasiwasi wenzio!” Suzie akamweleza huku akitikisa kitasa cha mlango lakini mlango ule haukufunguka. Cheupe akauendea na kuufungua, bado akiwa katika vazi lile lile, Suzie akajitoma ndani ya ‘getho’ la Cheupe na kujikalisha kitandani.

“Shoga vipi kujifungia siku nzima?” Suzie aliliza.

“Yaani we acha tu, mwili huu bado unauma sana ziwezi kufanya lolote nakwambia labda baada ya siku tatu mbele,” akajibu.

“Pole! Lilikuja jamaa hapa na moja kwa moja likakuulizia kwa jina kabisa, nikalielekeza chumba chako, mara naona anatoka,

“Nimemsikia akigonga lakini sikufungua,”

“Unakosa chapaa mama, anazo Yule, usijali kasema atarudi,” Suzie aliendelea kuchombeza.

“Aisee, namkumbuka sana mteja wangu, sijui kama nitaweza kwa sasa kuwa na mwingine, maana kila nikimkumbuka mwili unapoa,” Cheupe akajibu.

“Sasa, huyu kanambia atakuja, jitahidi basi mdogo wangu, pesa zisikupite mama, maisha yenyewe yako wapi,”

“Poa Suzie, akija mlete,” Cheupe akakubaliana na Suzi ilhari moyoni mwake alikwishaweka nadhiri ya kutolala na mwanaume yeyote mpaka maombolezo yaishe. Akabaki tena peke yake baada ya Suzi kutoka, akajibwaga kitandani upya huku akiicha kanaga yake ikiangukia upande wa pili na kuruhusu makalio yake kubaki nje ilhali yeye akiwa kalala kifudifudi, machozi yakamtoka na kuujaza mtandio uliokuwa usawa wa uso wake, akapitiwa na usingizi.
Hodi ilisikika tena ikibishwa kwa mtingo uleule wa mwanzo, akagutuka, akatazama saa katika simu yake ilikuwa saa nne usiku, akauendea mlango na kuufungua. Mlangoni palisimama kijana mmoja aliyeonekana shababi kwelikweli. Cheupe alimtazama juu hadi chini,

 “Sijawahi kumuona,” akajisemea moyoni huku akiuma moja ya vidole vyake.

“Karibu ndani,” akamkaribisha.

“Kamanda Amata hakuongea neon lolote, akavuta hatua ndani na kumwacha Cheupe nyuma akiufunga mlango kwa komeo na ufunguo.

“Hatuna viti, karibu kitandani,” akamkaribisha. Amata akaketi kitandani. Kilikuwa ni kitanda kidogo chenye shuka moja la maua maua lililotandikwa juu yake lakini halikuwa katika utaratibu kwa kuwa kulikuwa na mtu aliyelala hapo. Akatzama juu na kugundua kuwa ni chumba cha muda mrefu ambacho singibodi yake ilikuwa imechoka na kuna maeneo yaliyokuwa yakivuja. Kulikuwa na choo ndani yake, tv ndogo ya inchi 14 ilikuwa kimya karibu na kijikabati kidogo cha nguo. Macho yalipoenda upande wa pili wa chumba ndipo alipokutana na picha ya  Msesema  akisindikizwa na kijimshumaa cha shilingi hamsini.

“Bila shaka ni Cheupe!” Kamanda akaanza mazungumzo namna hiyo.

“Ndiyo mimi, karibu ujisikie nyumbani,” akjibu huku ajiweka kitandani, umbali kama wa lura mbili kutoka pale alipokuwa ameketi Amata.
Alikuwa na umbo la haja, toto la kinyaturu, jeupe lenye sura ya duara, kiuno kilichobebwa na makalio mawili yaliyoshiba na kutanguliwa na mguu wa maana.

“Alikosa nini mwanamke huyu hata hasiolewe?” akajiuliza Kamanda, hakupata jibu.

“Karibu sana, mwanaume umeumbika!” Cheupe akamkaribusha na kumsogelea Amata, akaanza kumshika shika mashavuni. Amata alisisimka mwili na kujikuta hashki zikimpanda ghafla hasa mwanamke huyo alipokuwa akibadilisha mikao pale kitandani.

“Mbona huongei kaka?” akauliza.

“Sina la kuongea, nilipokuwa nasikia Cheupe na sifa zako zilinifanya nikutafute,”

“He ! wanaume waongo nyie mwe!” Cheupe akamwambia Amata.
“Uongo wetu nini?”

“Si kama hivyo, eti umenitafuta wakati we wa hapa hapa tu, na kama sikosei ni mnywaji tu wa hapa Chako ni Chako labda uliniona hapa,” Cheupe akaeleza.

“Hapana, mi natoke Mwanza, ni mfanyabiashara, nimefika juzi tu hapa nikasikia watu wakikuongelea ndipo nikakutafuta, wewe ni mwanamke mzuri, mrembo, umeumbika, hebu simama kidogo…” akamwambia. Cheupe akasimama, mara hii kanga yake ikamdondoka, akabaki yeye.

“Nyuma au mbele?” akauliza.

“Ubavuni,” Amata akajibu. Cheupe akamwangalia kasha akageuka na kumpa ubavu. Kamanda Amata akameza mate kwa muonekano wa shepu la kinyaturu, “Msesema wala simlaumu, hapa lazima unase,” akawaza.

“Shilingi ngapi?” Kamanda akauliza.

“Pekupeku na sox?”

“Pekupeku,”

“Pekupeku, saa moja elfu ishirini na tano tu,” Cheupe akajibu huku kamgeuzia mgongo Amata, akiwa hajuia tu ni jinsi gani anampa shida kijana wa watu.

“Na sox!”

“Elfu kumi na tano kwa saa,”

“Ok, nataka usiku mzima,” Kamanda akamwambia na kumfanya Cheupe ageuke na kumwonesha upande wa mbele.

“Laki moja na nusu pekupeku, moja bila senti kwa sox,” Cheupe akajibu. Kamanda Amata akainuka na kumtaka ajiandae waondoke, wakati huo aliinua ile picha ya Msesema.

“Huyu ni nani?” akamwuliza Cheupe.

“Huyo ni marehemu, mbona una wivu mpaka kwa watu waliokufa?” Cheupe akajibu huku akijipaka losheni mwilini mwake.
“Marehemu?” akauliza.

“Ndiyo, kwani we mwenzetu uko wapi? Hujasikia ya Dodoma?” Cheupe akamwuliza Kamanda.

“Asee!” akaishusha na kuiweka palepale ile picha, akamwendea Cheupe na kusimama nyuma yake, mbele yao kukiwa na kioo kikubwa, Amata akaanza kumminyaminya mrembo huyo mwilini mwake, alpomminya  begani upande wa kushoto akapiga kelele za maumivu. Akamwachia.

“Vipi?” akauliza.

“Asssssss bega langu linauma asee,”

“Umefanya nini?” Kamanda akahoji.

“Nimepata ajali hapo jana usiku,” akajikuta kaeleza.

“Ajali, jana? Mbona Dododma jana kulitokea ajali moja tu, na we ulikuwemo?”

Cheupe akajikuta mtegoni, hakuwa na njia nyingine ya kuficha maelezo.

“Kwani we unasema ajali gani?” Cheupe akauliza.

“Hiyo ya Mheshimiwa,” Amata akaeleza kwa kifupi, akauona mshtuko dhahiri kutoka kwa Cheupe, na mapigo ya moyo wake akahisi yanabadilika.

“Ulikuwepo?” akamuuliza.

“Yeah, si unajua mi mfanya biashara, kila anayekuja naondoka naye, usiku uliopita nilimpa huduma huyu Mheshimiwa kwa masaa mane, nikakunja Laki moja yangu safi, wakati tunarudi ndipo tulipata hiyo ajali,” akaeleza.

“Pole sana, tuachane na hayo, vaa twende hotelini kwangu tukale maisha ‘abwelile kabwela’”

Baada ya kujiweka sawa, wakatoka na kuiacha bar hiyo inayojulikana kwa wingi wa nyama.

§§§§§
Mbala mwezi iliangaza mji wa Dodoma kwa madaha, ijapokuwa wengine walikuwa kwenye starehe na shamra shamra za mwisho wa wiki. Waheshimiwa Wabunge walikuwa katika maomboleza, Ijumaa hiyo hakukuwa na kikao chochote cha Bunge na mipango ya mazishi iliratibiwa na kamati maalumu iliyoundwa chini ya Spika. Ilipangwa jumamosi yaani kesho yake mwili wa marehemu ufikishwe katika viwanja vya bungwe, heshima zitolewe na kasha usafirishwe kwenda kwao Rukwa.

Obobo alikuwa kwenye mawindo yake ya kawaida, akijaribu kumtazama huku na kule mtu anayemtaka, Mheshimiwa Kibanio. Alipojihakikishia kuwa Mheshimiwa huyo yupo ofisini yaani pale Bungeni, yeye akaamua kwenda hoteli ya Dodoma ambako ndiko alipopanga kwa kipindi hicho cha vikao vya Bunge. Obobo alichukua tax na taratibu wakaiacha Jamatini mpaka kwenye mzunguko wa kanisa la Anglikana wakakunja kushoto kuichukua barabara ya Iringa, baada ya kuvuka relit u wakakunja kushoto mpaka Hoteli hiyo kubwa mjini Dodoma. Akamlipa dereva tax na kasha yeye akajivuta kwa miguu yake na kuingia mapokezi ambapo alikuta watu wengi wengi. Hapa na pale aligundua kuna ulinzi usio wa kawaida kwani baadhi ya mawaziri walikuwa wapo katika hoteli hiyo, alitazama huku na kule na kuziendea ngazi kasha akapanda taratibu kama mmoja wa wapangaji wa hoteli hiyo, moja kwa moja mpaka ghorofa ya pili na kukuta korido ndefu, alipopita milango kadhaa ndipo alipouona ule anaoutaka, 205, akaujongelea na kuufungua kwa funguo zake, akaingia taratibu na kuufunga nyuma yake.

Hakuwasha taa, alitumia simu yake kuangaza huku na kule, juu ya kimeza kidogo aliona kabrasha kadhaa zimewekwa akaenda na kufungua, akakuta ni mikataba ya gesi, umeme na matakataka mengine; akapekua hapa na pale, hakuona chochote anachokihitaji. “Faili la Escrow” alijiwazia, huku akiendelea kuangalia hapa na pale. Ndani ya kabati akakuta kabrasha lingine, akalivuta nje na kulipekua, ndani yake akakuta bahasha iliyokuwa wazi na ndani yake kulikuwa na karatasi kadhaa, akazichomoa zote na kuzitazama moja moja huku akitikisa kichwa kuhashiria ndizo anazozitafuta.

Akiwa katika kuzitazama vizuri akasikia mlango ukifunguliwa na watu waliokuwa wakiongea kwa Kiswahili walisikika masikioni mwake, akatulia kimya nyuma ya mlango, bastola yake mkononi, kwa hatua za haraka haraka kama umeme akajificha nyuma ya mlango kimya.
Mlango ukafunguliwa, Bwana Kibanio akaingia na watu wengine wawili.

“Una uhakika Mheshimimiwa kama uliliacha nyumbani?” mmoja akauliza.

“Ndiyo, chukua hapo mezani, mi naingia maliwato kidogo,” akaagiza. Yule bwana akaiendea meza na kuinua lile kabrasha pale juu, akalipekuwa na kulisoma kidogo.

“Ndiyo lenyewe?” Kibanio akuliza kutoka chooni.

“Ndiyo ndiyo, si hili la PAC?” Yule bwana naye akauliza.

“Ya, hilohilo, chukua kama lilivyo, nataka nikalifanyie kazi usiku huu ili keshoi kutwa tukianza vikao niwalipue mafisadi live,”

“Teh teh teh aaa mzee we nakuaminia,” Yule mwingine alitia chumvi huku bado akiwa analiperuzi lile kabrasha.

“Twen’ zetu” Mh. Kabanio alimwambia Yule jamaa kisha wakatokomea zao na kuufunga mlango. Obobo akatikisa kichwa kwa kulikosa lile kabrasha kijinga namna hiyo, akasubiri kama dakika mbili hivi, akafungua mlango na kutoka, moja kwa moja akateremka ngazi na kufika nje ya hoteli hiyo. ‘Nifanyeje sasa? Nimsubiri arudi au nimfukuzie nione anaingia kona zipi?’ alijiuliza pa si na majibu, akatylia muda mrefu bila kuamua, akili zilipomrudia akapata wazo la busara zaidi kwake, akaziendea taxi zilizo hapo na kuomba dereva ampeleke katika resort ya Uwanja wa Ndege amabko Mheshimiwa Sagaratumbo anapatikana huko.
Kutokana na barabara kuwa bila magari mengi usiku huo ilimchukua dakika kumi na tano tu kufika eneo hilo, wakalipana na dereva tax kisha akapitiliza moja kwa moja mpaka baa na kuagiza toti moja ya vodka huku akijaribu kusanidu jografia ya resoti hiyo. Watu walikuwa wakitoka na kuingia mabibi na mabwana waliokumbatiana waliokamatana viuno, baa nayo ilikuwa na watu wachache walioonekana kuwa na heshima zao.

Obobo akainuka tarati na kuelekea upande wa chooni ambako kulikuwa na njia nyingine ya kuweza kuifikia milango ya wapangaji. Akakitoa kijikaratasi chake katika mfuko wa suruali na kukisoma.
‘Uwanja wa Ndege Resort namba 22’ kilisomeka namna hiyo. Akapita mlango mmoja mmoja huku akisoma kwa haraka haraka, haikuwa rahisi kwa yeyote Yule kugundua anachokifanya. Alipouona ule mlango akasimama na kupachika funguo yake isiyoshindwa. Lakini kili alipoingiza ufunguo ulishindwa kufika mwisho, akachungulia na kugundua kuna funguo nyingine kwa ndani, ‘Nimemkuta’ akajisemea. Akasimama kwa dakika kama mbili hivi akivuta hisia za kusikiliza nini kinaendelea kama mtu huyo kalala au vipi.

Lakini alikuwa aksikia mikoromo na miguno kwa mbali kisha watu wanaoongea jambo fulani hivi, na mara nyingine alisikia  sauti za viungio vya kitanda kikilalamika, akayikisa kichwa. Akaingiza tena funguo yake na kuusukuma ule wa ndani ukaanguka na kwa haraka akaufungua mlnago na kuingia kisha kuufunga nyuma yake, akasimama mlangoni kama shetani.

“Shhhhhhhhh!” akawataka wasipige kelele, huku bastola yake nay a Segeratumbo zikitazamana.

“Tulia hivyohivyo kijana, kwa nini unaingilia starehe za watu?” Segeratumbo akamwuliza.

“Starehe unazijua wewe?” Obobo akaijibu kwa Kiingereza, alikuwa anaweza.

“Ah! We jambazi ee?” Segeratumbo naye sasa akabadili lugha.

“Shhhhhhh!!” Obobo akamnyamazisha tena, “Weka hicho kibastola chako chini,” akamwamuru.

Mheshimiwa Segeratumbo akajikuta akitetemeka kwa hofu huku Yule mwanamke aliyekuwa naye akiwa hajielewi na wala haelewi kinachoendelea. Obobo akanyosha mkono kama anayetaka kitu Fulani.

“Give it to me!” (Nipe) akamwambia Segeratumbo. Ukimya ukapita kati yao, Obobo sasa akawa akisogea pale kitandani huku akitamka lile neno na kurirudia mara  kwa mara. Yule mheshimiwa hakuelewa ni kitu gani anachotaka bwana huyo. Obobo akaunyakuwa mkoba wa Segeratumbo auliokuwa kwenye meza ya kusomea.

“Huu ndiyo ninaoutaka, ukimwambia mtu kama nimeuchukua, nakuua kesho tu,” akamwambia kisha akaondoka na ule mkoba na kumwacha akimwemwesa midomo, kulia anashindwa kupiga kelele haiwezekani.
Obobo akatoka na kuufunga mlango nyuma yake kisha akapotelea nje ya loji hiyo ambapo alichukua tax na kuondoka zake.

ITAENDELEA

SIMULIZI The Escrow Mission Episode 03

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment